Kama ilivyokuwa katika chaguzi tatu zilizopita, katika uchaguzi huu CUF ilikuwa imeshinda. Habari zinasema kuwa Maalim Seif alikuwa amepata 54%. Wapenzi wa CUF kama kawaida yao walianza kushangilia, wakajazana katika Hotel ya Bwawani kuishinikiza ZEC itangaze matokeo.
Kabla ya hapo baada ya ccm bara kupata taarifa hizo wakaona haiwezekani, ni lazima ccm itangazwe mshindi. Wanasema kamwe hawawezi kufanya kazi na CUF, kwanza sera zao ni tofauti, wakati cuf inataka serikali 3, ccm wanataka status qou.
Akatumwa mzee Mkapa kujaribu kushinikiza mambo, lakini ikawa ngumu, kwani tayari cuf wanajua wameshinda na jaribio lolote litakuwa kinyume na maridhiano. Mzee Mkapa akashindwa, akaomba msaada, ndipo alipotumwa mzee Mwinyi, kujaribu kuwalazimisha ZEC watangaze ccm mshindi, jamaa wakagoma, wakisema hawataki tena vurugu na mauaji, tuheshimu maamuzi ya wananchi. Mzee Ruksa akarudi Dar haraka kutoa taarifa, bado bara wakakataa, ni lazima ccm ishinde, mzee akaambiwa arudi tena ajaribu kuwasihi, akashindwa.
Sasa akaenda JK mwenyewe, yeye hakuwa na mjadala, akawaambia Karume na wenzake kuwa CCM ni lazima itangazwe washindi kama hamtaki Bara inaichukua Zanzibar kijeshi na kufuta baraza la mapinduzi na serikali yake, na kutangaza kuwa hakuna tena serikali ya Zanzibar. Akaitwa Maalim Seif akatishwa na kuambiwa dhahama inayoijia Zanzibar, na hakuna njia isipokuwa kukubali na kumpongeza Dr Shein. Akaambiwa aende kuwatawanyisha wafuasi wa cuf ambao sasa uvumilivu ulikuwa umewaishia na walitaka kuvamia ukumbi ili kujua kulikoni. Kwa busara Maalim Seif akawasihi watawanyike na waende nyumbani. HAPO NJAMA ZA KUCHAKACHUA ZIKAWA ZIMETIMIA.
Amini usiamini Wazanzibari hawana furaha si cuf wala ccm, wanajiuliza kumbe wazanzbari hawana sauti na wabara ndio wanawatawala nyuma ya pazia?
Hiyo ndiyo habari. Zanzibar wamemaliza sasa wanakamilisha uchakachuaji huku bara, na jinsi mambo yalivyo wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
MUNGU IBARIKI TANZANIA