Elections 2010 Kilichotokea Zanzibar - (Kutoka chanzo makini)

Mbalinga

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
1,714
1,370
Kama ilivyokuwa katika chaguzi tatu zilizopita, katika uchaguzi huu CUF ilikuwa imeshinda. Habari zinasema kuwa Maalim Seif alikuwa amepata 54%. Wapenzi wa CUF kama kawaida yao walianza kushangilia, wakajazana katika Hotel ya Bwawani kuishinikiza ZEC itangaze matokeo.

Kabla ya hapo baada ya ccm bara kupata taarifa hizo wakaona haiwezekani, ni lazima ccm itangazwe mshindi. Wanasema kamwe hawawezi kufanya kazi na CUF, kwanza sera zao ni tofauti, wakati cuf inataka serikali 3, ccm wanataka status qou.

Akatumwa mzee Mkapa kujaribu kushinikiza mambo, lakini ikawa ngumu, kwani tayari cuf wanajua wameshinda na jaribio lolote litakuwa kinyume na maridhiano. Mzee Mkapa akashindwa, akaomba msaada, ndipo alipotumwa mzee Mwinyi, kujaribu kuwalazimisha ZEC watangaze ccm mshindi, jamaa wakagoma, wakisema hawataki tena vurugu na mauaji, tuheshimu maamuzi ya wananchi. Mzee Ruksa akarudi Dar haraka kutoa taarifa, bado bara wakakataa, ni lazima ccm ishinde, mzee akaambiwa arudi tena ajaribu kuwasihi, akashindwa.

Sasa akaenda JK mwenyewe, yeye hakuwa na mjadala, akawaambia Karume na wenzake kuwa CCM ni lazima itangazwe washindi kama hamtaki Bara inaichukua Zanzibar kijeshi na kufuta baraza la mapinduzi na serikali yake, na kutangaza kuwa hakuna tena serikali ya Zanzibar. Akaitwa Maalim Seif akatishwa na kuambiwa dhahama inayoijia Zanzibar, na hakuna njia isipokuwa kukubali na kumpongeza Dr Shein. Akaambiwa aende kuwatawanyisha wafuasi wa cuf ambao sasa uvumilivu ulikuwa umewaishia na walitaka kuvamia ukumbi ili kujua kulikoni. Kwa busara Maalim Seif akawasihi watawanyike na waende nyumbani. HAPO NJAMA ZA KUCHAKACHUA ZIKAWA ZIMETIMIA.

Amini usiamini Wazanzibari hawana furaha si cuf wala ccm, wanajiuliza kumbe wazanzbari hawana sauti na wabara ndio wanawatawala nyuma ya pazia?

Hiyo ndiyo habari. Zanzibar wamemaliza sasa wanakamilisha uchakachuaji huku bara, na jinsi mambo yalivyo wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Habari hizo zinaweza kuwa kweli kwa vile tulikuwa tunafuatilia na CUF walikuwa wanaongoza kwa kura nyingi mno. Ghafla tukasikia kuwa hakuna taarifa zozote kutoka Zanzibar zitatangazwa mpaka hapo baadae. Zilipotoka, habari ikawa Shein imeshinda. It was hard for us to believe,lazima kulikuwa na namna!
 
inafanana na kweli lakini kwa waliomsikia mkapa redioni [akiwakilisha mawazo ya wahafidhina na wafuasi wa mwalimu]....alisema "wanasema napinga muafaka ..nasema hapa siupingi naunga mkono serikali ya mseto lakini serikali hiyo lazima iongozwe na CCM"
 
umesahau kusema-pia katika mvutano huo walimuahidi maalim nafasi ya waziri kiongozi!
 
Hii imekaa safi saaaaaana.

Wakati sisi Bara tunapigana na CCM, wenzetu mko busy saaana mkiisaidia. Kama si CUF, Chadema wangelishinda Kigoma majimbo mengi sana.

Kama Lipumba na CUF wangelitoa msaada kwa Slaa na kutupa mgombea mwenza wa maana, mambo yangelikuwa mengine kabisa sasa hivi. Sasa wote tumeingizwa Jando na CCM. Ila nyie lenu ndiyo baya zaidi maana ni lile la Kimasai, bila ganzi na mbele ya wanawake na unalazimishwa USILIE maana wewe ni Mwanaume (ehh, Mapanga shashasha).

Cha ajabu hata mwaka 2015, bado mtataka kuisaliti Chadema na kujifanya mko karibu na CCM na CCM bila hiyana wataendelea kuwa-do. Mwiba na kundi lako kumshambulia Dr Slaa kiko wapi sasa? Kimekula kwenu. Mlijifanya mnawaamini sana CCM, ona sasa. Mmekuwa kama Manyumbu mnaita Fisi awe Mkunga wenu, kaaazi kwelikweli.

Maadamu Lisu, Sugu, Wenje, Mbowe, Zitto, Mnyika wanaingia bungeni, ngoja ninywe Gongo langu hapa Sikonge.

To hell all of you, bila kujali wewe ni CUF, CCM, Chadema au sijui nani.

Mwakani MOTO utawaka pale DODOMA na Dom patakuwa hapatoshi.

Ahhhh, dada yangu Halima Mdee, mwaka 2015 tunaweza kuwa wote Dodoma nikiwakilisha Sikonge na kuwa mbunge wa kwanza wa Upinzani wa Mkoa wa Tabora. Ila leo, All of you u can go to hell, gongo langu uko wapi? Nyama Pori kwa wingi hapa nikisherehekea. Kesho nikiamka, naanza vita na waliochakachua matokeo ya SLAA. SLAA wewe ni Rais wangu bila kujali matokeo.

LALI MPOLA nawaambia wote.
 
Haya yoooteeeee yana mwisho wake! Na mara nyingi mwisho wake ni mbayaaaaaaa!
Mi yangu macho wenzetu walianzaga hivi hivi!

Afu watu mnasema Tanzania kuna Amani huu ni UTULIVU tuuuu! Ila sio AMANI!
 
Mbalinga, hadithi hii kakufundisha nani? Nani?
"Amini usiamini Wazanzibari hawana furaha si cuf wala ccm, wanajiuliza kumbe wazanzbari hawana sauti na wabara ndio wanawatawala nyuma ya pazia?"
Wewe ndiye unayeingia ndani ya wazanizibar ukaona hawana furaha?
Mi naona wewe ni mchochezi wa kisiasa numberi moja, wakati watu wanafurahia amani na utulivu, una siasa cha chuki na huna maana yeyote duniani, unaandika upuuzi wako wa kugawa watu wa zanzibar na pia wa bara na visiwani kwa habari ya kughushi, hata kama ni kweli jambo kama hili hata kama ni kweli kwa nini usinyamaze kwa usalama wa taifa!

mnafiki na ushindwe kwa jina la Alah/Yesu

mi sifungamani na upande wowote ila habari yako iwe ya kweli au sio hutumii busara hata ya hewa!
 
Hii imekaa safi saaaaaana.

Wakati sisi Bara tunapigana na CCM, wenzetu mko busy saaana mkiisaidia. Kama si CUF, Chadema wangelishinda Kigoma majimbo mengi sana.

Kama Lipumba na CUF wangelitoa msaada kwa Slaa na kutupa mgombea mwenza wa maana, mambo yangelikuwa mengine kabisa sasa hivi. Sasa wote tumeingizwa Jando na CCM. Ila nyie lenu ndiyo baya zaidi maana ni lile la Kimasai, bila ganzi na mbele ya wanawake na unalazimishwa USILIE maana wewe ni Mwanaume (ehh, Mapanga shashasha).

Cha ajabu hata mwaka 2015, bado mtataka kuisaliti Chadema na kujifanya mko karibu na CCM na CCM bila hiyana wataendelea kuwa-do. Mwiba na kundi lako kumshambulia Dr Slaa kiko wapi sasa? Kimekula kwenu. Mlijifanya mnawaamini sana CCM, ona sasa. Mmekuwa kama Manyumbu mnaita Fisi awe Mkunga wenu, kaaazi kwelikweli.

Maadamu Lisu, Sugu, Wenje, Mbowe, Zitto, Mnyika wanaingia bungeni, ngoja ninywe Gongo langu hapa Sikonge.

To hell all of you, bila kujali wewe ni CUF, CCM, Chadema au sijui nani.

Mwakani MOTO utawaka pale DODOMA na Dom patakuwa hapatoshi.

Ahhhh, dada yangu Halima Mdee, mwaka 2015 tunaweza kuwa wote Dodoma nikiwakilisha Sikonge na kuwa mbunge wa kwanza wa Upinzani wa Mkoa wa Tabora. Ila leo, All of you u can go to hell, gongo langu uko wapi? Nyama Pori kwa wingi hapa nikisherehekea. Kesho nikiamka, naanza vita na waliochakachua matokeo ya SLAA. SLAA wewe ni Rais wangu bila kujali matokeo.

LALI MPOLA nawaambia wote.

Mkuu nimecheka sana kwa kweli!
 
Cuf na ccm wana deal la kuidhoofisha Chadema wanafanya kwenye urais ccm iongoze na cuf wawe wapili chadema wapate nafasi ya tatu then wananchi wapunguze imani kwa chadema we have to be care men! That's true kuna e-mail nimezinasa kati ya Januari makamba na msemaji wa nje wa cuf zinaashiria hayo.
 
Hii hadithi ni ya kutunga na ya uchochezi. Haikithi vigezo vya kujadiliwa katika forum hii ya great thinkers. Tafadhali wapelekee magazeti ya udaku. Nina wasiwasi hata wao hawataiandika!!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom