Elections 2010 Kilichotokea Zanzibar - (Kutoka chanzo makini)

Hii imekaa safi saaaaaana.

Wakati sisi Bara tunapigana na CCM, wenzetu mko busy saaana mkiisaidia. Kama si CUF, Chadema wangelishinda Kigoma majimbo mengi sana.

Kama Lipumba na CUF wangelitoa msaada kwa Slaa na kutupa mgombea mwenza wa maana, mambo yangelikuwa mengine kabisa sasa hivi. Sasa wote tumeingizwa Jando na CCM. Ila nyie lenu ndiyo baya zaidi maana ni lile la Kimasai, bila ganzi na mbele ya wanawake na unalazimishwa USILIE maana wewe ni Mwanaume (ehh, Mapanga shashasha).

Cha ajabu hata mwaka 2015, bado mtataka kuisaliti Chadema na kujifanya mko karibu na CCM na CCM bila hiyana wataendelea kuwa-do. Mwiba na kundi lako kumshambulia Dr Slaa kiko wapi sasa? Kimekula kwenu. Mlijifanya mnawaamini sana CCM, ona sasa. Mmekuwa kama Manyumbu mnaita Fisi awe Mkunga wenu, kaaazi kwelikweli.

Maadamu Lisu, Sugu, Wenje, Mbowe, Zitto, Mnyika wanaingia bungeni, ngoja ninywe Gongo langu hapa Sikonge.

To hell all of you, bila kujali wewe ni CUF, CCM, Chadema au sijui nani.

Mwakani MOTO utawaka pale DODOMA na Dom patakuwa hapatoshi.

Ahhhh, dada yangu Halima Mdee, mwaka 2015 tunaweza kuwa wote Dodoma nikiwakilisha Sikonge na kuwa mbunge wa kwanza wa Upinzani wa Mkoa wa Tabora. Ila leo, All of you u can go to hell, gongo langu uko wapi? Nyama Pori kwa wingi hapa nikisherehekea. Kesho nikiamka, naanza vita na waliochakachua matokeo ya SLAA. SLAA wewe ni Rais wangu bila kujali matokeo.

LALI MPOLA nawaambia wote.

Duh! Hapo Sikonge nimekukubali!
 
Kama ilivyokuwa katika chaguzi tatu zilizopita, katika uchaguzi huu CUF ilikuwa imeshinda. Habari zinasema kuwa Maalim Seif alikuwa amepata 54%. Wapenzi wa CUF kama kawaida yao walianza kushangilia, wakajazana katika Hotel ya Bwawani kuishinikiza ZEC itangaze matokeo.

Kabla ya hapo baada ya ccm bara kupata taarifa hizo wakaona haiwezekani, ni lazima ccm itangazwe mshindi. Wanasema kamwe hawawezi kufanya kazi na CUF, kwanza sera zao ni tofauti, wakati cuf inataka serikali 3, ccm wanataka status qou.

Akatumwa mzee Mkapa kujaribu kushinikiza mambo, lakini ikawa ngumu, kwani tayari cuf wanajua wameshinda na jaribio lolote litakuwa kinyume na maridhiano. Mzee Mkapa akashindwa, akaomba msaada, ndipo alipotumwa mzee Mwinyi, kujaribu kuwalazimisha ZEC watangaze ccm mshindi, jamaa wakagoma, wakisema hawataki tena vurugu na mauaji, tuheshimu maamuzi ya wananchi. Mzee Ruksa akarudi Dar haraka kutoa taarifa, bado bara wakakataa, ni lazima ccm ishinde, mzee akaambiwa arudi tena ajaribu kuwasihi, akashindwa.

Sasa akaenda JK mwenyewe, yeye hakuwa na mjadala, akawaambia Karume na wenzake kuwa CCM ni lazima itangazwe washindi kama hamtaki Bara inaichukua Zanzibar kijeshi na kufuta baraza la mapinduzi na serikali yake, na kutangaza kuwa hakuna tena serikali ya Zanzibar. Akaitwa Maalim Seif akatishwa na kuambiwa dhahama inayoijia Zanzibar, na hakuna njia isipokuwa kukubali na kumpongeza Dr Shein. Akaambiwa aende kuwatawanyisha wafuasi wa cuf ambao sasa uvumilivu ulikuwa umewaishia na walitaka kuvamia ukumbi ili kujua kulikoni. Kwa busara Maalim Seif akawasihi watawanyike na waende nyumbani. HAPO NJAMA ZA KUCHAKACHUA ZIKAWA ZIMETIMIA.

Amini usiamini Wazanzibari hawana furaha si cuf wala ccm, wanajiuliza kumbe wazanzbari hawana sauti na wabara ndio wanawatawala nyuma ya pazia?

Hiyo ndiyo habari. Zanzibar wamemaliza sasa wanakamilisha uchakachuaji huku bara, na jinsi mambo yalivyo wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

MUNGU IBARIKI TANZANIA

Hadithi hii ni ya uongo. Siasa za Zanzibar bado zimejengeka katika ubaguzi wa Pemba na Unguja. Walipowekewa wapemba wawili, watu wa Unguja wakaamua to settle for the 'lesser devil', mpemba mwenye maslahi na Unguja pia. Watu wa Pemba wakashikilia msimamo wa CUF. Matokeo ndiyo hayo tumeyaona, ushindi wa margin ndogo isiyofikia 1%. Kwa hili mchawi ni wao wenyewe, na bahati nzuri dawa walishaiandaa hiyo ya serikali ya mseto. Hongera zao.
 
Mbalinga, hadithi hii kakufundisha nani? Nani?
"Amini usiamini Wazanzibari hawana furaha si cuf wala ccm, wanajiuliza kumbe wazanzbari hawana sauti na wabara ndio wanawatawala nyuma ya pazia?"
Wewe ndiye unayeingia ndani ya wazanizibar ukaona hawana furaha?
Mi naona wewe ni mchochezi wa kisiasa numberi moja, wakati watu wanafurahia amani na utulivu, una siasa cha chuki na huna maana yeyote duniani, unaandika upuuzi wako wa kugawa watu wa zanzibar na pia wa bara na visiwani kwa habari ya kughushi, hata kama ni kweli jambo kama hili hata kama ni kweli kwa nini usinyamaze kwa usalama wa taifa!

mnafiki na ushindwe kwa jina la Alah/Yesu

mi sifungamani na upande wowote ila habari yako iwe ya kweli au sio hutumii busara hata ya hewa!

Typical CCM nambari one. Eti hata kama ni kweli unyamaze kimya kisa amani. Nenda kasome shule kasoro itakuwa hapo tu.
 
Hii hadithi ni ya kutunga na ya uchochezi. Haikithi vigezo vya kujadiliwa katika forum hii ya great thinkers. Tafadhali wapelekee magazeti ya udaku. Nina wasiwasi hata wao hawataiandika!!

Kwa siasa za nchi hii i can easily believe that it is true. Madudu yoyote yanaweza kufanyika kwa CCM. Hakuna kinachoshindikana.
 
sijawahi kuisoma katiba ya zanzibar.kwani inakataza waziri kiongozi kutoka upinzani?
Katiba mpya imefuta nafasi ya waziri kiongozi na kuanzisha nafasi ya makamu wa kwanza wa rais na makamu wa piliw a rais. Makamu wa kwanza wa rais atatoka katika chama kilichoshika nafasi ya pili katika uchaguzi na makamu wa pili wa rais atatokana na chama kilichoshinda urais na ndiye atakuwa kiongozi wa shughuli za serikali katika baraza la wawakilishi
 
Nimekupata Mkuu Sikonge.

Ngoja na mimi niwape nikijuacho kwa uduchu.

Hapa tunapambana na jitu ka kale lenye umri mkuu na miguvu. Hatupambani na CCM bali Tunapambana na Ibilisi mwenyewe kutoka kuzimu ambaye kila dakika ipitayo hasira zake zinaongezeka.

Ibilisi siku zote ni lazima atawale kwa nguvu kinyume na hiari ya wengi.
Haogopi kuuwa ili kutimiza matakwa yake ya kudumisha utawala wake.

Hii ndiyo asili ya watu wengi ndani na nje ya serikali kuwa na Hofu kuu wakiogopa kitu fulani wasichoweza kukisema.

Wengi wanadhani watu wanawaogopa UWT, UWT ni watoto wadogo sana kwenye hizi duli au niseme wanjikomba tu kwenye so zima.

Fikiria tu,Hivi CCM wangethubutu kumvuna Roho kama Mbawala Bosi Mstaafu wa Mishushu yote Tanzania pale Moshi??

Bosi yule aliingia mkataba na Ibilisi baada ya kupata alichotaka, Mali ,alifikiri angweza kumpa kisogo Ibilisi na kufanya atakavyo. Ibilisi atakupa mali na mamraka yote duniani lakini roho yako ni mali yake. Hivyo Ibilisi hakusita kumkausha ili iwe mfano kwa wote wajifanyao kumchezea.


Watu wenye upeo wao mkuu akina Mkapa mnawaona wajikanyaga ovyo kila wakitoa hotuba zilizo andikwa kuzimu, hawana ujanja wa kufanya lolote kwa niaba yao hata wake zao. Kama hawagusi anga zake Ibilisi siku zote watadumu katika ufalme wake katika furaha yenye ukomo.


Kuna mkataba wa siri ya wazi kati ya Ibilisi na CCM.


Mtu wa kwanza wa CCM akija kukutia mcheche ukubali matokeo ukikataa anaondoka,mwingine atakuja vivyo hivyo wa mwisho atakutaka ukubali matokeo pia ukikataa atakupa 101 na Ibilisi mwenyewe, hapo ndipo neema na Upendo wa Mungu upitao Hekima za wanadamu wote huhitajika.


Kwa mtu dhaifu uliye jaza Hirizi kila pembe ya shati na kikoi chako ni lazima uanguke mbelle ya Bwana mkubwa huyu wa Giza na kusujudi manyoya na kwato za miguu yake.

Lakini kama hujanasa katika moja ya mitego yake itamanishayo katika kila pembe ya dunia kamwe huwezi kumwangukia Jitu huyu wa kale, atanguruma kwa hasira kama radi za masika hatimaye kama paka mwizi kuyoyoma uvunguni mwa Abbys.


Maalimu amepigwa 101 na Ibilisi mpakamwenyewe amesujudu.

Wenzetu wa CUF wanadhani umoja chini ya Imani ya dini utawasaidia, ndiyo kuna kaukweli fulani ukiangalia maeneo kadhaa ya nchi wamepata kura nyingi sana.Lakini kwa tathmini nzito kabisa hakuna kundi la udini liwe la Kiksrito au la Kiislamu liwezalo kushinda na kushika Dola Tanzania kwa kutumia Imani yake.
Viongozi wote wa vyama vya upinzani wanajua hilo CCM pia wanajua udhaifu huo na wanautumia kama mtaji namba moja wa kuwapunguza kasi wapinzani.Wote tunajua Nunda wetu ni CCM kuna haja gani ya kutumia air Time tuipatayo kwa Nadra kuvent shutma dhidi ya mgombea aliye nje ya Utawala kama sisi!!?

Naweza kutabiri kama Shemazi Yohana kwamba CCM watakuwa na wabunge wachache sana kiasi cha kushindwa kusimama kwa miguu yao. Bila aibu CUF wakiingiia Bungeni Safari hii wataunda serikali ya Mseto na CCM ili kuongeza nguvu ya CCM na kuwafanya waunde tena serikali ya pamoja yenye uvunda wote wa CCM.

CUF Watashangaa pale CCM watakapo uza sehemu ya ardhi ya Zanzibar kwa Maghaidi wa Ughaibhuni ili itumike kuendelea kunajisi nchi nyingine Duniani. Mimi naongea tu kama Mtabiri Mbuzi Shemazi Yohana.


Ibilisi ni Extraterestral Being ambaye anawezaishi katika Dimension moja na sisi kwa kujichanganya na kijichomeka ndani ya nafsi zetu wanadamu.Lakini pia Ibilisi anapatika 24/7 katika Dimension nyingine ambayo ni Pure Energy Dimension.Dimension ambayo hakuna Kiwiliwili wala Mada kuna kuwako tu.
“Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majesi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Waefeso 6:12
 
Maji yamemwagika....lakini miaka 5 sio mingi kwa hiyo ushauri wa bure kwa wapinzani ni kuungana tu. Kadiri mnavyoendelea kutafautiana (na CCM inachangia na kufurahia hilo) kwa tamaa binafsi na uchu wa uongozi, ndivyo mnavyoipa CCM kiburi. Matokeo yanadhirisha wazi kuwa bila ya kuungana SI RAHISI KUING'OA CCM. Sasa kazi kwenu, mimi langu :bowl:tu.
 
Sasa ninaweza kuunganisha nyuzi; ndani ya TBC1 tayari tulikuwa na taarifa rasmi kuwa Hamad alikuwa ameshinda uchaguzi kwa 52%, na tulishajiandaa kupokea maelekezo ya kutangaza matokep mara baada ya ZEC kuruhusu. Ikaja turning point...............
 
sishangai hasilani!!
sisiem baadhi ya mafisadi wanajua litakalotokea pindi upinzani ukishika nchi
 
Du, Wachangiaji.

Naona jana kinywaji kilikuwa kikali sana na mengine hata siamini niliandika ingawa yote nakubali kuwa yalitoka moyoni kwangu haswaa na siwezi kusingizia kinywaji. Nimefurahi kuwa kumbe kuna jamaa wa NCCR alishawahi kuwa mbunge wa Mkoa wa Tabora (jimbo). Basi mie labda ntakuwa wa kwanza Wilaya ya Sikonge. Ila hilo si muhimu sana nani wa kwanza na nani wa pili. Cha muhimu ni kuwa Mtanzania/Mnyamwezi ndiyo awe wa kwanza na siyo mimi.

Sikonge hali ni mbaya sana na umasikini wetu ndiyo tumekuwa watu wa YES SIR. Huku hata aje Savimbi kwa nguo za CCM basi atashinda. Itabidi kazi ya ziada kubadilisha hii hali. Ila si vibaya kujaribu maana Mipingo tunaogopa sana KUJARIBU na baadaye USHINDWE. Utafikiri ndiyo mwisho wa Dunia. Kama Mungu anataka upate hasara basi utaipata tu na kama hataki basi huipati. Woga wa nini?

Upande mmoja ni Huzuni na mwingine ni Faraja. Labda ndiyo Raha ya ushindi maana wanasema "Easy Come, Easy Go".

Noyaga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom