Kilichotokea New Orleans 2005

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,932
13,283
Mwaka 2005 mwezi wa nane,Tarehe 23 saa nane mchana,ktk jiji la New Orleans lililopo jimbo la Louisiana nchini Marekani,hali ya Hewa ilibadilika ghafla, baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kuanza kunyesha.
Watu waliichukulia Kama mvua ya kawaida tu, lakini kadri muda ulivyokuwa unasonga mbele ndipo mvua hiyo nayo ilizidi kunyesha.
Kwenye kitongoji kimoja cha jiji hilo kulikuwa na ndoa za mashoga zaidi ya 50 waliokuwa wakifunga ndoa siku hiyo, wakati mvua hiyo ikiendelea baadhi ya mashoga walifurahi na kusema kuwa ndoa yao ilikuwa ya Baraka kwa sababu ya mvua.
Mvua ilizidi kunyesha na Tufani kubwa za Radi na upepo mkali vikaanza kuambatana na mvua.
Giza nene lilianza kufunika jiji la New Orleans,umeme ulikatika,miti iling'olewa kwa dhoruba kali ya upepo.
Ilipofika saa Tano usiku,matumaini ya mvua kukatika ,yaliisha, mvua ikiambatana na upepo mkali iliongeza spidi ya kunyesha.
Taratibu baadhi ya nyumba zikaanza kuanguka.
Ilipofika kesho yake asubuhi, Serikali ya Marekani ilichanganyikiwa,kwa sababu hapakuwa na Dalili za mvua kukatika.
Wananchi wa jiji hilo waliona Dhahiri kabisa kuwa hiyo ilikuwa ni kiama cha mwisho wa Dunia, baadhi yao walichukua magari yao na kuanza kutoroka,si wote walifanikiwa kutoka nje ya huo mji,matajiri wenye Helkopta waliruka kwa tabu na kukimbia mji.
Wenye magari wengi,walikwama baada ya kukuta madaraja yemesombwa na maji.
Siku ya pili,mji mzima wa New Orleans ulikuwa umefunikwa na maji, pamoja na hivyo mvua haikuacha kunyesha.
Rais George Bush,aliruka na Helkopta kuelekea eneo hilo la maafa ili akajionee mwenyewe.
Alipokaribia hilo eneo ,Rubani ilimlazimu kurudi kwanza kwa sababu hali ya Hewa ilikuwa ni mbaya mno.
Siku ya Tatu, wananchi kwa maelfu walikuwa juu ya mapaa ya nyumba zao huku mvua ikiwa imepunguza Kasi ya kunyesha lakini ikiwa bado inanyesha.
Vikosi vya uokoaji wakitumia Helkopta walianza kuokoa mamia ya watu wakiwa juu ya mapaa ya nyumba zao.
Watu zaidi ya 1,750 walipoteza maisha.
Na wengine zaidi ya 120 hawakujulikana walipo hadi leo hii.
Baada ya siku 8, ndipo mvua ilikatika rasmi,na Rais Bush ndo akapata wasaa wa kwenda kushuhudia hilo janga akitumia Helkopta.
Moja kati ya Tukio lililoishangaza Dunia ni Iran kuutangazia ulimwengu kwamba ipo tayari kupeleka misaada ya kibinadamu Marekani.
 
Na Iran walipeleka?
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom