Kilichotokea Makambako ktk Ziara ya Rais pia kilitokea Tunduru,najiuliza Nani atamwambia ukweli Rais?

Nascoba

JF-Expert Member
Mar 16, 2012
310
160
Kama wewe ni mfuatiliaji wa tamthilia ya Sultan bila shaka utakubaliana nami kwamba sio tu ni ngumu kwa kiongozi kuwa na taarifa sahihi bali pia ni hatari zaidi anapozungukwa na watu wanaomsifia kwa lengo la kulinda maslahi yao.

Imekuwa ni kama fashion kwa kila mteule wa Rais akisimama sehemu kuzungumza ni lazima amtaje tena kwa kumsifia na kwa majina yake yote kamili kana kwamba wote wameambiwa ni jinai Kutokumtaja kila wapatapo fursa huku wakitumia kila nguvu kuhakikisha hajui au hapati taarifa sahihi za kinachoendelea ktk uhalisia.Labda wameambiwa kwamba anapenda sifa tu na kwamba ukimsifia anakuwa upande wako!

Wakati hotuba ya Rais ikiendelea pale makambako mara nikasikia Rais akiwaambia wana usalama wamwache na bango lake Mwananchi fulani aliekuwa ameminywa na kuchaniwa bango lake nikashangaa nguvu kubwa inayotumika kuzuia wananchi wenye mapenzi na Rais wao wasiweze kumfikishia kero zao hadi mwingine alifikia hatua ya kulalamika kwamba aling’olewa nywele.

Mara nikakumbuka jinsi wananchi wa Tunduru Mkoani Ruvuma ambavyo walisachiwa na hata kupigwa na kuondolewa ktk eneo la mkutano kisa kuwa na bango lenye ujumbe kwa Rais wao mpendwa.

Nikamkumbuka kilema mmoja aliepoteza mikono yake yote miwili ambae alisafiri kutoka mbali kijijini kwa matumaini ya kuja kumweleza Rais masaibu yake namna ambavyo aliburutwa kama jambazi na kutupwa nje ya eneo la mkutano.Najiuliza tutampata wapi Rais tumweleze kero zetu ikiwa ktk mikutano yake nguvu kubwa inatumika kuhakikisha wananchi hawafungui midomo yao?

Yule Mwananchi wa Makambako ujumbe wake pia ulifanana na hali halisi ya Tunduru maana ulihusu Idara ya maji.Kama kuna idara yenye watumishi wazembe,wasiowajibika wala kuwajibishwa na wanaoishi kwa mazoea miongoni mwa idara zote za serikali kwa hapa Tunduru namba moja ni idara ya Maji.

Hapa Tunduru siku tatu kabla ya ziara ya mheshimiwa Rais Tulipata maji mfululizo mchana na usiku.

Maji ambayo tulishasahau kama huwa yanapatikana na hata baada ya kuyaona wengine waliamua kuyaita maji ya magufuli kwa maana yamekuja kwa sababu ya ziara ya magufuli na ni kweli maana tayari yameshatoweka,kero ambao viongozi wote akiwemo mkuu wa wilaya na Mkurugenzi wanaijua lakini hawaitatui au hawana maarifa ya kuitatua.

Iliwezekanaje maji yakapatikana wakati wa ziara ya mheshimiwa Rais tu na sio kabla ya hapo au baada ya hapo?Bila shaka jibu ni moja tu kwamba viongozi hawa wamejawa na unafiki na hawana nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi au uwezo wao ni Mdogo ktk kutekeleza majukumu Yao.

Barabara za mitaa ambazo zilishajifunga kwa kutopitika zilianza kuchongwa na baadhi ya Mitaro kujengwa,Mitaro na barabara ambazo tangu mwaka jana hazijaguswa.

Kumbe na wenzetu Makambako wana miezi sita hawajaona maji lakini ghafla wakayaona maji ya magufuli.

Mara nikamsikia mheshimiwa Rais anamsifia mkuu wa Wilaya Tunduru ndugu Juma Homera na akasema hata kama kuna mkoa unazubaa zubaa anafaa hata kupewa mkoa.

Baada ya kauli hiyo nikajiridhisha kwamba mheshimiwa Rais hapati taarifa sahihi juu ya watendaji wake na utendaji wao.

Katika tamthilia ya sultan,mambo mengi yanatendeka lakini sultan Suleiman hapati taarifa na akipata haambiwi ukweli bali anafichwa.

Mheshimiwa Rais wananchi wengi wanafurahishwa sana na hatua mbali mbali anazochukua juu ya masuala mbali mbali ya nchi ukiondoa dosari mbili kubwa
Za pesa kuwa ngumu na uminywaji wa demokrasia

Angekuwa hero kwa Taifa
Lakini watendaji wake wengi hasa ktk Wilaya na mikoa ni bure kabisa,
Wananchi wanaponyimwa fursa ya kueleza ukweli wa kero zao kwa Rais,basi ni nani atamwambia ukweli Rais?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli ni kuwa hapendi hayo malalamiko, hasa yanapotolewa katika hadhira kama hiyo. Anachojidanganya yeye ni kuwa timu yake inafanya kila kitu hivyo hatuna tatizo. Sio walio chini ndio wanatumia nguvu kuzuia wenye malalamiko, bali ni onyo alilowapa. Huko kujidai kuingilia watu wapewe nafasi waeleze matatizo yao, ni kuumbuka na pia uongo wa kisiasa wa kutaka lawama ziende kwa wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama ni sahihi mwanaume kuwa mfuatiliaji wa tamthilia zinazousisha uanamke zaidi.

Mfano nimkute mwanaume mkubwa kabisa na madevu yake amekaa na mke wake na familia kwa ujumla wanatazama tamthilia yenye maudhui ya kike naweza nikaruka majoka balaa.
Ni maoni yangu.
 
sio kila kitu lawama ziende kwa magu,hao wakurugenzi wazembe na wafanyakazi idara ya maji hapo tunduru unadhani hawajijui ni wazembe ? lazima wanatafuta njia ya kuzima watu,na ndivyo ilivyo tanzania yote, pia mimi hua nakereka viongozi hasa mawaziri kumtaja rais kila mara,kuna siku waziri wa viwanda anakunywa maziwa then anasema bila magu yasingekuwepo hayo maziwa huko tanga wkati mimi nimeyanywa hata b4 magu kuwa rais
 
Magufuli ndio lawama! Masikosee kumpelekea lawama.
 
Hahaha mleta mada mwenyewe una matatizo, umelalamika kuna tatatizo, lakini mwanzo umesha jilidhisha kwamba eti ANADANGANYWA.

Ukweli ni kwamba hadanganywi, hata yeye uwezo wake ni mdogo, kwa maneno mengine kashindwa kuongoza.

Kama umeona hilo ni tatizo huko, fahamu liko kila mahala na niendelevu. Atajali vipi yeye ikulu yanatoka maji 24/7?

Hizo ni sisa za CCM miaka nenda miaka rudi hazijaanza leo. Jiulize mwenyewe, wakupe maji halafu kwenye kampeni watakwambia nini?

Tumezoea kuambiwa tutaletewa maji, Tangu uhuru mpaka kesho, sasa iweje udhani Anadanganywa?

Tumbili na Nyani ni jamii moja ingawa kitaalam ni wanatofauti lakini kikwetu wote wankula mahindi.

Viazi na mihogo shambani, ukienda shambani ukimkuta nyani na tumbili unawafukuza wote huwezi kusema eti tumbili ni afadhali kwenye uhalibifu wa mazao kuliko nyani.

Binafsi nadhani ,Rais, Wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya wote hawa ni wapigaji wa siasa tu hakuna mtendaji.

Wangeondolewa tukaanza upya. Kungekuwa na ugonjwa selective ningeomba waupate waugue na wafe CCM wote,kasha tuanze na system mpya ya kiutawala.
 
Mara nyingi kwa mwanadamu yoyote kile anatchotamani kukisikia zaidi kuhusu yeye ndicho ambacho huletewa na waliochini yake, Kama Baba anapenda kusikia kuhusu kufaulu ataletewa Habari hizo na wanawe hata kama zinaukakasi kwa kiasi gani bado watamletea kwa kuwa wanajua hependi kusikia changamoto watadanganya alimradi asipate taarifa sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sio kila kitu lawama ziende kwa magu,hao wakurugenzi wazembe na wafanyakazi idara ya maji hapo tunduru unadhani hawajijui ni wazembe ? lazima wanatafuta njia ya kuzima watu,na ndivyo ilivyo tanzania yote, pia mimi hua nakereka viongozi hasa mawaziri kumtaja rais kila mara,kuna siku waziri wa viwanda anakunywa maziwa then anasema bila magu yasingekuwepo hayo maziwa huko tanga wkati mimi nimeyanywa hata b4 magu kuwa rais
Hahaha mkuu watu wanezidsha kumuabudu hadi kero

Alipata kusema ziarani Tabora ''hayo mabango siyasomi..kamtandikie mkeo kitandani.'' baada ya kukereka na wingi wa mabango na matatizo kibaoo

ukitaka bango lisichanwe andika ''umeletwa na mungu na umewazidi awamu zote zilizokutangulia''

siyo unaandika "hatuna maji,ooh hatujui umeme tangia Uhuru, ooh hatumtaki Mkurugenzi... oohh Mara mradi wa stendi unahujumiwa...ooohhh hatuna vyoo.!!?''

Naye Anachokaga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wewe ni mfuatiliaji wa tamthilia ya Sultan bila shaka utakubaliana nami kwamba sio tu ni ngumu kwa kiongozi kuwa na taarifa sahihi bali pia ni hatari zaidi anapozungukwa na watu wanaomsifia kwa lengo la kulinda maslahi yao.imekuwa ni kama fashion kwa kila mteule wa Rais akisimama sehemu kuzungumza ni lazima amtaje tena kwa kumsifia na kwa majina yake yote kamili kana kwamba wote wameambiwa ni jinai Kutokumtaja kila wapatapo fursa huku wakitumia kila nguvu kuhakikisha hajui au hapati taarifa sahihi za kinachoendelea ktk uhalisia.labda wameambiwa kwamba anapenda sifa tu na kwamba ukimsifia anakuwa upande wako!
Wakati hotuba ya Rais ikiendelea pale makambako mara nikasikia Rais akiwaambia wana usalama wamwache na bango lake Mwananchi fulani aliekuwa ameminywa na kuchaniwa bango lake nikashangaa nguvu kubwa inayotumika kuzuia wananchi wenye mapenzi na Rais wao wasiweze kumfikishia kero zao hadi mwingine alifikia hatua ya kulalamika kwamba aling’olewa nywele .. mara nikakumbuka jinsi wananchi wa Tunduru Mkoani Ruvuma ambavyo walisachiwa na hata kupigwa na kuondolewa ktk eneo la mkutano kisa kuwa na bango lenye ujumbe kwa Rais wao mpendwa...
Nikamkumbuka kilema mmoja aliepoteza mikono yake yote miwili ambae alisafiri kutoka mbali kijijini kwa matumaini ya kuja kumweleza Rais masaibu yake namna ambavyo aliburutwa kama jambazi na kutupwa nje ya eneo la mkutano.najiuliza tutampata wapi Rais tumweleze kero zetu ikiwa ktk mikutano yake nguvu kubwa inatumika kuhakikisha wananchi hawafungui midomo yao?
Yule Mwananchi wa Makambako ujumbe wake pia ulifanana na hali halisi ya Tunduru maana ulihusu Idara ya maji.kama kuna idara yenye watumishi wazembe,wasiowajibika wala kuwajibishwa na wanaoishi kwa mazoea miongoni mwa idara zote za serikali kwa hapa Tunduru namba moja ni idara ya Maji...
Hapa Tunduru siku tatu kabla ya ziara ya mheshimiwa Rais Tulipata maji mfululizo mchana na usiku.
Maji ambayo tulishasahau kama huwa yanapatikana na hata baada ya kuyaona wengine waliamua kuyaita maji ya magufuli kwa maana yamekuja kwa sababu ya ziara ya magufuli na ni kweli maana tayari yameshatoweka,kero ambao viongozi wote akiwemo mkuu wa wilaya na Mkurugenzi wanaijua lakini hawaitatui au hawana maarifa ya kuitatua...
Iliwezekanaje maji yakapatikana wakati wa ziara ya mheshimiwa Rais tu na sio kabla ya hapo au baada ya hapo?bila shaka jibu ni moja tu kwamba viongozi hawa wamejawa na unafiki na hawana nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi au uwezo wao ni Mdogo ktk kutekeleza majukumu Yao.
Barabara za mitaa ambazo zilishajifunga kwa kutopitika zilianza kuchongwa na baadhi ya Mitaro kujengwa,Mitaro na barabara ambazo tangu mwaka jana hazijaguswa.
Kumbe na wenzetu Makambako wana miezi sita hawajaona maji lakini ghafla wakayaona maji ya magufuli.
Mara nikamsikia mheshimiwa Rais anamsifia mkuu wa Wilaya Tunduru ndugu Juma Homera na akasema hata kama kuna mkoa unazubaa zubaa anafaa hata kupewa mkoa...
Baada ya kauli hiyo nikajiridhisha kwamba mheshimiwa Rais hapati taarifa sahihi juu ya watendaji wake na utendaji wao.
Katika tamthilia ya sultan,mambo mengi yanatendeka lakini sultan Suleiman hapati taarifa na akipata haambiwi ukweli bali anafichwa.
Mheshimiwa Rais wananchi wengi wanafurahishwa sana na hatua mbali mbali anazochukua juu ya masuala mbali mbali ya nchi ukiondoa dosari mbili kubwa
Za pesa kuwa ngumu na uminywaji wa demokrasia
Angekuwa hero kwa Taifa...
Lakini watendaji wake wengi hasa ktk Wilaya na mikoa ni bure kabisa,
Wananchi wanaponyimwa fursa ya kueleza ukweli wa kero zao kwa Rais,basi ni nani atamwambia ukweli Rais?

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu aliyepoteza mikono nahisi ni yule alifungwa mipira na afisa mtendaji ikafanya damu isiflow km inavyotakiwa na kusababisha mikono yake kuoza hatimae kukatwa.
 
Jaribu kuwa positive na heshimu mawazo ya wenzako.Kwa muda ambao nimekuona kwenye hii forum umeonekana kuwa mjuaji sana,na Mara nyingi umekua ukipinga kila kitu..kulikua na haja gani ya kumshambulia mleta mada kisa kufananisha aliyoyaona na tamthilia ya sultan?

Usichokipenda wewe haimaanishi wengine wasikipende.
 
Shida inaanzie kwake kutokana na aina yake ya uongozi wa kutopenda maoni hasi,wakati wa kikwete hakuna mtu alikua ana hangaika kukagua mabango kwenye ziara zake. Raisi hapendi kukosolewa,kulalamikiwa kwa hiyo wale wanaozuia mabango ni kwa sababu ya kuogopa kumkwaza raisi.

Pia kuna shida ya serikali kuu kuhodhi pesa za serikali za mitaa,wilaya kama ya kyela imerudishiwa 26% ya fedha zake kiasi kwamba inakua ngumu kuwekeza kwenye maboresho ya huduma .Hata hayo maji mliyoyapata wakati wa ziara ya raisi inawezekana viongozi wa wilaya walitoa hela zao binafsi kwenye matengenezo ya muda mfupi ku-save face.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha mleta mada mwenyewe una matatizo, umelalamika kuna tatatizo, lakini mwanzo umesha jilidhisha kwamba eti ANADANGANYWA.

Ukweli ni kwamba hadanganywi, hata yeye uwezo wake ni mdogo, kwa maneno mengine kashindwa kuongoza.

Kama umeona hilo ni tatizo huko, fahamu liko kila mahala na niendelevu. Atajali vipi yeye ikulu yanatoka maji 24/7?

Hizo ni sisa za CCM miaka nenda miaka rudi hazijaanza leo. Jiulize mwenyewe, wakupe maji halafu kwenye kampeni watakwambia nini?

Tumezoea kuambiwa tutaletewa maji, Tangu uhuru mpaka kesho, sasa iweje udhani Anadanganywa?

Tumbili na Nyani ni jamii moja ingawa kitaalam ni wanatofauti lakini kikwetu wote wankula mahindi.

Viazi na mihogo shambani, ukienda shambani ukimkuta nyani na tumbili unawafukuza wote huwezi kusema eti tumbili ni afadhali kwenye uhalibifu wa mazao kuliko nyani.

Binafsi nadhani ,Rais, Wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya wote hawa ni wapigaji wa siasa tu hakuna mtendaji.

Wangeondolewa tukaanza upya. Kungekuwa na ugonjwa selective ningeomba waupate waugue na wafe CCM wote,kasha tuanze na system mpya ya kiutawala.
Hivi kuongoza taifa na kuongoza chama nani ana kazi ngumu?

Mbowe chama kimemshinda hamsemi mnaona rais tu,mwishowe mtataka rais ndiyo awaandike barua za dhamana mahakamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wewe ni mfuatiliaji wa tamthilia ya Sultan bila shaka utakubaliana nami kwamba sio tu ni ngumu kwa kiongozi kuwa na taarifa sahihi bali pia ni hatari zaidi anapozungukwa na watu wanaomsifia kwa lengo la kulinda maslahi yao.

Imekuwa ni kama fashion kwa kila mteule wa Rais akisimama sehemu kuzungumza ni lazima amtaje tena kwa kumsifia na kwa majina yake yote kamili kana kwamba wote wameambiwa ni jinai Kutokumtaja kila wapatapo fursa huku wakitumia kila nguvu kuhakikisha hajui au hapati taarifa sahihi za kinachoendelea ktk uhalisia.Labda wameambiwa kwamba anapenda sifa tu na kwamba ukimsifia anakuwa upande wako!

Wakati hotuba ya Rais ikiendelea pale makambako mara nikasikia Rais akiwaambia wana usalama wamwache na bango lake Mwananchi fulani aliekuwa ameminywa na kuchaniwa bango lake nikashangaa nguvu kubwa inayotumika kuzuia wananchi wenye mapenzi na Rais wao wasiweze kumfikishia kero zao hadi mwingine alifikia hatua ya kulalamika kwamba aling’olewa nywele.

Mara nikakumbuka jinsi wananchi wa Tunduru Mkoani Ruvuma ambavyo walisachiwa na hata kupigwa na kuondolewa ktk eneo la mkutano kisa kuwa na bango lenye ujumbe kwa Rais wao mpendwa.

Nikamkumbuka kilema mmoja aliepoteza mikono yake yote miwili ambae alisafiri kutoka mbali kijijini kwa matumaini ya kuja kumweleza Rais masaibu yake namna ambavyo aliburutwa kama jambazi na kutupwa nje ya eneo la mkutano.Najiuliza tutampata wapi Rais tumweleze kero zetu ikiwa ktk mikutano yake nguvu kubwa inatumika kuhakikisha wananchi hawafungui midomo yao?

Yule Mwananchi wa Makambako ujumbe wake pia ulifanana na hali halisi ya Tunduru maana ulihusu Idara ya maji.Kama kuna idara yenye watumishi wazembe,wasiowajibika wala kuwajibishwa na wanaoishi kwa mazoea miongoni mwa idara zote za serikali kwa hapa Tunduru namba moja ni idara ya Maji.

Hapa Tunduru siku tatu kabla ya ziara ya mheshimiwa Rais Tulipata maji mfululizo mchana na usiku.

Maji ambayo tulishasahau kama huwa yanapatikana na hata baada ya kuyaona wengine waliamua kuyaita maji ya magufuli kwa maana yamekuja kwa sababu ya ziara ya magufuli na ni kweli maana tayari yameshatoweka,kero ambao viongozi wote akiwemo mkuu wa wilaya na Mkurugenzi wanaijua lakini hawaitatui au hawana maarifa ya kuitatua.

Iliwezekanaje maji yakapatikana wakati wa ziara ya mheshimiwa Rais tu na sio kabla ya hapo au baada ya hapo?Bila shaka jibu ni moja tu kwamba viongozi hawa wamejawa na unafiki na hawana nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi au uwezo wao ni Mdogo ktk kutekeleza majukumu Yao.

Barabara za mitaa ambazo zilishajifunga kwa kutopitika zilianza kuchongwa na baadhi ya Mitaro kujengwa,Mitaro na barabara ambazo tangu mwaka jana hazijaguswa.

Kumbe na wenzetu Makambako wana miezi sita hawajaona maji lakini ghafla wakayaona maji ya magufuli.

Mara nikamsikia mheshimiwa Rais anamsifia mkuu wa Wilaya Tunduru ndugu Juma Homera na akasema hata kama kuna mkoa unazubaa zubaa anafaa hata kupewa mkoa.

Baada ya kauli hiyo nikajiridhisha kwamba mheshimiwa Rais hapati taarifa sahihi juu ya watendaji wake na utendaji wao.

Katika tamthilia ya sultan,mambo mengi yanatendeka lakini sultan Suleiman hapati taarifa na akipata haambiwi ukweli bali anafichwa.

Mheshimiwa Rais wananchi wengi wanafurahishwa sana na hatua mbali mbali anazochukua juu ya masuala mbali mbali ya nchi ukiondoa dosari mbili kubwa
Za pesa kuwa ngumu na uminywaji wa demokrasia

Angekuwa hero kwa Taifa
Lakini watendaji wake wengi hasa ktk Wilaya na mikoa ni bure kabisa,
Wananchi wanaponyimwa fursa ya kueleza ukweli wa kero zao kwa Rais,basi ni nani atamwambia ukweli Rais?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa Makambako ulichokisema kuhusu maji ni uongo. Makambako maji yapo muda mrefu tu, labda umesema ni salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama ni sahihi mwanaume kuwa mfuatiliaji wa tamthilia zinazousisha uanamke zaidi.
Mfano nimkute mwanaume mkubwa kabisa na madevu yake amekaa na mke wake na familia kwa ujumla wanatazama tamthilia yenye maudhui ya kike naweza nikaruka majoka balaa.
Ni maoni yangu.
kumekucha nenda shule Dogo watu wanaongea mambo ya msingi wewe unaleta blabla hapa
 
Biashara ya maji huko Tunduru na Makambako inalipa Sana nini? Dumu la Lita 20 bei gani huko?

Pambaneni na wanaouza maji huko. Kama mtandao wa maji upo na Siku ya ziara ya Mh. maji yalitoka maana yake kuna mchezo mchafu unaendelea huko wa kuuza maji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama ni sahihi mwanaume kuwa mfuatiliaji wa tamthilia zinazousisha uanamke zaidi.

Mfano nimkute mwanaume mkubwa kabisa na madevu yake amekaa na mke wake na familia kwa ujumla wanatazama tamthilia yenye maudhui ya kike naweza nikaruka majoka balaa.
Ni maoni yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaan nilipoona tu mstari wa kwanza wa tamthiliya ya sultan nikaishia hapo hapo. Wandugu kaongea nini humo mliosoma!?
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom