Kilichotokea kwenye uchaguzi mdogo wa Marudio ni dalili mbaya 2020

LENGISHO

Senior Member
Sep 15, 2017
169
245
Nmejaribu kuutafakari uchaguzi wa mdogo wa marudio katika kata 43 na matukio yaliyotokea kipindi cha kampen na siku ya uchaguzi pia najaribu Kuvuta taswira namna uchaguzi mkuu utakavyokuwa 2020 na hata ule uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 ,

Naitafakari kauli kama hii tena Kutoka kwa Mkuu wa Kaya " itakua ni ajabu kama mkrugenzi unapewa gari na mafuta, unalipwa mshahara halafu siku ya uchaguzi unamtangaza mpinzani eti ameshinda: Mh. Dr Magufuli.

Hii kauli ilitoka siku nyingi sana kabla ya 26/11/2017 ambapo ilikua siku ya uchaguzi kata 43, ambazo CDM Imeshindwa vibaya sana kwa kuambulia kata 1 kati ya kata 43 ., tunakubali lakini je tunaendaje 2019 na 2020? tunabeba taswira gani ya matukio yaliyotokea katika uchaguzi wa marudio ?

Niwakumbushe tu 2019 kuna uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji nchi nzima, 2020 kuna uchaguzi wa serikali kuu kwa maana ya rais, wabunge na madiwani.

Uchaguzi huu uliofanyika jana tarehe 26/11/2017 uliogubikwa na ukiukwaji wa haki za binadamu ( watu wamekatwa kwa mapanga, watu wameuawa ( aliyekuwa katibu wa CDM katika kata moja ya uchaguzi wa marudio Tabora) .. wakala wa CDM walivyokatwa na mapanga Arumeru, Wagombea Udiwani walivyopigwa na kujeruhiwa ( Moshi ,hai kata ya Bomambuzi..)..hakika hii ni dhahiri kuwa Jeshi la polisi limeshindwa kazi yake, serikali ya Mzee wa Chato nayo imeshindwa kabisa kuheshimu haki za raia wake......

Hii inatupa picha kuwa yamkini hata lile tukio la Kushambuliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu serikali inahusika 100% , Hata lile la kkupotea kwa Ben Saanane nayo itakuwa inahusika, hata ile miili iliyookotwa Kule zanzibar,mto ruvu, pwani, na rufiji yamkini nayo inahusika .... wananchi wanapata ujasiri wa kusema na kuamini hivyo kwa sababu serikali kupitia jeshi la polisi limekaa kimya hadi sasa, maana kuna maeneo pia yaliripotiwa kuwa jeshi la polisi liliwashikilia na kushirikiana na msimamizi wa uchaguzi kuwatoa nje mawakala wa CDM kule mkoani Arusha .............

pengine 2020 wapinzani wakauawa zaid na serikal ikafumba macho,

je Utawala wa Kikoloni Umerejea ? je utawala wa wakina Hitler,Idd Amin Dada , Benito Musolin, Umerejea tz ?
 
" itakua ni ajabu kama mkrugenzi unapewa gari na mafuta, unalipwa mshahara halafu siku ya uchaguzi unamtangaza mpinzani eti ameshinda: Mh. Dr Magufuli.
Kauli hii ni mbaya sana, mwenye busara atasikitika na mwenye mihemko atafurahia.
 
Ndg hizi vurugu zilikuepo hata 2015 ila upande mmoja ulikua haujiamini
Rafu nyingi sana watu walijifanya mawakala wengine walijifanya wasimamizi
Ilikua vurugu tupu baadhi ya maeneo vikosi maalum na magari yalikua yanabeba masanduku na hakuna wa kukemea polisi walikua kama mgambo waogaa weee
Walishindwa wapi washike wapi waache
Kwanini ilikua hivyo?? Kutojiami kwa serikali kile kipindi sasa hivi mmh kalagi baho mchezo wa kuishi
 
" itakua ni ajabu kama mkrugenzi unapewa gari na mafuta, unalipwa mshahara halafu siku ya uchaguzi unamtangaza mpinzani eti ameshinda: Mh. Dr Magufuli.
Kauli hii ni mbaya sana, mwenye busara atasikitika na mwenye mihemko atafurahia.
Duh hivi mimi nipo Tz kweli? Sijaisikia hii! Eeh Mungu baba wewe ndiwe msemaji wa mwisho!
 
Bavicha na Bawacha wamechanganyikiwa.. endeleeni kupiga siasa zenu za porojo kwenye mitandao mkijidanganya mtachukua nchi kwa siasa nyepesi na za kizushi kama mnazozifanya..

Wenye akili zetu tulishawadharau machadema na mabavicha kwa kupinga pinga kila jambo na kuyatetea majizi na mafisadi. 2020 mkipata wabunge wa kuchaguliwa watano tu shukuruni Mungu..
 
Chadema mnaingizwa chaka na mbowe, Nassari anasema madiwani wananunuliwa Mbowe anawaondoa wasigombee! Sijui mtapata akili lini manyumbu.
 
Chadema mnaingizwa chaka na mbowe, Nassari anasema madiwani wananunuliwa Mbowe anawaondoa wasigombee! Sijui mtapata akili lini manyumbu.
wengi wenu Mmenyweshwa Unga wa Ndere....sijawaelewa kabisa... ina maana mnashabikia vitendo vya kutekwa, kuuawa na hata kushambuliwa kwa baadhi ya wafuasi wa upinzani? natamani ingekuwa ni ndugu zenu wameshambuliwa..... inamaana hata hamkupata clip zilizosambaa mitandaoni kuona namna watu walishambuliwa huko Arumeru ?
 
Back
Top Bottom