Nimeandika hapa ni baada ya kupata habari toka humu jamvini inayohusu Uchina kutaka kulichukua na kuwa chini yao shirika mamlaka ya umeme la Zambia,na hii ni baada ya kushindwa kulipa mkopo usio na masharti toka kwa wachina. Hadithi hii haina tofauti na kilichotokea hapa kwetu kwa TAZARA,tulipatiwa mkopo mkubwa sana na wachina usio na riba wala masharti yoyote,tumeshindwa kulipa na ndio maana hata kufikiria kulibinafsisha inakuwa ngumu.
China ndio wenye kauri ya mwisho,tafakuri yangu inachagizwa na huu mkopo ulioahidiwa na Uchina ktk mkutano wa hivi karibuni,tuwe makini sana na hela za wachina,kama hakuna ulazima wa hela hizi ni bora tuachane nazo,tusikope bali wapewe fulsa ya kuwekeza tu.