Kilichotokea kwa madee wakati akiigiza ndani ya gari la polisi.

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
Madee.
Kuna uwezekano ukawa umesikia sana watu wakizungumzia stori za msanii Madee wa Tiptop connection kuandika kitabu na kucheza movie inayohusiana na maisha yake, lakini nauhakika haujasikia kisa kilichomkuta polisi wakati wa utengenezaji wa hiyo movie.Kwenye

sehemu ya movie yake kulikua na scene inayotaka aigize kama kakamatwa na polisi tena akiwa ndani ya gari la polisi, wote tunafaham

kwamba hata waigizaji wa movie za kibongo huwa kwenye sehemu zinazohusu polisi ni ngumu kupata polisi halisi au vifaa halisi vya polisi wa kibongo, ndio maana huwa wanatengeneza sare zao na kuigiza kama polisi wenyewe.
Sasa Madee yeye alipata bahati ya kuigiza ndani ya gari la polisi kabisa na polisi halisi wa kituo cha polisi urafiki wakiwemo ndani ya movie, na wakaanza kushoot.
.
Madee anasema "nilipofika kituoni pale tayari nilikua nimempigia mshkaji wangu mmoja ambae ni polisi pale akaniambia hamna noma we ibuka tu, tulipofika tukaanza kushoot ndani ya gari la polisi wakiwa tayari wamenipiga pingu ila watu wengine wa pembeni wakaanza

kushangaa Madee kakamatwa, cameraman akawa anaendelea kushoot ila hafla tukaanza kuona wakubwa wa polisi wakaanza kutonyana baadae kidogo wakaja, wakaanza kumind na kuuliza nani kawaambia mrekodi video? Camera mliyoitumia ikwapi mliokua

mnashoot nayo? fungueni tuangalie….. wakapekua pekua lakini hawakukuta kitu manake Camera man alikua mjanja akawapa camera nyingine na tayari tulikua tumemaliza ile scene"
Dee ameamplfy zaidi kwamba "japo tulikua tumeshamaliza kushoot washkaji zangu wale

ambao ndio polisi walionipa hiyo chance waliniomba kwamba itakua msala wakaomba tusiitumie hizo picha itakua noma tutawafukuzisha kazi, basi ikabidi kweli tuachane nayo ila tukaingia gharama tukachukua gari kama la polisi na kulibandika stika"
Movie mpya ya Madee

inatoka kwenye mwezi june au july 2012, na mpaka sasa haijamalizika lakini imetumia zaidi ya shilingi milioni 8 kwenye matayarisho ambapo waliogiza humo ndani ni pamoja na Dogo janja, Tunda Man na Dully Sykes, wengine sio mastaa ni washkaji wa Madee wa mtaani

ambao walihusika kwenye maisha ya ukweli ya Madee.
Madee ametoa single mpya inaitwa ‘HISTORIA' ambayo ndio inaambatana na kitabu na hiyo movie, vyote vinazungumzia maisha yake kabla ya kuwa Madee, yani kabla hajaingia kwenye umaarufu.Umeipenda Hii Story? Share na Washkaji:

KILICHOTOKEA KWA MADEE WAKATI AKIIGIZA NDANI YA GARI LA POLISI. « Millard Ayo

 
Kituo cha polisi ni ofisi, kuna protocol zake. Hauwezi kuwasiliana kishksji ktk swala siriasi kama hilo.
 
Back
Top Bottom