Kilichotokea Igunga: Tafsiri Yangu (Makala, Raia Mwema)

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Na Maggid Mjengwa
UKWELI ni majeruhi wa kwanza pande mbili zinapoingia kwenye mapambano. Ndivyo inavyokuwa. Maana, kwenye vita yeyote iwayo, risasi ya kwanza huelekezwa kwenye ukweli. Ndio, ukweli hufichwa na uongo hutamalaki hata kama utapewa jina jingine, kuwa ni propaganda.

Ni nini basi tafsiri ya kilichotokea Igunga?
Igunga kumejitokeza ishara za yanayotarajiwa kutokea huko twendako. Na tujipe kazi ya kuzisoma ishara hizo za nyakati. Kuna niliyoyaona na yanifanyayo niendelee kutafakari. Kuna mapya pia yanayojitokeza hata baada ya matokeo kutangazwa. Yanatutaka tufikiri kwa bidii zaidi.

Kubwa nililoliona ni pigo tulilolipata sote kama taifa. Kwamba Igunga imetudhihirishia, kuwa tuna safari ndefu katika ujenzi wa demokrasia yetu na kuifanya nchi yetu kuwa ya kisasa zaidi. Tumeingia kwenye siasa za vyama kukamiana na kuwa na ushabiki kama wa vilabu vya mpira. Kama ni ujenzi wa nyumba ya ghorofa hamsini, basi, tuko kwenye kukusanya kokoto. Hatujaanza hata kuchimba msingi.

Tumeona kule Igunga, kuwa vyama vikubwa vilivyoshiriki uchaguzi huo vimetumia fedha na rasilimali nyingi kugombania kiti kimoja. Hi isi ishara njema.
Na katika muktadha huo huo, nadiriki kuandika, kuwa kama CCM itaondolewa madarakani 2015 na CHADEMA inayoonekana sasa, basi , CHADEMA haitakuwa chama bora tawala ikiwa na CCM dhaifu kama ilivyo sasa kwenye kambi ya upinzani ifikapo 2015.

Labda si wengi walioona, lakini, kuna ukweli kuwa, kuna kubwa limetokea Igunga. Kuwa CUF imekwenda Igunga, imejichimbia kaburi na imejizika yenyewe. Walichovuna CUF Igunga si kingine bali ni janga la kisiasa. CUF wamefanya vibaya sana pamoja na kuanza na kinachoitwa mtaji wa kura 11,000. Na Naibu Katibu Mkuu wa CUF bara, Julius Mtatiro ameonyesha ujasiri wa kisiasa kukiri hadharani kilichowatokea.

Tumesikia, kuwa CUF wameitwa 'CCM B'. Si Wana Igunga tu, hata Watanzania wengi wanaonekana kukubaliana na CHADEMA na kuwaona CUF kwa na sura hiyo. Kama wanataka wafufuke, CUF wana lazima ya kujipanga upya.

Na kibaya hapo ni ukweli, kuwa CUF wamepoteza nafasi ya kuwa chama cha pili kikubwa cha upinzani bara baada ya CHADEMA. Na NCCR Mageuzi wajitafakari namna watakavyorudi tena kwenye ulingo wa siasa. Wakizicheza vibaya karata zao, basi, CHADEMA, wamekamata mhuri wa ' CCM C' na hawatakuwa na mkono mzito kwenye kuugonga kwenye paji la uso wa NCCR – Mageuzi.

Na si jambo jema kwa nchi kama ni CHADEMA tu itakayobaki kuwa chama kikubwa cha upinzani na kinachoaminika kuwa kina sura hiyo ya upinzani , kwamba CHADEMA si kibaraka wa chama tawala. Maana, siku ile CCM na CHADEMA watakapoamua kuunda Serikali ya Mseto , basi, nchi yetu itabaki bila ya chama cha upinzani. Hiyo ni hatari kwa demokrasia tuliyodhamiria kuijenga.

Igunga imetudhihirishia kuwa bado tuna viongozi wa hovyo hovyo, wanaoamini kuwa WaTanzania wote ni watu wa hovyo hovyo, bila kutambua kuwa ni wao, kama viongozi, ndio watu wa hovyo hovyo wanaotufanya WaTanzania wote tuonekane kuwa ni watu wa hovyo hovyo.

Na kuna taasisi tatu katika nchi hii ambazo zinaweza kabisa zikatufikisha kwenye kuwaona watu wetu wakichinjana na tukabaki kuililia nchi yetu huku tukijalumu kuwa tuliona ishara lakini hatukuwa wakweli kwa nchi yetu. Kwamba tuliamua kukaa kimya tukiendekeza njaa zetu na kuisaliti nchi yetu tuliyozaliwa.

Ni taasisi gani hizi zinazoweza kutufikisha kwenye umwagaji damu?
Tume ya Uchaguzi, Jeshi la Polisi na Vyombo vya habari. Siku zote nimesisitiza, kuwa historia ni mwalimu mzuri. Katika nchi zetu hizi, taasisi hizo tatu ndio zimekuwa chanzo cha maafa ya nchi nyingi za Kiafrika. Wahenga walisema; kujifunza kuanzie kwa jirani yako.

Ndio, tumeona hata kwa jirani zetu wa Kenya. Kwamba Tume ya Uchaguzi, Jeshi la Polisi na Vyombo vya habari vilichangia vurugu, mauaji na hasara kubwa kuafuatia matokeo ya uchaguzi mkuu wa Kenya uliopita.

Leo WaKenya wamepata Katiba mpya na kuanza kusonga mbele, lakini, wakiwa na makovu na hata machungu yaliyobaki kwa yaliyotokea huko nyuma. WaKenya walikuwa na uwezo wa kuzuia kilichotokea. Lakini, nao pia, walikuwa na viongozi wa hovyo hovyo waliodhani WaKenya wote ni watu wa hovyo hovyo. Na matokeo ya dhania hiyo dunia nzima imeyaona.

Hivyo basi, kule Igunga WaTanzania tumeshaziona ishara, kuwa kama nchi yetu itakwenda kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015 bila kuufanyia mabadiliko ya kimsingi mfumo wetu wa uchaguzi ikiwamo uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi, bila kuwa na Katiba itakayolifanya Jeshi la Polisi kutenda haki kwa raia na vyama vyote vya siasa kwa wakati wote na bila kuwa na vyombo huru vya habari , basi , sihitaji kuwa na maarifa ya elimu ya nyota kuweza kutabiri machafuko ya kisiasa yakayopelekea madhara makubwa ya kijamii na kiuchumi kwa nchi yetu.

Maana, WaTanzania kwa asili ni watu watulivu na wenye kupenda amani. WaTanzania hawa kwa kawaida watakwenda kwenye mikutano ya siasa na watawasikiliza wanasiasa. Na siku ya kupiga kura watakwenda kupiga kura kwa amani.

Ni vyama vya siasa na baadhi ya wanasiasa ndio wenye kutumia hila , ghilba na hata , kwa kutumia fedha, hutokea wakagharamia vurugu ili baadae kwa kuvilipa vyombo vya habari na hata baadhi ya wana habari, watajenga taswira ya uongo juu ya uwepo wa vurugu na hata kusukuma lawama kwa wapinzani wao wa kisiasa.

Kisha , jeshi la polisi nalo, kwa ama kutojiamini kwa baadhi ya viongozi wa jeshi hilo au kusukumwa kisiasa, nao wataingia kwenye mapambano na wafuasi wa vyama na hata viongozi wa vyama. Na hapo ndipo chuki inapozaa chuki na silaha inapozaa silaha. Ni balaa.

Na uwepo wa Tume ya Uchaguzi isiyo huru unapelekea Tume kuwa na viongozi wasiojiamini, hivyo basi, kuendesha shughuli za uchaguzi katika hali ya mashaka na hata kuegemea upande mmoja. Na katika nchi zetu hizi, siku zote, tabu inakuja kwenye shughuli ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo. Joseph Stalin wa Urusi ya zamani alipata kutamka; Katika uchaguzi wowote ule, mpiga kura si anayeamua matokeo, bali mhesabu kura!

Tunachojifunza kwenye kauli hiyo ya Jeseph Stalini ni ukweli, kuwa kikubwa katika mchakato wa uchaguzi ni uwepo wa imani kwa wanaondesha mchakato huo. Kama vyama vya siasa na hata wapiga kura watakosa imani na aliyeteuliwa kuendesha mchakato na hata kuhesabu kura zao, basi, matokeo ya chaguzi yanaweza kuwa chanzo cha vurugu za kisiasa.

Na si tuliona? Kuwa nchi nzima ilihamia Igunga. Kuna wengi tuliopumua kwamba ya Igunga yamepita bila madhara makubwa. Turudi sasa kwenye mengine ya kila siku. Maana, hata msomaji wangu, mchuuzi wa samaki pale Soko Kuu Igunga naye amepumua. Ni baada ya kukoswakoswa panga alipokuwa akipita nje ya Hotel ya Peak pale Igunga siku ile vurugu zilipoanza.

Na hapo ndipo tulipofikia WaTanzania, kwamba chaguzi zetu zimekuwa chanzo cha mashaka badala ya kutupa matumaini ya kwenda mbele. Na sasa ni kuanzia ngazi ya udiwani. Haya ndio mambo ya hovyo hovyo yanayotufanya tuonekane kuwa ni watu wa hovyo hovyo. Tuna uwezo na kila sababu ya kuandaa taratibu za kuendesha mambo yetu kistaarabu. Nahitimisha.

MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo

umesharudi toka sweeden? wewe ni mwandishi mojawapo unayeegemea kwa magamba kumbe unatambua kuwa ukiwa mwandishi unatakiwa usiwe na upendeleo.Anza kwanza wewe halaf uhamasishe na wengne
 
... kama kuna mtu yeyote katika taasisi husika aliyesoma juu ya kijipnde tu hiki kuhusu mabaya yaliojiri Igunga basi naamini kamwe hawatolala usingizi kwani bila HAKI na uwanja tambalale mapema yote hii basi tuhesabu tu viwango vya machafuko 2015.

Hakuna hata mmoja atakayetangaza chochote kitu hata akikaza misuli ya usoni hata akasikilizwa mwaka huo. KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHGUZI hala hala kabla ya 2015 ili tukaokoe sura mbaya inayonukia bila kulazimika kuwaita akina Shimbo kuja kuwatisha wapiga kura wala nini.

Nasema, kama mtu alisoma kweli vema yaliojiri Igunga; jukwaani, gizani pamoja na usimikwaji wa jeshi binafsi ya CCM - 'CCM GREENGUARD MUNGIKI', tusidanganyike kununua muda na mabadilo yaa katiba mwisho tukakosa yote.
 
Nafikiri somo kubwa kutoka Igunga ni CCM kujaribu katika siku za usoni kubadilisha zile hisia za wananchi wengi kabisa kuwa chenyewe kinahusika pamoja na vyombo vya dola katika uchakachuaji wa kura katika uchaguzi uwe wa diwani, mbunge au hata kitaifa. Ushindi wowote ule wa CCM hauna maana ikiwa wananchi wengi - kuanzia watoto wadogo kwenye shule ya chekechea mpaka wazee wa miaka zaidi ya themanini - wana hisia kama hizi. Wananchi wa Kenya walikuwa na hisia kama hizi juu ya chama kikongwe nchini humo cha KANU mpaka mwaka 2002 kilipotolewa madarakani na kusambaratika.

Ikumbukwe kuwa kuondoka madarakani kwa KANU kulitokea wakati wananchi walipochoka kabisa na hila zake za uchakachuaji na pia wakubwa [wawekezaji na wafadhili wa magharibi] kuona kuwa interests zao hazitaweza kuendelea kulindwa na serikali ya KANU. Nafikiri hapa Tanzania wale wanaoki-support CCM kwa hali na MALI wanafikia level ya kutaka kukitosa. Uamuzi wao utakuwa influenced sana na uchaguzi ndani ya CCM wa mwaka 2012. Uchaguzi huo wa CCM wa 2012 ndio utakao determine kama CCM itoswe au la - kama vile ule uchaguzi wa KANU pale viwanja vya Kasarani Nairobi mwaka 2001 wa kumchagua Uhuru Kenyatta kuwa mrithi wa Rais Moi . Baada ya uchaguzi huo wa KANU kina Raila Odinga walitoka kwenye chama hicho na kujiunga na wapinzani na hasa pale Raila aliposema Kibaki TOSHA kama mgombea pekee wa Urais wa upinzani.

Natabiri kuwa baada ya uchaguzi wa CCM 2012 watatokea kina Raila wa Tanzania watakaokwenda Chadema na kusema SLAA TOSHA kama mgombea pekee wa upinzani wa urais 2015. Matokeo ya uchaguzi wa Igunga utakuwa ni mwanzo wa vyama vya upinzani kuungana chini ya CHADEMA kuiondoa CCM madarakani. Hili litaepukika tu ikiwa kama uchaguzi ndani ya CCM mwaka 2012 utakuwa huru na wa haki ili kuleta viongozi wapya kabisa ambao sii mafisadi. Pia ikiwa uchaguzi ndani ya CCM wa mwaka 2012 hautakuwa na uchakachuaji basi hii itapunguza zile hisia za wananchi wengi kuwa ni CCM mpya na inaweza kuaminiwa kuendelea kutawala nchi. Hizi shughuli za kujivua magamba za sasa ni usanii tu na hazitaisaidia CCM.
 
Kaka Maggid umeongea kweli tupu lakini umekosea sana kutokuongelea suala la udini. Udini ulijitokeza wazi wazi Igunga. Sijui kwa nini haukutaka kuandika japo mstari mmoja kuhusu hilo.
 
i
Na Maggid Mjengwa
UKWELI ni majeruhi wa kwanza pande mbili zinapoingia kwenye mapambano. Ndivyo inavyokuwa. Maana, kwenye vita yeyote iwayo, risasi ya kwanza huelekezwa kwenye ukweli. Ndio, ukweli hufichwa na uongo hutamalaki hata kama utapewa jina jingine, kuwa ni propaganda.

Ni nini basi tafsiri ya kilichotokea Igunga?
Igunga kumejitokeza ishara za yanayotarajiwa kutokea huko twendako. Na tujipe kazi ya kuzisoma ishara hizo za nyakati. Kuna niliyoyaona na yanifanyayo niendelee kutafakari. Kuna mapya pia yanayojitokeza hata baada ya matokeo kutangazwa. Yanatutaka tufikiri kwa bidii zaidi.

Kubwa nililoliona ni pigo tulilolipata sote kama taifa. Kwamba Igunga imetudhihirishia, kuwa tuna safari ndefu katika ujenzi wa demokrasia yetu na kuifanya nchi yetu kuwa ya kisasa zaidi. Tumeingia kwenye siasa za vyama kukamiana na kuwa na ushabiki kama wa vilabu vya mpira. Kama ni ujenzi wa nyumba ya ghorofa hamsini, basi, tuko kwenye kukusanya kokoto. Hatujaanza hata kuchimba msingi.

Tumeona kule Igunga, kuwa vyama vikubwa vilivyoshiriki uchaguzi huo vimetumia fedha na rasilimali nyingi kugombania kiti kimoja. Hi isi ishara njema.
Na katika muktadha huo huo, nadiriki kuandika, kuwa kama CCM itaondolewa madarakani 2015 na CHADEMA inayoonekana sasa, basi , CHADEMA haitakuwa chama bora tawala ikiwa na CCM dhaifu kama ilivyo sasa kwenye kambi ya upinzani ifikapo 2015.

Labda si wengi walioona, lakini, kuna ukweli kuwa, kuna kubwa limetokea Igunga. Kuwa CUF imekwenda Igunga, imejichimbia kaburi na imejizika yenyewe. Walichovuna CUF Igunga si kingine bali ni janga la kisiasa. CUF wamefanya vibaya sana pamoja na kuanza na kinachoitwa mtaji wa kura 11,000. Na Naibu Katibu Mkuu wa CUF bara, Julius Mtatiro ameonyesha ujasiri wa kisiasa kukiri hadharani kilichowatokea.

Tumesikia, kuwa CUF wameitwa 'CCM B'. Si Wana Igunga tu, hata Watanzania wengi wanaonekana kukubaliana na CHADEMA na kuwaona CUF kwa na sura hiyo. Kama wanataka wafufuke, CUF wana lazima ya kujipanga upya.

Na kibaya hapo ni ukweli, kuwa CUF wamepoteza nafasi ya kuwa chama cha pili kikubwa cha upinzani bara baada ya CHADEMA. Na NCCR Mageuzi wajitafakari namna watakavyorudi tena kwenye ulingo wa siasa. Wakizicheza vibaya karata zao, basi, CHADEMA, wamekamata mhuri wa ' CCM C' na hawatakuwa na mkono mzito kwenye kuugonga kwenye paji la uso wa NCCR – Mageuzi.

Na si jambo jema kwa nchi kama ni CHADEMA tu itakayobaki kuwa chama kikubwa cha upinzani na kinachoaminika kuwa kina sura hiyo ya upinzani , kwamba CHADEMA si kibaraka wa chama tawala. Maana, siku ile CCM na CHADEMA watakapoamua kuunda Serikali ya Mseto , basi, nchi yetu itabaki bila ya chama cha upinzani. Hiyo ni hatari kwa demokrasia tuliyodhamiria kuijenga.

Igunga imetudhihirishia kuwa bado tuna viongozi wa hovyo hovyo, wanaoamini kuwa WaTanzania wote ni watu wa hovyo hovyo, bila kutambua kuwa ni wao, kama viongozi, ndio watu wa hovyo hovyo wanaotufanya WaTanzania wote tuonekane kuwa ni watu wa hovyo hovyo.

Na kuna taasisi tatu katika nchi hii ambazo zinaweza kabisa zikatufikisha kwenye kuwaona watu wetu wakichinjana na tukabaki kuililia nchi yetu huku tukijalumu kuwa tuliona ishara lakini hatukuwa wakweli kwa nchi yetu. Kwamba tuliamua kukaa kimya tukiendekeza njaa zetu na kuisaliti nchi yetu tuliyozaliwa.

Ni taasisi gani hizi zinazoweza kutufikisha kwenye umwagaji damu?
Tume ya Uchaguzi, Jeshi la Polisi na Vyombo vya habari. Siku zote nimesisitiza, kuwa historia ni mwalimu mzuri. Katika nchi zetu hizi, taasisi hizo tatu ndio zimekuwa chanzo cha maafa ya nchi nyingi za Kiafrika. Wahenga walisema; kujifunza kuanzie kwa jirani yako.

Ndio, tumeona hata kwa jirani zetu wa Kenya. Kwamba Tume ya Uchaguzi, Jeshi la Polisi na Vyombo vya habari vilichangia vurugu, mauaji na hasara kubwa kuafuatia matokeo ya uchaguzi mkuu wa Kenya uliopita.

Leo WaKenya wamepata Katiba mpya na kuanza kusonga mbele, lakini, wakiwa na makovu na hata machungu yaliyobaki kwa yaliyotokea huko nyuma. WaKenya walikuwa na uwezo wa kuzuia kilichotokea. Lakini, nao pia, walikuwa na viongozi wa hovyo hovyo waliodhani WaKenya wote ni watu wa hovyo hovyo. Na matokeo ya dhania hiyo dunia nzima imeyaona.

Hivyo basi, kule Igunga WaTanzania tumeshaziona ishara, kuwa kama nchi yetu itakwenda kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015 bila kuufanyia mabadiliko ya kimsingi mfumo wetu wa uchaguzi ikiwamo uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi, bila kuwa na Katiba itakayolifanya Jeshi la Polisi kutenda haki kwa raia na vyama vyote vya siasa kwa wakati wote na bila kuwa na vyombo huru vya habari , basi , sihitaji kuwa na maarifa ya elimu ya nyota kuweza kutabiri machafuko ya kisiasa yakayopelekea madhara makubwa ya kijamii na kiuchumi kwa nchi yetu.

Maana, WaTanzania kwa asili ni watu watulivu na wenye kupenda amani. WaTanzania hawa kwa kawaida watakwenda kwenye mikutano ya siasa na watawasikiliza wanasiasa. Na siku ya kupiga kura watakwenda kupiga kura kwa amani.

Ni vyama vya siasa na baadhi ya wanasiasa ndio wenye kutumia hila , ghilba na hata , kwa kutumia fedha, hutokea wakagharamia vurugu ili baadae kwa kuvilipa vyombo vya habari na hata baadhi ya wana habari, watajenga taswira ya uongo juu ya uwepo wa vurugu na hata kusukuma lawama kwa wapinzani wao wa kisiasa.

Kisha , jeshi la polisi nalo, kwa ama kutojiamini kwa baadhi ya viongozi wa jeshi hilo au kusukumwa kisiasa, nao wataingia kwenye mapambano na wafuasi wa vyama na hata viongozi wa vyama. Na hapo ndipo chuki inapozaa chuki na silaha inapozaa silaha. Ni balaa.

Na uwepo wa Tume ya Uchaguzi isiyo huru unapelekea Tume kuwa na viongozi wasiojiamini, hivyo basi, kuendesha shughuli za uchaguzi katika hali ya mashaka na hata kuegemea upande mmoja. Na katika nchi zetu hizi, siku zote, tabu inakuja kwenye shughuli ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo. Joseph Stalin wa Urusi ya zamani alipata kutamka; Katika uchaguzi wowote ule, mpiga kura si anayeamua matokeo, bali mhesabu kura!

Tunachojifunza kwenye kauli hiyo ya Jeseph Stalini ni ukweli, kuwa kikubwa katika mchakato wa uchaguzi ni uwepo wa imani kwa wanaondesha mchakato huo. Kama vyama vya siasa na hata wapiga kura watakosa imani na aliyeteuliwa kuendesha mchakato na hata kuhesabu kura zao, basi, matokeo ya chaguzi yanaweza kuwa chanzo cha vurugu za kisiasa.

Na si tuliona? Kuwa nchi nzima ilihamia Igunga. Kuna wengi tuliopumua kwamba ya Igunga yamepita bila madhara makubwa. Turudi sasa kwenye mengine ya kila siku. Maana, hata msomaji wangu, mchuuzi wa samaki pale Soko Kuu Igunga naye amepumua. Ni baada ya kukoswakoswa panga alipokuwa akipita nje ya Hotel ya Peak pale Igunga siku ile vurugu zilipoanza.

Na hapo ndipo tulipofikia WaTanzania, kwamba chaguzi zetu zimekuwa chanzo cha mashaka badala ya kutupa matumaini ya kwenda mbele. Na sasa ni kuanzia ngazi ya udiwani. Haya ndio mambo ya hovyo hovyo yanayotufanya tuonekane kuwa ni watu wa hovyo hovyo. Tuna uwezo na kila sababu ya kuandaa taratibu za kuendesha mambo yetu kistaarabu. Nahitimisha.

MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo

Umekwepa kuongelea Bakwata kutumiwa kama dekio 2010 na 2011- Igunga,napata wasiwasi kama wewe ni "mwandishi huru au mtumwa au mateka"
Zipo tetesi kuwa Rostam Aziz ndiye aliyeratibu ishu ya kutumia udini,kwa ku-finance viongozi wa Bakwata ili kumsaidia JK mwaka jana. Igunga imejidhihirisha wazi,vipo vikundi vya Kiislam vimekuwa vikizunguka huku na huku na kufanya miadhara yenye lengo la kuwagawa watanzania,navyo inasemekana vinagharamiwa na Rostam na JK.

Vilevile katumia vodacom kutuma SMS chafu dhidi Dr Slaa.

Ukweli utabaki ukweli.Hizi mbinu si nzuri hata kidogo,ipo siku Hawa CCM watagharamia manunuzi ya silaha za jadi na za kisasa against civil society.
 
Kaka Maggid umeongea kweli tupu lakini umekosea sana kutokuongelea suala la udini. Udini ulijitokeza wazi wazi Igunga. Sijui kwa nini haukutaka kuandika japo mstari mmoja kuhusu hilo.

Mara nyingi huwa anaandika makala zake anaegemea ccm, na udini unakuzwa na magamba.
 
ccm na silaha 2.jpg

kilichotokea igunga ni hicho hapo juu.
 
Umesema vizuri sana lakini suala la udini kwa nini hukuligusia?Hii mambo mnafanya waandishi Wa habari Wa kuficha mambo ilihali kila mmoja analitambua sio kitu kizuri kabisa ktk kulijenga taifa letu hili.
Udini mimi ninaamini ni sumu mbaya sana Kama itatumika ndivyo sivyo sababu kikichotokea Igunga hasa kwa BAKWATA kutumika ndivyo sivyo wananchi hatufurahishwi kabisa na hali hiyo.Mwalimu Julius Nyerere baba Wa Taifa letu hili aliwahi kukemea jambo hili.Waandishi Wa habari mnatumika vibaya sana sababu ya njaa zenu mnasahau utaifa,mnaubadilisha uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo.
 
na udini ulukuwepo Bwana Maggid, tena siku hizi wakubwa wa ccm wametumia kama silaha yao mpya
 
Umesema vizuri sana lakini suala la udini kwa nini hukuligusia?Hii mambo mnafanya waandishi Wa habari Wa kuficha mambo ilihali kila mmoja analitambua sio kitu kizuri kabisa ktk kulijenga taifa letu hili.
Udini mimi ninaamini ni sumu mbaya sana Kama itatumika ndivyo sivyo sababu kikichotokea Igunga hasa kwa BAKWATA kutumika ndivyo sivyo wananchi hatufurahishwi kabisa na hali hiyo.Mwalimu Julius Nyerere baba Wa Taifa letu hili aliwahi kukemea jambo hili.Waandishi Wa habari mnatumika vibaya sana sababu ya njaa zenu mnasahau utaifa,mnaubadilisha uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo.

UDINI WA BAKWATA Mgejja hakuona kama ni agenda hapa, nimeshangaa sana pia........................
 
Ndugu zangu,

Nawashukuru kwa kuyasoma mawazo yangu. Nami nimenufaika sana na michango yenu ya fikra. Na kuna wanaonilaumu kuwa sikugusia suala la udini.

Nilishaliongelea hilo la udini juma la jana. Labda isingekuwa vibaya nikalirudia kwenye makala yangu mliyosoma. Sikufanya hivyo, nanyi mmefanya. Hakuna kilichoharibika, maana, nimeweka msisitizo kwenye taasisi tatu; Tume ya Uchaguzi, Polisi na Media, kwamba kwa mtazamo wangu, kama zingefanya kazi yake kwa uadilifu na kutanguliza mbele maslahi mapana ya nchi yetu, basi, vingeweza kuzuia hata kusambaa kwa sumu ya udini. Tunajua, mathalan, anayehubiri chuki ya udini anasaidiwa na media kusambaza sumu yake ya udini.

Na hapa ni makala yangu ya Mwananchi Jumapili Oktoba 2, siku ulipofanyika uchaguzi mdogo Igunga. Niliongelea juu ya dhambi ya ubaguzi inayotutafuna, ikiwamo udini pia. Soma tafadhali;
Dhambi ya ubaguzi imeanza kututafuna

Na Maggid Mjengwa,

Ndugu zangu,
Kule Igunga leo Jumapili wanafanya uchaguzi mdogo kujaza kiti cha ubunge kilichoachwa wazi na Rostam Aziz. Tunawatakia uchaguzi mwema na wa amani.

Juma la jana niliandika, kuwa yanayotokea Igunga ni kielelezo cha uwendawazimu wetu. Maana, katika mengi, tumeona hata mbegu za chuki zikipandwa kule Igunga. Kuna wanaopandikiza chuki miongoni mwa Watanzania. Na kule Igunga tumeona pia karata chafu ya udini ikitumiwa.

Tafsiri yangu; dhambi ya ubaguzi imeanza kututafuna. Maana, udini ni karata ya hatari kwa mwanasiasa kuicheza katika nchi kama Tanzania. Anayecheza karata ya udini katika siasa ni mtu asiyeitakia heri nchi yetu. Na achezaye karata ya udini kimsingi ni mbaguzi. Anataka Watanzania waanze kubaguana kwa misingi ya kidini. Na chanzo cha yote haya ni ubaguzi wa kisiasa ambao tumekuwa nao kwa takribani miaka 50 sasa.

Ubaguzi wa kisiasa ni pale wachache wanapoona wengine hawastahili kushiriki siasa na uongozi wa nchi. Kufanikisha azma yao hiyo watatumia mbinu zote ikiwamo hila na ghilba kwa umma.

Ndugu zangu, sisi ni Watanzania na hii ni nchi yetu. Watanzania hatuna utamaduni wa kubaguana kwa misingi ya kikabila na kidini. Tuwapuuze wote wanaofanya jitihada za kutugawa kwa misingi ya udini, ukabila, rangi na hata siasa. Watanzania ni Watanzania. Mshikamano wetu na mashirikiano ya kindugu ndio yanayotufanya tupigiwe mfano Afrika na duniani.

Tunachoshuhudia sasa mwelekeo mbaya kwa taifa letu. Kwani, kwa asili na
utamaduni, Watanzania tumeishi kwa amani na kuchanganyikana bila kujali tofauti zetu za kidini na kikabila.

Kama taifa, ni jambo jema na la bahati kubwa kuwa nchi yetu haina dini. Kila Mtanzania, kwa mujibu wa Katiba, ana uhuru wa kuabudu dini atakayo. Ana uhuru pia wa hata kutoabudu katika dini ye yote ile. Na hakika, Watanzania hatuna udini. Ni bahati mbaya tu kuna wachache, kwa maslahi yao, wanapandikiza
dhana hii ya udini kwa Watanzania.

Nilipata kupigiwa simu na msomaji wangu akiwa kijiji cha Mwambata, Masasi. Alijitambulisha kwa jina la Edward Hassan. Nilimdadisi juu ya mchanganyiko wa Edward na Hassan katika jina lake. Akaniambia; kuwa huko maeneo ya kusini ni kawaida sana. Utamkuta mtu anaitwa Dominick Rashid, John Ramadhan
na mengineyo. Ni majina yanayotokana na dini za kimapokeo toka kwa Waarabu na Wazungu. Lakini, Watanzania wana majina ya asili ya koo zao. Majina yasiyotokana na dini za kimapokeo. Mengi ni majina yenye maana fulani.

Ndio, Watanzania tumechanganyika kiasi hata kwenye koo zetu tunatofautiana katika imani za kimapokeo; Ukristo na Uislamu. Ni kawaida kabisa katika ukoo mmoja kuwakuta Waislamu na Wakristo.
Kinachowaunganisha wanaukoo hawa ni mila zao za jadi ikiwamo matambiko yao.

Na leo hii, katika nchi yetu, kuna familia zenye wanafamilia wa imani tofauti za kimapokeo; Uislamu na Ukristo. Ni kawaida kumkuta mama Mkristo na baba Muislamu au kinyume chake. Ni kawaida kuwakuta watoto wa familia
moja wenye kufuata imani tofauti.

Swali linakuja; hivi wenye kuhubiri chuki za kidini wanafahamu kuwa watachochea
hata vita vya kikoo? Maana, koo zetu nazo zina tofauti za kidini, hususan dini hizi tulizozipokea toka kwa Wazungu na Waarabu.

Ndugu zangu ,
Kuna kila dalili, kuwa sasa baadhi ya viongozi wa kidini na wanasiasa, kwa
maslahi yao, wanafanya juhudi za kutugawa Watanzania kwa misingi ya kidini. Tusikubali kugawanywa na tukafikia kuchinjana. Watanzania, Wazalendo wa nchi hii, tuna kila sababu ya kuihami nchi yetu dhidi ya chuki hizi za kidini na kisiasa.

Naam. Uzoefu unatufundisha, kuwa kuwasha moto ni jambo jepesi sana, lakini, kuuzima moto, yaweza kuwa ni kazi ngumu sana. Moto ulioanza kwenye nyumba moja ya nyasi kijijini, waweza kusambaa haraka na hata kuteketeza nyumba nyingine, mali na kuhatarisha maisha.

Nimekumbushia mara kadhaa, kuwa historia ni mwalimu mzuri. Mwezi Aprili 6, mwaka 1999 katika iliyokuwa Hoteli ya Kilimanjaro, Bi Joy Mukanyange , aliyekuwa Balozi wa Rwanda hapa Tanzania, alituambia Watanzania juu ya kile alichokiona lakini sisi Watanzania hatukukiona. Ilikuwa ni katika mjadala rasmi wa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya watu wa Rwanda ya mwaka 1994.

Bi Mukanyange alisema: ” Naogopa., kwani nimeanza kuona dalili zinazojengeka za mgawanyiko wa kidini nchini Tanzania na eneo lote la Maziwa Makuu, hali ambayo inaweza kusababisha mauaji ya halaiki kama yale yaliyotokea nchini mwetu mwaka 1994,” alisema Balozi huyo wa Rwanda kabla ya kuendelea kutoa ufafanuzi wa historia ya Rwanda na matukio yaliyosababisha maujai yale ya Wanyarwanda ya wao kwa wao.

Ndugu zangu, na tufanye yote tuwezayo kuzuia utabiri wa Bi Mukanyange usitimie. Maana, Wahenga walisema; ”Kamba hukatikia pabovu”. Kamwe huwezi kuwavuruga Watanzania na kuwafanya wachinjane kwa sababu za kudai kuna upendeleo wa ukabila au wa kisiasa. Nchi hii ina makabila zaidi ya
125 na utitiri wa vyama vya siasa.

Mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa wachinjane ni kwenye masuala ya imani. Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye kamba inayotuunganisha Watanzania. Nahitimisha.
MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
 
Wadau, nimevutiwa na kuguswa sana na Mraba wa Maggid, kwenye Raia Mwema la 5 Oktoba 2011 kuhusu kilichotokea Igunga; Tafsiri yake. Nanukuu baadhi ya busara zake;

"Igunga imetudhihirishia kuwa bado tuna viongozi wa hovyo hovyo,wanaoamini kuwa Watanzania wote ni watu wa hovyo hovyo, bila kutambua kuwa ni wao, kama viongozi, ndio watu wa hovyo hovyo wanaotufanya Watanzania wote tuonekane kuwa ni watu wa hovyo hovyo."

to be continued...
 
continued....
Busara za Maggid kuhusu kilichotokea Igunga;
"kuna taasisi tatu ktk nchi hii ambazo zinaweza kabisa kutufikisha kwenye kuwaona watu wetu wakichinjana na tukabaki kuililia nchi yetu; huku tukijilaumu kuwa tuliona ishara lakini hatukuwa wakweli kwa nchi yetu. kwamba tuliamua kukaa kimwa tukiendekeza njaa zetu na kuisaliti nchi yetu tuliozaliwa.Tume ya Uchaguzi, Jeshi la Polisi na vyombo vya habari...Ktk nchi zetu hizi, taasisi zetu hizi tatu ndio zimekuwa chanzo. ."

...to be continued...
 
Back
Top Bottom