Kilichonishtua Juu Ya Dr Slaa Pale Mwembetogwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilichonishtua Juu Ya Dr Slaa Pale Mwembetogwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Sumaku, Oct 3, 2010.

 1. S

  Sumaku Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Maggid Mjengwa,

  Iringa ni ngome ya CCM. Jana jioni Dr Slaa alitua Iringa na kuvuta umati mkubwa wa watu. Nilikuwapo pale Viwanja vya Mwembetogwa. Nini aliongea na kina nini ndani yake, nitachambua hapa kwa ufupi;
  Nilifika viwanja vya Mwembetogwa saa kumi na robo jioni. Tayari Dr Slaa alishatua. Watu walikuwa wengi sana. Pamoja na uzoefu wangu wote wa kujipenyeza kwenye kundi la watu nikiwa na kamera, bado kwangu safari hii ilishindikana. Niliishia kutafuta sehemu ya juu kidogo nyuma ili walau nipate picha ya Dr Slaa akihutubia. (Picha ya kwanza hapo juu blogiini imepigwa na Francis Godwin.)

  Nimekaa Iringa tangu mwaka 2004 na nimeudhuria mikutano yote ya kampeni za Urais kuanzia Jakaya Kikwete, Mbowe, Lipumba hadi Mrema, lakini niweke wazi. Mkutano wa jana pale viwanja vya Mwembetogwa umevunja rekodi zote katika kujaza watu kwa mujibu wa kumbukumbu zangu za tangu 2004. Katika chaguzi ziliopita kuna watumishi wa Serikali waliokuwa wakienda kwenye mikutano ya vyama vya upinzani kwa kunyata. Walikuwa na hofu ya kuonekana wanaunga mkono upinzani na kuonekana kwao kwenye mikutano ya akina Mbowe, Zitto na Lipumba ingetafsiriwa kuwa hawaipigii kura CCM. Jana kulikuwa na watu wa aina zote, hata makada wa CCM walifika pia.

  Kwenye hotuba yake ya takribani dakika 43 Dr Slaa alijikita katika maeneo makubwa matatu;
  Uchaguzi wenyewe; alianza kwa shambulizi dhidi ya Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ( JWTZ) na Polisi kwa tamko lao juu ya uchaguzi. Dr Slaa naye akasema ametoa tamko lake akiwa Njombe kushutumu hatua hiyo ya jeshi na polisi akisema kuwa ni kuwatisha wapiga kura.

  Dr Slaa akagusia pia masuala ya elimu akisisitiza azma ya Chadema kutoka elimu bure kuanzia chekechea. Katika eneo hili Dr Slaa alifanikiwa pia ( kisiasa) kukwepa kutoa ufafanuzi wa ni kwa namna gani. Kuna mahali alifanikiwa sana alipojaribu kulinganisha na wakati wake alipokuwa shuleni na hali ilivyo sasa.

  " Ndugu zangu, leo mtoto anakwenda shule anaambiwa abebe na ndoo!" Alisema Dr Slaa. Niliwasikia wasikilizaji wakimalizia na " mafagio, makwanja…"

  Hapo Dr Slaa aliweza kupenya kwenye kero na matatizo ya kila siku ya wapiga kura. Na ni mambo haya ambayo wapiga kura wanayaelewa zaidi kuliko kashfa za EPA, IPTL, Deep Green na nyinginezo ambazo akina Dr Slaa na wanasiasa wengine wameshindwa kuziweka katika lugha nyepesi ikamfanya mpiga kura wa Kihesa awaelewe. Mpiga kura ambaye bado anaumiza kichwa kila siku kutafuta senti za kununulia mafuta ya taa na michango ya madawati ya watoto wake.

  Dr Slaa aligusia kwa kirefu pia suala la uchumi na namna Serikali yake itakavyohakikisha Tanzania inanufaika na rasilimali zake. Kuna wakati kwenye hotuba yake alijichanganya kido aliposema wachagueni wabunge wa Chadema ili kwenye kikao cha bajeti cha Julai mwakani wapige mapanga bajeti tupate fedha za elimu na mengineyo. Dr Slaa alisahau kuwa yeye ndiye atakayeunda Serikali na lazima aonyeshe kwa wapiga kura kuwa ndivyo itakavyokuwa.

  Staili ya Dr Slaa
  Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kumsikiliza Dr Slaa akihutubia ' live'.

  Nguvu zake:
  - Dr Slaa ana mvuto. Anavuta wasikilizaji. Anaongea kwa staili inayomfanya mtu aamini kuwa dakika ijayo ana kitu cha muhimu zaidi atakitamka. Watu wanavutika, wanabaki kumsikiliza.
  - Anaongea kwa staili ya kimahubiri. Ana uzoefu katika hilo. Kuna wakati anayaacha matokeo ya anachoongea kwa Mungu na watu.
  - Ametokea ndani ya CCM. Anafahamu kuwa walio wengi anaowahutubia kwa kawaida ni wapiga kura wa CCM. Dr Slaa anafahamu, wanachokitafuta wanaomsikiliza walikuwa nacho, wamekipoteza, kwa uzembe. Hata Baba wa Taifa angefufuka pale Mwembe togwa angetamka; " Eh, hivi Dr Slaa naye amerudi CCM!". Ndio, jana pale Mwembetogwa Dr Slaa alikuwa anazungumzia CCM ya Mwalimu.
  - Dr Slaa mara kwa mara anatumia nafsi ya tatu; " Wanasema Dr Slaa…." Anayesema hayo ni Dr Slaa.
  - Hasimami mahala pamoja jukwaani. Anatembea tembea huku akigeukia hadhira yake.
  - Anachangamka jukwaani. Aliweza hata kurukaruka kidogo. Inawavutia wanaomsikiliza.

  Udhaifu wake:
  - Anaanza hotuba yake kwa kuonyesha ana haraka kidogo. Wanaomsikiza nao wanapata ' stress' ya namna fulani. Watu wanaanza kuangalia saa zao pia. Details hizo zinaweza kumtoa nje msikilizaji.
  - Wakati mwingine anaonyesha jazba kidogo. Maneno kama ; " Kama Kikwete mwanamme…" Anatakiwa ayaepuke. Yanaweza kutafsiriwa vibaya na katika nchi nyingine wanaharakati wa jinsia wanaweza kumjia juu.
  - Anatoa maagizo, anatoa siku saba.. hata kabla hajaingia Ikulu. Labda angetamka zaidi " CHADEMA tunataka'. Kuna wapigakura wanaohofia kumwingiza madarakani mwenye silika za udikteta.
  - Dr Slaa hakuzungumzia KATIBA na umuhimu wa kuanzishwa kwa mchakato wa kuandika KATIBA mpya kwa nchi yetu. Wapiga kura wengi leo wameanza kuelewa kuwa KATIBA yetu ni chanzo cha matatizo yetu mengi. Haitoshi tu kubadilisha marais na vyama. Huko ni sawa na kuyatoa maji kwenye ndoo ya bati na kuyaingiza kwenye ndoo ya plastiki. Na kubadili ni kuyatoa maji kutoka kwenye ndoo ya plastiki kuarudisha kwenye ndoo ya bati! Maji ni yale yale. Ndio maana , zawadi kubwa kwa sasa kwa Watanzania katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru ni kuanzisha mchakato wa kuandika KATIBA mpya shirikishi itakayoirudisha nchi yetu kwenye reli. Na hakika imeanza kuwa KIU kubwa ya Watanzania.
  - Huenda Dr Slaa hapati muda mwingi wa kutafuta taarifa zenye kuwagusa watu walio mbele yake kumsikiliza. Kuwa watu wengi walijazana pale Mwembetogwa jana kwa mtazamo wangu kunachangiwa pia na namna CCM ilivyoboronga katika kumpata mgombea ubunge jimbo la Iringa Mjini. Miongoni mwa waliomsikiliza Dr Slaa jana pale Mwembetogwa ni wanachama na wapenzi wengi wa CCM. Na ajabu kubwa kabisa; Dr Slaa tangu mwanzo hadi mwisho wa hotuba yake hakutamka jina la " Mama Monica Mbega". Mgombea Ubunge wa CCM, Iringa Mjini. Hata mgombea wa CHADEMA Mchungaji Msigwa alipopewa dakika tatu na Slaa aongee, naye hakutamka jina la " Monica Mbega" na kwanini wana Iringa Mjini wasimchague Monica Mbega.

  Mengineyo;
  Tatizo la CHADEMA na vyama vingi vingine vya upinzani linabaki pale pale; oganaizesheni. Wengi katika umati ule uliokusanyika pale Mwembetogwa hawajui zilipo ofisi za CHADEMA mjini. Hawawajui makada wa Chadema. Mkutano kama ule ilikuwa ni fura kwa Chadema kuwatambulisha makada wa Chadema na wapi wapenzi wa Chadema waende kupata taarifa za chama chao.

  Badala yake, wengi wa waliokwenda pale Mwembetogwa kumsikiliza Dr Slaa wamerudi majumbani kwao. Na atakayewatembelea tena kuzungumzia uchaguzi ni Balozi wao wa nyumba kumi.

  Naam. Demokrasia yetu bado changa. Na ishara za jamii inayotaka mabadiliko inaonekana. Tuwe na ujasiri wa kutoa maoni yetu kwa kutanguliza MASLAHI YA TANZANIA KWANZA. Hata Roma haikujengwa kwa Siku Moja.

  Maggid
  Iringa.
   
 2. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,835
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  CHADEMA ndio chama chenye kitakacholeta mabadiliko nchi, Lakini kabla hatuafika huko wanatakiwa kuwa smart sana!
   
 3. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Chupi inawabana CCM ya wanyang'anyi, maharamia, mafisadi wateka nyara wa rasilimali zetu... life is process na huu ndiyo mwisho wa dhuluma kuu mliotufanyia sisi wanyonge wa TANZANIA...Slaa hana haja ya kueleza kila kitu, watanzania tunafahamu kilichopo nyuma ya pazia iliyopasuka..
   
 4. M

  Masauni JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe tushakuzoea pro-CCM? Analysis zako hazina mashiko
   
 5. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2010
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Slaa anafanye vitu kwa kujiamini,kwa kuwa anauhakika na anachokitamka,huwa hakurupuki.kama kasoro ama mapungufu hata kikwete anayo mapungufu kibao ktk hutuba zake.jamaa yangu yuko iringa amaniambia ijawah tokea iringa..
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mjengwa mbona hukutuambia ulichokiona uwanja wa Sanora alipotembelea JK na pia kutoa uchambuzi wa strengths na weaknesses zake. Bado inaonekana unaogelea kwenye dimbwi la kutaka kutuaminisha CCM na JK are perfect na wengine ni wakulinganishwa.
   
 7. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Nimeupenda uchambuzi wako wa leo Maggid. Na je unasemaje kuhusu tathimini yako ya juzi kwamba Dr Slaa hakubaliki mikoa ya kusini na kwamba atashika nafasi ya tatu katika uchuguzi wa mwaka huu? Upo tayari kukanusha kauli yako?
   
 8. M

  Masauni JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mjengwa nadhani unapoteza muda tu kutaka kutuaminisha kuwa CCM is the best. Watu tulishaamua JK OUT. narudia tena analysis zako sio za kisomi kabisa.
   
 9. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Analysis yako nzuri. Dr. Slaa afanyie kazi weakness identified.
   
 10. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280

  Mjengwa na rafiki yake Michuzi ni waganga njaa wa CCM ; huku kujidai anafanya analysisi ya Slaa ni kujibaraguza tu!! Level ya education yake haimruhusu kuweza kuelewa Dr. Slaa anafafanua nini!! He is just a bogus blogger.
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nyomi la jana Mwembetogwa acha kabisa,kizuri ni kuwa watu wamekuja wenyewe
   
 12. F

  Fanfa JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2010
  Joined: Sep 25, 2009
  Messages: 538
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Maggid,
  Naomba kujua kama umati ule CHADEMA waliwasomba watu kwa malori, pamoja na kuwavalisha T-shirt za CHADEMA, na kuwajaza mifukoni mwao jao buku buku. Je kulikuwa na mbwembwe za bendi (TOT), Bongo Flava n.k ili tuweze kujua kama watu walifuata Fiesta ama walienda kumsikiliza Dr. Slaa

  Ukitujibu haya tutajua kama Iringa mjini ni ngome ya CCM au CHADEMA.

  Tunakushukuru kwa kukiri kuwa haijawahi kutokea tangu uhuru watu wengi hivyo kwenda kwenye mkutano wa kampeni. Kumbuka kuwa watanzania wa leo sio wa enzi zile wanajua wanachokifanya na hata wanachokitaka


   
 13. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu, umesahau wale wavaa sidiria. Walikuwapo pia!
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Maggid is becomeing very interesting these days, ana point nzuri tatizo kazishabikia mno kiasi kwamba ni perepete

  Je unajua ofisi za epa, richmond na kagoda??? nope huzijui... lakini za chadema zinajilikana kwa wapenzi na zaidi inatokana na upenzi... je wew unajua ofisi za ccm wangingombe?? kama unajua basi wewe ni ccm na kama unajua za chadema njombe basi wewe ni chadema

  maggid is slowly failing to be neutral kama mwandishi

  eniwei, he has lost popularity long ago na sasa yeye na nakaaya could swin in the same boat
   
 15. C

  Chesty JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,335
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 180
  Hivi Mjengwa mbona hakutupa tathmini ya Kikwete wakati anawafokea na kuwakashifu wafanyakazi pale Diamond Jubilee? Hata hivyo good job!, Sikujua Dr. Slaa alivuta maelfu Iringa kuliko mtu mwingine yeyote. Hilo limenipa tumaini. Big up!
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  Oct 3, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Alishindwa kuuza gazeti lake KWANZA JAMII aliloanzisha kwa sababu ya kukosa wasomaji. Lilikuwa linajaa pumba tu na hakutaka kuiga Mwanahalisi au Raia Mwema anayoandikia hivi sasa.

  lkn pengine ana lake lengo -- huenda akadondokewa na u-DC. Lakini ajabu ni kwamba kwa nini makala zake hazionekani katika UHURU na MZALENDO? Anajua fika kuwa magazeti hayo huishia kufungia mandazi na kuuzwa kwa kilo. Maggid ni mtu wa ajabu kweli kweli.
   
 17. m

  mozze Senior Member

  #17
  Oct 3, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Well, Mjengwa ameshindwa kuficha uhalisi wake. Amejaribu sana kuonyesha yuko neutral lakini anapoteza ujasiri huo.

  Mjengwa umetumia kigezo gani kusema Iringa ni Ngome ya CCM? Kama umekubali kuwa umati ulio uona umevunja rekodi, hata za CCM kwa nini umenaza na Iringa ni ngome ya CCM?
  Kwa nini umejichimbia zaidi kuchambua hotuba za Slaa na hukufanya hivyo kwa wagombea wengine kama Kikwete?
  Kwa nini umeangalia zaidi mapungufu?
  Je kulikuwa na ugumu gani kufanya utafiti wa haraka tu, kujua kama watu waliofika waliridhika na hotuba ya Slaa? Na matarajio yao yalikuwa nini?
  Kwa nini hukuwauliza hao unaosema wana CCM waliokuja, wakueleze kilichowavutia ni nini wakati Kikwete alipokuja walipewa T-shirts, vyakula na usafiri ndio wakaenda kwenye mikutano?
  Je kwa nini hawakuja na T-shirts kwenye mkutano huo? mana T-shirts kazi yake ni kutangaza na tunatangaza kwa watu wasiojua.

  Uwe makini na Chambuzi zako, wewe sio kila kitu ni vyema ungeweka maoni ya watu waliohudhuria mana hao ndio wapiga kura, wewe hata ukimpigia Kikwete wao wanajua nani wa kumpigia. Japo tunathamini mawazo yako lakini usitake kutupotosha.
   
 18. m

  maggid Verified User

  #18
  Oct 3, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Acid,

  Usijihangaishe sana kuniandama, huwezi kunizuia kuandika fikra zangu. Ulishaandika huko nyuma, kuwa ulishaacha kunisoma siku nyingi. Kinachokufanya unisome tena ni nini? Au ndio unakula matapishi yako? Mimi ni maggid tu. Sijawahi kuutafuta umaarufu na wala sina haja nao. Labda wewe ndio unaonipa 'umaarufu' wa bure kwa kuniweka kundi moja na Naakaya! Ahsante sana.
   
 19. m

  maggid Verified User

  #19
  Oct 3, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Marksman,

  Unaandika usichokijua. Sasa hilo ni tatizo lako. Kama unahitaji msaada wa kujuzwa, omba.
   
 20. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #20
  Oct 3, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maggid; You are finishing/firing yourself-OUT
   
Loading...