Kilichonikera/kunifurahisha kuhusu Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilichonikera/kunifurahisha kuhusu Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 12, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 12, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Najua wapo waliokerwa hasa na dhana kuwa miaka "hamsini" haihusiani na "Tanzania" wala "Tanzania Bara" bali yanahusiana na "Tanganyika". Hawa walipenda maadhimisho yaitwe kwa haki kabisa kuwa ni ya uhuru wa "Tanganyika". Tukiondoa hilo ambalo ni dhahiri kwa baadhi ya watu kuna vitu vingine vimekera sana kiasi kwamba unatamani hata siku kuu nzima ingeahirishwa hadi tuweze kuipatia.

  Umeona toka Januari - Rais alipotangaza maadhimisho haya makubwa - taasisi zikifanya maonesho, matangazo ya kiile kinachoitwa "mafanikio ya miaka hamsini". Lakini kilele cha yote ni maadhimisho makubwa yaliyofanyika Alhamisi usiku (sijui mikoani walifanya nini siku hiyo) na yale ya Uwanja wa Uhuru. Na kati ya hapo pote kuna mengi yamefanyika.

  a. Je umefurahia kuwa maadhimisho yameenda kama ulivyotarajia?
  b. Je, kuna vitu ambavyo ulidhani vitafanywa lakini havikufanyika?
  c. Je vile vilivyofanyika vimefanyika kwa uzito unaoonekana.
  d. Taarifa za sasa kwamba tumetumia karibu bilioni 70 kufanikisha maadhimisho haya unaamini yameendana na hela zilizotumika au ni fedha kidogo sana au nyingi sana?


  Kama unaona hakuna kilichokukera bila ya shaka kipo kilichokufurahisha sana na unatamani yakifanyika ya Muungano basi yafanane na haya.
   
 2. t

  tisa desemba JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  vilivyonikera:-

  1.sisi wafanyakazi wa serikali kuchangishwa pesa ili kuwezesha sherehe hizi.
  2. tuzo kwa anna makinda aka bi k .....:embarassed2:
   
 3. T

  Tanganyika jeki JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2011
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu Mwanakijiji - unayeishi jijini. Ngoja nikusimulie; Kuna jamaa yangu analalamika. Ana kadi za michango 8, ni za arusi, kipaimara, send off, kitchen party (kwa mkewe). Nikamuambia, 'acha kulipa kama hutaki'. Akaniangalia kwa ghadhabu! 'Unaishi nchi gani?', aliuliza. 'Tanzania', nilimjibu. 'sasa usilolijua kuwa ni lazima nilipe, ni nini!'. Aliendelea, 'unajua inaniuma kuwa nimemkatalia anko kumlipia sehemu ya ada ya shule ya mtoto wake ambayo ni sh. 60,000 tu, nikisema sina'. Hili limenifurahisha. Kutimiza utamaduni wetu. Kutumia 'mabilioni' kusheherekea miaka 50 ya uhuru, arusi, kipaimara, graduation, ubatizo,birthday, muungano wa tz na zbr, ushindi wa kishindo wa mbunge, kuteuliwa kuwa mkurugenzi nk.
   
 4. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #4
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Wakati baraza la maaskofu Catholic wanajenga shule kama kumbukumbu ya uhuru, Serikali inapika ubwabwa na miposho mikubwa mikubwa ambayo kimsingi imewaaneemesha watu wale wale. Kimsingi hakuna kitu hata kimoja kilichonifurahisha ambacho serikali kama serikali imefanya katika maadhimisho haya.
   
 5. T

  Tanganyika jeki JF-Expert Member

  #5
  Dec 12, 2011
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu Mwanakijiji - unayeishi jijini. Ngoja nikusimulie; Kuna jamaa yangu analalamika. Ana kadi za michango 8, ni za arusi, kipaimara, send off, kitchen party (kwa mkewe). Nikamuambia, 'acha kulipa kama hutaki'. Akaniangalia kwa ghadhabu! 'Unaishi nchi gani?', aliuliza. 'Tanzania', nilimjibu. 'sasa usilolijua kuwa ni lazima nilipe, ni nini!'. Aliendelea, 'unajua inaniuma kuwa nimemkatalia anko kumlipia sehemu ya ada ya shule ya mtoto wake ambayo ni sh. 60,000 tu, nikisema sina'. Hili limenifurahisha. Kutimiza utamaduni wetu. Kutumia 'mabilioni' kusheherekea miaka 50 ya uhuru, arusi, kipaimara, graduation, ubatizo,birthday, muungano wa tz na zbr, ushindi wa kishindo wa mbunge, kuteuliwa kuwa mkurugenzi nk. Hilo limenifurahisha! Serikali kwa vitendo imedumisha utamaduni 'wetu watanzania'. Kwa kwa kweli ni sikivu na inajali 'maslahi ya watanzania'.
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Dec 12, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Siku moja FIELDMARSHALL ES alisema viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe. Hili swali hata mimi huwa najiuliza kila siku. Kwa nini mtu yuko mstari wa mbele kuchangia kitchen party, harusi lakini sio elimu. Au wote tumekuwa waswahili tunapenda "shughuli na kula" kuliko mambo serious? Au ndio yale ya Nyani Ngabu, ndivyo tulivyo?
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  -Tunasherekea kitu gani hasa kwa hali ilivyo nchini hususan huduma za jamii!
  -Walipewa nishani waliostahili?
  -Hata kusimama kwa dk moja na kumkumbuka Mwalimu na waasisi wengine waliotangulia mbele ya haki hatukuweza!
  -Ni majina yale 17 tu ndiyo yaliyostahili kusomwa na JK? Zuberi Mtemvu alikosekana vipi kati ya wengi wengine.
  -
   
 8. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #8
  Dec 12, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  SHEREHE YA MIAKA 50 YA UHURU Sawa lakini ukitafakari je miaka 50 inaoana na mafanikio yaliyofikiwa?Kwangu mimi sherehe za uhuru ni mradi mwingine wa "MAFISADI"Kuchota pesa za walalahoi kwani naimani ya kua zaidi ya asilimia 60 au zaidi imeishia mifukoni mwa MAFISADI.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 9. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #9
  Dec 12, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,545
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu advocatejasha habari za urusi!!!! ninafurahi kuona unavyoguswa na maisha ya walalahoi tz....ambayo kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na mafisadi.......ningependa siku moja nawe urudi tz ili tushirikiane kupambana na ufisadi kwa nafasi zetu....by the way yule jamaa justine aliyeugua sana moyo mlifanikiwa kumrudisha tz baada ya ile wake up call??kama amerudi tz ningependa kuwapongeza kwani naskia urusi mnaishi kwa taabu sana haswa kipindi hiki ambapo warusi kidogo wamekuwa na standard poa za kimaisha si kama zamani ambapo mlikuwa mnapanda ndege kwa dola 50 kwenda kustarehe ulaya.....by the way ebu mkuu tujuze kuhusu siasa za urusi kwasasa kwani nimesikia hali si shwari kwa Putin vile kumekuwa na maandamano ya kumpinga...hali yaweza kuwa mbaya akirudi kuwa rais huyu bwana......anyway......mungu ibariki tz......mrudi tz jamani tupamabane pamoja....fimbo ya mbali haiui nyoka.....
   
 10. T

  Tanganyika jeki JF-Expert Member

  #10
  Dec 12, 2011
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kuna rafiki yangu akimnadi kwa mara kwanza JK kuwa rais alisema: JK ni mtu wa watu, presentable, ana huruma. Alienda mbali nakunieleza jinsi alivyohudhuria msiba wa jirani yao akiwa waziri wa mambo ya nje. Akiniangalia usoni na kung'amua mashaka yangu, alisema ofcourse ni msafi! Nilitishika!! Sikumjibu kitu. Rafiki yangu, msomi huyu ni zao la jamii km ilivyo kwa JK. Angalia familia zetu, ambazo baba ni rais aka mfalme wa familia na niambie km unaona kuna uongozi madhubuti wa familia pale. Mtoto anajifunza taratibu toka kwa babaye! Rais , waziri, mkurgenzi ajaye! Oh. God forbid!!
   
 11. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Akaenda mbele zaidi kwa kusema ".....waliotunukiwa na waadilifu na wameendelea kuisaidia jamii......". Ila hakusema vigezo hivyo vilipatikana kwa wahusika kupigiwa kura, au ni jinsi alivyojisikia mwenyewe. Amejaribu tu kuwakumbusha kuwa ana sababu ya kumwondoa Sitta kwenye usipika na kumweka Makinda. Pia ana najibu kwa waliomweka madarakani(ENL) na sasa anawageuka.

  Sasa tusubiri bunge lijalo la mama aliyeshinda Noble price ya JK.
  Natunaini yupo mbunge atakayeomba mchanganuo wa matumizi ya garama zote za "Sherehe"
   
 12. T

  Tanganyika jeki JF-Expert Member

  #12
  Dec 12, 2011
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Pointi nzuri. Nani alisema uhuru ule wa watanganyika? Je, watanganyika hao ni lini wamekuwa wamilika wa nchi yao? Mfano muungano wa tanganyika na z'bar, wananchi walishiriki kuamua, maziko ya tanu na asp? Vipi khs mfano ushiriki wa tz kwenye jumuia ya afrika mashariki? Wameshiriki kuamua? Wameridhia? Sherehe ilileta sherehe kwa baadhi ya 'wamiliki nchi'. Kwa posho, tenda mbalimbali, nk vipi khs mkulima na kilimo kwanza chake asiye na posho? Mwalimu na wanafunzi wasumao chini ya mwembe? Na malimbikizo yao vipi? Watz tunaishi kikongo tunajipiga mikorogo nyusoni mwetu, tuonekane wa maana. Tunataka kuvaa km wao ili kwa mwonekano tuwe km wao. Wakati tunalala na kula kwa shida! Laiti tungejisumbua kujua 'mwanaume yule askari aliyejiua lindoni' kwanini kafanya hivyo, tungesitisha sherehe
   
 13. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #13
  Dec 12, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Rafiki yangu mwanakijiji,
  Kwangu mimi sioni kama kulikuwa na umuhimu wa kutumia karibu bil 70 kusherehekea. Hivi tunapongezana nini? Nini tofauti kati ya wakoloni tuliowafukuza na viongozi waliopo madarakani? Wanaishi ktk nyumba zile zile za wakoloni na kuendeleza sheria zile zile.
  Nitataja mifano michache.
  Wakoloni walikuwa wanajenga hospitali, bara bara, shule kiduchu ukilinganisha na mapato wanayovuna nchini kwetu, tulilalamika tukawatimua. Leo vipi? Kodi inayokusanywa inaendana (Proportional ) na tunachokivuna - yaani huduma ya hosp, bara bara na ubora wa elimu. My response is NO.
  Wakoloni walivuna mengi wakapeleka kwao kwa faida yote. Tukawafukuza. Vipi leo? Madini, wanyama hai wanabebwa mchana kweupe? Tunasherehekea nini ?
  Wakoloni walikusanya kodi ambayo haikuwasaidia watz,tukawafukza. Leo kila kitu kinatozwa kodi hadi marehemu analipa kodi kwa kuwa hata jeneza inalipiwa kodi- VAT. Tunasherehehekea nini?
  Nyerere alipaochia ngazi, 80% wanajua kusoma na kuandika( KKK), Leo ni 63- 65% watz wanajua kkk ( takwimu za UN) Tunarudi nyuma halafu tusherekee tena au tuomboleze?
  Miaka 50 baada ya uhuru wanakufa akina mama wajawazito 24 hadi 36 kwa siku wakati wa kujifungua kutokana na huduma mbovu. Tunasherekea vifo vya wamama na shangazi zetu AU tuomboeleze?
  2011 tumeambiwa Tz ni nchi ya KWANZA Afrika na ya 3 duniani kupokea misaada. Misaada inayoishia mifukoni mwa wajanja. Tunasherekea umatonya wa kimataifa?
  Serikali inajisifia takwimu za kuongezeka kwa idadi ya vyuo vikuu, lakini hawatoi takwimu ya tija inayotokana na wanafunzi hao wa vyuo vikuu?
  Rais katuambia 30% ya mapato ya serikali yanapotea kifisadi. Hii ni zaidi ya bil 4 ukilinganisha na tril 13 ya bajeti ya mwaka huu? Ni pesa nyingi sana. Je, tusherekee jinsi tunavyoibiana?
  Mkuu mimi naomboleza, sisherehekei. Sina cha kusherehekea. Kinachonikera ni watu kusherehekea msibani.
   
 14. kajwa

  kajwa Member

  #14
  Dec 12, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwanzoni sikutaka kabisa kuhangaika na haya "maadhimisho"....
  Kero yangu ya kwanza ilikuwa ni tumezidisha (serikali) chumvi katika vitu/masuala ambav/yo labda mimi ni kipofu wa hayo "mafanikio"...
  Ila sasa hili la hizi bilioni ndio limenichefua zaidi japo nililihisi toka mwanzo
   
 15. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #15
  Dec 12, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,992
  Likes Received: 3,742
  Trophy Points: 280
  kutimiza miaka hamsini kwa kitu chochote au jambo lolote is a milestone achievement.

  kero yangu kubwa ni kwa hii milestone kufikiwa huku nchi ikiwa na ombwe la uongozi ambalo halijawahi pata kutokea.
  so, si jambo la kushangaza nikufahamisha kuwa kero yangu hii si ya jana wala juzi but it's dating back to 2005 baada ya jina la ccm presidential candidate kujulikana.
   
 16. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #16
  Dec 12, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  YALIYONIKERA:
  1. 1. Gharama kubwa zilizotumika pasipo ulazima.....Anyway huu ni ugonjwa wa kitaifa,na ni hereditary. Nikikumbuka pesa nilizotoa kama michango ya harusi mwaka huu na zile nilizotoa kama msaada kwa elimu au matibabu ...au hata chakula kwa wenye uhitaji; nakosa usemi katika hili.
  2. Hakuna documentation yeyote ya KITAALAMU,iliyo HONEST, inayonyambua njia tuliyoichukua kufikia miaka 50 ya uhuru. Tumetoka wapi,tumepita wapi,tulikumbana na nini,tulishindwa wapi,tulifaulu wapi,sababu zilikuwa zipi,...n.k. Mwanangu akitafuta official document ya compilation ya miaka hamsini ya uhuru sijui atakwenda maktaba ipi? Akibhatika kupata andiko lolote lile,je litakua limeandikwa na nani?Litakua na ukweli kiasi gani?Atajifunza nini?
  3. Mkuu wa kaya,ambaye jubilei hii imemwangukia akiwa madarakani kutokufanya chochote fitting to the ocassion...walau kwa adress moja ambayo tungeikumbuka wakati wa jubilei nyingine. Walau kuzinduliwa kwa mpango wa maendeleo wa miaka 50 ijayo...Kimya tuu,aaagh! Tumeishusha wenyewe viwango vyake!
  4. Sherehe kutawaliwa na majeshi tuuuuuu,as if ni siku ya mashujaa!Mara maonesho ya karate,mara vifaru,mara virungu na mabomu ya machozi,mara mbwa na farasi.....aaaah jamani!Hakuna kweli kingine?
  5. Kukosekana kwa SIGNATURES za maana za miaka hamsini ya uhuru.Tungesema tuchukue miradi mikubwa ya kimaendeleo tuliyoitekeleza katika miaka hii 10 towards the jubilee,tutaonesha nini? Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni....Ninaona vitu kama, Mkapa bridge,Umoja bridge,Barabara ya kati-magharibi,uwanja mpya wa taifa...halafu....kipo nilichosahau?Nikumbushwe tafadhali! Naona kama tungefanya sherehe hizi miaka 5 iliyopita,walau zingeleta maana kidogo. Lakini kinachokera zaidi ni kutokuwepo kwa mambo kama haya mathalani:


  • [*=2]Kuzinduliwa kwa treni mpya walau 2 za abiria na mizigo - "Treni ya uhuru" kwa nfano.
   [*=2]Kuzinduliwa kwa brand new mchuchuma coal plant - "Uhuru Power Plant"
   [*=2]Kuzinduliwa kwa ndege walau moja kubwa ya Air Tanzania - Ikaandikwa "uhuru" pale kwenye kichwa cha twiga..
   [*=2]Kufunguliwa rasmi kwa shule za kata zenye walimu,maabara,maktaba na umeme, nchi zima...zote zikaitwa shule za uhuru
   [*=2]Kufunguliwa mgodi mpya mmoja tu wa dhahabu ambamo serikali ina 51% ya shares..
  Hizo ni ndoto zangu tu nilizoziota usiku wa kuamkia tarehe 9/12. Nilivyoamka na kukuta si kweli...NIKAKERWA MNOO!!:shock:
   
 17. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #17
  Dec 12, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Miaka 50 si haba. Na mnyonge mnonge lakin hakhi yake mpani. Ni vizuri kumshukuru Mola kwakufika hapo pasi rabsha za aina yoyote.

  Tuliokuwa uwanjani tuliona fahari kubwa sana kwa vile vikosi vya ulinzi na usalama walivyotuonyesha. Walionyesha mpaka namna wanavyoweza kuwadhibiti watu wakiwa wanaleta rabsha ndani ya himaya ya taifa. Na tukumbuke hata ukiwa masikini basi usijitupe.

  hapa nachelea kusema kama fadha hizo walizotumia kwa maandalizi ni sahihi na zote zimetumika kama ilivyokusudiwa basi ni kheir ila kama kuna ujanja basi hapo ni lazima tulaani.

  mazuri ni mengi sana tumeonyeshwa ingawa uwazi na usahihi wa data utaona unakuwa na Mushkeri. Nilibahatika kutembelea uwanja wa Sabasaba (siku hizi Mwl Nyerere ..) uliopo Kilwa rd. Nilitembelea mabanda mengi sana lakini nitalizungumzia moja la Elimu. Hapa niliona Takwimu za ajabu sana. wanasema wakti mnapata uhuru kulikuwa na shule za msingi 41 na sasa kuna shule zaidi ya 40,000. Sekondari zilikuwa xx na sasa zipo zaiid ya 30,000. Lakin takwimu hizo hazitaji idadi ya watu wakati huo na sasa kulinganisha na ubora na ratio yao.

  nafikiri kuna safari ndefu sana katika kupiga maendeleo katika Tz. Ni lazima watu wawe makini na wadadisi, wachapakazi na wakali sana kwa yule au wale wanaoharibu mali za umma.

  Kuna mengi ya changamoto na yanahitaji barza maalum kuyajadili hususan katika nyanja ya kukuza uchumi.
   
 18. Julieth Ms

  Julieth Ms Senior Member

  #18
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KInacho niuma zaidi watoto wetu wanakaa chini shule hakuna madawati, madarasa hakuna, mahospitalini wagonjwa wanalala chini kitandani wawili wawili
   
 19. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #19
  Dec 12, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,467
  Likes Received: 3,732
  Trophy Points: 280
  yanakera sana sana..... miaka 50 kwa walionufaika kula hiyo 70b
   
 20. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #20
  Dec 12, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  -Kero yangu ni kukurupuka kusheherekea miaka 50 ya uhuru wakati tulikuwa hatujui tunasheherekea nini!!!
   
Loading...