Kilichompoza profesa peter Msola kukosa uwaziri unakijua ?

lwangwa

Member
Sep 8, 2010
91
0
Taraifa hii utaletewa si muda mrefu ,lakini kuwa ufupi tu Peter Msolla aliingilia maslahi ya jasusi wa shirika la Irani Rostam Azizi,Profesa peter msolla alipopeleka mswada wa sheria kwenye baraza la mawaziri ilikupata baraka ya kupitishwa uliokuwa ukiyataka makampuni yote ya mawasiliano pamoja na simu kuweka bayana mapato yao ikiwemo kampuni inayomilikiwa na Rostam Aziz vodacom ambayo anamiliki hisa asilimia sitini ya hisa zote kwenye kampuni hiyo.

Mswada ule ulipata baraka kwa baraza la mawaziri,Jk Rais asiye jiamini anayemtegemea Rostam Aziz na Edward Lowassa kutwala nchi kwakuwa anawaogopa na kweli anawaogopa tunajua ,na tunajua lakini profesa msolla akaitwa na Jakaya Kikwete kwa wakati mwingine weweze kubadili baadhi ya vipengele ili kuwalinda majambazi wezi wakubwa hao wa makampuni ya simu .ambao wanabadili majina ya kampuni kila baada ya miaka mitano ,msolla kwa uadilifu wake alipingana na ushauri wa bosi wake kikwete akakataa kufanya tofauti na vile baraza la mawaziri walivyopitisha mswaada huyo .

Nawambia watanzania Rostam Aziz ni jasusi hamtaki kunielewa huyu mtu anaivuruga nchi ,subirini taarifa kamili
 
Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,830
2,000
Taraifa hii utaletewa si muda mrefu ,lakini kuwa ufupi tu Peter Msolla aliingilia maslahi ya jasusi wa shirika la Irani Rostam Azizi,Profesa peter msolla alipopeleka mswada wa sheria kwenye baraza la mawaziri ilikupata baraka ya kupitishwa uliokuwa ukiyataka makampuni yote mawasiliano pamoja na simu kuweka bayana mapato yao ikiwemo kampuni inayomilikiwa na Rostam Aziz vodacom ambayo anamiliki hisa asilimia sitini ya hisa zote kwenye kampuni hiyo.

Mswada ule ulipata baraka kwa baraza la mawaziri,Jk Rais asiye jiamini anayemtegemea Rostam Aziz NA Edward Lowassa kutwala nchi kwakuwa anawaogopa na kweli anawaogopa tunajua ,na tunajua lakini akakaitwa na profesa msolla na Jakaya Kikwete kwa wakati mwingine weweze kubadili baadhi ya vipengele ili kuwalinda majambazi wezi wakubwa hao wa makampuni ya simu .ambao wanabadili majina ya kampuni kila baada ya miaka mitano ,msolla kwa uadilifu alipingana na ushuri wa kidhaklimu wa kikwete akakataa kufanya tofauti na vile baraza la mawaziri walivyopitisha .

Nawambia watanzania Rostam Aziz ni jasusi hamtaki kunielewa huyu mtu anaivuruga nchi ,subirini taarifa kamili

Nilishasema.

Kikwete siyo Rais.

Ila anataka watu wamuite Rais kama sifa tu.

Nchi inaongozwa na wenyewe.

Nampongeza Prof. Msolla.

Nadhani kuna haja ya wasomi wa nchi hii kuungana na kujitenga na CCM.

Vinginevyo nchi hii itakuwa ya mahala pa mateso kwa kila mtu asiye na pesa.
 
RedDevil

JF-Expert Member
Apr 30, 2009
2,373
2,000
Nasubiri taarifa kamili mkuu ili nitoe maoni yangu, kwa sasa nakaa kando.
 
Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,291
1,250
Msolla ameharibu sana bodi ya mikopo ya elimu ya juu kaajili ndugu zake hawafanyi kazi yeyote !
 
Sir Leem

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
576
225
Kuna wakati Mwanakijiji alimshambulia sana Huyo Prof. Msola alipokuwa Waziri wa Elimu ya Juu kwa kutowajibika
 
Newvision

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
446
0
Juu ya Rostam lolote laweza kuwa kweli ila Reverend Masanilo una hakika na unalosema? uwe mkweli na unayosema tunajua ni kweli Prof Msollla hakufanikiwa sana kutengeneza Baraza la Mikopo na hata aliyetoka pia lakini hao ndugu katika Baraza la Mikopo ni akina nani hatuwezi kuamini tu unachosema give us facts?
 
Iza

JF-Expert Member
Jan 8, 2009
2,000
2,000
Kama unakosa madaraka kwa kusimamia ukweli...ni ujasiri ambao wengi wetu hatunao.
 
lwangwa

Member
Sep 8, 2010
91
0
Msolla ameharibu sana bodi ya mikopo ya elimu ya juu kaajili ndugu zake hawafanyi kazi yeyote !

Kwa hili la kunyimwa uwaziri na kusimamamia anachokiamini msolla nampongeza ,kwenye elimu hilo ni jambo lingine tusihamishe mada ,msola kanyimwa uwaziri kwasababu aliingilia maslahi ya Rostam Aziz tena jasusi
 
Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
1,195
Nilishasema.

Kikwete siyo Rais.

Ila anataka watu wamuite Rais kama sifa tu.

Nchi inaongozwa na wenyewe.

Nampongeza Prof. Msolla.

Nadhani kuna haja ya wasomi wa nchi hii kuungana na kujitenga na CCM.

Vinginevyo nchi hii itakuwa ya mahala pa mateso kwa kila mtu asiye na pesa.

Tuwakaribishe Chadema....
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,834
2,000
Taraifa hii utaletewa si muda mrefu ,lakini kuwa ufupi tu Peter Msolla aliingilia maslahi ya jasusi wa shirika la Irani Rostam Azizi,Profesa peter msolla alipopeleka mswada wa sheria kwenye baraza la mawaziri ilikupata baraka ya kupitishwa uliokuwa ukiyataka makampuni yote ya mawasiliano pamoja na simu kuweka bayana mapato yao ikiwemo kampuni inayomilikiwa na Rostam Aziz vodacom ambayo anamiliki hisa asilimia sitini ya hisa zote kwenye kampuni hiyo.

Mswada ule ulipata baraka kwa baraza la mawaziri,Jk Rais asiye jiamini anayemtegemea Rostam Aziz na Edward Lowassa kutwala nchi kwakuwa anawaogopa na kweli anawaogopa tunajua ,na tunajua lakini profesa msolla akaitwa na Jakaya Kikwete kwa wakati mwingine weweze kubadili baadhi ya vipengele ili kuwalinda majambazi wezi wakubwa hao wa makampuni ya simu .ambao wanabadili majina ya kampuni kila baada ya miaka mitano ,msolla kwa uadilifu wake alipingana na ushauri wa bosi wake kikwete akakataa kufanya tofauti na vile baraza la mawaziri walivyopitisha mswaada huyo .

Nawambia watanzania Rostam Aziz ni jasusi hamtaki kunielewa huyu mtu anaivuruga nchi ,subirini taarifa kamili
lwangwa, taarifa yako ni nzuri tuu tena yenye thamani kubwa kwa Watanzania, kuwadhibitishia Prof. Msolla ni bold kihivyo na ametendwa kwea sababu ya kutishia interest za watu.

Umeharibu, pale unapoweka feelings zako na emotions. Kwa ushauri tuu, sio vibaya ukiiga jinsi baadhi ya wana jf wanavyowasilisha mada mfano mzuri ni Mzee Mwanakijiji.

Hivyo ungeanza na kuweka facts kwenye para ya kwanza na kumalizia with para ya MY TAKE hapo sasa ndiyo unaweka maoni yako, mtazamo wako na feelings zako. ili kutenganisha hard facts na emotions zako. Kwenye taarifa yako kamili zingatia hili itakuwa more credible. Ni ushauri tuu, sio lazima uufuate!
 
lwangwa

Member
Sep 8, 2010
91
0
Jitahidi kuzama katika fikra sio kila kitu anapojibu mtu ni kweli ,unajuje aliyekuletea taarifa hizi hataki kuunguza picha yake na data ulizopewa ni miongoni mwa kampuni ambayo hayaweki bayana mapato yake ,ndiyo kisa cha serikali kushituka kutunga mswada washeria, hii leo atakwambia nini huyo unayedhania mekuja na data sahihi p/se my dear friend go beyond of your scope.
 
asagulaga

Member
Feb 8, 2010
86
95
Nilishasema.

Kikwete siyo Rais.

Ila anataka watu wamuite Rais kama sifa tu.

Nchi inaongozwa na wenyewe.

Nampongeza Prof. Msolla.

Nadhani kuna haja ya wasomi wa nchi hii kuungana na kujitenga na CCM.

Vinginevyo nchi hii itakuwa ya mahala pa mateso kwa kila mtu asiye na pesa.

Ninakushangaa sana ndugu. Unasema Kikwete siyo rais sasa rais nani? Je alipindua alipindua serkali? Je kuna sehemu unaweza kueleza kuwa alipitishwa na chama chake isivyo halali? Je hakuchaguliwa na wananchi wa Tanzania kupitia sanduku la kura? Kueleza kuwa Kikwete siyo rais ni kupingana na demokrasia ambayo imetengenezwa katika misingi ya katiba yetu. Tafadhali usiwadhalilishe watanzania na wewe mwenyewe ambaye ulipiga kura siku hiyo. Kama kuna matatizo kuna forum zake. Otherwise forum hii itaharibiwa na watu wenye uchu wa madaraka na madiktator.
 
Unashangaa nini?

Kwanza: Sikumpigia kura. Naturally, mimi kama nafsi Kikwete siyo Rais.

Pili: Kuna watu wana maslahi yao binafsi katika nchi. Ili kufanikisha harakati zao za kimaslahi na biashara, waliona ni heri watafute mtu kutoka chama chenye nguvu, wampandikize, awe amiri jeshi, then wafanye mambo yao bila bughudha ... ndiye huyo Mkwere.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom