Kilichomponza Tundu Lissu ni maneno haya aliyoandika JamiiForums...

Nadhani tufike mahali tusilazimishe kila mtu aone watawala waliopita au waliopo ni miungu watu na hawahitaji kukosolewa ama kusemwa kulingana na mtizamo wa watu.

Nadhani kinachomponza Lisu ni kusimamia ukweli katika utawala wa Chamadola kinachoongoza serikali na si chama tawala cha serikali.

Hicho ndo kitu pekee kinachomponza Lisu kwa sasa ila sio mitazamo yake kuhusu watawala waliopita basi kama ndivyo hata kule visiwani kusingekuwa na watu mana wote wangeshaponzwa kwa kuuzungumzia muungano batili
 
Binafsi nilichangia kwenye uzi huo. Siyo muhimu kuyaleta hapa kwa sasa. Lakini nnaamini, kama ilivyo kwa wanasiasa wote kuwa ni ma "opportunist" huja JF na kusoma nini jamii inasema na kuchukua wanayoona na kuyatumia kwenye siasa zao. Lissu ni mmoja wao. Ni "opportunist" aliyetumia mawazo ya kinadharia ya wachangiaji wa JF na biila kufikiri gharama (cost) zake akayapeleka bungeni na kuyajengea hoja.
Kama ulivyosema kuwa ni mtazamo wako, then you are right. But sifa moja kubwa ya Lisu ni kuwa ana independent thinking, originality of concepts/ideas na ndiyo maana ana courage ya kusema Nyerere alikosea hapa na pale. Na kweli nyerere alikuwa na mapungufu makubwa, tena sana kama binadamu. Naye analikili hili katika moja wapo ya hotuba zake! Ila alikuwa na uzalendo wa kweli! Ni uthubutu ambao wewe na mimi hatuna , ingawa tunaeza kuwa tunaona mapungufu ya Nyerere.
Nihitimishe, kama unaweza tafuta kitabu kiitwacho: Julius K Nyerere, Servant of God or Untarnished Tyrant. Kitafute ukisome ingawa huku ni vigumu kukipata (kilipigwa marufuku, unwanted literature). Kisome ukiwa na positive mind of an academician, bila biasness ya u-CCM or negativity towards Lisu. Nilikisoma Denmark na sikuweza kukileta maana I was not ready to risk being assassinated kwa kukutwa na forbidden, banned literature/kitabu hicho. Pascal Mayalla
 
Nafahamu, kigugumizi kinachowapata kwenye uzi huu ni kama kigugumizi kilichowapata kwenye uzi niliounukuu post namba moja.

Tunashindwa kusema ingawa Tundu Lissu tunampenda lakini hakupaswa kumsema Marehemu Mzee Nyerere au tunashindwa pia kusema Tundu Lissu hicho sivyo kinachomgharimu kwa kuwa alisema ukweli!

Tunaweza kutafuta mchawi kumbe wachawi tupo JF.
Marehemu hasemwi au? Hiyo umeitoa kwenye kitabu Kipi cha dini?
Au maluwe luwe yako na uwoga wa mizimu ya kwenu
 
Tundu lissu kaongea mengi sana..la mwisho ni lile la kusema tume aliyounda rais ya kuchunguza makinikia chini ya yule profesa wa chuo kikuu ilikuwa ni ya kipuuzi..kuna mtu nikamwambia tu kwa kauli hii lazima wamuue..nilijiongelea tu..haikumaliza wiki..nakumbuka alihojiwa kwenye viunga vya mahakama kuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kamba hukatikia pabovu. Kumbuka hilo.

Hili la Tundu Lissu kumsema marehemu mzee Nyerere uliliona ni sawa tu?
 
Tundu Lissu kwa kusema aliyoyasema kuhusu marehemu mzee Nyerere hayana uzito wowote?
Yana uzito mkubwa sana lakini tukiangalia kwa upana kipindi alichoyasema hayo maneno ni kitambo kidogo na ilikuwa ni awamu ya nne, na hii ya uchwara ni awamu ya tano. Kutokana na mtiririko wa matukio ya watu kupotea awamu hii, Ben wa saanane, aizory gwanda, na wengine kutekwa na kuachiwa, zito kutishiwa kifo hadharani, yaani chochote utakacho jaribu kuhoji kikiwa ni against na namba moja au yule chairman wa pale jengo la dom, hashtag Cag, kwa hiyo ukiunganisha hizo dot unapata kwamba awamu ya tano imetamalaki, hashtag Phd

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tundu Lissu kwa kusema aliyoyasema kuhusu marehemu mzee Nyerere hayana uzito wowote?
Muungano vipi.............?????!!!! Historia ni Pana na hapa wengi watayapata............!!! Mataifa makubwa..........mtatiana vidole kwenye macho wenyewe kwa wenyewe kumbe siyo...........!!!! Historia Bhanaaaaaaaaaaa....................
 
Namba hukatikia pabovu. Kumbuka hilo.

Hili la Tundu Lissu kumsema marehemu mzee Nyerere uliliona ni sawa tu?
Ni la hovyo..wakati mwingine unaweza kuwa na ujumbe mzuri au jambo zuri..ila uwasilishaji ukawa mbovu..ye alitaka kuonyesha dharau na fedheha kama kawaida yake..hakuishia hapo..kuna wakati alirudia mara tatu kauli yake kuwa nchi hii haijawai kuwa na rais wa hovyo kama huyu..
Alikuwa kila siku anafikiria zaidi namna ya kukejeli na kufedhehesha mamlaka kuliko jimbo lake na wapiga kura wake..ila jambo moja alisahau kuwa dunia ina kanuni zake..sasa anapiga yowe dunia nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
S
Si marehemu, ni hayati baba wa Taifa . TL kaponzwa na kumshambulia Rais Magufuli kwa hoja zenye ukweli wa maudhi kama dikteta uchwara, acacia saga , issue ya ndege nk. Ingekua hio issue, basi JK angemmaliza kipindi kile.
Unafahamu maana ya marehemu na hayati?

Nyerere si kapewa title ya "mwenye Rehema" na kanisa katoliki? Unakataza nini sasa?
 
Back
Top Bottom