Cicero
JF-Expert Member
- Jan 20, 2016
- 2,924
- 3,072
Do you know how annoying it is ukifamyiwa kitu kama hiki? Simulizi yako haijatuambia kama ni uongo ticket yake iliuzwa…...na kwa nini kwenye video kuna wateja wanaruhusiwa kupita ila yeye anakatazwa?Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limetangaza kumfungia msanii Diamond Platnumz na mwenzake Rayvanny kufanya maonesho yoyote ndani au nje ya nchi kwa muda usiofahamika. Si hivyo tu, bali pia wamelifutilia mbali Tamasha la Wasafi Festival ambalo limekuwa gumzo kubwa katika siku za hivi karibuni.
Sababu zinazotolewa na Basata, ambazo zina ushahidi wa wazi, ni kwamba msanii huyo amekiuka maelekezo aliyopewa na Basata, ya kuacha kuperform wimbo wa Nyegezi (Mwanza) uliofungiwa na Basata kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kukiuka maadili ya Kitanzania.
Tukio la Diamond kupigwa pini na Basata, limekuja muda mfupi baada ya Mbongo Fleva huyo kusababisha hali ya sintofahamu katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza baada ya video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonesha 'bwa mdogo' huyo akiwatemea mbovu wafanyakazi wa uwanja huo, kwa kile alichodai kwamba wamemchezea rafu kwa kuuza tiketi alizozifanyia booking mapema na kusababisha ashindwe kusafiri kurejea Dar baada ya kumalizika kwa shoo yake jijini Mwanza.
Madai hayo yalililazimu shirika la ndege la ATCL kutoa tamko rasmi na kukanusha madai ya Diamond ambapo taarifa ilieleza kwamba hakuna aliyeuza tiketi yake isipokuwa yeye ndiye aliyefanya makosa kwa kuchelewa kufika uwanja wa ndege hivyo kwa mujibu wa kanuni na taratibu, alipoteza sifa za kusafiri na ndege hiyo hivyo kuomba kupangiwa siku iliyofuatia.
Kabla ya ATCL kutoa ufafanuzi huo, watu wengi waliotazama video hiyo, waliamini kwamba kweli ATCL wamefanya uzembe, wamepiga dili kwa kuuza tiketi ya Diamond na kundi lake kwa watu wengine, kwa lugha nyepesi Diamond aliwaaminisha watu kwamba ATCL si waaminifu kwa wateja wake na ndiyo maana wameuza tiketi ambazo zilishafanyiwa booking kwa watu wengine.
Ikumbukwe kwamba ATCL ni shirika la serikali na serikali ya awamu ya tano imewekeza nguvu kubwa kulihuisha shirika hilo lililokuwa mahututi kwa kununua ndege mpya na kulifanya sasa angalau liwe na uhai baada ya kudoda kwa muda miaka mingi. Tayari ndege tano zimeshafika nchini na zinafanya kazi na matarajio ni kuleta mashine kubwa zaidi, Airbus mapema mwezi huu.
Wakati serikali ikihangaika kuhakikisha ATCL inapata wateja wa uhakika na kujiendesha kwa faida, anatokea 'mwehu' mmoja na kuibua tuhuma ambazo zinawafanya wateja wapoteze imani na shirika hilo na hivyo kulikosesha wateja na mapato.
Diamond ambaye kwa heshima na taadhima, alialikwa wakati moja kati ya ndege hizo ikiwasili nchini, badala ya kuwa balozi wa kuwahimiza watu wengine watumie huduma za ATCL, yeye anahujumu kwa kuibua tuhuma za uongo zenye lengo la kuikosesha ATCL wateja na mapato.
Fyekelea mbali ili siku nyingine ajifunze kuwa na adabu na uzalendo! Siku zote serikali inaweza kuwa inajua kwamba unafanya makosa lakini kwa sababu hugusi maslahi yake, ikakuacha uendelee kukosea! Ndiyo, kwani Diamond ameanza kuidharau Basata leo kwa kuimba Nyegezi? Upo ushahidi wa mpaka video akiwa Zanzibar na kwingineko, alionekana akiwaimbisha mashabiki kijanja.
Kama ishu ingekuwa ni hiyo tu, Basata wangeweza kuweka pamba masikioni au kuitana kishkaji, Mngereza alikuwepo kwenye uzinduzi kule Mtwara, kwa hiyo kwao siyo adui tena bali mlezi, wangeweza kunena kwa lugha moja wakayamaliza ili kuepusha hasara ya mamilioni ambayo sasa ataipata kwa kufungiwa.
Diamond, man up! Don't mess with the government!
DIAMOND WANYOOSHE we want quality service sio upumbavu wa uzalendo uzalendo my ASS!