Kilichomkumba aliyekuwa Rais wa Liberia hayati Samuel Kanyon Doe....

Leornado

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,533
196


Nadhani hii ni baada ya wananchi na waasi wa hii nchi kuchoshwa na manyanyaso ya raisi wao wakamtenda hivi baada ya kumpindua miaka ya 1990s.

African presidents take care kwani uvumilivu wa wananchi wenu una kikomo yasijekukuta haya ndugu yangu...
 
Hii habari ni kweli kabisa.

Attempt yangu ya kwanza ya PhD ilikuwa political anthropology nikitazama patriotism from the perspective of tribal loyalty, bahati mbaya ile project niliiachia hatua za awali baada ya funding kukatika ghafla. Lakini nilikuwa nimeshajifunza mambo mengi, mojawapo ni hili.

Supervisor wangu aliniunganisha na mtu wa Liberia anaitwa James Youboty tukawa marafiki na akawa ananitumia data nyingi. Ali-scan vitu vingi sana akanitumia, ikiwemo hata hotuba za mwisho za Samuel Doe alipokuwa anajitahidi kuungana na Prince Johnson ili kwa pamoja wamshinde Charles Taylor.

Kulikuwa na details za jinsi Doe alivyotumia machifu wa kabila lake la Krahn kutoka eneo la Grand Gedeh, minutes za vikao nk. Jinsi askari wa kabila la Krahn walivyosimama kidete nyuma ya Doe hadi siku yake ya mwisho.

Kikubwa kuliko vyote ambavyo James aliniruhusu kuona ni maktaba yake ya kanda za VHS zenye detail za mateso yote ambayo Prince Johnson alimfanyia Doe, ni ukatili wa ajabu mno na niliamini kuwa wale askari wake na yeye mwenyewe walikuwa wavuta bangi, huwezi kumtenda binadamu mwenzio hivyo!

Kabla ya kifo chake ambacho kilitokana na kuvuja damu nyingi, Samwel Doe alikatwa masikio yote mawili na uume wake ulikatwa kwa singe lakini haukumalizikia, ndiyo unapoona hapo kwenye picha uume ulikuwa umevilia damu.

Jambo moja pia ni kuwa James alikuwa kabila moja na Doe kwa hiyo alitoa sana story ya upande mmoja. Na pia kuweza kuwa na details zote za mateso ya Doe ilinipa picha kuwa alihusika na intelligence system yao pia (ingawa alidai ni mwandishi wa habari, lakini kuna kila ushahidi kuwa ni zaidi ya hapo). Kule US, wale mashushushu wa enzi ya Doe na familia zao wana umoja wao una nguvu sana.

James pia ameandika kitabu kinaitwa 'A Nation in Terror', ambacho pia alinipa a signed copy. Kina fine details za mateso na kifo cha Samuel Doe ambaye huyu James anamsifu kupita kiasi kama shujaa wa Liberia
 
Aiseee hii ni hatari, lakini hawa wengine hata hawajifunzi.
 
Kithuku Thanks Kithuku. Naona tunakuwa wazito kusoma mambo ya historia. Tunarudia makosa yale yale
 
Last edited by a moderator:
Masikio Chwap....mimi ninahuruma kidogo...ntamnyoa mtu mamvi yake asiyotaka kuyanyoa...abaki kipara

Samuel-Doe.jpg
 
Ikifika Tz naona watu ndo wataelewa maana ya peoples power huwezi endesha watu kama watoto wako au familia yako
Mbaya zaidi kwa kwenda kinyume na matakwa yao
Munge aipushie karibu ilo janga
 
Aiseee hii ni hatari, lakini hawa wengine hata hawajifunzi.
..Na hawana haja ya kujifunza kwani wanajua kabisa hakuna mwenye guts za kufanya hayo waliofanya watu wa Liberia so usijiumize roho bure.. Kama juzi tu FFU walipoanza kurusha mabomu ya machozi mkalainika na kukubali kuchakachuliwa matokeo ndio mtaweza kufanya hayo aliyofanyiwa Doe??? Never never ever:nono::nono::nono:
 
Hayo ni mawazo yako tuu, ila ni vizuri kujikumbusha yaliyotokea kwa wenzeti ili na sisi yasitutokee Nancy.

Sipendi yatokee wala nini ila ni vizuri kuwa yalitokea
 
Hayo ni mawazo yako tuu, ila ni vizuri kujikumbusha yaliyotokea kwa wenzeti ili na sisi yasitutokee Nancy.

Sipendi yatokee wala nini ila ni vizuri kuwa yalitokea


Kwenye red: ni Vizuri kujua kuwa yalitokea halafu tuepukane nayo
 
Jamani sisi wengine ni new generation na historia ya dunia hatuijui vizuri.
Nimekuwa nikisikia story nyingi zinazohusu viongozi kadhaa wa Africa.
Leo ningependa sana kujua history ya Samweli Doe ambae aliwahi kuwa
rais wa Liberia!.
1.kwanza aliingiaje madarakani na ni mwaka gani?
2.Alikuwa ni msomi au mbumbumbu?
3.Je, ni kweli alikuwa dictator?
4.Aliondolewa madarakani kwa sanduku la kura au alipinduliwa?
5.Je, ni kweli aliburuzwa barabarani huku akikatwa viungo vyake kimoja
badala ya kingine? au ni uzushi tu?
6.Mwisho- aliondoka ikulu ya Liberia mwaka gani na kufa mwaka gani?

MaGreat thinker naomba mnisaidie kwa hili na faida kwa watu wengine ndani ya jf.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom