Kilichojiri kwenye Uzinduzi wa Mtambo wa Umeme wa Gesi, Kinyerezi Dar es Salaam

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,180
Wanabodi

Niko eneo la Kinyerezi kuwaletea Uzinduzi wa Mtambo Wa Gesi wa Kinyerezi 1 unaifanywa na Rais Dr. Jakaya Kikwete.

Kwa sasa wangeni mbali mbali wakiwemo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao wameishawasili na burudani mbalimbali zinaendelea.

Andamana nami kukuletea kila kinachoendelea hapa.
Karibuni.
Paskali

[h=1]RAIS KIKWETE AZINDUA MRADI WA UMEME GESI ASILIA KINYEREZI OKTOBA 12, 2015[/h] Leave a reply


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe na kufunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua rasmi mtambo wa kufua umeme kutokana na Gesi Asilia huko Kinyerezi jijini Dar es Salaam.Mradi huo umejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 400.Kushoto ni mwakilishi wa benki ya African Development Bank(ADB) Bi Tonia Kandiero na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Bwana Felchesmi Mramba.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea mradi wa kufua umeme kutokana na gesi asilia muda mfupi baada ya kuzindua mradi huo huko Kinyerezi jijini Dar es Salaam



UFUAJI WA UMEME KUTOKANA NA GESI ASILIA

1. UTANGULIZI

Serikali kupitia TANESCO imekamilisha miradi mitano (5) na inatekeleza miradi mingine saba (7) ya kufua umeme kwa kutumia nishati ya gesi asilia katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Lindi. Kiasi cha umeme unaofuliwa kwa sasa kwa kutumia gesi asilia unafikia Megawati 546 na miradi iliyopo kwenye utekelezaji itakapokamilika inatarajiwa kuongeza ufuaji wa umeme kutokana na gesi asilia kufikia Megawati 2,475.

Miradi hii ipo kwenye hatua mbalimbali ya utekelezaji na inatarajia kukamilika kati ya mwaka 2015 na 2019. Kukamilika kwa miradi hii kutakidhi mahitaji ya umeme nchini na kuondoa utegemezi wa mitambo ya kufua umeme kwa njia ya maji ambayo kiwango cha ufuaji wa umeme kimeshuka kutokana na kushuka kwa kina cha maji kwenye mabwawa, hali ambayo kwa kiwango kikubwa imesababishwa na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuendelea kwa shughuli za kibinadamu kwenye mito inayotiririsha maji kwenye mabwawa hayo. Kiwango cha umeme kinachozalishwa kutokana na vyanzo vya maji ni Megawati 561.

Miradi inayotekelezwa katika Kituo cha Kinyerezi pekee ni minne (4); Kinyerezi I, Kinyerezi II, Kinyerezi III na Kinyerezi IV. Miradi mingine miwili (2) inatekelezwa mkoani Lindi ambayo ni Kilwa Energy na Kilwa Power Plant. Mradi mmoja utatekelezwa mkoani Mtwara. Utekelezaji wa miradi hii ya kufua umeme inaenda sambamba na utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya kusafirisha umeme kutoka katika vituo hivyo vya kufulia umeme na kuingiza kwenye gridi ya taifa. 2. ONGEZEKO LA UFUAJI UMEME KUTOKANA NA KUKAMILIKA KWA BOMBA LA GESI ASILIAJumla ya vituo vinavyofua umeme kwa kutumia gesi asilia kwa sasa ni vitano (5) vyenye uwezo wa kufua umeme kama ifuatavyo: Ubungo I (102MW), Ubungo II (105MW), Songas (189MW), Tegeta (45MW) na Symbion (T) Ltd (112MW). Vituo hivi vilikuwa vinafua umeme chini ya uwezo wake kwa sababu ya upungufu wa gesi asilia kutoka Songosongo. Kukamilika kwa bomba kubwa jipya la gesi kutoka Mtwara kutawezesha ufuaji wa umeme katika vituo hivi kuongezeka kwa Megawati 200.3.

UTEKELEZAJI WA MIRADI KATIKA KITUO CHA KINYEREZI – DAR ES SALAAM
Serikali kupitia TANESCO inatekeleza na kusimamia miradi minne (4) ya kufua umeme katika kituo cha Kinyerezi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na miradi hii iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji. 2.1 Mradi wa ujenzi wa kufua umeme Kinyerezi (I) wa Megawatti 150 kwa kutumia gesi asilia Mradi huu unahusu ununuzi, usanifu, utengenezaji wa mitambo na viambata vyake, usafirishaji, ujenzi na ufungaji wa mitambo, ujenzi wa miundombinu, ujenzi wa laini mbili za msongo wa kilovoti 132 na 220, ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoozea umeme (substation), ukamilishaji na ukabidhi wa mitambo ya kufua umeme.

Gharama za mradi huu ni dola za Kimarekani 183 milioni na unagharimiwa na serikali ya Tanzania. Ujenzi wa mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya TANESCO na Kampuni ya Jacobsen Elektro AS kutoka Norway na Mshauri Lahmeyer International kutoka Ujerumani.

Maendeleo ya utekelezaji wa mradi :-Ujenzi wa mradi wote umekamilika. Mkandarasi yuko katika hatua ya ufuaji wa umeme ambapo mtambo mmoja baada ya mwingine imeanza kuwashwa na kuingiza umeme moja kwa moja kwenye gridi ya taifa. Kituo hiki kina mitambo miwili (2) aina ya LM 6000 yenye uwezo wa kuzalisha kiasi cha megawati 35.95 kila moja na mitambo mingine miwili (2) ya aina hiyo hiyo yenye uwezo wa kufua Megawati 44 kila moja. Mitambo yote ni mipya na imetengenezwa na kampuni ya General Electric ya Marekani. Picha hapo chini inaonyesha mitambo ya Kinyerezi IKukamilika kwa mradi wa Kinyerezi 1 utaongeza uwezo wa ufuaji wa umeme kutokana na gesi asilia kwa Megawati 350.

Kiwango hiki kitakachoongezeka kinatosha kufidia upungufu wa umeme uliojitokeza baada ya kufunga kituo cha kufua umeme cha Mtera (Megawati 80) na endapo kituo cha Kidatu (Megawati 204) pia kitafungwa. Hivyo wananchi na wateja wa TANESCO hawana haja ya kuhofu kuhusu hali ya upatikanaji wa umeme wa uhakika.2.2 Mradi wa ujenzi wa mtambo wa Kinyerezi (II) Megawatti 240 kwa kutumia gesi asilia Mradi huu unahusu ununuzi, usanifu, utengenezaji wa mitambo na viambata vyake, usafirishaji, ujenzi na ufungaji wa mitambo, ujenzi wa miundo mbinu ya ndani na nje ya kituo (k.m. barabara n.k.), ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoozea umeme (substation), ukamilishaji na ukabidhi wa mitambo ya kufua umeme.

Gharama za mradi ni dola za Kimarekani 334 milioni na unagharimiwa kwa asilimia 85 za mkopo kutoka serikali ya Japan na asilimia 15 zitatolewa na serikali ya Tanzania. Mkandarasi wa mradi huu ni kampuni ya SUMITOMO kutoka Japan. Mradi huu unatarajiwa kukamilika 2017.Maendeleo ya utekelezaji wa mradi;-Ufadhili wa mradi kwa njia ya mkopo umepatikana kutoka benki ya SMBC na JIBIC (85%), mkataba wa mkopo umekamilika tangu mwishoni mwa mwezi Machi 2015, vile vile serikali imeanza kutoa mchango wake wa 15% na tayari mkandarasi amefungua ofisi ya utekelezaji wa mradi, na anatarajia kuanza ujenzi eneo la mradi mwezi Novemba mwaka huu wa 2015.Mkandarasi ambae ni SUMITOMO ya Japan amekabidhiwa eneo la mradi kwa ajili ya utekelezaji wa mradi, Uchaguzi wa aina ya mitambo itakayofungwa umekamilika, Mchakato wa kumpata mtaalam mshauri umekamilika, Upembuzi yakinifu pamoja na unaohusu mazingira umekamilika. NEMC wametoa cheti cha mazingira kwa ajili ya kuruhusu uendelezaji wa mradi katika eneo hili.

2.3 Mradi wa ujenzi wa mtambo wa Megawatti 300 awamu ya kwanza kwa kutumia gesi asilia Kinyerezi (III)Mradi huu unatekelezwa kwa njia ya ubia (PPP) kati ya serikali kupitia TANESCO na kampuni ya Shanghai Electric Power Company ya China. Utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kufua Megawati 300. Mradi huu unatarajiwa kukamilika mwaka 2017.Maendeleo ya utekelezaji wa mradi;-Kampuni ya ubia imeundwa na kusajiliwa hapa nchini kwa kufuata utaratibu wa nchi. Upembuzi yakinifu umekamilika na kuwasilishwa Wizara ya Fedha kwa ajili ya kupata kibali cha serikali cha kuendelea na hatua nyingine za mradi.

2.4 Mradi wa ujenzi wa mtambo wa Kinyerezi (IV) Megawatti 330 kwa kutumia gesi asilia Mradi huu unatekelezwa kwa njia ya ubia (PPP) kati ya Serikali kupitia TANESCO na GCL Development Limited (GCL) na China-Africa Investment and Development Co., Ltd (CAIDC) zote za China. Mradi utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kufua Megawati 330. Mradi huu unatarajiwa kukamilika mwaka 2017.
Maendeleo ya utekelezaji wa mradi;-
Upembuzi yakinifu umekamilika na inatarajiwa kuwalishwa Wizara ya Fedha kwa ajili ya kupata kibali cha kuendelea na hatua zinazofuata za mradi. 3.0 UTEKELEZAJI WA MRADI WA KITUO CHA KUFUA UMEME MKOA WA MTWARAMradi huu unatekelezwa kwa njia ya ubia (PPP) kati ya Serikali ya Tanzania kupitia TANESCO na Kampuni ya Symbion (T) Ltd ya Marekani. Mradi utakapokamilika utaongeza megawati 400 kwenye grid ya Taifa. Mradi unatarajiwa kukamilika 2019.

Maendeleo ya utekelezaji wa mradi

Kampuni ya Symbion inafanya upembuzi yakinifu na unatarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka 2015.4.0 UTEKELEZAJI MRADI WA VITUO VYA KUFUA UMEME MKOA WA LINDI
Miradi miwili ya kufua umeme katika mkoa wa Lindi eneo la Kilwa; Kilwa Energy Ltd unatekelezwa na mwekezaji binafsi na mwingine unaofadhiliwa na World Bank utatekelezwa kwa njia ya PPP. Miradi itakapokamilika itaongeza megawati 570 kwenye gridi ya Taifa. Mradi unatarajiwa kukamilika 2018.
Maendeleo ya utekelezaji wa Miradi.

TANESCO na Kilwa Energy Company LTD (KECL) imeshakamilisha mkataba wa kuuziana umeme (PPA) na mradi unaofadhiliwa na World Bank kupata mtaalamu elekezi atakayesimamia upatikanaji (procurement) wa mwekezaji atakeyewekeza kwa ubia na Serikali kupitia TANESCO.5.0 UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MIUNDO MBINU YA USAFIRISHAJI UMEME KUTOKA KWENYE VITUO VIPYA VYA KUFUA UMEME.

Serikali kupitia TANESCO inatekeleza miradi miwili ya miundo mbinu ya kusafirisha umeme ya kV 400 kutoka kwenye vituo vipya ya kufua umeme kutokana na gesi asilia; Mradi wa njia ya umeme ya msongo wa kilovolti 400 kutoka DSM – Tanga - Arusha(North East Grid) na mradi wa njia ya umeme ya msongo wa kilovolti 400 kutoka Somanga Fungu - Kinyerezi.

Mradi wa DSM – Tanga _ Arusha utagharimu USD 692,698,599.00 na mradi wa Somanga - Kinyerezi utagharimu USD 150millioni. Miradi hii inatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2019.
Maendeleo ya miradi

Utekelezaji wa mradi wa DSM – Tanga - Arusha unagharimiwa na mkopo kutoka katika Bank ya Exim ya China kwa asilimia 85% na asilimia 15% itatolewa na serikali. Serikali ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha mkopo.

TANESCO inakamilisha taratibu za kupata mkopo kutoka Benki ya TIB kwa ajili ya kutelekeza mradi wa usafirishaji umeme kutoka Somanga - Kinyerezi.

6.0 HITIMISHO
Ufuaji wa umeme kutokana na gesi asilia unatarajiwa kuondoa kabisa tatizo la upungufu wa umeme nchini na kuondoa kabisa utegemezi wa awali wa ufuaji wa umeme kutoka vyanzo vya maji. Hata hivyo Shirika bado linaendelea kutumia vyanzo vya maji katika kuzalisha umeme. Vyanzo hivyo vitatumika zaidi hali ya mabwawa ikiwa nzuri kwa kuwa ndicho chanzo rahisi cha kufua umeme ukulinganisha na vyanzo vingine.
 
imebidi nitupie picha habari bila picha hainogi haya ndiyo maandalizi
12115544_972945286196921_1397797669958286374_n.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom