Kilichojiri kwenye Uzinduzi wa Mtambo wa Umeme wa Gesi, Kinyerezi Dar es Salaam

Nadhani Mengi au Manji nk. ndo angekuwa mtu sahihi wa kuzindua hiyo mitambo maana tumeambiwa na mali ya mtu binafsi siyo ya serikali halafu hao ccm wangeenda kama wageni waalikwa bila kumsahau Kinginge.

...mchanganua wa gharama na ufadhili kwa maana ya umiliki umeelezwa kwenye Thread ya Pasco sasa ambacho hujaelewa ni nini?
Au una tatizo la kusoma habar ndefu? Kwami kwenye Thread imeeleza serikali kupitia Tanesco inamiliki share ngapi, lakini kwa vile kichwani umejaza mihemko ya kisiasa huoni.
 
Wanabodi

Niko eneo la Kinyerezi kuwaletea Uzinduzi wa Mtambo Wa Gesi wa Kinyerezi 1 unaifanywa na Rais Dr. Jakaya Kikwete.

Kwa sasa wangeni mbali mbali wakiwemo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao wameishawasili na burudani mbalimbali zinaendelea.

Andamana nami kukuletea kila kinachoendelea hapa.
Karibuni.
Paskali


Utekelezaji wa mradi wa DSM – Tanga - Arusha unagharimiwa na mkopo kutoka katika Bank ya Exim ya China kwa asilimia 85% na asilimia 15% itatolewa na serikali

Hivi tumerogwa au ni ujinga? 85% Wachina? Sasa huo mradi si ndio wao. Mo&$%$&er CCM. Mmeiuza nchi yetu kwa Wachina
 
Baada ya VUTA-NKUVUTE ya muda ule, hatimaye gesi asilia imetoka huko Lindi na Mtwara. Leo mtambo wa kufua umeme wa gesi umezinduliwa na Rais Kikwete pale Kinyerezi,Dar es Salaam. Huo ni uthibitisho kuwa gesi imetoka huko hadi Dar.

Sasa nasubiri kuona kama wananchi wa Lindi/Mtwara wameisamehe CCM na bado wanaiamini kuwaongoza huko. Iko wazi, wana-Lindi/Mtwara waliapa kuiangusha CCM mwaka huu uchaguzini.

Waisome:mad:the big show VUTA-NKUVUTE Sizinga na wengineo
 
Waliona tunalalamika sana watu wa Dsm kuhusu umeme. Wengi wetu unatusaidia kutengenezea juice za ukwaju na kuangalia ligi za ulaya kwenye tvs zetu kwani tuna bet sana!
 
Jana rais wetu kazindua kituo cha kuzalisha umeme Kinyerezi tunashukuru kwani kwetu na ofisini kwangu ni wiki sasa umeme haujakatika
Hili sio omni bali ni haki yetu

Mlituambia gesi ndio suluhisho la umasikini tunaomba unite za umeme zipunguzwe sasa iligarama za maisha zipungue.
 
Manga mseke unaongea kwa upande wako ila sehemu kubwa Tanzania ina haki gani?mfano Mimi wa Mwanza mgao kama kawaida toma miezi huko nyuma na tupo tu tunasubiri October 25 ili tupumlie hapo
 
Hakuna cha ges hapa. Subiri uchaguzi uishe uone. Kama ni gesi mbona bei ya umeme inaongezeka. Kama ni ges mbona mikoani hali ya umeme ni mbaya sana.
 
Ccm wanataka kutuona wa tz wa 1980 enzi za mwalimu

jana nilishangaa jk aliposema kuwa tanesco wawashe mitambo yote!!! ina maana walikuwa wanafanya makusudi kutoiwasha? wakati juzi tu tuliambiwa hiyo mitambo inawashwa kwa utaratibu maalumu? je wanasiasa wana uelewa mkubwa zaidi kuliko wataalam!!
 
Zile siku mia za lowassa ikulu kwanza itakua kureview hii mikataba ovyo ya gesi na kununua mitambo ya kuzalishia umeme,maana tunaoumia ni wananchi,bora mitambo tuimiliki wenyewe,mabadilikoooooooooo
 
Tumethubutu tumeweza ccm mbele kwa mbele.
mukisikia changa la moto ndiyo hili, yaani mungu anatupa gas, tunaahidiwa reliability ya umeme watu wanashangilia, kwanza uchaguzi ukiisha tanesco bei juu 20% , pili mimi nakaa mtwara sina nyumba ya umeme, nafaidika nini na gas itokayo mtwara? hii imekuwa kama migodi ya geita ya dhahabu, watu wamepewa bure , wanchi taabani na umasikini, hatuelezwi wawekezaji wa gas wanalipa kiasi gani, tanesco wanalipa kiasi gani, jamani tufanye nini ili tuokoke na majanga haya, sina haja ya kufurahia umeme wa tanesco, kwani kila siku naulipia , na ni wao umeme hawana, kuwa nao leo siyo sifa, ni haki itokayo na luku yangu, toka zako
 
Zile siku mia za lowassa ikulu kwanza itakua kureview hii mikataba ovyo ya gesi na kununua mitambo ya kuzalishia umeme,maana tunaoumia ni wananchi,bora mitambo tuimiliki wenyewe,mabadilikoooooooooo

Atakuwa bize kuhakisha amewafunga ccm na ada mashuleni zimekuwa bila kusahau kumtoa babu seya gerezani.
 
Back
Top Bottom