Kilichojiri bungeni Tarehe 13 April (Muswada wa mafao)

Wao wamechukua pesa yoote kufanyia matakwa yao ya kisiasa leo anaweweseka kufanya mambo yatakayochimbia kaburi chama chao..nawasubiri watoe muongozo wao fake waone!hivi bunge gani limepitisha upuuzii huu??sijasikia likijadiliwa kabisa!inaonekana wamepenyeza kisanii kushirikisha wabunge dhaifu..wale wanaolala na kuamkia kupiga makofi kumbe hoja ilikuwa kuwatoa nje wanaolala!!aibu!!natamani kura ingekuwa week ijayo!! Wangeiba zoote maana wasingepata hata zao na wake zao wasingepata
 
Shirika kama Nssf inajenga nyumba Arusha je wananchi ambao watakua wameacha/wameachishwa kazi kwa mazingira yeyote na ambao sasa hawaruhusiwi kuchukua mafao yao mpaka miaka 55 au 60 watakuwa na shares katika hizo nyumba maana bila shaka pesa zao ndizo zinazo tumika ktk huo ujenzi?
 
Ni dhahiri huu ni mkakati wa kuwadhulumu wanyonge haki zao, hivi hii si ndiyo hiyo iliyoandikwa kwenye vitabu, kuwa walio nacho wataongezewa, na wale ambao hawana, hata kile kidogo watany"anganywa??!!

Hata hivyo, kwa maoni yangu huu ni mkakati wa mapema kabisa wa kujiimarisha, hawa magamba a.k.a mabwepande, wa kuanza kukusanya pesa kwa ajili ya uchaguzi 2015! kwani si wanajua kuwa wakati huo pesa kama zile za 2005 za EPA-Kagoda, hazitakuwepo?

Sasa mnategemea wafanye nini kwa hii situation ambayo CDM wamewabana kwenye half ground kwenye mpambano, ambao wanaona dhahiri, bila kucheza rafu game watapoteza!!!
 
Kuwa mtumishi katika nchi kama Tanzania ni kama janga.Kama hali hi hii hata ufanisi katika utumishi utatoka wapi?
 
Katika hili wametusaliti. Hii issue inaathiri wengi sana. Kuna watu watalazimishwa kusubiri hadi umri wa kustaafu ambao hata hivyo hawa-qualify kwa mfano kwa kutotimiza miezi 180 ya kuchangia. How do you treat these people? Kwa umuhimu wa hili suala, hata kama wangezidiwa kwa uwingi wa wabunge wa CCM, walikuwa na wajibu wa kuujulisha umma kwenye mikutano yao kwamba walijitahidi kuzuia lakini wakazidiwa na magamba, kitu ambacho hawakufanya. Katika hili nao ni wasaliti.

Kuna mtu kaachishwa kazi leo baada ya kampuni iliyomuajiri kufilisika. Ukimwambia mtu huyu asubiri hadi 2015 atakapoing'oa CCM ndipo apewe hela yake sijui kama utaeleweka ikizingatiwa ukweli kuwa kwa uhaba wa ajira tulionao hana uhakika kama atapata kazi tena, na lini ataipata. Sheria hii ni ya kinyama.

Mi nilisema humu siku moja kuwa hakuna kinachotokea kwa bahati mbaya kwenye siasa, ila kuna watu hawakunielewa.
Na nilisema hakuna chama tawala wala upinzani.

Kuna vitu fulani vinafanyika kwa makusudi kwa maslahi ya watu fulani. Sisi tunadangawanya na mijadala inayofanyika mjengoni lakini mwisho wa siku wanachokitaka wanasiasa(wote kwa pamoja) ndicho kinachofanyika.

Sisi tutaishia kupiga kelele na kutishia oh mi ntajilipua, sijui magamba hivi sijui chadema vile na mwisho wa siku wote kimyaa.
Hiyo ndo "sihasa" bana.

Hapa la msingi ni kubadilika kama kinyonga... Ukifungwa mlango m1, we tafuta mingine basi.
 
hii issue inasikitisha saaaana, mi naunga mkono kulaani hili dili maana ni yale yale tangu enzi zile. Lakini tukiangalia kwa makini nani ana uwezo wa kuing'oa CCM?

Sisemi kama mtu aliyetumwa bali naangalia hali halisi yaani "current circumstance" sipati picha CCM ikiachia ngazi bila fujo au mtafaruku kwahiyo inabidi hapa tufanye mpango very carefully maana imani itavunjika to the detriment of taifa letu. "The stakes have been raised, CCM has everything to lose and nothing to gain except more ill gotten wealth". Jah kaya ashakula mkate na Obama, nani atamwambia kitu?

Hamna mpango unaopita huku bila baraka za wakuu huko majuu angalia Syria na Libya na jinsi upinzani ulivyozorota mpaka decisions were made outside as to what to do. Mi nashauri wapinzani wa CCM wacampaign nchi za watu kutafuta support because bila outside support, mnapoteza muda tu.

Mikataba ishapigwa sahihi, kilichobaki ni kuheshimu mikataba iliyosainiwa or else mzungu atakutafutia kiongozi ambaye atamheshimu. Real ish!
 
Bunge lina tatizo kubwa la ufahamu. Wabunge walio wengi hawawezi kunyambulisha mambo ya kitaifa au yale yanayojadiliwa Bungeni. Wengi huzungumza Bungeni kwa kuwa sponsored. Namaanisha wanapewa chochote nje ya jengo ili waseme kitu fulani, au wanafundishwa wakaseme nini bungeni wakati mwingine kigumu kuliko hata ufahamu wao.

Hiyo utaiona jinsi walivyo pre-programmed. Mtu atakuwa ni mchangiaji (say) wa tatu, lakini wawili waliotangulia wanakuwa wamezungumzia kitu muhimu sana kitaifa, lakini huyu akisimama utasikia anaendelea na yake. Siku hizi wanasema eti 'wanajikita'. Matokeo yake atasema mengine kabisa na anweza hata kupoteza mutililiko wa hoja.
 
Mkurugenzi wa SSRA ndani ya jahazi leo sijui kama kiu na hoja zetu zitapata majibu.

Clouds ni yao hao. Huyo Mkurugenzi wa SSRA aweke mdahalo na Tundu Lissu akione chao moto.

Hiyo sheria ni ya ukandamizaji kwa mfanyakazi. Hayo mashirika ya hifadhi kazi yao ni kupeleka hizo pesa zetu kwenye miradi ya serikali kwa manufaa ya kisiasa.
Shinikizo kubwa limeanza sasa kutaka JK arudishe hiyo sheria Bungeni irekebishwe kama ilivyokuwa ile ya kuunda Tume ya Katiba.

Anyway, hii sheria kandamizi inazidi kuashiria mwisho wa serikali hii inayokandamiza wananchi.
Wananchi bila kujali vyama wala itikadi wanaipinga kwa nguvu zote.
 
Kwenye hili wabunge wote wanastahili kulaumiwa na ndo hapo inafika hatua hata sisi tunakuwa challenged na wanamagamba wajingawajinga. Haiwezekani sheria ya namna hii ikapita kimyakimya na sisi tunakuja kustuka leo.

Hivi wabunge waliuliza ushirikishwaji wa wadau? Mtu asiniambie walishirikishwa vyama vya wafanyakazi au waajiri maana huyo hawezi kusemea watu mamia na maelfu ya wafanyakazi.

Narudia kwa hapa wabunge wote walifanya brandaz.
 
Narudia tena hata wanaCDM walaumiwe kwenye hili. CDM waambie wanamagamba kupitia bunge kwamba TUMEKATAA SHERIA HII na tunataka tusikie sauti zenu kwenye hili.

Haiwezekani mnatuambia wadau walishirikishwa wakati kuna makampuni hayaruhusu vyama vya wafanyakazi kwenye ofisi zao sasa hawa wafanyakazi wa ofisi kama hizi walishirikishwa kupitia nani?

Kuna mijadala humu ndani wabunge huwa naona wanajitokeza na kuchangia wengine kwa mbwembwe. JITOKEZE NA HILI. SHAME*100 kwa bunge letu lenye upeo mdogo sana wa kuchambua mambo na kuhoji..
 
soma hansard ya bunge ya tarehe 13 april kumbe bunge lilipitisha hoja kana kwamba inamashiko kwetu.
wabunge ni wawakilishi wa wananchi wapo bungeni kupeleka kile ambacho tunawaagiza sasa nashidwa kufaham vizuri kwenye mswaada wa Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa Mwaka 2012, je Myika hayo ndo wanafanya kazi wanaishi ubungo walikutuma. je Stealla manyanya,halima mdee hayo ndo ulitumwa na wanchi wa jimbo lako au tukifika pale tunatumia utashi wetu binafsi na kwadharau wananchi waliokupa ridhaa hiyo tena kwa kukesha kulinda kura zako kusudi utete matatizo yao?

http://polis.parliament.go.tz/PAMS/docs/HS-7-4-2012.pdf

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ni vyenzo muhimu za kutekeleza Sera ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii ili kuongeza ustawi wa wananchi na nchi kiuchumi na kijamii. Hata hivyo, marekebisho yaliyowasilishwa ni machache ambayo hayashughulikiwi kikamilifu, malengo ya sera husika na mapendekezo mbalimbali ambayo Wabunge tuliyatoa katika Mkutano wa Nne wa Bunge mwaka 2011 kuhusu masuala ya kuzingatia katika marekebisho.

Hivyo, katika majumuisho, Serikali ielekeze ni nini hatma ya mapendekezo mengine ambayo Wabunge
tuliyatoa ambayo hayajaingizwa katika Muswada tunaoujadili katika Mkutano huu wa Bunge.

Aidha, wigo wa mjadala wa hifadhi ya jamii unapaswa kupanuliwa hususan wakati wa mchakato wa Katiba mpya ili kuhakikisha hifadhi ya jamii inakuwa ni haki ya lazima ya wananchi wote. Uamuzi huu uende sambamba na kuweka mfumo wa kikatiba, kisera na kisheria ambapo kila mwananchi kupitia mfumo wa hifadhi ya jamii kwa wote (Universal Social Security) atapata gawio kutoka katika mapato ya rasilimali na
maliasili za nchi ikiwemo madini, mafuta, gesi asili na kadhalika.

Mfumo wa hifadhi ya jamii unapaswa kuhusisha pia wananchi walio kwenye sekta isiyo rasmi, wazee wote ikiwemo waliokuwa wakulima na wafanyabiashara ndogo ndogo na vijana wasiokuwa na ajira kwa marekebisho ambayo yamewasilishwa sasa; yaongezewe nguvu zaidi katika masuala muhimu mawili
ambayo yanagusa kwa kiwango kikubwa wananchi ikiwemo wa Jimbo la Ubungo:-

Mosi, kudhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii dhidi ya uwekezaji usiokuwa na tija kwa wanachama na usiolinda kikamilifu fedha za wachangiaji wa mifuko husika. 13 APRILI, 2012 143

Pili, kuhakikisha wigo wa mafao unapanuliwa na kuwezesha wanachama kupata stahili zote na kwa wakati. Nguvu hizo zinapaswa kuongezwa kwa Serikali kuwasilisha jedwali la marekebisho juu ya vifungu vifuatavyo:-

(i) Kifungu cha 15 kinachoongeza kifungu cha 29A – kuviainisha na taratibu na tamaduni muafaka za mirathi.

(ii) Kifungu cha 21 kinachofanyiwa marekebisho kifungu cha 49 – kuwianisha mamlaka ya Benki Kuu na yale ya mamlaka ya udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
kuhusu uwekezaji.

(iii) Kifungu cha 66 kinachoongeza kifungu cha 71B – kuondoa mkanganyiko uliopo kati ya kifungu na
maelezo ya pembeni kuhusu mamlaka yenye dhamana ya kupokea taarifa.

(iv) Kifungu cha 150 kinachoongeza kifungu cha 49 A(2) – kiwango cha tozo kizingatie faida za uwekezaji ili wanachama wasibebeshwe mzigo wa gharama. Katika majumuisho, Serikali ieleze pia hatua ilizochukua
kutokana na tuhuma mbalimbali za ufisadi katika matumizi na uwekezaji wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kati ya mwaka 2005 mpaka 2010, ili kufungua ukurasa mpya wenye kuzingatia uwajibikaji.
 
MSIBA HUU HAPA!

Sehemu ya Nne ya Muswada inapendekeza marekebisho katika Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Sura 50 (The National Social Security Fund Act, Cap.50) ili kuboresha utendaji wa kazi kwa ufanisi. Sehemu hii inapendekeza marekebisho katika Sheria hii kwa lengo la kuainisha Sheria hii na Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Sura 135. Marekebisho yanayopendekezwa katika sehemu hii ni pamoja na kufuta baadhi ya tafsiri ya maneno na kuweka tafsiri mpya.

Vile vile tafsiri ya maneno mapya imeongezwa. Marekebisho mengine yanayopendekezwa yana lengo la kuipa Bodi uwezo wa kuamua kiwango cha juu cha pensheni atakayopewa mwanachama kwa mwezi kwa kuzingatia tathmini ya mali na madeni ya mfuko.
13 APRILI, 2012
317 Muswada aidha, unapendekeza kufanywa marekebisho kifungu cha 62 cha Sheria kwa kuweka masharti ambyo yanitaka Bodi ya Wakurugezi kutekeleza Sera ya uwekezaji kwa kufuata miongozo inayotolewa na mamlaka.

Sehemu ya Tano ya Muswada inahusu marekebisho katika Sheria ya Mfuko wa Mashirika ya Umma, Sura 372 (The Parastatal Organisations Pensions Scheme Act, Cap.372) marekebisho haya yanahusu jina la Sheria, dhamira ni kuepuka dhana ya kuwa mfuko huu ni kwa ajili ya kuhudumia sekta ya mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali tu, wakati sheria yenyewe inahusu pia waajiriwa wa makampuni binafsi na watu kutoka katika sekta isiyo rasmi.

Jina la Sheria limerekebishwa na badala yake kuwa "PPF Pensions Fund Act, 2011" kwani kuendelea kutumia neno "Parastatal" kunakinzana na sera ya Serikali ya kujiondoa katika umiliki wa mashirika ya Umma.

Vile vile inapendekezwa kufanywa marekebisho katika sheria hii ili kutambua wanachama ambao ni waajiriwa waliopo katika majaribio, mwanachama kubadili ajira, kuendelea kutambua uanachama wa mwanachama baada ya kuacha kazi au kujihudhuru ni baadhi tu ya mapendekezo muhimu
yanayopendekezwa katika sehemu hii.

Sehemu hii pia inaweka majukumu ya mwajiri, ikiwa ni pamoja na kusajili wafanyakazi wapya kwenye Mfuko wa PPF kwa wale ambao si wanachama wa mfuko wowote na kuwasilisha michango kamili ya wafanyakazi pale ambapo wafanyakazi hao wamesimamishwa kazi kwa nusu mshahara.

Aidha, marekebisho haya yameweka wazi umri wa kustaafu kwa hiari kwa mwanachama kuwa ni kuanzia umri wa miaka hamsini na tano isipokuwa uanachama wake utakoma pale ambapo mwanachama huyo atatimiza umri wa miaka 60.

Inapendekezwa pia kwamba mwanachama aliyechangia aweze kulipwa pensheni hata pasipo kukamilisha kiwango cha chini cha muda wa kulipwa pensheni. Mwanachama huyo anapostaafu apewe michango yake na ya mwajiri pamoja na riba.

Sehemu ya Sita inapendekeza
.
 
Wadau nimeshangaa kusikia kuwa Mhe Raisi kasaini sheria ya kikandamizi kwa watu wake eti mtu kuchukua fedha zake za NSSF,PPF na mifuko mingine ya jamii sharti afikishe miaka hamsini? Sasa tuseme na hilo kachomekewa au kashauriwa vibaya au hakusoma kasaini tuu?

Kwa sababu ukiangalia data za maisha ya Mtanzania umri wa kuishi ni almost fifty years (50) sasa ukingoja achukue fedha zake alizojiwekea haliba kwa hiari yake eti baada ya miaka hamsini na tano una maana gani?

Tuseme kuwa fedha huko NSSF, PPF na kwingineko hakuna zimeliwa kama tulivyo ona hapa, wanafanya mbinu ya kukusanya na kurundika ata least kuwe mafao ili watu wakipiga kelele na kwenda mahakamani tayari kutakuwa na amount fulani ya fedha?

Kwa nini huyu Raisi wetu aliyesema kuwa ataleta maisha bora kwa kila Mtanzania amegeuka kuwa mkandamizaji kwa kila namna, wizi kwenye mabenki, EPA,RICHIMOND,KAGODA, MEREMETA , MIKATABA YA WIZI KWENYE MIGODI, imekuwaje amegeuka kiasi hiki?

Mikataba ya kikandamizi ni mingi saana nchi inafilisika kisa ni kuwa na Raisi asiye na huruma na watu wake, hadi tufikie uchaguzi kama alivyosema juzi itakuwaje?
 
Maisha bora kwa kila Mtanzania ni hahadi iliyotolewa na Raisi kupata kura kuingia madarakani sio uzushi ni ukweli mtupu, sasa kiko wapi???
 
Ndugu wanachama, swala la kupigani haki yetu tusiichie TUCTA maana hao inasemekana walihusishwa wakati wa kuunda hii sheria ya kishetani. mapendekezo yangu ni kuwa tuunde jumuiya ya wafnayakazi wa sekta binafis ianze mchakato wa kupeleka swala hili mahakamani maana inasemekana hata idadi ya wabunge waliokuwa bungeni siku hiyo ambayo ilikuwa ijumaa karibu na wikiendi hawakukidhi matakwa ya kisheria ya kuitwa kikao cha bunge, yaani hawakufikia nusu ya wabunge wote.kwa hiyo tunaweza kui-challenge sheria hii mahakamani. hatua mabadala ni jumuiya hii kukaa na kukubaliana na chama cha waajiri kutopeleka kabisa michango badala yake kuwapa wafanyakazi directly. ili tuone kama hawatafunga ofisi zao.

Wale wafanyakazi wa sekta binafsi wa Arusha, naomba tukutane siku ya jumamosi mahali na saa tutakayo kubaliana ili kuweka msimamo wa paamoja.
"SHAME ON THE MPS WHO ATTENDED AND ENCTED SUCH A SATANIC LAW"

Naoma kuwasilisha.
 
Mbona akina John Komba, maji Marefu, kafumu na wengine hawalaumiwi, wanalaumiwa akina Mnyika tuu?

hao ndio tunawategemea kuwakilisha matatizo ya vijana ambao inatupasa kusubiria miaka 10 hadi 25 kupata haki yetu inayochukuliwa katika mishahara yetu.
 
hao ndio tunawategemea kuwakilisha matatizo ya vijana ambao inatupasa kusubiria miaka 10 hadi 25 kupata haki yetu inayochukuliwa katika mishahara yetu.
Sasa mbona mliwachagua na akina John Komba na Maji marefu?
 
Sasa mbona mliwachagua na akina John Komba na Maji marefu?

Nani aliwachagua? na walio wachagua wanajua sababu ya kuwachagua bt mimi ninawabana wanaonihusu na wale niliona wanaweza wakaunganisha nguvu kati kulikomboa taifa letu.
sioni msingi wa maswali yako rudi kwenye mjadala kwani hakuna umuhimu wa kumjadili komba na uwepo wake bungeni.
 
hao ndio tunawategemea kuwakilisha matatizo ya vijana ambao inatupasa kusubiria miaka 10 hadi 25 kupata haki yetu inayochukuliwa katika mishahara yetu.

Hivi hao wabunge wa CCM ambao huwa wanasinzia harafu wakishituka na kukuta mama makinda anasema Nafikiri walisomea Ndio wameshinda ..hata kama upinzani wamesema hapana kutokana na Idadi yao ndani ya Bunge
harafu jibu lenyewe kama hawanaga uhakika (Nafikiri )ndo nini?


Cha msingi ni kuweka wapinzani wengi ndani ya bunge Serikali hii inatakiwa iondoshwe madarakani haifai ,imechachoka kifikra
 
Back
Top Bottom