muhogomtamu
JF-Expert Member
- Apr 5, 2012
- 412
- 69
Haifungu kwenye kacm kangu,ni click open,inasomeka invalid web
Mkuu si utumie kikokotoa mpakato?!
Haifungu kwenye kacm kangu,ni click open,inasomeka invalid web
" Muswada
umeandaliwa kwa kuwashirikisha Wadau wote wa Sekta ya
Hifadhi ya Jamii, wakiwemo Wafanyakazi, Waajiri na Serikali,
ikiwemo Mifuko yenyewe kupitia Vikao vya Wadau na pia
Baraza la Ushauri wa Masuala ya Kazi Jamii na Uchumi, yaani
RESCO. Kimsingi, wadau wote waliunga mkono mapendekezo
yaliyomo katika Muswada huu."
Huyu Waziri ni muongo. Hivi lini tulishirikishwa wafanyakazi??
Nimejaribu kupita kwa haraka haraka lakini sijaona ukurasa unaozuia kuchukua hela yetu kabla ya kustaafu. Please alieona huo ukurasa naomba aniambie ili nijaribu kuupitia manake bado siamini ninachoendelea kukisikia!!
Katika hili wametusaliti. Hii issue inaathiri wengi sana. Kuna watu watalazimishwa kusubiri hadi umri wa kustaafu ambao hata hivyo hawa-qualify kwa mfano kwa kutotimiza miezi 180 ya kuchangia. How do you treat these people? Kwa umuhimu wa hili suala, hata kama wangezidiwa kwa uwingi wa wabunge wa CCM, walikuwa na wajibu wa kuujulisha umma kwenye mikutano yao kwamba walijitahidi kuzuia lakini wakazidiwa na magamba, kitu ambacho hawakufanya. Katika hili nao ni wasaliti.Nawapa benefit of doubt wabunge wa vyama vya upinzani kwa maana jinsi sheria zinavyopitishwa ("wanaoafiki waseme ndiyoo" etc) huwezi kutegemea wapinzani wasilkilizwe. Issue ni kuwang'oa magamba 2015 ili sheria za kipuuzi kama hii zibadilishwe
" Muswada
umeandaliwa kwa kuwashirikisha Wadau wote wa Sekta ya
Hifadhi ya Jamii, wakiwemo Wafanyakazi, Waajiri na Serikali,
ikiwemo Mifuko yenyewe kupitia Vikao vya Wadau na pia
Baraza la Ushauri wa Masuala ya Kazi Jamii na Uchumi, yaani
RESCO. Kimsingi, wadau wote waliunga mkono mapendekezo
yaliyomo katika Muswada huu."
Huyu Waziri ni muongo. Hivi lini tulishirikishwa wafanyakazi??
kabla hujalaumu, soma ukurasa wa 142, uone mnyika alisema nini na wewe unataka nini huku ukiuelewa mfumo wa bunge lako chini ya MAGAMBA
Kwa interest rate ya NSSF ya 1.8%, hiyo 15m baada ya miaka 25, taking into consideration the sky rocketing inflation rate, itakuwa na thamani sawa na 5k.Hii ni dhuluma ya wazi. Wanajua kwamba si rahisi kwa <60% ya Watanzania kufikia umri huo wengi watakuwa wamekufa kutokana na maisha duni wanayoishi, kwa hiyo pesa yao itafia ndani. Kama nimeacha/kuachishwakazi leo ambapo nina umri wa miaka 35, na mafao yangu ya NSSF ni milioni 15. Je baada ya miaka ishirini bila ajira, hayo mafao yatakuwa yameongezeka? Kama hayatakuwa yameongezeka, kwanini msinipe sasa ili nihangaikie kwenye biashara ambapo kiwango mtakachonipa ni kile kile hata kama ingekaa baada ya miaka mia? Zaidi sana hiyo pesa itakuwa imeshuka thamani sana tu.
Wadau nimesoma hii document na nafikiri wapinzani walifanya sehemu yao!
Ndiyo. Utalipwa riba ya 1.8%.Ngoja mimi niulize kama nikiacha kazi na miaka 35, Je mwajiri wangu ataendelea kunichangia michango yangu ya NSSF/PPF mpaka nitapofikisha miaka 55 au 60 ya kuchukua mafao yangu?
Kama mwajiri hatanichangia na pesa yangu ikaendelea kuwa ile ile, Je thamani yake itakuwaje baada ya miaka 20 nitakapofikisha miaka 55 ya kustaafu?. Taking into consideration inflation rate ya Tanzania ina stand 20% kwasasa.
Je kwa miaka hiyo 20 ambayo NSSF/PPF watakuwa na pesa yangu, mind you nitakuwa sichangii wala mwajiri hanichangii, Je nitalipwa na RIBA nitakapokwenda kuchukua mafao yangu.