Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kikao cha 7, mkutano wa 3
Kipindi cha maswali na majibu kwa waziri mkuu.
Swali: Operesheni tokomeza ilisababisha silaha za wananchi kuchukuliwa, ni lini wananchi watarudishiwa silaha zao ili kujilinda na wanyama wakali?
Majibu: Baada ya uhakiki unaofanywa na jeshi la polisi, silaha zitarudishwa kwa wahusika.
Aidha jeshi hilo linatakiwa kuharakisha uhakiki huo.
Swali: Unaonaje ukatoa maamuzi ya barabara zinazojengwa ziwekwe mitaro na makalavati?
Majibu: Ushauri umepokelewa na serikali itawasisitiza wataalam kuyaweka.
Aidha walio mabondeni wanashauriwa kuondoka.
Swali: Serikali imefikia kwa kiwango gani ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami barabara zinazounganisha mikoa hasa mkoa wa Lindi?
Majibu: Mkakati wa serikali unaendelea kwa kufanikisha mpango huo. Aidha mkoa wa Lindi tayari umeunganishwa na mikoa mingine kwa lami ispokuwa Morogoro.
Swali: Serikali imejipangaje kudhibiti maafa yanayotokana na mvua zinazonyesha hasa kwa skimu ya Igunga?
Majibu: Mkakati uliopo ni kuimarisha skimu hiyo kwa kushirikiana na wizara ya kilimo ili kuimarisha miundombinu hiyo.
Swali: Serikali kuingia mikataba ya uwekezaji bila bunge kushirikishwa, je ni chombo gani kinachotumika badala ya bunge kushughulikia mikataba hiyo?
Majibu: Tunamtumia mwanasheria mkuu wa serikali kupitia mikataba hiyo ili kupunguza muda wa bunge kupitia mikataba hiyo.
Aidha mikataba ya Halmashauri itakayoenda kwa mwanasheria mkuu ni ile inayoanza na bilioni moja, hii ni kupunguza ulimbikizaji wa mikataba kwa mwanasheria mkuu.