Kilichoandikwa na TANZANIA DAIMA la jana: DK Slaa alishinda urais kwa 64%

kama hamkumchagua Jakaya wengine tulimchagua, mtanung'unika mpaka lini
 
kama hamkumchagua Jakaya wengine tulimchagua, mtanung'unika mpaka lini
Mwisho wa manung'uniko ni kuwagonga mafisadi madarakani....na mkiendelea na ubabe basi mwisho wa manung'uniko ni damu kumwangika zaidi maana iliyo mwangika zanzibar,maswa,musoma,arusha na kwingineko mnaona haitoshi mavi ya mbwa nyie..
 
wat to do then?......hebu tupeane solution sasa baada ya ku breakisha hiz newz!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Dawa moja tu. Matokeo ya urais yatangazwe vituoni, kituo kwa kituo. Unaondoa mianya ya uchakachuaji.
 
Siku zote mtenda maovu hulipwa hapahapa duniani, na mwisho wa ubaya ni aibu. Aibu aliyonayo kikwete ni kutokana na maovu aliyoyatenda, mipango yake mingi ya kuongoza nchi hii imekwama mradi wa shule za kata unafanya vibaya, matatizo ya umeme na dowans, kuporomoka kwa uchumi, kupanda kwa gharama za maisha, migomo ya wanachuo, mabomu ya gongolamboto, ufisadi na mengine mengi yanamkosesha amani ya kuwa mwenye furaha
 
Suala sio kuiba kura tu, bali ni kwamba alipanga kuiba kura mapema. Moja ya ushahidi ni pale Shimbo alipotoa vitisho kwa watz, ili kumhakikishia Kikwete kuwa asiogope kutekeleza mpango wake wa kuiba.
 
Dk Willbrod Slaa ndiye alieshinda kwa kiti cha urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchanguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu Tanzania Daima limeelezwa.
Taarifa za kuaminika kutoka kwa vigogo wa idara hiyo ya usalama waTaifa zinasema Dk Slaa aliekuwa akiwania kiti cha hicho kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alishinda uraisi kwa kuzoa asilimia 64ya kura zote zilizopigwa kwa nafsi hiyo lakini kwa makusudi matokeo halali yalichakachuliwa kumpa ushindi Jakaya Kikwete wa chama cha Mapinduzi (CCM). Mtoa taarifa wetu kutoka ndani ya idara hiyo amelithibitishia gazeti hili kuwa mbali na kujizolea asilimia 64 ya kura zote zilizopigwa Dk slaa aliongoza kwa kupata kura nyingi kwenye mikoa 10 dhidi ya kikwete alieongoza kwa kura chache katika mikoa iliyosalia
Katika matokeo hayo yaliyovujishwa ndani ya siku tatu zilizopita inadaiwa kuwa kikwete alipata asilimia 27 tu ya kura zote zilizopigwa kwa nafasi hiyo ya urais huku asilimia 9 ya kura hizo ikienda kwa vyama vingine kikiwemo chama cha wananchi (CUF). Taarifa hizo ziliendelea kuwa matokeo ya urais yalibadilishwa katika hatua ya ujumlishaji wa kura kwenye majimbo mbalimbali ambapo pale Dk Slaa alipoongoza kwa kura nyingi sana kura hizo zilikuwa zikipunguzwa ili kukaribiana na zili za kikwete.
“unajua kura hazikuibiwa vituoni, matokeo ya vituo karibu yote yalikuwa halali. Kura ziliibiwa katika majumlisho jimboni na na kwenye majumlisho yaliyofanywa na tume.
Na walitumia udhaifu wa mawakala wa chadema katika majumuisho kuhangaikia zile za ubunge tu na kujisahau kwenye urais. Kama wangekuwa makini katika majumuisho ya urais, maeneo mengi matokeo yasingebadilishwa sana..” alisema kigogo mmoja wa usalama wa taifa kwa sharti la kutotajwa jina lake. Matokeo zaidi ya urais yanaelezwa yalichakachuliwa katika majumlisho ya mwisho ya kura nchi nzima ambapo tume ya taifaya uchanguzi (NEC), inadaiwailipunguza kura za Dk Slaa hata zile zilizokuwa zimeshudiwa kwa pamoja na mawakala wa vyama vya pinzani.
“Mfano wa majimbo ambayo kura zake zilibadilishwa dakika za mwisho na tume ni Ubungo, Musoma mjini, Mbeya mjini, Arusha mjini, Ilala, kawe, Geita, Kilombero, Moshi mjini, Tarime na Songea mjini…” Taarifa zaidi za matokeo hayo ya urais yanayodaiwa kuwa ndiyo halali na sahihi badala ya yale yaliyotangazwa na NEC, zilivujishwa na vigogo wastaafu wa usalama wa taifa ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini.
Hata hivyo, usalama wa Taifa ulikanusha vikali kuhusika katika kuchakachua matokeo ya urais mara baada ya Dk Slaa mwenyewe kutoa malalamiko yake kupitia vyombo ya habari

Haya Mods chomoeni na hii

Hii ni laana inayoitafuna nchi mpk ss!..
 
Hili halina ubishi hata Kikwete toka uvungu wa roho yake anajuwa kuwa rais aliyechaguliwa na wananchi wa Tanzania ni Dr Slaa, yeye anabaki kuwa rais wa NEC na TISS.Ndiyo maana hata siku ile anaapishwa hakuwa na amani toka ndani alikuwa anatabasamu la woga na hofu ya dhambi aliyoitenda, na dhambi hii haitamuacha salama atabaki kuwa hofu siku zote.
Ni kweli mkuu,inawezekana hofu hii ni kubwa sana kiasi kwamba akiikumbuka wakati akihutubia jukwaani hali inakuwa tete sana wote mliona kwenye tv kilichotokea tena si mara moja,aiseeee!!!!
 
Mola mtukufu mwenye mamlaka juu ya huu ulimwengu atawahukumu waongo na kuwabaini waongo.DUNIA TUNAPITA
 
Bado hamjakubali kushindwa japo mda wa alieshinda unaelekea ukingoni.
 
Back
Top Bottom