Kilichoandikwa na TANZANIA DAIMA la jana: DK Slaa alishinda urais kwa 64%

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Dk Willbrod Slaa ndiye alieshinda kwa kiti cha urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchanguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu Tanzania Daima limeelezwa.
Taarifa za kuaminika kutoka kwa vigogo wa idara hiyo ya usalama waTaifa zinasema Dk Slaa aliekuwa akiwania kiti cha hicho kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alishinda uraisi kwa kuzoa asilimia 64ya kura zote zilizopigwa kwa nafsi hiyo lakini kwa makusudi matokeo halali yalichakachuliwa kumpa ushindi Jakaya Kikwete wa chama cha Mapinduzi (CCM). Mtoa taarifa wetu kutoka ndani ya idara hiyo amelithibitishia gazeti hili kuwa mbali na kujizolea asilimia 64 ya kura zote zilizopigwa Dk slaa aliongoza kwa kupata kura nyingi kwenye mikoa 10 dhidi ya kikwete alieongoza kwa kura chache katika mikoa iliyosalia
Katika matokeo hayo yaliyovujishwa ndani ya siku tatu zilizopita inadaiwa kuwa kikwete alipata asilimia 27 tu ya kura zote zilizopigwa kwa nafasi hiyo ya urais huku asilimia 9 ya kura hizo ikienda kwa vyama vingine kikiwemo chama cha wananchi (CUF). Taarifa hizo ziliendelea kuwa matokeo ya urais yalibadilishwa katika hatua ya ujumlishaji wa kura kwenye majimbo mbalimbali ambapo pale Dk Slaa alipoongoza kwa kura nyingi sana kura hizo zilikuwa zikipunguzwa ili kukaribiana na zili za kikwete.
“unajua kura hazikuibiwa vituoni, matokeo ya vituo karibu yote yalikuwa halali. Kura ziliibiwa katika majumlisho jimboni na na kwenye majumlisho yaliyofanywa na tume.
Na walitumia udhaifu wa mawakala wa chadema katika majumuisho kuhangaikia zile za ubunge tu na kujisahau kwenye urais. Kama wangekuwa makini katika majumuisho ya urais, maeneo mengi matokeo yasingebadilishwa sana..” alisema kigogo mmoja wa usalama wa taifa kwa sharti la kutotajwa jina lake. Matokeo zaidi ya urais yanaelezwa yalichakachuliwa katika majumlisho ya mwisho ya kura nchi nzima ambapo tume ya taifaya uchanguzi (NEC), inadaiwailipunguza kura za Dk Slaa hata zile zilizokuwa zimeshudiwa kwa pamoja na mawakala wa vyama vya pinzani.
“Mfano wa majimbo ambayo kura zake zilibadilishwa dakika za mwisho na tume ni Ubungo, Musoma mjini, Mbeya mjini, Arusha mjini, Ilala, kawe, Geita, Kilombero, Moshi mjini, Tarime na Songea mjini…” Taarifa zaidi za matokeo hayo ya urais yanayodaiwa kuwa ndiyo halali na sahihi badala ya yale yaliyotangazwa na NEC, zilivujishwa na vigogo wastaafu wa usalama wa taifa ambao hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini.
Hata hivyo, usalama wa Taifa ulikanusha vikali kuhusika katika kuchakachua matokeo ya urais mara baada ya Dk Slaa mwenyewe kutoa malalamiko yake kupitia vyombo ya habari



Haya Mods chomoeni na hii
 
Hili halina ubishi hata Kikwete toka uvungu wa roho yake anajuwa kuwa rais aliyechaguliwa na wananchi wa Tanzania ni Dr Slaa, yeye anabaki kuwa rais wa NEC na TISS.Ndiyo maana hata siku ile anaapishwa hakuwa na amani toka ndani alikuwa anatabasamu la woga na hofu ya dhambi aliyoitenda, na dhambi hii haitamuacha salama atabaki kuwa hofu siku zote.
 
Big up saana kumbe mkwere anajua ye si rais ila rais in bunduki.
Ndo maana huwa haongei sana
 
Big up saana kumbe mkwere anajua ye si rais ila rais in bunduki.
Ndo maana huwa haongei sana
daah hili linaukweli hata siku ya uhuru wa Tanganyika hakutoa hatuba kabisa na sikuile ya kuapishwa hakuongea kama kawaida yake yaani ukifatilia utagundua siku hizi hachongi sana ilaelekea hana amani moyoni mwake
 
Dhuluma ni dhuluma ukidhulumu nafsi haiwezi kuwa salama! Dini zote zinakataza Dhuluma kwa hiyo kudhulumu ni kinyume cha maandiko ya Mwenyezi Mungu kwenye vitabu vyake vitakatifu maana hakuna Dini hata moja inayoshurutisha au kushabikia watu kudhulumiana. Unapokuwa umedhulumu na unajua kuwa umedhulumu halafu unaapa kwa kutumia kitabu kitakatibu kilicho kataza dhuluma hakika kiapo chako kitakuwa hakina baraka na kitakuwa unafiki mbele ya Mungu unayemtaja!

Manung'uniko ni mengi juu ya kutangazwa na tume ya uchaguzi NEC kuwa JK ndio mshindi wa uraisi. Kwa habari zilizotoka jana zinatufanya tuendelee kuamini kuwa Haki ya wananchi imenyang'anywa kwa dhuluma na ghiriba hivyo kupokwa fursa ya kuongozwa na Rais waliyempenda kupitia sanduku la kura. Hapa inatufundisha nini?! Kama dhuluma ni dhambi basi kila kura iliyoibiwa itakuwa ni dhambi kwa mwizi huyo na aliyepewa kura hiyo. Kila mwananchi aliyedhulumiwa, aliye faidi na dhuluma hiyo ana dhima mbele ya mwenyezi Mungu.

kiongozi aliyepata nafasi kwa dhuruma atapa baraka za utawala uliotukuka kutoka kwa Mwenyezi Mungu?! Kama sauti ye wengi ni sauti ya Mungu je lawama zetu na manung'uniko yetu anayapokeaje kiongozi aliyepoka dhuluma ya walio wengi? SLaa amelalamika kuwa uchaguzi ulivurugwa kwa makusudi kwa kumpendelea mgombea wa CCM. Cha kushangaza sio NEC wala Raisi mwenyewe kukanusha taarifa hizi. Tumejifunza mengi kwenye uchaguzi huu ila inatosha kusema uongozi wa DHULUMA usio kuwa na BARAKA za wengi kwa kuwanyang'anya haki zao ni uongozi usiompendeza Mungu na hakika dhambi yake haita iweka salama nafsi ya Mtu huyo kwa kuwa aliapa kwa kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu.

Naomba kuwasilisha.
Mtoi
 
Ukweli unabakia pale pale sisi hatukumchagua JK kuwa Raisi wetu.....sasa hii nchi anaiongoza kwa ridhaa ya nani?
 
Whether TDaima ni la chadema au lah ukweli ni kuwa JK hajapita kihalali ata yeye mwenyewe analijua ilo
 
Ukweli unabakia pale pale sisi hatukumchagua JK kuwa Raisi wetu.....sasa hii nchi anaiongoza kwa ridhaa ya nani?
Mkuu hili liko wazi kabisa kuwa JK anaongoza nchi hii kwa ridhaa ya Usalama wa Taifa na vibara wake....tutamfanya nini? na katiba ndiyo hiyo inasema rais hapingwi kokote
 
Watawezaaa kulishitaki?
yaani kitendo cha kulishitaki mimi naona itakuwa burundani kwa sisi walala hoi maana tutapata na yaliyojificha....yaani nikitendo cha kumchukua kichaa halafu ukamfungia kwenye nyumba ya vioo na huku ameshikilia rungu.....
 
Mmoja anasema Tanzania Daima ni la CHADEMA, nimtake radhi kama haelewi kiingereza kwani naomba asome usemi huu "Anyone who walks into a church becomes a christian, Does also walking into a garage make you a car"?Muhimu ni Concept sio hisia kwa sababu Baba yangu ni mhindi wa Indepence street lazima niwe na fedha.
 
Jaji Makame hasiishie kunungunika, ili kukata mzizi wa fitina aishauri serikali kuunda tume huru ya kuhakiki kura zilizopigwa kwa kila upande.
 
Hizi habarii zina mshtuko mkubwa sanaa.........naogopa kuzitafakurii maana zinatisha...kuna docs zinapitishwa mtandaoni....kuonyesha kiwkete amepata 44.31 na Slaa amepata 44.26 sasa sijajuaa kama kweli ama la.....mikoa wamegawana JK ana 11 Slaa ana 10
 
Hili halina ubishi hata Kikwete toka uvungu wa roho yake anajuwa kuwa rais aliyechaguliwa na wananchi wa Tanzania ni Dr Slaa, yeye anabaki kuwa rais wa NEC na TISS.Ndiyo maana hata siku ile anaapishwa hakuwa na amani toka ndani alikuwa anatabasamu la woga na hofu ya dhambi aliyoitenda, na dhambi hii haitamuacha salama atabaki kuwa hofu siku zote.
Hata sasa ana hofu. Angalia tu alivyoongeza safu ya walinzi. Ahahahahahahahaha
 
Jakaya hakuwahi kushinda. Nimeshangaa nilipogundua kuwa hata zile nilizozisimamia mimi na mgombea wa Chadema akashinda kwa kura nyingi nilishangaa kuona badala yake alionekana kamshinda kwa tofauti ya kura kidogo. Kikwete aliiba kura sio siri na yeye anajua.
 
Back
Top Bottom