kilicho sababisha wizi wa shaba bandarini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kilicho sababisha wizi wa shaba bandarini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanewi, Sep 13, 2012.

 1. k

  kanewi JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 214
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Mwezi mmoja kabla ya kurudi bungeni kukamilisha vikao vya bajeti mh.mwakyembe(MB)ailikutana na wafanyakazi wa TAzara katika kipindi ambacho hawana mishahara ya miezi mitatu,waziri kwa kauri yake akawaahidi wafanyakazi wale kuwa atawapa mishahara miwili na ikiwezekana na watatu.

  Mbele ya wafanyakazi wale akawaahidi kuwa atashughulikia kero zote zinazohusu uongozi ndani ya uwezo wake kisheria na kuzungumza na waziri mwenzie wa zambia ili mengine yanayohusu mashauriano wajadiliane,.pia akawaomba wafanyakazi wale pamoja na kutokuwa na mishahara hiyo wafanye kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na special task ya kukarabati mabehewa yatakayo tumika kwenye town train.

  Mwanamama mmoja alipagawa na ahadi ile kwani hakuamini.. Mwakyembe akashangiliwa kwa mbwembwe sana na vifijo ikafikia kila mfanyakazi akaona kama huyu ndo waziri kuliko wote waliowahi kutokea,.siku,mwezi,miezi ikakatika,.vipi mhsahara wa mwakyembe? wakajiuliza wafanyakazi wa tazara,ikadiliki wengine kusema kuwa ahadi ile aliitoa kwa sababu ya hofu ya kutokukarabatiwa kwa mabahewa yake,.wafanya kazi njaa ijawavuruma,wengine wakafukuzwa kwenye nyumba za kupanga,wengine wakaachwa na wake zao wengine watoto walio kuwa shuleni wakafukuzwa,.mazingira yaliandaliwa na waziri kwa sababu njaa hile iliwafanya wafanyakazi wasio na uwezo wa kustahimili wakaona kilichopo mbele kinaweza kuondoa njaa ila hili liko wazi(mtu mwenye njaa ni rahisi sana kurubuniwa kuiba kuliko asiye na njaa)kilio hiki mwakyembe alikipata pia.

  Ikumbukwe pia kamati ya miundo mbinu ilipokaa kabla ya bunge ndani ya ukumbi wa TAZARA wakati wanajiandaa kwenda bungeni kwenye bajeti,walielezewa tatizo la mishahara ya wafanyakazi kukosa kwa miezi mitatu na kuendelea,mwenyekiti wa kamati mh. mama Malechela alitamka ndani ya kamati na uongozi mzima wa tazara kuwa,namnukuu:"hivi mtu akiiba kwa hari hii mtamlaumu?",kauri hii ilibezwa na waziri pamoja na naibu wake,.

  Ndo tunayaona sasa na kiukweri si kama wizi haufanyiki ndani ya hii mamlka kwani wafanyakazi wanaishije??wizi unafanyika kila kukicha na kila mtu anaiba kwenye nafasi yake ili aweze kuishi sema tukio lile limekuwa ZA MWIZI AROBAINI,.naomba waraka huu umfikie mwakyembe kwa aliekaribu nae na amuambie kuwa wizi huu yeye ndo muandaa mazingira kwa kutokutimiza ahadi zake wakati wafanyakazi walimuita na kumuelezea kilio chao,.
   
Loading...