Juzi tarehe 14 Mei,2016 Maalim Seif alitua Pemba na kupokelewa kishujaa katika historia ya siasa za Zanzibar. Wafuasi walijipanga njiani wakitokea maeneo mbali mbali. Shangwe hizo si za kawaida kwa waliobahatika kuona video yake.
Masuali ni mengi yaliyopo katika ziara yake hii ya siku nne
Wengine wanasema anajifariji na kuhuisha matumaini ya wafuasi baada ya kupoteza mchezo kwa kukubali kususia na kuwaacha CCM wakijifaragua peke yao na wao kuwa nje ya utawala kwa miaka mengine mitano
Wengine wanasema ni mwanzo wa mapambano na kudai haki yao iliyoporwa tarehe 25 Oktoba, 2015
Wengine wanafika mbali kwa kusema anahamasisha uasi kwa dola ili isusiwe na wananchi na hatimae kuuangusha utawala wenyewe wanaouita Batili. Hili limekuwa likichagizwa na kauli zake mwenyewe.
Nguvu za Maalim
Kwa ukweli kama kuna watu walifikiri wafuasi wake wamekata tamaa kwa kile kilichotokea basi wamepotea. Kinachofanyika kule Pemba katika ziara yake ni mshangao na watawala hawaaamini. Ana heshima zote na utii wa hali ya juu. Ana umati mkubwa na hamasa sana.
Hili la ziara yake ni tumaini kwa wafuasi.
Kauli tata.
Kutaka wananchi wasiipe ushirikiano SMZ kwa sababu ni batili na wasusie hata kodi . Hii ni kwa mujibu wa baadhi ya vyombo vya habari taarifa za tarehe 16 na 17 Mei, 2016
Yeye mwenyewe kujiita rais na wafuasi wake kuamini hivyo.
UPANDE WA DOLA
Licha ya kile kinachoendelea bado dola inaruihusu kiongozi huyu kuendelea na ratiba zake na bado harudi nyuma. Uzoefu wetu viongozi wa upinzani hupata shida sana kuruhusiwa kufanya ziara za aina hii bila kubughudhiwa lakini hii ni tofauti.
Maswali.
Kuna nini nyuma ya ziara hii na yale yanayojitokeza wana Jf leteni ufafanuzi wenu.
Hivi kwa anachokifanya maalim ni kuwa dola inamgwaya na kumuona ameisha au kuna kitu wanakihofu juu yake?
Ukifuatilia utagunduwa wafuasi ni kama vile wana tumaini fulani. Kwa hali ya mambo ilivyo ikiwa tayari serikali imeundwa, Baraza la wakilishi linaendelea na kazi zake inawezekana kweli kukawa na tumaini la kupatikana haki ya CUF kama wanavyosema viongozi wao?
Kwangu mimi safari hii ni zaidi ya safari.
Nachelea muda.