Kilicho nyuma ya madaktari kuomba radhi ni maagizo toka juu

Ningekuwa serikali ningelipa hawa madaktari matapeli laki moja tu kwa mwezi.
 
Anaye wasema vibaya madaktari ni kilaza, tena anafikiri kwa kutumia masabuli ya chadem. Daktari yeyote ni mtu msomi, anaona mbali, sio vilaza wanaoona mwisho wa vidole vyao vya miguu. Hakika madaktari walilofaoya ndio uungwana.
Kuhusu chadema kuwa nyuma ya mgomo ule wa madaktari, ilikuwa wazi hata ktk shughuri za bunge, wabunge wa chadema walitokwa mishipa kusapoti mgomo.

Mkuu SUPERXAVERY, seriously??
 
wamepewa shilingi ngapi kutoa tamko la kisaliti namna hiyo..na tusiwasikie tena wakilialia..njaa bwana



Unafikiri hata wamepewa hela basi? Mimi nina mdogo wa jamaa yangu na yeye ni muathirika wa mgomo huu(Intern) amepauka uraiani sasa hivi kutwa kutupiga mizinga tu.Hawa madogo hawakufikiria vizuri kuwa wenzao madaktari wanamishemishe mjini na wameshakuwa certified wao wakakurupuka tu. wapo mtaani wamepauka kama muhogo wa kuanikwa.
 
Ni usanii mwingine wa serikali na chama tawala CCM. CHAKUSIKITISHA NI KWAMBA BAADHI YA MADAKTARI WAMEAMUA KUWASALITI WENZAO KWA KUSHAURIWA NA SERIKALI,WAMEWASALITI AMBAO WALIKUA KARIBU KUPOTEZA MAISHA YAO(DR. ULIMBOKA),WAMEWASALITI WATANZANIA NA WAMEISALITI DHAMIRA YAO,WAMEISALITI HESHIMA YAO.SASA NIMEAMINI TANAZIA SERIKALI NA CHAMA TAWALA KINAWEZA CHAKACHUA MPAKA AKILI ZA WATU TUNA SAFARI NDEFU KWENDA KWENYE UKOMBOZI!!!!!!!!!.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
mwenzenu kitu kilichonishangaza ni kuwa,viongozi wa madaktari waliotangaza na kusimamia mgomo sio hao walioomba msamaha na kuapa kutogoma tena!!

"TISS AT WORK"
 
Unafikiri hata wamepewa hela basi? Mimi nina mdogo wa jamaa yangu na yeye ni muathirika wa mgomo huu(Intern) amepauka uraiani sasa hivi kutwa kutupiga mizinga tu.Hawa madogo hawakufikiria vizuri kuwa wenzao madaktari wanamishemishe mjini na wameshakuwa certified wao wakakurupuka tu. wapo mtaani wamepauka kama muhogo wa kuanikwa.

Mkuu MWILI NYUMBA, hata hawa "madogo" yet wangeweza kufanya hizo mishemishe hapa mjini, kwani wengine wanapataje??..issue ni kwamba wanataka wasijishughulishe eti waitwe?! seriously?..nchi hii hii, uitwe?
..na issue nyingine walipaswa kujua kwakuwa wako nje kikazi(hospitalini).. wangefanya mishemishe hizo, ili kuwaweka mjini, si kwa mshahara sawa wakiokuwa wanaupata, ila hata pungufu yake..tatizo dharau, ooh! mimi chini ya ule niliyokuwa naupata kazini, sitaki!! sasa hii ndio shida ya kuwa maskini JEURI.
 
JK hoyee! JK Hoyee, safi sana JK, walijaribu madaktari wameshindwa, wamejaribu walimu wameshindwa, nani sasa ataweza? JK hoyee![/QUOTE]

Wewe unaemshangilia Kikwete uwezo wako wa kuona unaishia mita 20. We unafikiri mgomo umeisha? nenda mashuleni uone, angalia kama kuna mtu mwenye uwezo wake kama anapeleka mtoto shule za serikali? Walimu na madaktari wamehamua kutulia kwa sababu serikali ni jeuri na haitikisiki hata kama huduma ni mbovu. Tazama Kenya wanavyojali wananchi wao, madaktari wanagoma na wanasikilizwa. Mungu akusamehe maana ujui unachoshangilia
 
Je kazi itafanyika?????jaman kwa sasa muhimbili bila chochote ndugu yangu leo anafanyiwa operation,ila baada ya kitu kidogo kutoka,wapo waliokaa zaid ya mwez
 
Kama wamelazimishwa kuomba radhi, wataomba na kurudi kazini, lakini yaliyomo miyoni mwao tutayaona wakati wakitoa huduma.
 
Jamani msiwalaumu hawa madokta wetu tatizo njaa, maintern wapo vijiweni hawaruhusiwi hata kuajiriwa na private sekta mnategemea nini lazima tu watakubali yaishe, kweli adui yako mwombee njaa.
 
nlijua hili hawajakurupuka kuomba msamaha
na waliomba ni hawa interns bwana wadogo
hawana msimamo na hawa.
ila kuwahusisha chadema ni sawa na kumdanganyia mtoto pipi
ni ujinga na uendawazimu kuwahusisha ili kukichafua chama makini
chadema ndio walioratibu pia mpango wa kumteka Ulimboka nadhani ndio walivosema pia
 
Jamani msiwalaumu hawa madokta wetu tatizo njaa, maintern wapo vijiweni hawaruhusiwi hata kuajiriwa na private sekta mnategemea nini lazima tu watakubali yaishe, kweli adui yako mwombee njaa.

Mkuu whistle blower, sikubali na wewe katika hili, with varieties of courses daktri alizosoma kuanzia first year anaweza kupata ajira sehemu nyingine pia, ISIPOKUWA HOSPITALINI, unaweza kwenda kufanya even your Internship katika private sector, lakini ugumu ni kwamba ukisha ajiriwa sehemu moja, huwezi fanya sehemu(hospitali) nyingine, ..unless umesajiliwa(registrar, specialist, consultant specialts nk).

Tatizo ni kwamba hawa intern doctors hawakuwa na moyo wa subira, mambo mazuri hayataki haraka Mkuu, ni wazi Serikali ilipata pigo(doa kisiasa, kitaifa, nk) lakini pia hata wao walipata pigo in the same measure(kuwa mitaani)...as an alternative, walitakiwa kufanya kazi sehemu zingine(tofauti na hospitali) kwa kuwa cheti kinaruhusu hadi pale mambo ambapo yangekuwa sawa kisheria, lakini kiburi(hawawezi kujidhalilisha kufanya kazi za "chini" matokeo yake ndiyo haya.)
 
Back
Top Bottom