Kilicho ndani yako ni kikubwa, kuliko maisha unayoishi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilicho ndani yako ni kikubwa, kuliko maisha unayoishi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jun 28, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  [h=2]Kilicho ndani yako ni kikubwa, kuliko maisha unayoishi![/h] Wednesday, June 1, 2011
  [h=3][​IMG][/h] [h=3]Bwana Yesu apewe sifa, Mungu alivyoweka ndani yako ni vikubwa kuliko maisha unayoishi, Mungu ametuumba kwa mfano wake, amepuliza pumzi yake kwetu ili tuishi na kutembea kama watu wanaotoka kwenye ufalme wake.[/h] [h=3]Unaishi maisha ya taabu, magonjwa, huzuni, kulia sana, kukataliwa na kukosa matumaini. Mungu hajaviweka hivyo vitu ndani yako adui amevipanda JUU yako ili usione na kutafakari yaliyo NDANI yako, ameweka pazia kuubwa usione mbele, amefunga ufahamu wako, usitambue na kuuona mpango mzuri, Mungu aliokupangia kabla haujazaliwa, kabla ya misingi ya ulimwengu haijawekwa. Fumbua macho yako uone kilicho NDANI yako![/h] [h=3]Umejaa uzima, umejaa ujuzi na maarifa, umejaa mafanikio, wewe umeumbwa tofauti kwa jinsi ya ajabu na kushangaza Zaburi 139:14. Umeumbwa ili ufanikiwe kila jambo, Shetani ni simba anayeunguruma na kukutisha kwa yale unayopitia, anakufanya usione kusudi la Mungu kwenye maisha yako. Usijione kama panzi, usijione haufai,Wewe ni wa thamani mno! Basi mshangilie Mungu kwa ajili ya vitu ameweka ndani yako, kwa ajili ya uzima, karama na vipaji vilivyo ndani yako, changamka sasa! Ukachipuke kwa jina la Yesu.[/h]
   
Loading...