Kilicho muua Malcolm X hiki hapa

kwahiyo na unasapoti kua waliomuua malcom x walifanya vizuri? au umetoroka milembe RIP MALCOM X.
 
kwahiyo na unasapoti kua waliomuua malcom x walifanya vizuri? au umetoroka milembe RIP MALCOM X.

No one killed Malcolm X He killed himself by his own teachings
 
485595_607560952597131_723057490_n.jpg
 
kawadanganye wengine siyo mimi kwa malcom x juha mkubwa.


Elijah-Muhammad-9417458-1-402.jpg

Elijah Muhammad told the annual Savior's Day convention on February 26, "Malcolm X got just what he preached", while denying any involvement with the murder.[SUP][182][/SUP] "We didn't want to kill Malcolm and didn't try to kill him", Muhammad said. "We know such ignorant, foolish teachings would bring him to his own end."



Haya ni maneno ya Elijah Muhammad. Kiongozi na muasisi wa National Of Islam ( NOI). Huyu ndiye aliyemkaribisha MALCOLM X kwenye harakati na hayo ndio maneno aliyoyasema baada ya kifo cha Malcolm. Ingekuwa kibongo bongo halafu miaka hii ingesemwa " Alicho kisema Elijah Muhammad kuhusu kifo cha Malcolm X ". Anyways siko hapa kumdanganya mtu, i was just sharing this information. It must be useful to some
 
“Moja ya vitu ambavyo ningependa vijana wajifunze siku hizi, ni kujiona wao wenyewe, kujisikiliza wao wenyewe, na kufikiria wao wenyewe. Na hapo ndio wataweza kufikia uamuzi wa busara kwa ajili yao wenyewe.”
Malcolm X akiongea na vijana wapigania haki zao huko Mississipi (1965).
“Hata wale wamchukiao wanaelewa uerevu wa akili zake- sio wa kawaida, hautabiriki na wa kipekee…”
Kuhusu Malcolm X katika gazeti la The New York.
Malcolm X alizaliwa kama Malcolm Little Mei 19, 1925 huko Omaha, Nebraska. Baba yake, Earl Little alikuwa mchungaji asiyeogopa kusema ukweli, na pia alikuwa msaada mkubwa sana wa kiongozi wa harakati za Weusi (Black Nationalist) wakati huo wa Marcus Garvey. Malcolm X alilelewa katika imani ya kisabato na mama yake.
Maisha ya Malcolm mwanzoni yalikumbwa na masaibu mengi. Kwa mfano, mwaka 1929 nyumba yao iliyopo Lansing, Michigan ilichomwa moto na kundi la wazungu lenye chuki; akiwa na umri wa miaka sita tu wakati baba yake alipokufa katika kifo kibaya sana; mama yake akawekwa katika hospitali ya watu wenye matatizo ya akili (mtindio wa ubongo); akachukuliwa kwenda kulelewa katika vituo vya kulelea watoto wasio na uwezo; mwalimu wake alivunja ndoto zake za kuwa mwanasheria, alimwambia kazi hiyo haiendani na maniga (weusi), akamuusia awe fundi seremala akimsisitiza hata Yesu alikuwa seremala. Akaacha shule japokuwa alionesha ana uwezo mkubwa wa akili; akatumia muda wake mwingi Boston, Massachusetts kufanya kazi za ajabu ajabu; japokuwa kazi yake ya mwanzo ilikuwa kung’arisha viatu; akasafiri kuhamia Harlem, New York ambapo akafanya uhalifu sana; kabla ya mwaka 1942, alikuwa mwongozaji vikundi vya madawa ya kulevya, umalaya, ukahaba, na kamari; na ilipofika mwaka 1946, alihukumiwa kwenda jela kwa miaka 10 kutokana na kukutwa na kosa la ujambazi (wizi wa kutumia silaha).
Malcolm X alijiongezea elimu yake wakati yuko jela. Ilikuwa humo humo gerezani ndio ambapo aliimeza Dictionary (aliihifadhi kichwani kamusi ya kiengereza yote), alisoma Biblia na kila kitu kuanzia somo linalohusu mabaki ya kale (Archeology) mpaka Somo la Uzazi na Kurithiana (Genetics). Wakati yupo humo gerezani, Malcolm akafata imani ya Waislam weusi na baada ya kuachiwa kutoka gerezani, akawa mjumbe katika Chama cha Waislamu Weusi (Nation of Islam) na kuchaguliwa kuwa msemaji wao. Nation of Islam ni kundi lilolopotoka linalojinasibisha na Uislamu. Alijitoa toka katika Nation of Islam mwaka 1964 na kuanzisha kikundi kingine kiitwacho Muslim Mosque, Inc na pia akaunda Chama cha Umoja wa Wamerika Weusi (Organization of Afro-American Unity), kundi ambalo linatetea uzalendo wa watu weusi. Baadhi ya Waislamu wa Kisunni walimuusia sana Malcolm kuusoma Uislam wa kweli. Malcolm X alikubali ushauri ule ambao ukamfanya ajiengue kutoka katika Nation of Islam na baadae kukiri:
“Katika chuo kimoja ambapo nilipita kuongea katika mikutano isiyo rasmi, wengi kati ya watu weupe wamekuwa wakinifuata wakijitambulisha kama waarabu, wa Mashariki ya Kati, au wanatoka kaskazini mwa Afrika na wapo hapa kimasomo, kikazi au wengine wana makazi ya kudumu. Wakawa wananiambia pamoja na maneno yangu ya kuwachukia wazungu, ni kweli sikosei ninavyojichukulia kuwa ni Muislamu lakini walihisi niusome vizuri Uislamu, nitauelewa na kuukubali. Kama mfuasi wa Elijah (kiongozi wa Nation of Islam), nilikasirishwa na walichokuwa wakikisema. Lakini baada ya hali hii kujirudia kwa muda, nikajiuliza mwenyewe, kama kweli mtu yuko kidhati katika kuitangaza na kuifata dini hii, iweje mtu arudi nyuma katika kujiongezea maarifa ya kuijua dini hiyo zaidi na zaidi?”
Mmoja wa hao Waislamu waliojitolea alikuwa Dkt. Mahmoud Youssef Shawarbi ambae nae aliongozwa na kauli ya Mtume “Mmoja wenu hawezi kuamini mpaka ampendelee mwenzake kile akipendacho.”[1] alimshauri Malcolm kuukubali Uislam wa kweli. Baadae Malcolm alifunga safari kwenda kuhiji Makkah ambapo aliugundua Uislam wa ukweli na akawa Muislam wa Kisunni akatoa shahada upya (mwenyewe) na kubadili jina lake kuwa Al-Hajji Malik Al-Shabbazz. Malcolm alikuwa na furaha baada ya kukamilisha Hijja yake akisema amefurahi kuwa mweusi wa kwanza kwa wazaliwa wa Marekani kuhijji. Siku zake za kuhiji zilileta mabadiliko kuhusu msimamo wake wa kuchukia weupe. Akasema:
“Kulikuwa na makumi ya elfu ya mahujaji kutoka sehemu mbalimbali Duniani, walikuwa watu wa rangi zote, kuanzia wale wazungu wenye macho ya rangi ya samawi mpaka Waafrika Weusi. Lakini wote tulikuwa tukishiriki katika ibada kuonesha imani ya mshikamano na umoja ambayo katika maisha yangu ya Marekani sikuwahi kuota kuwa itawezekana…Marekani inapaswa kuufahamu Uislam, kwa sababu hii ndiyo dini iliyoondoa tatizo la ubaguzi wa rangi katika jamii wakati dini hii iliposhushwa. Katika kuzunguka kwangu katika mataifa ya Waislamu nimekutana, nimeongea na hata kula pamoja na watu ambao Marekani walikuwa wakichukuliwa ni weupe (wazungu).- lakini kwa hawa ile tabia chafu ya kibaguzi ya uweupe imeondoshwa katika fikra zao kutokana na Uislamu wao. Sijawahi kuona kabla, upendo huu wa dhati ambao unatekelezwa bila kuzingatia tofauti zao za rangi.”
Wakati akiwa Hijja, aliandika barua kwa wasaidizi wake wa chama chake kipya (Muslim Mosque) kule Harlem na kuwaomba wazisambaze kwenye vyombo vya habari. Aliandika:
“Sijawahi kushuhudia ukarimu mkubwa na roho ya undugu wa kweli kama niliouona, ule wa rangi zote katika ardhi takatifu, nyumba ya Ibrahim, Muhammad na mitume wote waliopita. Kwa wiki nzima sikuwa mzungumzaji ila ni kushangazwa tu kwa yale mapenzi yalioneshwa kwangu na wale watu wenye rangi tofauti….najua mnaweza kushangazwa na maneno haya yanayotoka kinywani mwangu. Ukweli Hijja hii, imenilazimisha kubadili fikra zangu nilizokuwa nazo mwanzoni na sasa nimeamua kutumia upande mwengine wa shilingi kwa baadhi ya mambo niliyokuwa nayaamini. Hili halijakuwa gumu kwangu. Japokuwa nimekuwa nikiiamini imani yangu kidhati, siku zote nimekuwa mtu mwenye kujaribu kukumbana na ukweli, na kuukubali uhalisia wa maisha. Siku zote nimekuwa ni mwenye kukiwacha kichwa changu wazi ili kiweze kwenda mkono kwa mkono na utafutaji mzuri wa ukweli. Katika kipindi cha siku hizi kumi na moja zilizopita, nimekula chakula kutoka katika sinia moja, nimekunywa kwa kutumia bilauri moja, na nimelala katika sehemu moja –huku tukiabudu kuelekea kwa Mungu mmoja, pamoja na Waislamu wenzangu, ambao macho yao ni ya rangi ya kisamawati, wenye nywele zenye umanjano, na wenye ngozi yenye weupe pe! Ila kwa maneno na matendo ya Waislamu hawa weupe, nimejihisi kama niko pamoja na wenzangu (Waislamu weusi) kutoka Nigeria, Sudan na Ghana. Kwa kweli kila mtu alikuwa kaka wa kweli kwa mwenzake, kwani ile imani ya kuabudia Mungu mmoja imeondoa kule kujiona kutoka vichwani mwao, kutoka tabia zao na hata kutoka katika hulka zao. Nimeona kweli kama wazungu wa Marekani wangekubali kuabudia Mungu mmoja basi bila shaka wangekubali umoja wa binadamu pia kuepuka kuwadhuru wenzao kwa sababu ya tofauti ya rangi tu. Kwa ubaguzi huu unaoenea Marekani kama saratani isiyo na tiba, tulitegemea wale wazungu wanaojiita wana mioyo ya kristo basi wangelivalia njuga tatizo hili kwa kufanya harakati za kulitokomeza. Huu ndio ulitakiwa uwe muda mahsusi wa kuiokoa Marekani kutokana na janga hili kubwa – janga lililoimaliza Ujerumani baada ya kuwamaliza Wajerumani wenyewe. Waliponiuliza kuhusu lipi lililokuvutia katika Hijja nikajibu ni huu udugu wa kweli, watu aina tofauti, wenye rangi tafauti, tokea maeneo tofuati duniani wanakuja kukaa pamoja na kuwa kitu kimoja! Kwa kweli jambo hili limenionesha nguvu za Upekee (U-moja) wa Mungu. Wote tumekuwa tukila kimoja, tukilala sehemu moja, kila kitu tulikifanya kwa pamoja katika kumuelekea Mungu mmoja.”
Malcolm X akarudi kutoka Hijja akiwa mtu tofauti, akiwa yuko katika silika yake ya asili kama alivyo mtoto asiye na dhambi hata kidogo, kabla ya kubadilishwa na mazingira. Mtume wa Uislam, Muhammad (Swala llahu Aleihi Wasalam) amesema, “Yule anayekuja kwenye nyumba ya Mungu (Kaa’ba) akiwa na niya ya kuhiji na asiwe mwenye kusema au kutenda ovu, basi atarudi akiwa kama mtoto mchanga aliyetoka kwa mama yake muda mchache uliopita.”[2]. Kutokana na hivyo, kule kuchukia weupe kwa Malcolm-X kulisafishwa baada ya kujifunza Uislamu huu wa kweli.
Na tarehe 27 Disemba 1964, Malcolm alisema, “Nadhani hii ndiyo sababu kwanini Uislamu unaenea siku hadi siku. Uislamu hauna ubaguzi wa rangi hata kidogo katika mafundisho yake. Hakuna mafundisho yanayokutaka umhukumu mtu kwa rangi yake. Hata uwe na rangi gani katika Uislamu, utabaki kuwa Muislamu na utabaki kuwa ndugu yetu.”
Malcolm alibahatika kutembelea maeneo tofauti tofauti ulimwenguni na kukutana na watu mbali mbali wenye haiba kubwa. Miongoni mwa nchi alizotembelea ilikuwa ni Saudia Arabia ambapo alikutana na Muhammad Faisal; mjukuu wa mfalme; Ghana ambapo alikutana na Kwame Nkurumah, Misri ambapo alikutana na Gamal Abdel Nasser; Aljeria na kukutana na Ahmed Ben Bella, kiongozi mkuu wa mapambano ya Aljeria dhidi ya wakoloni Wafaransa, na alikuwa waziri mkuu wa mwanzo wa Aljeria (1962-63) na akawa rais wa kwanza (1963-65). Pia, Malcolm alitembelea Nigeria ambapo akafanya muhadhara mkubwa chuo kikuu Ibadan. Nchi nyingine ni Ethiopia, Tanzania, Guinea, Sudan, Senegal, Ufaransa, Liberia na Morocco. 21 Sept 1960, Malcolm alikutana na Fidel Castro katika hoteli ya Theresa, Harlem. Tarehe 3 Disemba mwaka wa 1964, Malcolm alikuwa Uingereza akishiriki mdahalo, Oxford. Yeye akawa upande wa kutetea kichwa cha mdahalo kilichobeba ujumbe “Siasa Kali (isiyo na kadiri) Katika Kuutafuta Uhuru Sio Kosa, na Siasa Poa (mwendo wa kiasi) Katika Kutafuta Haki Siyo nzuri.” Kwa Kiengereza kichwa cha mdahalo ni “Extremism in the Defense of Liberty is No Vice; Moderation in the Pursuit of Justice is No Virtue” Na mdahalo huo ulirushwa na televisheni kwa taifa zima na BBC. Katika mdahalo, Malcolm X alijitamba kwa fakhari kabisa, “Uislamu ni dini yangu, namuamini Allah, na namuamini Muhammad.”
Akiwa anafanya muhadhara katika ukumbi wa Manhattan 21 Februari 1965, washika mitutu watatu walimsogelea Malcolm karibu na jukwaa na kummiminia risasi 15. Malcolm akiwa na miaka 39, alitangazwa ameshaaga dunia mara tu mwili wake ulipowasili katika hospitali ya kidini ya Columbia, New York. Akazikwa katika makaburi ya Ferncliff huko Hartsdale, New York. Ossie Davis (1917-2005), mwigizaji na mwongozaji filamu wa kimarekani, mshairi, mwandishi na mpiganaji wa haki za binaadam, alitoa hotuba katika msiba huo wa Malcolm X, aliyeipa kichwa “Mwanamfalme Mweusi Aliyeng’aa”:
“Kuna wale watakaotufunza kumchukia na kutomkumbuka. Watakaotufunza kujinusuru kwa kutomuandika katika zamu zetu hizi. Wengine watauliza ni lipi mnalojivunia kwa kiumbe huyu mwenye hasira, mtukutu, mtata, na jeuri na sisi tutamuangalia tukitabasamu. Wengine watasema – jiupusheni naye kwani hakuwa binaadamu bali ni shetani, katili, mchochezi maovu na adui wa watu weusi pia na huyu tutamuangalia na kutabasamu. Watamwita mbaguzi, mwenye chuki, mtu ambaye ataharibu tu katika harakati zenu za kujikwamua! Tutajibu kwa kusema: Walishawahi kuongea kweli na Malcolm? Walishawahi kumgusa? Walishawahi kumsogelea na kupata tabasamu lake? Hivi walimsikiliza kidhati kweli? Je alishawahi kufanya hayo mnayomzulia? Je kweli kashawahi fanya lolote lenye hila? Na je ni kweli alijihusiha na ugomvi au vurugu zozote? Kwa maana hiyo kama hukumjua basi jaribu kumjue. Na kama ungemjua basi ungeelewa kwanini tunamkumbuka na kumuheshimu.”
Dkt. Martin King wa pili, alishtushwa na taarifa za kifo chake. Martin aliandika:
“Hatukuiona njia ya jicho kwa jicho kama njia ya kuondoa tatizo la ubaguzi wa rangi, lakini siku zote nimekuwa nikimuona Malcolm kama mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuweka kidole chake pale kwenye mzizi wa tatizo. Alikuwa ni mzungumzaji mzuri sana kwa yale aliyoaamini, na hakuna atakayediriki kukataa kuwa Malcolm alikuwa akiumizwa sana na matatizo ya rangi yaliyokuwa yakitupata.”
Vyombo vya habari kutoka mataifa mbalimbali vilijawa na simanzi nzito kwa kuondokewa na mtetezi na mwanaharakti huyu mkubwa mwenye asili ya Afrika katika historia ya Marekani. Mathalan, The Daily News of Lagos, Nigeria liliandika, “Malcolm X alijitolea na kuwa na msimamo katika harakati za kujikwamua na ubaguzi kwa ajili ya ndugu zake na hakuna anayepinga hilo…alipigania na kufa kwa kile alichokiamini. Bila shaka atapata nafasi yake katika jumba kubwa la mashahidi.”
Waislamu hawaoni kauli yenye kumpa heshima Malcolm X kuliko aya hii ya Qur’an:
“Wala msiseme kuwa wale walio uwawa katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni maiti; bali hao ni wahai, lakini nyinyi hamtambui.” [Q 2:154].
Marekani, picha ya Malcolm imekuwa ikitumika katika stempu za posta. Na shule nyingi, mitaa, na barabara zimekuwa zikipewa jina lake kwa ajili ya kumkumbuka. Baadhi ya vyuo na shule hizo ni Malcolm X Community College huko Chicago, Malcolm X Liberation University ya Durham, N.C, The Malcolm X Society, Malcom X Shabazz High School iliyopo Newark, New Jersey, Malcolm Shabazz City High School nayo iliyopo Madison, Wisconsin; mtaa wa Reid uliopo Brooklyn, New York ulibadilishwa na kuwa Malcolm X Boulevard; mwaka 2005 chuo kikuu Columbia kilitangaza ufunguzi wa kituo cha elimu walichokiita Malcolm X and Dr. Betty Shabazz Memorial and Educational Center. Afrika ndio kawaida kabisa kuona mabasi yameandikwa Malcolm X au watu wamevaa fulana zenye picha yake. Hayo yote tisa, kumi; Malcolm X alijitolea kusambaza Uilslamu sio tu Marekani bali kwa wote dunia nzima. Kutoka kwake katika kundi lililopotoka la Nation of Islam na kuingia katika Uislamu sahihi kuliacha athari hadi kwa mtoto wa Elijah Muhammad, Wallace Muhammad ambae baada ya kifo cha baba yake alikiongoza chama cha Nation of Islam kufuata yale aliyofanya Malcom kwa kufuata Uislamu sahihi. Na kwa kweli, kitabu cha historia yake “The Autobiography of Malcolm X” kimewafanya wengi waingie katika Uislamu.
Malcolm X alioana na Betty X (aliyezaliwa kama Betty Sanders) maeneo ya Lansing, Michigan mwaka 1958. Walikuwa na watoto wa kike sita, Atallah Shabazz aliyezaliwa Novemba 1958, Qubilah Shabazz (Disemba 1960), Ilyasah Shabazz (Julai 1962); Gamillah Shabazz (Julai 1964) na mapacha Malaak na Malikah Shabazz waliozaliwa baada ya kifo chake Septemba 1965.
Mwanahistoria Robin D.G Kelley aliandika:
“Malcolm X kashaitwa majina mengi: mwanaharakati wa weusi, baba wa taifa la weusi, mdini, msiri, mjamaa, na kitisho kwa jamii. Maisha yake, siasa na itikadi zake zinakubaliwa kwa sehemu ndogo…Malcolm amekuwa mfano wa mtihani wenye machaguo huru ambapo kila mtu anaweza kuandika alivyoelewa yeye kuhusu siasa na itikadi zake. Chuck D kutoka kundi la Rap liitwalo Public Enemy na Jaji wa mahakama Clarence Thomas wote wanamwita Malcolm X kama shujaa wao.”
Baadhi ya Dondoo Zake Mashuhuri
1. “Mtu asiyesimamia chochote basi ataanguka kwa chochote.”
2. “Hakuna atakayekupa uhuru, hakuna atakayekupa usawa na haki, kama wewe ni mwanaume nenda ukaichukue.”
3. “Sababu za wazayuni kuhalalisha uvamizi wa Izrael katika ardhi ya Palestina hazina mashiko ya kiakili wala kihistoria.”
4. “Hautakiwi uwe kipofu kwa uzalendo wa nchi yako mpaka unashindwa kupigania ukweli. Baya ni baya tu, haijalishi liwe liwemafanywa na nani au kusemwa na nani.”
5. “Shule yangu ilikuwa vitabu na maktaba nzuri…nilitumia maisha yangu yote kule nikiwa nasoma, nikitimiza azma yangu ya udadisi.”
6. “Elimu ni pasipoti yetu ya baadae, kwani kesho iko kwa ajili ya wanaojitayarisha nayo leo.”
7. “Tangu nikiwa mdogo nilijifunza kama unahitaji jambo basi fanya kelele.”
8. “hatuwi na fujo kwa mtu ambaye hatufanyii fujo.”
9. “Dhumuni letu ni kuwa na uhuru kamili, usawa na haki kwa njia yoyote ile itakayohitajika.”
10. “Ukweli upo katika upande unaoonewa”
11. “Huwezi kutenganisha amani na uhuru wa kweli, kwa maana hakuna atakayekuwa na amani kama hana uhuru.”
12. “Hutakiwi kuwa mtu tu, eti ili upiganie haki yako, unachotakiwa kufanya ni kuwa mtu mwerevu, mjanja.”
13. “Kama hautakuwa tayari kufa kwa ajili yake, basi liondoe neno ‘uhuru’ katika kamusi yako”
14. “Gharama ya uhuru ni kifo.”
15. “Mimi ni yule mtu niliye kama wewe unavyofikiri ulivyo…Ukitaka kujua nitakufanya nini, jaribu kufikiria ingekuwa wewe ungefanya nini. Nitafanya hilo hilo kwako tena nitaongeza kidogo.”
16. “Hata iwe heshima ya ukubwa gani wanayoionesha kwangu mimi, hata uwe utambuzi gani wanaotumia hawa wazungu kutambua uwepo wangu mimi, ili mradi bado heshima hiyo haioneshwi kwa kila mmoja wetu bado siooni na siihitaji heshima hiyo kwangu.”
17. “Haimaanishi kuwa nahamasisha utumizi wa nguvu na vurugu, lakini pia sipingi kutumia njia hii kwa ajili ya kujilinda. Siiti njia hii ni ya vurugu tunapoongelea kisasi bali naiita ukuaji wa akili.”
18. “Utamshukuru vipi mtu kwa kukupa kitu ambacho tayari chako? Na cha kushangaza ni pale unapawaona watu wakishukuru kupewa sehemu tu ya kile ambacho tayari ni chao.”
19. “Ni muda wa kufa shahidi sasa, na kama ikatokea kuwa miongoni mwao, basi itakuwa kwa ajili ya udugu wetu. Na hilo ndilo jambo pekee litakaloweza kuokoa taifa hili.’
20. “Haiwezekani ubepari uendelee kuwepo, kimsingi huu mfumo wa ubepari unahitaji damu ya kunywa. Ubepari ulikuwa kama tai, lakini sasa umeshakuwa kinda lake. Ulikuwa na nguvu ya kunyonya damu ya yeyote bila kujali unanguvu au la. Lakini sasa umekuwa mfumo wakioga, ukinyonya damu ya wasiojiweza tu. Kwa uhuru huu,unaowafikia mataifa mbalimbali, ubepari umekuwa ukijeruhi wachache, unanyonya damu ya wachache, na unakuwa dhaifu kila siku. Naimani kwa kipindi kifupi, utamalizika kabisa.”
21. “Mfumo mpya wa maisha uko njiani kuja, ni jukumu letu kujitayarisha ili tuchukue sehemu zetu, tulizo na haki nazo katika maisha hayo.”
22. “Mimi ni mfuasi wa ukweli, bila kujali nani kausema. Natetea haki, bila kujali nani anapinga au nani anatetea. Mimi ni mwanadamu, na naunga mkono yeyote au chochote kitakacho mfaidisha mwanadamu.”
23. “Naamini dini inayoamini uhuru. Kwa dini yoyote ambayo haitaniruhusu nipigane kwa ajili ya kutetea watu wangu, bora na iende tu dini hiyo.”
24. “Mimi ni Muislamu, kwa sababu ndiyo dini inayofundisha jicho kwa jicho na jino kwa jino. Inakufundisha kuheshimu kila mtu, na kujali haki za wote. Lakini pia inafundisha iwapo mtu akitokea akakukanyaga kwa kukuonea, kata miguu yake. Nitabeba shoka la dini yangu kila mahali.”
25. “Hakuna mafundisho katika kitabu chetu yanayotuagiza tuumie kimya kimya. Dini yetu inatufundishe tuwe waerevu. Kuwa mtu wa amani, kuwa na huruma, tii sheria, na umuheshimu kila mtu; lakini akitokea mtu na kunyanyua mkono wake kwako usisite kumpeleka kaburini.”
26. “Mimi ni Muislamu na nitaendelea kuwa hivyo. Dini yangu ni Uislamu.”
27. Sio tu Marekani ndio wanaotakiwa kuufahamu na kuuelewa Uislamu bali ni watu wa dunia nzima.”
28. “Kwa kila umuonapo mtu anafanikiwa kuliko wewe, huwa anafanya jambo ambalo wewe hulifanyi.”
29. “Kukaa tu mezani hakukupi chakula. Unatakiwa ukile kile kilichokuwa katika sahani. Kuwa hapa Marekani hakukufanyi wewe uwe mmarekani. Kuzaliwa hapa marekani hakukufanyi pia uwe mmarekani.”
30. “Kama nikifa huku nikifanikisha kuileta nuru yoyote, nikiwa nimesambaza ukweli wowote utakaosaidia kuua sumu ya saratani hii ya ubaguzi inayoshambulia mwili wa Marekani, basi shukrani zote zinamstahiki Allah na makosa yote yatabaki kuwa yangu.”
31. “…Kwa njia yoyote ile itakayohitajika”
32. “Sifa zote njema zinamstahiki Allah, Mola wa walimwengu wote.”
Pia inatupasa tuifikirie kwa makini hotuba ya kukumbukwa ya Malcolm iitwayo The Field Negro and The House Negro (Mweusi wa Msituni au Mweusi wa Nyumbani). Kwa sababu watu duniani (na tena watu wa rangi zote) huwa wanaganyika katika makundi haya mawili. Na baada ya hotuba hii jiulize mwenyewe kama wewe ni Field Negro au ni House Negro! Na sasa naomba tumkaribishe kaka Malcolm X aweze kutunasihi:
“Kulikuwa na aina mbili za watumwa. Kulikuwa na yule wa nyumbani na mwengine anayezurura. Yule wa nyumbani aliishi katika nyumba na bwana wake. Alivaa vizuri. Alikula vizuri pia kwani alikula kile kilichoachiwa na bwana wake. Akiwekwa darini au chini kabisa mwa nyumba (katika msingi), hata hivyo bado aliishi karibu na bwana wake. Waliwapenda wamiliki wao kuliko hata hao mabwana kujipenda wenyewe. Walidiriki kujitolea hata maisha yao ili kuilinda nyumba ya mmiliki wake. Tena kwa haraka kuliko hata huyo bwana mwenyewe. Kama tajiri wake akisema, “Tuna nyumba nzuri hapa” basi yule mnigro atarukia, ‘Kweli bosi, tuna nyumba nzuri.” Kila wakati ambapo bosi atatumia ‘sisi’ na yeye hatosita kutumia neno hilo. Hivyo ndivyo walivyokuwa.
Kama nyumba ya bosi ikashika moto, yule mtumwa atakimbia zaidi kuuzima moto kuliko hata mwenye nyumba mwenyewe. Kama bwana akiumwa, utamkuta mtumwa wake akiuliza, vipi bosi hata sisi tunaumwa (kwa hali ya kumsikitikia na kumliwaza bosi wake)!? Alijitahidi kumtambua bosi wake zaidi ya bwana wake kujitambua mwenyewe. Na hata ukienda kumtembelea mwenzako huyu ukimuasa mtoroke! Utakuta anakuangalia kwa jicho la mshangao na kusema, “He! Umewehuka!? Una maana gani unavyosema tutoroke?! Wapi nitakaa katika nyumba nzuri kama hii? Wapi nitavaa nguo nzuri kuliko hizi? Wapi nitakula chakula kizuri kuliko hiki?” Huyo ndiyo Nigro wa nyumbani. Kwa kipindi hiko, aliitwa ‘Niga’ wa nyumbani. Na hivyo ndivyo tuwaitavyo sasa, kwani bado tunao humu ndani wanazunguka zunguka kuturudisha nyuma mitaani.
Huyu Mnegro wa kisasa anampenda bosi wake sana. Anataka aishi karibu naye. Atadiriki kufanya kazi ya ziada pamoja na kusifu ili apate nafasi ya kuishi karibu na mabosi wake (wazungu), na kutamba kwa wenzake, “Mimi ndio Mnigro pekee hapa. Ndio pekee katika kazi hii na ndio pekee katika shule hii.” Tunakwambia wewe sio chochote zaidi ya mtumwa wa nyumbani tu kama wale wanigro wa zamani. Na kama mwenzake akija kukushauri kuondoka hapa, unasema kile kile alichosema mnigro wa kale katika mashamba, “Unamaanisha nini ukisema tuondoke? Tutoke Marekani? Nchi hii nzuri ya wazungu? Sijasahau lolote Afrika.” Na wakati umeiacha akili yako Afrika.
Katika kipindi hiko hiko cha kilimo cha kutumia watumwa, kulikuwa na kundi la pili ambalo ni la Mnigro asiye na makazi kwa bosi wake. Hawa walikuwa wengi. Sema kweli hawa walikiona cha moto. Walikula yaliyosazwa ndani. Walikula vile vilivyoachwa na watu wale wachafu (nguruwe) ndani. Siku hizi mnaita Chit’lins (chakula kitokanacho na utumbo wa nguruwe). Zama hizo waliziita kama zilivyokuwa, matumbo! Na baadhi yenu bado ni walaji matumbo hayo hapa.
Mnigro huyu wa shambani alipigwa kuanzia asubuhi mpaka jioni. Aliishi bandani tu. Alivaa mitumba. Alimchukia bwana wake. Nasema alimchukia bwana wake na inaonyesha alikuwa na akili. Yule wa nyumbani alimpenda bwana wake huyu alimchukia, tena kwa kuwa walikuwa wengi, waliwachukia mabwana zao. Kama nyumba ya bosi wao ikishika moto, wala hutamkuta akijisumbua kuuzima moto ule, bali akijitenga kuomba dua upepo uzidi kuvuma na moto uongezeke. Kama bwana wa watumwa akiumwa, basi wataomba afe kabisa. Kama mtu akija kwa hawa na kuwaambia watoroke. Hawaulizi tunaelekea wapi bali walihisi sehemu nyengine yoyote ni bora kuliko ya hapo. Tunao watumwa hawa Marekani ya sasa, na mimi ni miongoni mwao. Hatusikii siku hizi wanigro wakilalama eti, “Serikali yetu ina matatazo’ bali wanasema “Serikali ina matatizo”. Nishawahi kumsikia mmoja akisema, “Wanaanga wetu” na wakati hata haruhusiwi kusogelea maeneo hayo. Au mtu atumie “Jirani zetu, wanaanga wetu au wanamaji wetu” kwa hawa wazungu, bila shaka atakuwa karukwa na akili. Nasema huyu Mnigro atakuwa karukwa na akili.
Kwa kuwa bwana wa watumwa wa zama hizo alimtumia Tom kulinda wenzake, ndio hicho hicho kinachofanyika sasa kwani hawa vibaraka sio lolote zaidi ya kuwa ni wajomba Tom wa kisasa tu. Kina wajomba Tom wa karne ya 20 wanatumika kutulinda sisi na wanaturudisha nyuma. Wanatufanya tupende amani ambayo ni ya uongo. Tusiwe na vurugu. Huyo ni yule yule Tom anaekufanya uwe hivyo ili uendelee kutawaliwa. Ni sawa sawa umeenda kwa tabibu wa meno ambaye anataka kutoa jino lako, utampiga tu pale atapoanza kuvuta jino. Sasa itabidi akuweke vitu katika taya zako ili usikie ganzi, na hapo utakuwa unaumia kwa amani kabisa. Damu itakuwa inamwagika katika taya zako na wewe hauhisi chochote kinachoendelea. Eti kwa sababu kuna mtu amekufanya uumie kimya kimya! Hahaha!
Wazungu wanatufanyia jambo hilo hilo mitaani humu. Anapotaka kukufunga fundo kichwani mwako, kukutumia atakavyo na asiwe na hofu ya wewe kupigana naye, huwa wanawatumia hawa kina wajomba Tom, wanaojifanya viongozi wa dini kama ile ganzi ya kwenye meno, wakituelekeza tusiache kuumia ila tuumie kimya kimya! Kama mchungaji Cleage alivyosema, wanatufundisha damu yetu imwagike mitaani. Hii ni aibu ukizingatia yeye ni mchungaji wa dini. Kama ni aibu kwake nadhani mnaelewa kwangu itamaanisha nini.
Hakuna kitu kama hicho katika kitabu chetu Qur’an kama nyie mnavyoiita Koran! kitufundishacho kuumia kwa amani. Dini yetu inatutaka tuwe na akili. kuwa na ustahifu (uungwana) lakini pia kuwa na amani ya kweli. Tii sheria. Mheshimu kila mtu. Lakini kama mtu akijaribu kunyanyua ‘kamkono’ chake kukudhuru, usisite kumpeleka kaburini. Hii ndio dini bora. Tena ndio ile ile dini ya zamani. Hii ndio dini mama na baba walikuwa wakiiota. Jicho kwa jicho, jino kwa jino, kichwa kwa kichwa na (uhai) maisha kwa (uhai) maisha. Hii ndio dini bora. Na kwa yeyote anayepinga dini hii isifundishwe, ni mbwa mwitu anayetaka kukufanya chakula chake.
Hivi ndivyo ilivyo kwa wazungu hawa wa Marekani. Ni mbwa mwitu na wewe ni mbuzi. Muda ambao sijui mchungaji, au padri anakufundisha usimkimbie mzungu huyu na tena anakufundisha usimpige vita mzungu si jengine ila atakuwa mnafiq kwako na kwangu mimi pia. Uweke maisha yako rehani kiasi hicho?! La hasha, yalinde maishe yako, linda uhai wako. Ndio jambo lenye thamani zaidi kwako. Na hata kama ikatokea unahitaji kukata tamaa nayo basi jitahidi iwe mechi suluhu.
Mabwana hawa wa watumwa waliwachukua kina Tom, wakiwavalisha vizuri, wakiwalisha vizuri na hata kuwapa elimu kidogo. Waliwakabidhi makoti marefu na kofia nzuri juu na watumwa wengine wote wawatazame wao. Kisha ikawa rahisi kuwatawala wale waliobakia kupitia Tom. Nyenzo hiyo hiyo iliyotumika kipindi hicho ndiyo itumikayo leo. Anamchukua Mnigro mmoja na kumfanya mashuhuri, anamjenga, anamtangaza na kumfanya awe mzungumzaji na kiongozi wa wanigro.”
 
Back
Top Bottom