Kilango sasa awageukia akina Slaa
*Awataka wasiparamie hoja yake, wasubiri majibu
*Asema hoja ya Commodity Import Support si mpya
Na John Daniel, Dodoma
MBUNGE wa Same Mashariki, Bibi Anne Kilango-Malecela (CCM), ameitaka kambi ya upinzani bungeni, kuacha kuparamia hoja yake na wabunge wenzake wa CCM.
Hiyo ni hoja ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na ya Commodity Import Support (Mfuko wa Fedha za Kuagizia Bidhaa Nje) ya sh. bilioni 216, kwa maelezo kuwa kinachosubiriwa juu ya masuala hayo ni majibu na si kujidai kuiwasilisha upya kama walivyofanya juzi.
Amesema umefika wakati Watanzania wakiwamo Wabunge wa upinzani kutambua, kwamba wabunge wa CCM wako imara na makini kutetea maslahi ya Taifa kwa kuihoji Serikali pale kunapokuwa na dalili za upungufu katika utendaji na kuondoa kabisa dhana potofu, kwamba kazi hiyo hufanywa na wapinzani tu kama inavyodhaniwa.
Akizungumza na Majira jana, Bibi Kilango alisema amesikitishwa na alichokiita kuibiwa hoja na wapinzani na kuiwasilisha bungeni kama jambo jipya, wakati zikiwa zimepita siku nne tu tangu alipozungumzia masuala hayo kwa uchungu na kwa ukali na kugusa hisia za Watanzania.
Kwanza nikwambie tu kwamba kilichofanywa na wapinzani ni kuthibitisha uhalali na umuhimu wa hoja yangu ya wiki iliyopita na ujasiri wangu kama Mbunge wa CCM, lakini wamenishtua kwa kujidai kwamba ni hoja mpya na kuitaka Serikali itoe majibu wakati nilishasema bila majibu ya uhakika hapatatosha.
Unajua umefika wakati Watanzania hasa wapinzani waelewe kwamba sisi Wabunge wa CCM tuna uwezo mkubwa wa kuihoji Serikali na ndiyo kazi yetu, wafute fikra mbaya kwamba kazi ya kuihoji Serikali ni yao, hapana, mimi Mbunge wa CCM nilitimiza wajibu wangu na kila mtu anajua hivyo, wapinzani watulie wasubiri majibu yatakayotokana na hoja yangu na si wao kurudia kile kile nilichosema, alisema Bibi Kilango.
Alisema licha ya wenzao hao kurudia hoja hiyo, lakini pia walithibitisha ujasiri wake wa kutoa hoja zenye mwelekeo wenye maslahi kwa Taifa na kutoa siri yake ya kuzungumza kwa uchungu na ukali kuwa inatokana na wadhifa wake wa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, hivyo hawezi kukubali kuona Serikali iliyotokana na chama chake ikipata dosari mbele ya wananchi.
"Hivi sasa Rais wetu ana mzigo mzito sana, kuna mambo mengi yanamsumbua, ndiyo maana mimi Mjumbe wa NEC na Mbunge wa CCM, nina wajibu wa kuisimamia Serikali ya CCM, ni wajibu wangu na bado nasisitiza, kwamba sitarudi nyuma mpaka majibu ya uhakika yatakapopatikana, hapo ndipo nitakuwa nimeitendea haki nchi yangu na nitakuwa nimemsaidia Rais wetu, alisisitiza Bibi Kilango.
Mbunge mwingine wa CCM aliyeonesha nia ya kuungana na Bibi Kilango kutaka majibu sahihi juu ya masuala hayo ni Mbunge wa Kishapu, Bw. Fred Mpendazoe, aliyetaka Serikali kuwa makini zaidi na kuonya kuwa zama za uongo zimepitwa na wakati.
Akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani bungeni juzi, msemaji wa kambi hiyo katika Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Dkt. Willibrod Slaa, aliitaka Serikali kutoa majibu ya uhakika kuhusu fedha za EPA na sh. bilioni 216 za Commodity Import Support, kwa maelezo kwamba muda unazidi kwenda bila hatua za wazi dhidi ya watuhumiwa kuchukuliwa.
http://majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=7051