Kilango sasa awageukia akina Slaa

Sam

JF-Expert Member
Jun 6, 2006
415
89
• Kilango sasa awageukia akina Slaa

*Awataka wasiparamie hoja yake, wasubiri majibu
*Asema hoja ya Commodity Import Support si mpya

Na John Daniel, Dodoma

MBUNGE wa Same Mashariki, Bibi Anne Kilango-Malecela (CCM), ameitaka kambi ya upinzani bungeni, kuacha kuparamia hoja yake na wabunge wenzake wa CCM.

Hiyo ni hoja ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na ya Commodity Import Support (Mfuko wa Fedha za Kuagizia Bidhaa Nje) ya sh. bilioni 216, kwa maelezo kuwa kinachosubiriwa juu ya masuala hayo ni majibu na si kujidai kuiwasilisha upya kama walivyofanya juzi.

Amesema umefika wakati Watanzania wakiwamo Wabunge wa upinzani kutambua, kwamba wabunge wa CCM wako imara na makini kutetea maslahi ya Taifa kwa kuihoji Serikali pale kunapokuwa na dalili za upungufu katika utendaji na kuondoa kabisa dhana potofu, kwamba kazi hiyo hufanywa na wapinzani tu kama inavyodhaniwa.

Akizungumza na Majira jana, Bibi Kilango alisema amesikitishwa na alichokiita kuibiwa hoja na wapinzani na kuiwasilisha bungeni kama jambo jipya, wakati zikiwa zimepita siku nne tu tangu alipozungumzia masuala hayo kwa uchungu na kwa ukali na kugusa hisia za Watanzania.

“Kwanza nikwambie tu kwamba kilichofanywa na wapinzani ni kuthibitisha uhalali na umuhimu wa hoja yangu ya wiki iliyopita na ujasiri wangu kama Mbunge wa CCM, lakini wamenishtua kwa kujidai kwamba ni hoja mpya na kuitaka Serikali itoe majibu wakati nilishasema bila majibu ya uhakika hapatatosha.

“Unajua umefika wakati Watanzania hasa wapinzani waelewe kwamba sisi Wabunge wa CCM tuna uwezo mkubwa wa kuihoji Serikali na ndiyo kazi yetu, wafute fikra mbaya kwamba kazi ya kuihoji Serikali ni yao, hapana, mimi Mbunge wa CCM nilitimiza wajibu wangu na kila mtu anajua hivyo, wapinzani watulie wasubiri majibu yatakayotokana na hoja yangu na si wao kurudia kile kile nilichosema,” alisema Bibi Kilango.

Alisema licha ya wenzao hao kurudia hoja hiyo, lakini pia walithibitisha ujasiri wake wa kutoa hoja zenye mwelekeo wenye maslahi kwa Taifa na kutoa siri yake ya kuzungumza kwa uchungu na ukali kuwa inatokana na wadhifa wake wa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, hivyo hawezi kukubali kuona Serikali iliyotokana na chama chake ikipata dosari mbele ya wananchi.

"Hivi sasa Rais wetu ana mzigo mzito sana, kuna mambo mengi yanamsumbua, ndiyo maana mimi Mjumbe wa NEC na Mbunge wa CCM, nina wajibu wa kuisimamia Serikali ya CCM, ni wajibu wangu na bado nasisitiza, kwamba sitarudi nyuma mpaka majibu ya uhakika yatakapopatikana, hapo ndipo nitakuwa nimeitendea haki nchi yangu na nitakuwa nimemsaidia Rais wetu,” alisisitiza Bibi Kilango.

Mbunge mwingine wa CCM aliyeonesha nia ya kuungana na Bibi Kilango kutaka majibu sahihi juu ya masuala hayo ni Mbunge wa Kishapu, Bw. Fred Mpendazoe, aliyetaka Serikali kuwa makini zaidi na kuonya kuwa zama za uongo zimepitwa na wakati.

Akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani bungeni juzi, msemaji wa kambi hiyo katika Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Dkt. Willibrod Slaa, aliitaka Serikali kutoa majibu ya uhakika kuhusu fedha za EPA na sh. bilioni 216 za Commodity Import Support, kwa maelezo kwamba muda unazidi kwenda bila hatua za wazi dhidi ya watuhumiwa kuchukuliwa.

http://majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=7051
 
SPIKA ATOE KWANZA ZILE TAARIFA ZA UCHAWI KWASABABU KUNA MAMBO YA AJABU AJABU YANAENDELEA HUKO BUNGENI.
UCHUNGU WA KUKAMATWA MAFISADI NI WA WANANCHI...NA WA KURUDISHWA PESA NI WA ccm NA KILLANGO.
ETI UCHUNGU!
UCHUNGU WANAUJUA ccm WALIOUZA NCHI?
AKAE PEMBENI LA SIVYO NITAKUJA KUFUNGA SAFARI KUMSAPOTI OBAMA WAKE!
 
Hoja ya zamani ni ya kurudi kwa pesa ambazo mkullo alishasema zimerudishwa kiasi flani!
Pesa ambazo Kikwete aliwaambia wafadhili ni za wananchi na Mkullo akasema hazikuwa na mwenyewe!
BOT Ni benki inayohifadhi fedha za serikali.
Serikali ni ya wananchi!
Sasa pesa ni za nani?
Plan B...WAZALENDO WAPEWE NCHI!
MAMA KAA PEMBENI USIJE KUTA UMEGEUKA KUWA MJUMBE WA SHETANI!
KWANI SASA TUMEGUNDUA MNATAKA SIKU YA MWISHO YA MIJADALA AMBAYO NI IJUMAA HII IFIKE KABLA HATUJAJUA MUSTAKABALI WA NCHI!
 
Hoja ya zamani ni ya kurudi kwa pesa ambazo mkullo alishasema zimerudishwa kiasi flani!
Pesa ambazo Kikwete aliwaambia wafadhili ni za wananchi na Mkullo akasema hazikuwa na mwenyewe!
BOT Ni benki inayohifadhi fedha za serikali.
Serikali ni ya wananchi!
Sasa pesa ni za nani?
Plan B...WAZALENDO WAPEWE NCHI!
MAMA KAA PEMBENI USIJE KUTA UMEGEUKA KUWA MJUMBE WA SHETANI!
KWANI SASA TUMEGUNDUA MNATAKA IJUMAA IFIKE KABLA HATUJAJUA MUSTAKABALI WA NCHI!

Jamani si tuliambiwa hapa tumpe muda afanye kazi yake na tukakubaliana vipi tena? Mimi nashauri tumpe muda mpaka 2015. Mzee Mushi angalia lugha yako.
 
Jamani si tuliambiwa hapa tumpe muda afanye kazi yake na tukakubaliana vipi tena? Mimi nashauri tumpe muda mpaka 2015. Mzee Mushi angalia lugha yako.

Nashukuru.Lugha ipi hiyo mkuu?
Ila siamini macho yangu!
Tungeomba Six arelease ripoti ya uchunguzi wa "Unga unga" mara moja kama akiweza na pia aongeze muda wa mijadala kama kanuni za bunge zinamruhusu.
 
.....hii mambo ya hoja yangu kama watoto wa third grade sounds like a pure selfish, nilianza kumwamini huyu mama with some reservations,thought she was for betterment of our country lakini seems she stuck into this old fashioned politics za ujiko ujiko!
 
Koba Mama keshaharibu.
Penye ukweli...Uongo hujitenga!
Kama hii kweli ni jamii forum..Basi atakayeshinda hoja halali bungeni ndiyo wa kupewa nchi.
 
Selfish Indeed yaani hawa watu wa CCM wakati mwingine wanaboa sana, Jamani hizi hoja sio za CCM wala Wapinzani bali ni hoja za Watanzania ambao usiku na mchana wanahangaika na maisha yao ya kila siku huku MAFISADI wakizidi kuiba mali za nchi yetu. Inabidi hawa wabunge wakumbuke hawakuchaguliwa waende bungeni na Watanzania ili washindane kuona nani ametoa hoja fulani au nani amechukua hoja ya mwingine. Wabunge wanatakiwa wawe pale kutetea maslahi ya watanzania regardless ya nani ametoa hiyo hoja initially au hata kama hiyo hoja itarudiwa na mwingine, kitu muhimu ni kutetea Maslahi ya Taifa. Stop bickering guys kwa sababu sasa mnaanza kuboa hatuko kwenye mashindano ya kutoa hoja.
 
.....hii mambo ya hoja yangu kama watoto wa third grade sounds like a pure selfish, nilianza kumwamini huyu mama with some reservations,thought she was for betterment of our country lakini seems she stuck into this old fashioned politics za ujiko ujiko!

Usimhukumu labda wamenukuu vibaya. Tusubiri kesho. Nilisha sema kuhusu hii hoja ya ufisadi na Rev. Kishoka akaelezea vizuri kabisa. Hizi hoja za kuropoka majibu yake huwa ni ya kuropoka na mtu yeyote anaweza kudai ownership. Kwa sasa lazima ukubali hoja ya ufisadi ni ya CCM na anayeiongoza ni huyu mama. Kama wapinzani wanataka kumpokonya itakuwa ngumu sana kwa maana hadi baadhi ya wapinzani waliingia mkenge. Nashauri tumwachie tu hii hoja aangaike nayo badala ya kuanza kung'ang'ania. Tusubiri kesho wapinzani watadai hoja ni hayo.
 
Hivi we sam uko sawa kichwani?
 
Selfish Indeed yaani hawa watu wa CCM wakati mwingine wanaboa sana, Jamani hizi hoja sio za CCM wala Wapinzani bali ni hoja za Watanzania ambao usiku na mchana wanahangaika na maisha yao ya kila siku huku MAFISADI wakizidi kuiba mali za nchi yetu. Inabidi hawa wabunge wakumbuke hawakuchaguliwa waende bungeni na Watanzania ili washindane kuona nani ametoa hoja fulani au nani amechukua hoja ya mwingine. Wabunge wanatakiwa wawe pale kutetea maslahi ya watanzania regardless ya nani ametoa hiyo hoja initially au hata kama hiyo hoja itarudiwa na mwingine, kitu muhimu ni kutetea Maslahi ya Taifa. Stop bickering guys kwa sababu sasa mnaanza kuboa hatuko kwenye mashindano ya kutoa hoja.
Mzee hadi wewe? Mbona hata wiki haijapita umeshabadilisha mawazo? Kwa hiyo tukubaliane kabisa hapa kama wapinzania watadai kesho kuwa hoja ni yao nao pia watakuwa wanaboa au CCM tu wakidai hoja ni yao wanaboa?
 
Sam kama watu wameamua kurudi upande wa wazalendo tuwape nafasi ila wakitoka nje ya msitari ndiyo tuwakumbushie.
Sisi ni watu wenye masamaha!
FMES alisahaanza..Na wengine tuwaruhusu tu.
Ndio jf hii...Hata mimi nilishasamehewa na niko hapa nakata issue.
 
...agree, inaonekana anafanya posturing juu ya kitu flani! anataka ujiko kwa kujifanya yupo hivi wakati kumbe yupo vile! misiasa ya bongo inatia migraines tu saa ingine!
Tulimpa Killango muda!
Hakuwa anaongelea jipya lolote lile!
Huyu Sitta hapatani kabisa na Chenge kwasababu anataka issue zijadiliwe.
Spika angekuwa na mizengwe basi hata bunge lingeshaishiwa nguvu sasa hivi!
Tumpe muda kama wengine walivyopewa!
Si muda wa wiki ama mwezi..NO!
Vikao vinaendelea!
Alikataa issue ya Zimbabwe isiyateke mazungumzo ya ufisadi!
Hiyo ni hatua nzuri na sasa tumuunge mkono la sivyo tutakuwa hatuitakii mema nchi yetu!
 
...agree, inaonekana anafanya posturing juu ya kitu flani! anataka ujiko kwa kujifanya yupo hivi wakati kumbe yupo vile! misiasa ya bongo inatia migraines tu saa ingine!
hahahahhahahhaha....
Mzee nakusubiri kwa Obama tu wewe maana nilishawambia ni bomu mnajifanya hamuelewi.. naombea ashinde uchaguzi nipate cha kuongea for 4 years. Mzee njoo CNN political ticker.
politicalticker.blogs.cnn.com
Umenifurahisha sana kwenye comment yako umenifanya niondoke sasa itatosha kwa leo.
 
Sam na wewe ni sapota wa BUSH NA TSIVANGIRAI?
AMA NI SINCLAIR PEKE YAKE?
 
At the end of the day the truth is that when the opposition brought up this issue on ubadhirifu katika BOT, EPA, wasemaji wa CCM walisema hawa ni waongo. Leo CCM inajidai kuwa wao ndio wanaopambana na mafisadi ilhali wakati ule walisema kila kitu BOT ni shwari. Sasa badala ya kushirikiana na upinzani kuisafisha Tanzania yetu CCM inataka ku- hijack hili swala kwamba ni wao ndio wameanzisha huu mchakato wa kupambana na ufisadi. Wamesahau jinsi walivyozomewa mikoani? Very interesting indeed!
 
Mimi Mama Hillary Clinton. Sina mtu kwa sasa.
Kama hivyo na wewe bado unahitaji msasa!
Clinton mwenye uhusiano na FISADI YOUNG ALIYETOA MANENO MACHAFU NA BADO MKAMKARIBISHA KWENYE MUSTAKABALI WA NCHI MLIYOIUZA?
Acha hizo na wewe ukae kwa wazalendo jumla!
NB:Wale niliokuwa nikiwaambia uchaguzi wa marekani unaihusu Tanzania na nikasema wakae mkao wa kiuhuru uhuru wakabisha...Waendelee kuleta ubishi niwaletee uthibitisho kama bado hawaoni!
 
Mzee Es na Mkjj, naomba muongee na mama kumsaidia!! Nadhani sasa ataharibu, hayo mambo ya kuown hoja ni childish na ni ushamba wa hali ya juu!!

Mama yeye asishindane na upinzani, yeye amkome nyani na sisi wananchi tunatambua na kuelewa nani ni shujaa.

Sasa nilidhani mzee Malecela kakosea, lakini inaonekana labda wanashindwa kuelewa mambo kwa ufasaha.

Mtu yeyote anayetetea mali za wananchi ni shujaa, whether ameanza mwaka 47, mwaka 70, mwaka 90 au hata kesho. Sisi wananchi hatujali ni mbunge wa chama gani sababu haitusaidii reason za kutetea, sisi tunajali kutetewa tu.

Mama asiwe na wasiwasi tunamuheshimu kwa aliyofanya kwa hiyo sifa zitakuja, na kwa kweli wananchi tuna makapu yamejaa ya sifa za kumwaga wala hawezi kuziweka zote kwake, na wengine tutawapa
 
Ninaamini wananchi wa Tanzania wana uwezo wa kuchambua mchele na pumba. Kwa hiyo kwa CCM kujaribu kuhijack swala hili ni kupoteza muda tu. Wanao uwezo wa kuonyesha kuwa CCM kuna wazalendo wanaoipenda nchi yao na watashirikiana na mzalendo yeyote bila kujali chama anachotoka au itikadi yake ya siasa kuhakikisha kuwa ufisadi unapigwa fullstop ndani ya nchi. They are in the drivers seat they need to show that they are driving responsibly.
 
Back
Top Bottom