BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,082
Kilango apasua jipu
2008-07-17 12:07:12
Na Victor Kwayu, PST, Same
Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Bi. Anna Kilango Malecela, amesema mkakati alionao sasa ni kuendelea kukemea baadhi ya viongozi na watu wachache wanaoonyesha mwelekeo wa kuendelea kumiliki na kuhodhi mapato ya nchi kwa maslahi yao binafsi.
Aliyasema hayo jimboni kwake jana wakati akizungumza na wanahabari katika mahojiano maalum.
``Ni vyema niwaelimishe wananchi kikamilifu kwamba, wabunge wote wanaoendelea kuchachamaa bungeni au majukwaani wanachokitafuta ni kikubwa zaidi kuliko kupambana na mafisadi,`` alisema.
Aliongeza kuwa, uamuzi huo unatokana na ukweli kwamba wapo baadhi ya viongozi wachache pamoja na kikundi kidogo kinachoendelea kuhodhi mapato ya nchi isivyo halali.
Alisema kwa kipindi kifupi, baadhi ya viongozi ndani ya serikali wameonekana kutoridhika na kipato wanachokipata na badala yake wametumia mianya ya madaraka waliyonayo kumiliki fedha na rasilimali za nchi isivyo halali.
``Endapo kwa umoja wetu kama wabunge ndani ya Bunge hatutapambana na hali hii, hatua ya watu wachache wenye uchu na fedha za walalahoi kutalipeleka taifa mahala pabaya`` alionya.
Aliitaka jamii kutambua kuwa wabunge wote wanaochachamaa bungeni au majukwaani wanachokitaka ni kikubwa zaidi kuliko kupambana na mafisadi.
Alisema kinachopiganiwa ni kuwa na mgawanyo sawa wa rasilimali za nchi kwa manufaa ya kila raia na sio kwa kundi la wachache kujilimbikizia utajiri kwa njia zisozo halali.
Bi. Anne alisema ingawa uamuzi wa wabunge hao licha ya kuwa ni mgumu na utakaoleta matokeo baadaye unapaswa kuungwa mkono na kila mwananchi kwakuwa serikali imeonyesha nia ya kukabiliana na vitendo hivyo.
``Rais wa nchi ameonyesha kukerwa na hali hii ya vitendo vya wazi kwa baadhi ya viongozi... hatua hiyo inatupa moyo kwa sisi wabunge kuendelea na mapambano haya kwa ajili ya kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania.``
``Kwa msingi huo, tunaomba wananchi watuombee ili pamoja na mambo mengine tuweze kuyafikia malengo hata kama matokeo hayataonekana sasa lakini vizazi vijavyo vishuhudie jitihada zetu``, alisema.
Alisema baadhi ya wananchi wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya kuwepo mgawanyiko miongoni mwa wabunge kwa kuona baadhi yetu tukihitaji mabadiliko na wengine wakipuuza.
Alisema wabunge wengi wanataka mabadiliko wakati wachache wanayapinga na kwamba wanaofanya hivyo kuhofia mabadiliko hayo yatagusa maslahi yao binafsi.
``Nasisitiza kwamba ni vyema tukawaacha hata kama wakitubeza...hatutakata tamaa kwa hili kwakuwa ni la maslahi ya wananchi na taifa``, alisema.
Katika hatua nyingine, mbunge huyo aliwataka wabunge wa CCM kuwa mstari wa mbele kukosoa viongozi wanaokiuka wajibu wa kazi kwa maslahi binafsi.
Alisema akiwa mbunge wa CCM na mjumbe wa Halmashauri Kuu hatapenda kuona chama na serikali vikitetereka.
Mbunge huyo alikuwa katika ziara ya siku mbili jimboni mwake iliyokuwa imelenga kuzindua ujenzi wa visima 30 vya maji safi katika tarafa ya Mamba Vunta pamoja na kujionea maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kisasa cha kusindika tangawizi ya wakulima wa kata za Mamba Miyamba, Bwambo na Mpinji.
SOURCE: Nipashe