Kilango amvutia pumzi Mwangunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilango amvutia pumzi Mwangunga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Oxlade-Chamberlain, Jul 14, 2009.

 1. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, amesema hoja yake ya kulitaka Bunge liunde kamati teule ya kuchunguza wizi wa nyara za serikali anaivutia pumzi akisubiri majibu ya uchunguzi unaofanywa na polisi wa kimataifa ‘Interpol’.
  Hata hivyo, alisema amefurahishwa na majibu yaliyotolewa Jumamosi iliyopita bungeni na Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, juu ya ukweli wa sakata la wizi na utoroshaji nje wa nyara za serikali.
  “Waziri alivyokiri juzi kwenye majibu yake amenisaidia sana. Mimi kufuatilia Interpol inatoa majibu gani…Kila mara sisi wabunge tutakuwa tunafuatilia,” alisema Kilango.
  Kilango alisema hayo katika mahojiano maalum na gazeti hili nyumbani kwake mjini hapa jana akiwa kwenye mapumziko ya muda mfupi baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo mwishoni mwa wiki katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
  Kilango ambaye juzi alifanyiwa upasuaji mdogo hospitalini hapo na kuruhusiwa jana asubuhi, alisema baada ya kutoa mchango wake na nia yake ya kuwasilisha hoja binafsi, alichotaka kusikia ni majibu ya Waziri Mwangunga kwa kuwa suala hilo alilifanyia utafiti na alikuwa na majibu yote.
  “Nilikuwa nataka aseme ukweli na kweli alijibu vile nilivyotaka…Ndio maana baada ya majibu yale mimi nilitoka kwa kuwa nilikuwa na 'appointment’ (ahadi ) hospitali ya kufanyiwa upasuaji,” alisema.
  Kilango alisema hakuwa na nia ya kuwasilisha hoja hiyo, lakini alichotaka kusikia kwenye hotuba ya wiziri ni juu ya wizi wa nyara hizo.
  Alisema suala hilo ni kubwa na wabunge wataendelea kulifanyia kazi kwa kuwa majibu yake yamesaidia wao kufuatilia suala hilo na kupata ukweli.
  “Nilitaka aseme kwenye wizara yake tunaibiwa kiasi gani, lakini yeye hakuzungumzia suala hilo,” alisisitiza mbunge huyo machachari, ambaye amekuwa akitoa mchango mkubwa wakati wa kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu ufisadi.
  Alisema wabunge wanachopigania ni rasilimali za taifa zisiende mikononi mwa watu wachache. “Hatukwenda bungeni kuvaa magauni, tumekwenda kutetea wananchi wetu,” alisema wakati wa mahojiano hayo.
  Kilango alisema wabunge ndio wanaopaswa kumsaidia rais ili nchi iweze kuwa na utawala bora.
  “Kitu kinachonikera ni kwamba hata Rais Barrack Obama (wa Marekani) juzi, alisema nyinyi Waafrika umaskini mnajitakia wenyewe kwani mna rasilimali za kutosha,” alisema Kilango.
  Hata hivyo, Kilango alitoa tahadhari kuwa wabunge wanapohoji juu ya hoja mbalimbali bungeni, hawamhoji mtu (akimaanisha waziri ) bali wanahoji taasisi ya waziri. Alisema kuna kauli zinazotolewa na baadhi ya wabunge kuwa ni mbaya zinazoweza kuhatarisha amani.
  Kilango alisema katika baadhi ya kauli hizo ni pale baadhi ya wabunge wanaposema mawaziri Waislamu wanabanwa na wabunge Wakristo.
  “Kauli hii isisikike tena, kama kuna watu wenye kauli hiyo waache mara moja,” alisema mbunge huyo, ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
  Akijiadili hotuba ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii bungeni wiki iliyopita, Kilango, alitaja makontena ya nyara za serikali yaliyokamatwa nchini Vietnam na Ufilipino, na kumtaka Waziri aseme yalipitaje bandari ya Dar es Salaam na nani walihusika.
  Waziri Mwangunga alithibitisha kukamatwa kwa makontena hayo na watu wanaoshikiliwa kwa utoroshaji huo wa nyara kupitia bandari ya Dar es Salaam.
  Hii ni mara ya pili katika kipindi cha mwaka huu Waziri Mwangunga kuwa katika kikaango baada ya kubanikwa tena Aprili mwaka huu juu ya ada za vitalu vya uwindaji wa kitalii, ambavyo vilipandishwa kwa azimio la Bunge, lakini wizara yake ikalipuunza Bunge na kuvishusha.
  Kikaango hicho kilitokana na hoja binafsi ya Mbunge wa Kwela (CCM), Chrisant Mzindakaya, aliyetaka kujua sababu za waziri huyo kupuuza azimio la Bunge na kutaka akemewe. Hata hivyo, baada ya maombi ya Mwangunga na kujieleza kwa kirefu, Mzindakaya aliiondoa hoja yake na kusisitiza kwamba watendaji serikalini wasaidie mawaziri si kuwakomoa.
   
 2. b

  bangusule Senior Member

  #2
  Jul 14, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 185
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  uharibifu mkubwa wa mazingira ktk msitu wa Chome wilayani Same unaendelea na Anna Kilango amekaa kimya. badala yake anamsakama Shamsa Mangunga kwa matatizo yaliyotokea kabla hajateuliwa waziri wa maliasili. hiyo yote ni kutaka aandikwe ktk magazeti.

  ANNA KILANGO ANALILIA UWAZIRI. kama angekuwa na uchungu na maliasili za Tanzania basi angeanza kukomesha uchimbaji udongo wenye bauxite unaosafirishwa kwa magendo toka Same kwenda Kenya na ukataji miti kiholela ktk msitu wa Chome.
   
 3. nkawa

  nkawa Senior Member

  #3
  Jul 14, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 181
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo chacha...nyani haoni.......Je kuna nini?
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  I dont see anything new in this woman!
  Kwa kubaki ndani ya CCM na kwenda Busanda kukinusuru chama cha kifisadi sioni kama ana hoja yoyote katika upayukaji wake.
  May be ni kweli anataka uwaziri...
   
Loading...