Kilaini: Mwanamke aliyejipa upadri ameasi Kanisa Katoliki

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,223
1,671
Dar es Salaam. Kitendo cha mtandao wa wanaharakati wanaopigania wanawake kupewa daraja la upadri ndani ya Kanisa Katoliki, Marekani, kimepingwa na baadhi ya viongozi wa kanisa hilo nchini.

Hivi karibuni, Lilian Lewis (75) wa Michigan, Marekani alipewa daraja hilo, jambo linalotishia mtandao huo kutengwa na Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican.

Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki Bukoba, Methodius Kilaini alisema jana kuwa hatua hiyo ni sawa na kuliasi kanisa Katoliki.

"Watu kama hao watakuwa wamejifukuzisha kanisa… ni vikundi tu vinavyoibuka na mambo yao lakini havina nafasi katika kanisa. Hata Kenya walijitokeza watu waliopewa daraja la upadri wakati wameoa, wakatengwa," alisema na kuongeza:

"Siyo mara ya kwanza, zamani Kanisa Katoliki lilikuwa peke yake chini ya Papa mmoja, lakini wakajitenga Walutheri na Anglikana, kwa hiyo siyo ajabu leo ukisikia hivyo."

Alipoulizwa kuhusu nafasi ya wanawake katika kanisa hilo, alisema kuwa japo linawaheshimu wanawake, bado hawapewi huduma hiyo.

"Kwa sababu hata Yesu Kristo aliwapenda na kuwaheshimu wanawake na hata mama yake, lakini hakuwateua kuwa mitume wake. Hata sisi tunafuata hivyohivyo. Upadre ni huduma siyo cheo," alisema Kilaini.

Padri Jovin Bakekela wa Kanisa Katoliki Parokia ya Makuburi, Dar es Salaam, aliwakosoa wanaharakati hao akisema wamejitenga wenyewe ndani ya kanisa.

"Sheria za kanisa haziwatengi wanawake, hata wakati wa Pasaka, wanawake hupewa nafasi kubwa, lakini hawateuliwi katika daraja la upadri," alisema

"Utume umegawanyika katika nafasi nyingi; kuna walei, kuna sisters, kuna fathers, hayo yote huwezi kuyachanganya. Kuwa padri siyo kupanda cheo, hata waumini nao wana utumishi, kwa hiyo wanawake nao wana utumishi wao. Upadre wa kuteuliwa ni daraja kama vile Yesu alivyoteua wanafunzi wake 12, siyo kwamba hakuwaona kina Mariam Magdalena au Suzana."Chanzo:Mwananchi

 
Upadre ni huduma si cheo hata Yesu hakuteua mitume wanawake ingawa aliwaheshimu ,utumishi si upadre tu.......safi Kilaini...
 
Back
Top Bottom