Hi, tunatoa huduma na msaada wa IT

OleSoft

Member
Jan 21, 2020
24
19
Huduma zetu ni kama: Hotel Management System, School Management System, Hospital na Radio Stream Hosting.
Pia tunatoa msaada wa IT

Kwakuwa sisi ni wageni hapa, tunaomba sapoti yenu wanaJ

Tupo Dar es salaam & Mwanza
Contact: 0783652386
E-mail: ramasie@oledoinyo.com
Au
ramasie40@gmail.com
OleSotf%20Logo.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1: unapofungua Example Domain na password yako ni abc900 mdukuaji ataiona kama ilivyo hivyo yaani abc900 hii ni kwakuwa site hiyo haipo salama.

2: unapofungua Example Domain na password yako ni abc900 mdukuaji ataiona password hiyo ikiwa kama hivi 12@&$;"+$/!$+( kwahiyo atashindwa kukudukua kwasababu password yako halisi hajafanikiwa kuiona.

Ni muhimu sana kutumia site ikiwa secure : http kirefu chake ni Hypertext Transfer Protocol na hutumia Port 80 hii ni njia inayotumika kuita website kutoka kwenye server, yaani mfano unahitaji maji kutoka MTUWASA au IRUWASA, DAWASCO/DAWASA (mfano) utahitaji bomba la maji ili kuweza kuyapata maji hayo.

Baada ya kupata maji ambayo yanapita kwenye bomba ambapo kwenye web au internet ni (http) yaani Hypertext Transfer Protocol : utahitaji kufunga bomba kwa kisanduku na kufuri ili kulinda maji watu wasije jichotea/kuiba. Kitendo hicho kwenye website inakuwa (https) yaani Hypertext Transfer Protocol Secure - ambayo inatumia port 443. Nitaeleza kwa upana zaidi kuhusu Port 80 & 443 ! Kama unaswali uliza. Pia tunatoa huduma za Radio Stream - Podcast na msaada wa IT.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachofunga na kufanya data zisiweze kuibiwa ni kipi?

Na kifungo hicho kinawekwaje?
 
Kifungo chake ni SSL CERTIFICATE : hii tunaita Secure Sockets Layer. Ambayo baada ya kuinstall kwenye web, itakupa security kutoka http protocal kwenda https protocal.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa, SSL certificate, lakini SSL certificate inafanya kazi vipi? Inawezaje kuzuia mtu asione data zilizofungwa?

Umetaja teknolojia inayotumika tu, hujaelezea inafanya kazi vipi.
 
Kwa kifupi:
unapoinstall SSL kwenye website yako:
: User anapoingia type website yako kwenye browser, browser itafanya connection na server
: server itatuma ile copy ya SSL ambayo umeinstall kwenye website yako ikiambataba na server's public key kwenda kwa browser
: browser itakagua, na ikiridhika na hiyo SSL, browser itafanya encryption na kurudisha kitu kinaitwa session key kupitia ile server's public key
: baada ya kurudi, hapo server ita dencrypt hiyo session key kupitia server's private key - na kuanza kuencrypt data zote (session key)
: Mwisho-server na browser zitafanya kazi moja tu ya kuecrypt sesseion key, na hapo itakuwa tayari kwa matumizi na salama kwa users.

N.B kitendo hiko hufanyika kwaharaka sana bila wewe kuona au kujua. Nimeeleza kwa ufupi, maana Tukianza kuichambua kiundani jinsi SSL inavyofanya kazi ni darasa kabisa pale St.Joe ! (SSL inagenerate keys tatu, ambazo ni private key, session key na public key) Kama nitakuwa nimebugi mahali usisite kunieleza, ili niongeze ujuzi na watu wengine wajue zaidi.
Ahsante.

Unaenda sawa, tunamenya kitunguu, ukimenya kitunguu kuna magamba ya nje yale unayatoa, na kila unavyomenya unakutana na magamba mengine ya ndani mpaka unafika ndani kabisa.

Mpaka hapo uko sawa kwa ninavyojua, ila hujaeleza hiyo public/private key encryption yenyewe inafanya kazi vipi? Kitu cha msingi kabisa kinachoiwezesha kufanya kazi bila kuhatarisha data ni kipi? Na kitu kinachoogopwa kabisa katika dunia ya sasa kinachoweza kuhatarisha encryption hiyo ni kipi?

Unaweza kuona naleta ubishi, lakini ukielewa haya ya msingi ni vizuri sana. Nilikutana na maswali haya kwenye interview miaka kama 14 iliyopita hapo Morgan Stanley, Manhattan.

Kwa style hii hii ya kumenya kitunguu, yani unamjibu mtu sawa, halafu ukimjibu sawa anakupeleka level ya kina zaidi, mpaka ajue ujuzi wako unaishia wapi.
 
safi, nimekupata - narudia kusoma tena swali lako ! Hii ni muhimu, nimekubaliana na wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom