Kila ripoti ukiikubali bila kujiuliza na usipokuwa mkali tangu mwanzo, utadanganywa tu

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,637
1,863
Nakumbuka enzi za JK mtu mmoja aliweza ku-attend seminars tatu kwa siku. Na wengine walikaa chini ya mti kuandika report ya uongo. Haya niliyashuhudia mwenyewe kwa macho yangu na wala simsingizii mtu.

Kuna hospitali moja hapo Dar iliingia ubia wa matibabu na taasisi fulani kilichokuwa kinafanyika ni aibu tupu. Yani check zinaandikwa tatu (hela ya kituo, hela ya mwenye kituo, hela ya bosi wa taasisi hiyo ya umma).

Kiongozi Huwa watu wanamsoma mapema ni mtu wa aina gani. Je, anapenda umbea? Je, anafanyia kazi mambo ya mtandaoni? Je, ni mpole au mkali? Utawala wake ni wa aina gani? Je, ni mtu wakufuata diplomacia au ana element za dikteta.

Ripoti nyingi zinaandikwa kukingana na namna wanavyomuona kiongozi mkuu. Kiongozi anatakiwa awe na intelligensia yake. Hapo ndipo ripoti zitakuwa za ukweli.

Mtanzania wa asili anaitaji kutawaliwa na mtu mwenye element mbili yani dikteta lakini pia na diplomatic.

Nimeshangaa namna traffic walivyoanza kuomba rushwa bila uoga. Huyu ndiye mtanzania wa asili.

Nikiri kuwa watu waliyomchukia hayati Magufuli ni politicians na wafanyabiashara. Kama kuna mwananchi alimchukia Hayati JPM ni kwa sababu ya propaganda za wafanyabiashara na wanasiasa au chuki za mtu binafsi. Labda Hayati JPM alikosa diplomatic language kwa hao niliyowataja hapo juu.

Yani combine both diplomatic and dictatorship kumtawala Mwafrika hasa Mtanzania. Ukionekana wewe ni pure diplomatic utaliwa na tutarudi enzi zile za unanijua mimi? Njoo kesho, toa kidogo, bado mchakato, mtandao unasumbua n.k
 
SSH anakuambia Traffic police wasitoe fines wataishia kuchukua rushwa tu wasipotoa fines, au anategemea police wataanza kumkumbusha dereva sheria za barabarani, tuna Rais asiyejua kabisa reality ya mtaani.
 
SSH anakuambia Traffic police wasitoe fines wataishia kuchukua rushwa tu wasipotoa fines, au anategemea police wataanza kumkumbusha dereva sheria za barabarani, tuna Rais asiyejua kabisa reality ya mtaani.
Alisema yeye na Hayati ni kitu kimoja. Sasa anatakiwa katika ukali wa JPM achangaye upole kidogo sana.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom