Kila nikikumbuka mabaya niliyotendewa adrenaline inapanda

The Mongolian Savage

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
6,191
13,614
Mzuqa wanajamvi

Hii hali hata sasa hivi imenitokea. Yaani nikivuta kumbukumbu ya mabaya niliyofanyiwa zamani na sasa hivi nashikwa na hasira mbaya sana. Moyo unaenda kasi nashindwa hata kupata usingizi.

Usaliti, uonevu, dhuluma na kusingiziwa. Hivi vitu vinaniuma sana. Unakuta adrenaline inapanda vibaya sana nakujikuta unawaza mabaya tu kulipiza kisasi ila baadaye ikishuka unajikuta umepoa. Ila sasa kila mara hizi kumbukumbu zinajirudiaga kila siku.

Hapa ndio Mwenyezi Mungu anahitajika sana. Kuna binadamu ni waonevu sana yani nikikumbuka. Watu hawajui duniani tunapita tu.
 
kuna wakati unasamehe na kusonga mbele bila kujali changamoto na mikingamo mbali mbali unayokabiliana nayo kwenye maisha.
 
Ni matumizi mabaya ya akili kushinda kutwa unatafakari mabaya yaliyopita.Unaacha kuitumia akili kuwaza ya mbele umekalia kuwaza ya nyuma
 
kuna wakati unasamehe na kusonga mbele bila kujali changamoto na mikingamo mbali mbali unayokabiliana nayo kwenye maisha.
Ila hata ukisamehe kuna haya maumivu ya ndani ndani. Hakuna kitu kibaya kama emotional torture. Ningekuwa na ungonjwa wa presha sijui afya yangu ingekuwaje. Sometimes i develop hate to some kind of people
 
hiyo hali hata mimi ninayo, najaribu kuiondoa lakini inashindikana, unasamehe lakini kusahau inashindikana, huu ni dalili ya ugonjwa wa PTSD ( Post Trauma Stress Disorder) , ni ugonjwa mbaya sana wa kisaikolojia, eeh mungu saidia niipite hii hali.
 
Back
Top Bottom