live on
JF-Expert Member
- Dec 30, 2018
- 790
- 1,264
Nimefungua biashara mwezi wa tisa nikaona ni bora niende TRA ili nifanye biashara kwa kufuata sheria za nchi na nilipe kodi.
Kutokana na biashara yangu nikakadiriwa kodi laki moja na hamsini kwa mwaka; sikuwa na shida na hilo.
Lakini kitu kilichonishangaza baada ya kuprintiwa makaratasi yangu ya makadirio nikaambiwa hiyo laki na hamsini inatakiwa niilipe kabla ya tarehe 31 December
Nikamwambie yule dada biashara nimeanza mwezi huu wa tisa na hizi kodi naona hapa mmezigawanya katika robo 4 mimi inanihusu hi robo ya mwisho sasa kwa nini nilipie na hizo robo 3 kipindi ambacho biashara haikuwepo?
Yule dada akaniambia system ndio imesetiwa hivyo haijalishi biashara umeanza lini unatakiwa ulipe kodi yote ya mwaka mzima
Naomba TRA mnijibu maswali mzima?
1) Nani aliyeiseti hiyo system ya kuwaibia walipa kodi ni kwamba elimu yake ndogo au alifanya kusudi ili kutukomoa tunaotaka kulipa kodi kwa hiyari?
2) Kwa elimu yangu ndogo niliyo nayo kodi inalipwa baada ya kufanya biashara na kupata income sasa iweje mnadai kodi katika kipindi ambacho biashara haikuwepo?
3) mmenikadiria income yangu ni laki tano kwa mwaka ambayo kodi yake ndiyo hiyo laki na hamsini sasa iweje income nitakayo ipata kwa miezi 4 muichaji kodi ya mwaka mzima?
4) Haya mahesabu ya kodi mnayo yafanya ndivyo mlivyo fundishwa huko chuoni kwenu pale kijitonyama au mnatoa kichwani kwenu ili kuwa vunja moyo walipa kodi?