Kila nikiangalia bajeti ya ndoa nafikiri mara mbili mbili...

Mimi nitoe uzoefu wangu, nilifanya harusi yangu na niliiandaa kwa mwezi mmoja na nusu. Hata mimi initially nilikuwa naogopa hivihivi. Nilikuwa nimepanga kuandaa harusi ya 8mill lakini nikachangisha hela ikafikia 4mill, hivyo bajeti hii ya 4m iliniwezesha kufanya harusi DSM magari ya maharusi, na wazazi rafiki alijitolea yalikuwa magari 3. Mengine yalitoka ndani ya hiihii m4.
Matokeo yake nilitumia hii bajeti na nikabakiwa na salio ya laki5. Mimi mwenyewe nilishangaa.
Lakini haya yote yanawezekana ikiwa kamati ipo committed na haipendi anasa.
Wife na matron pamoja na saloon na mades walitumia laki4, mimi na best man tulitumia lak6, wazazi niliwambia wajitegemee coz hata mchango wao niliwatolea. Kwa hiyo waweza ona ukijumlisha zote hizo utapata almost 8m kwa kila kitu. Make it simple and don't complicate. Oa usiogope gharama wewe ndo unaamua harusi iweje.
 
Kama unataka kuoa lazima bi harusi afanyiwe harusi, kama hauna pesa wala usijitie aibu.

No, dont judge a book on top of its cover. Yeye ameeleza hali halisi nandivyo ilivyo. Cha kufaa ni kumshauri aanzie wap tena amwambiej mchumba wake kuwa harus ya garama sio ishu
 
Namshukuru Mungu nimewahi kushuhudia Harusi za mamilioni mengi kama 13 na 10 hivi lakini tabgu nije Dodoma nimeamini Mungu hakutaka nife kihoro ameniponya kwa hili na kuniokoa na maghalama ya kuwalisha Waswahili walafi, maana nilishuhudia harusi ya mfanyakazi mwenzetu haikuzidi 2.5m na pia nyingine nyingi church hazizidi hata 1m. Kweli dar walafi sana
 
Ndugu zanguni ila usipofanya sherehe ndugu wanalawama sana,ukizingatia sisi tunakotoka mikoa ya kaskazini, ni kama laana vile, ukoo mzima unaweza hata kukutenga na huyo mkeo maana hawatawatambueni, chenchede nae anakuwa kama hasomeki kabisa..mawazo tu wakuu, woga wangu unasimamia katika mchanganuo uliotolewa na mrembo by nature hapo juu, ambao ni ukweli kabisa na haupingiki...huu utaratibu uliopo kwa sasa ni kutiana umaskini tu wakuu..
 
kwa wanawake ndoa ni fantasy...the way they think about weddings is different to the way men do...men just want that day to come n go and go back to your hotel room and bang ur wife...bt for women its all about THE DAY..aamke aende salon mara hiki mara avalishwe make up sijui hiki na kile...aaphhhuwwww
 
Pia kuna wanakamati wengine wapiga dili kweli, hawarudishi chenji alafu wana tabia ya kudouble bei za vitu au kuweka cha juu. Mimi nakumbuka nilifanya harusi yangu kwa pesa yangu mwenyewe. Nililipa ukumbi laki 2usafiri wa kutoa wazee kijijini na kuwarudisha pamoja na malazi dar kama laki 3, msosi pamoja na vinywaji kwa washkaji na wanandugu haikufika milioni. Kwa majumuisho haikuzidi 2.5 m.
Ila Mungu mkubwa nilipata zawadi na pesa vyenye thamani kama ya 6-8 m.sikumbuki vizuri maana ni miaka 9 iliyopita.

Kwa hiyo kaka, wewe andaa pesa yako kidogo ya kulisha ndugu wa pande zote, na ka ukumbi flani hivyi na pesa ya kupiga picha. baasi umemaliza. Usitegemee michango kabisa utakua kichaa hapa mjini kwa mawazo na pia utagombana na watu wengi sana, mimi mwenyewe nina card zaidi ya 20 hapa ofisini lakini nishaapa sichangii harusi ng'o, labda msiba.
 
mkaliwakitaa .....wala usiogope na huyo mpenzio asikutishe. cha muhimu ni ukae chini uongee naye umuelimishe kuwa harusi kuuubwa haina maana kitu kidogo na intimate ndo the best thing kwa nyie wote. (nisamehe kwa kuchanganya lugha kiswanglish kimezidi hehehehe)

sasa basi kitu ambacho unaweza mpagawisha nacho ni gauni lake get her the nicest gown that she has been dreaming of. halafu ikija kwenye ku-cut costs muangalie guest list yenu maana wageni wengi ndo huwa wanafanya gharama kuongezeka. mnatengengeza list kulingana na marafiki mlio nao common, halafu mnachanganua ndugu zenu wote lakini pia mind you si kila ndugu has to be invited hapa ni only the closest ndugu ambao unawasiliana nao mara kwa mara. sio kwa sababu ni mtoto wa mjomba ambaye anaishi wapi sijui na wala hamuwasiliani ndo uanze kumuweka kweye list. hivyo hivyo pia kwa wafanyakazi wenzenu kama mnafanya kazi. sio kila mfanyakazi mwenzako wa kumualika kuna wale ambao uko nao karibu zaidi let's say mnaofanya idara moja.

hiyo list itakupa estimates za gharama zote kuazia chakula, vinywaji, ukumbi, etc etc. it is very simple kama mtakuwa mnaandaa wenyewe, you take part in every stage na si kuachia kamati tuu. na kama ni michango hao wageni mtakaokuwa mmeorodhesha mkiwaomba watawachangia tena bial hiyana.
 
Last edited by a moderator:

very many thanks to you JS!! this is the best solution for me sofar..ubarikiwe ...
 
  • Thanks
Reactions: JS
Juzi jumamosi, nimetoka kufanya harusi ya ndugu yangu mpendwa, nilikuwa mmoja wa wanakamati, na wedding hiyo japo ilikuwa ya kawaida tu hesabu zake kwa haraka zilikuwa 25m hivi.

Kila nikiwaza hiii bajeti ya harusi na nyingine zilizopita, naona ts wastage of money kwakweli na nachelea kuoa maana kila nikimchimba kichenchede changu utasikia mimi, n my wedding nataka hiki na kile na kile...kichwa kinaniuma..Nikiwaza kuhusu ndugu..lazima watanilaumu nikioa bila kufanya sherehe kubwa..jamani kwani kufanya sherehe kubwa ya ndoa ni lazima?? Kwanini tusiwekeze katika miradi fedha kama hizi na kupunga anasa?? My thought..

Kaa na mtarajiwa wako na then mpange bajeti ambayo iko ndani ya uwezo wenu. Msiige watu, mtaumia na pengine kuishia kukopa ili mlishe na kufurahisha watu, halafu baadaye mje kuishi kwa maisha ya shida na kulipa madeni yasiyo na tija.

Nimeona na kushirikia harusi nyingi sana, nimehudhuria ya kuanzia milioni mbili mpaka ya milioni 40! Lakini hakuna jipya ndugu yangu, kikubwa ni kukabidhiwa mpenzi wako kihalali, mbele ya mashahidi. Mshauri mwenzio aache tamaa.

Tafakari!
 
....Katika hali ya kawaida kabisa, kama wewe ni mwanaume na unataka kuoa, ASEEEE JIANDAE KWA MAMBO HAYA:

1. Kujitambulisha ukweni. Hapo utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo mtarajiwa ukajitambulishe huko. Kama mfano mkeo anatokea "TABORA", na mnaishi Dar, andaa nauli ya watu wawili, malazi kwa siku mbili, na utagharamia shuhuli hiyo ya utambulisho. We tenga 500,000. Hapo tuna assume mkeo atajitegemea. Otherwise 800,000 itakutoka.
2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie nyumbani ni MOSHI utatakiwa umpeleke huko "Uru-Kimanganuni". Sio umlete hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio kwenu! Andaa nauli yako na atakaekusindikiza, nauli ya binti na mwenzie, na gharama za vinywaji na chakula siku hiyo. Utahitaji kama 700,000
3. Kifuatacho ITV ni kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane (Ba Mkwe, Ma Mkwe, Ba Ubatizo, Ma Ubatizo, Mjomba, Shangazi, Kaka mtu na Dada mtu) kutoka Tabora uwalete Moshi. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We acha ubishi, tenga 800,000 tu.
4. Kwani we wazazi wako wanajua unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda TABORA! Watu watano. Utahitaji kuwa na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna imejensi.
5. MAHARI ndio topic tatanishi inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye hiyo safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe 2,000,000.
6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua ya kawaida kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete unaweza ita marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe kabisa. Mi simo
7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi. Tengeneza kadi za mwaliko wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza gharama zote ni juu yako. Andaa 500,000. Swali la kwanza kwenye kikao: "We una shing ngapi?" Sema 1,000,000.
8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu kuna cheka time)
9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa bana!!
10. "Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?" 300,000!
11. "Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send…" 400,000!
12. "Baby, rafiki yangu Maimartha alinunua gauni la harusi China yani lilimpendezajee" 700,000!
13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000 maana utalia lia sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala hutarudishiwa.
14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda mwenyewe? Ndugu wawili watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off utatakiwa kutoa sijui blanketi la bibi, vitenge vya mashangazi, na vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000 uende navyo ili kupunguza gharama. Beba 200,000 za wale mashangazi watakaoibuka ghafla!
15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.
16. Fotokopi hiyo hapo juu (namba 15) kwa wazazi wako. 150,000
17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.
18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji kama 500,000
19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000
20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa wakapambwe saluni. 200,000
21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele na black kibishi 40,000
22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo, so utalipa malazi ya siku mbili 200,000
23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini ya 800,000 kwa angalau siku 3.
24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae hakuchanga anakupigia simu "Mangi eeeeh, Sasa tunavunja lini kamati?" Pesa yote iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja kamati ni za nani?? 500,000!
25. SASA MNAANZA MAISHA YA UNYUMBA. 14,180,000 poorer.ASEEEEEE, YAANI UKIYAFIKIRIA HAYA, NDO YANAPOKUJA YALE YA "Brey Ehhh, we yako lini bana???" NAYE ANAWAJIBU "Aseee, mi bado nipo nipo kwanza"!!

​Hii imekaa vema. Kwa idhini yako naomba niitumie katika shughuli zangu za kila siku.
 
Juzi jumamosi, nimetoka kufanya harusi ya ndugu yangu mpendwa, nilikuwa mmoja wa wanakamati, na wedding hiyo japo ilikuwa ya kawaida tu hesabu zake kwa haraka zilikuwa 25m hivi.

Kila nikiwaza hiii bajeti ya harusi na nyingine zilizopita, naona ts wastage of money kwakweli na nachelea kuoa maana kila nikimchimba kichenchede changu utasikia mimi, n my wedding nataka hiki na kile na kile...kichwa kinaniuma..Nikiwaza kuhusu ndugu..lazima watanilaumu nikioa bila kufanya sherehe kubwa..jamani kwani kufanya sherehe kubwa ya ndoa ni lazima?? Kwanini tusiwekeze katika miradi fedha kama hizi na kupunga anasa?? My thought..

...Si unawajua baadhi ya Wabongo wanavyotaka show off ya mavitu makubwa? kuchangisha michango chungu nzima ya harusi ambayo inaunguzwa kwa siku moja au mbili tu kwa sherehe kubwa sana kisha maharusi wanaenda kuanzia maisha katika chumba kimoja cha kupanga si ajabu hawana hata furniture za kuanzia maisha au kama wanazo ni choka ile mbaya!!! Harusi yao ilifana sana na walipendeza ile mbaya....Shilingi milioni 15 zimeungua kwa usiku mmoja....maharusi wako nyumba ya kupanga ndani ya chumba kimoja....Fikiria kama ingefanywa sherehe ya harusi labda ya milioni moja tu halafu milioni 14 wakapewa wote wawili ili kuanzia maisha!!!! Tuamke Wabongo!!!!! na kuachana na show offs ambazo hazina tija katika maisha yetu ya kila siku.
 
Sioi leo, Sioi kesho, wala Mtondogooo,
Sioi mchana, sioi usiku, wala Majogoo,
-FA
 
Ukiishi kwa niaba ya ndugu,marafiki n.k hayo ndo matatizo yake,kwanini usiishi vile unavyotaka wewe?
 
nimefanya harusi mwezi mmoja uliopita tena mkoani ilikula 20 MIL.alafu ilikuwa ya kawaida tu.muhimu jaribu kuwashirikisha ndugu,jamaa na marafiki watakupiga tafu wala usihofu.muhimu panga badget itakyoendana na watu na uwezo wako pia.

Usikate tamaa na wala usirudi nyuma.
 
Juzi jumamosi, nimetoka kufanya harusi ya ndugu yangu mpendwa, nilikuwa mmoja wa wanakamati, na wedding hiyo japo ilikuwa ya kawaida tu hesabu zake kwa haraka zilikuwa 25m hivi.

Kila nikiwaza hiii bajeti ya harusi na nyingine zilizopita, naona ts wastage of money kwakweli na nachelea kuoa maana kila nikimchimba kichenchede changu utasikia mimi, n my wedding nataka hiki na kile na kile...kichwa kinaniuma..Nikiwaza kuhusu ndugu..lazima watanilaumu nikioa bila kufanya sherehe kubwa..jamani kwani kufanya sherehe kubwa ya ndoa ni lazima?? Kwanini tusiwekeze katika miradi fedha kama hizi na kupunga anasa?? My thought..

Really hii fasheni inatuumiza sana.
Sijui nani kaanzisha hii, sasa hivi hadi vijijini kuna kadi.
Njia ya pekee ni kujiangalia wewe ni nani BASI.
 
Kaa na mtarajiwa wako na then mpange bajeti ambayo iko ndani ya uwezo wenu. Msiige watu, mtaumia na pengine kuishia kukopa ili mlishe na kufurahisha watu, halafu baadaye mje kuishi kwa maisha ya shida na kulipa madeni yasiyo na tija.

Nimeona na kushirikia harusi nyingi sana, nimehudhuria ya kuanzia milioni mbili mpaka ya milioni 40! Lakini hakuna jipya ndugu yangu, kikubwa ni kukabidhiwa mpenzi wako kihalali, mbele ya mashahidi. Mshauri mwenzio aache tamaa.

Tafakari!good advice... sijui ni sifa au ndo huo umagharibi..itegemee na urefu wa kamba vinginevyo hapana
 
Back
Top Bottom