Kila nikiangalia bajeti ya ndoa nafikiri mara mbili mbili... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kila nikiangalia bajeti ya ndoa nafikiri mara mbili mbili...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by stroke, May 21, 2012.

 1. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,394
  Likes Received: 6,578
  Trophy Points: 280
  Juzi jumamosi, nimetoka kufanya harusi ya ndugu yangu mpendwa, nilikuwa mmoja wa wanakamati, na wedding hiyo japo ilikuwa ya kawaida tu hesabu zake kwa haraka zilikuwa 25m hivi.

  Kila nikiwaza hiii bajeti ya harusi na nyingine zilizopita, naona ts wastage of money kwakweli na nachelea kuoa maana kila nikimchimba kichenchede changu utasikia mimi, n my wedding nataka hiki na kile na kile...kichwa kinaniuma..Nikiwaza kuhusu ndugu..lazima watanilaumu nikioa bila kufanya sherehe kubwa..jamani kwani kufanya sherehe kubwa ya ndoa ni lazima?? Kwanini tusiwekeze katika miradi fedha kama hizi na kupunga anasa?? My thought..
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mwambie kama anataka hivyo anavyotaka agharamie yeye. .

  Wewe uko tayari kulipia pete ya ndoa na uchumba, plus pilau na vinywaji vya wanafamilia. Kama hivyo havitoshi agharamie mwenyewe au asubirie tu mpaka azeeke ndo aje kuolewa.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  u can say that again...
   
 4. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  njoo kwangu,sihitaji watu zaidi ya gauni la harusi....:yawn:
   
 5. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kama unataka kuoa lazima bi harusi afanyiwe harusi, kama hauna pesa wala usijitie aibu.
   
 6. a

  assuredly4 JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 1,215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  shida kubwa ni aina za vinywaji. kama ulipitia vizuri bajeti ya ndoa utaona ilimezwa na Bia. ukitaka kupunguza gharama wambie harusi yako hutaki ndoa. usiwambie mapema subiri wachangie kisha mwishoni waambie haitakuwa na pombe

  pili fupisha muda wa sherehe kila mtu muwekee soda tatu na maji 2

  mm harusi yangu iligharimu kati ya sh.2.8mn -3mn na ilikuwa nzuri usipime kila mtu alishangaa
   
 7. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2012
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mmh, wewe ukiwa bwana harusi, ulishuhudua watu wakishangaa juu ya harusi yako,... au walikupaka mafuta kwa mgongo ya chupa?
   
 8. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,335
  Likes Received: 2,659
  Trophy Points: 280
  fanya ndoa simple tu mkuu maneno ya ndugu wala yasikusumbue, anayetambua ndoa ni Mungu na ndiye aliyetoa agizo hii habari ya sherehe sometimes ni ulafi wetu tu waswahili...mara nyingi utakuta watu wanajisemesha "harusi ya fulani chakula kilikua kidogo utadhani hatukuchanga, kwanza kuku walikaukiana...!"
   
 9. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  :lol::lol::lol::lol:
   
 10. Pianist

  Pianist JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Tatizo watu wengi hasa wanawake(wanaotarajia kuolewa) hufikiri ndoa ni ile sherehe(harusi). Ndoa sio kitu cha siku moja, ndoa inajumuisha vile wanaooana watakavyoishi baada ya kuwa pamoja. Sidhani kama kuna haja ya kuchangisha watu na kutumia gharama kubwa kwa ajili ya siku moja tu.
  Pia hii ni kama fasheni ambayo mara nyingi huwezi kuizuia, nadhani siku moja tutazinduka na kuanza kuchangishana kwa ajili ya elimu badala ya harusi
   
 11. Binti Magufuli

  Binti Magufuli JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 7,460
  Likes Received: 763
  Trophy Points: 280
  ....Katika hali ya kawaida kabisa, kama wewe ni mwanaume na unataka kuoa, ASEEEE JIANDAE KWA MAMBO HAYA:

  1. Kujitambulisha ukweni. Hapo utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo mtarajiwa ukajitambulishe huko. Kama mfano mkeo anatokea "TABORA", na mnaishi Dar, andaa nauli ya watu wawili, malazi kwa siku mbili, na utagharamia shuhuli hiyo ya utambulisho. We tenga 500,000. Hapo tuna assume mkeo atajitegemea. Otherwise 800,000 itakutoka.
  2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie nyumbani ni MOSHI utatakiwa umpeleke huko "Uru-Kimanganuni". Sio umlete hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio kwenu! Andaa nauli yako na atakaekusindikiza, nauli ya binti na mwenzie, na gharama za vinywaji na chakula siku hiyo. Utahitaji kama 700,000
  3. Kifuatacho ITV ni kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane (Ba Mkwe, Ma Mkwe, Ba Ubatizo, Ma Ubatizo, Mjomba, Shangazi, Kaka mtu na Dada mtu) kutoka Tabora uwalete Moshi. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We acha ubishi, tenga 800,000 tu.
  4. Kwani we wazazi wako wanajua unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda TABORA! Watu watano. Utahitaji kuwa na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna imejensi.
  5. MAHARI ndio topic tatanishi inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye hiyo safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe 2,000,000.
  6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua ya kawaida kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete unaweza ita marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe kabisa. Mi simo
  7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi. Tengeneza kadi za mwaliko wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza gharama zote ni juu yako. Andaa 500,000. Swali la kwanza kwenye kikao: "We una shing ngapi?" Sema 1,000,000.
  8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu kuna cheka time)
  9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa bana!!
  10. "Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?" 300,000!
  11. "Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send…" 400,000!
  12. "Baby, rafiki yangu Maimartha alinunua gauni la harusi China yani lilimpendezajee" 700,000!
  13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000 maana utalia lia sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala hutarudishiwa.
  14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda mwenyewe? Ndugu wawili watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off utatakiwa kutoa sijui blanketi la bibi, vitenge vya mashangazi, na vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000 uende navyo ili kupunguza gharama. Beba 200,000 za wale mashangazi watakaoibuka ghafla!
  15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.
  16. Fotokopi hiyo hapo juu (namba 15) kwa wazazi wako. 150,000
  17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.
  18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji kama 500,000
  19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000
  20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa wakapambwe saluni. 200,000
  21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele na black kibishi 40,000
  22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo, so utalipa malazi ya siku mbili 200,000
  23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini ya 800,000 kwa angalau siku 3.
  24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae hakuchanga anakupigia simu "Mangi eeeeh, Sasa tunavunja lini kamati?" Pesa yote iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja kamati ni za nani?? 500,000!
  25. SASA MNAANZA MAISHA YA UNYUMBA. 14,180,000 poorer.ASEEEEEE, YAANI UKIYAFIKIRIA HAYA, NDO YANAPOKUJA YALE YA "Brey Ehhh, we yako lini bana???" NAYE ANAWAJIBU "Aseee, mi bado nipo nipo kwanza"!!
   
 12. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135


  Ndowa ya mkeka ndio suluhisho!
   
 13. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Kwanini unamtatiza kijana? Hivyo kuna kipimo cha gharama ya ndowa? Cha muhimu kuweko maharusi na padri au kadhi na kama kuna utata Mkuu wa wilaya anatosha. Kwani Kabedi cha PRETA hakipo?
   
 14. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  sherehe kubwa ni masifa tu
   
 15. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Kwani ukioa bila gharama kubwa haitakua ndoa?mambo mengine ni kujitakia tu..ukitaka fanya kitu simple alika watu wachache,kusiwe na pombe..gharama itakua ndogo sana!
   
 16. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Haya matatizo tumeyataka wenyewe. Na kweni lazima kufanya harusi, kasema nani hiyo kitu.
   
 17. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2012
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,660
  Likes Received: 1,492
  Trophy Points: 280
  haya makitu hayana muda....yataisha yenyewe tu..watu warudi kwen basics....
   
 18. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  umetisha Mrembo by Nature...mm ntapita shortcut...au ntazima moto tu!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #19
  May 22, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,660
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  haya mambo ya harus ukisema unataka ufurahishe watu,unajikaanga mwenyewe..ndo yale yale,kwenye harus mtu anapanda li-mark X la kufa mtu then after haruc mnabanana kwenye magari ya mbagala na Tandika..ya nn yote hayo jaman.. Kutafutiana ubaya tu na watu..oooh hajanichangia,oooh subiri na yake si itakuja...
   
 20. K

  Kiganda Senior Member

  #20
  May 22, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Si vibaya kufanya sherehe kubwa ila pia tuangalie na mambo ya msingi. Utakuta mtu hata plot ya 20x20 hana lakini anapanga harusi ya mil.10.
   
Loading...