Kila niisikiapo sauti ya Mzee Mangula iliyojaa mamlaka na unyenyekevu nafarijika sana

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Katika miamba ya siasa, utawala na uongozi kwenye nchi hii sio rahisi kushindwa kutaja jina la mzee Philip Mangula, makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara. Ni moja ya watu ambao wameacha historia muhimu sana na ingewekwa kwenye vitabu ingefaa sana kwa vizazi vijavyo. Ikimpendeza aandike kitabu cha maisha yake ya kisiasa.

Kiufupi, nimekuwa nikimfuatilia na kufuatilia hotuba zake kwa kipindi kirefu sana. Tofauti na viongozi wengine, sauti anayoitoa huwa imejaa mamlaka na ya unyenyekevu mkubwa. Ni mtu ambaye anazungumza kwa uangalifu na kuchagua maneno ya kuzungumza tofauti na viongozi wa kileo.

Uongozi wake ni mfano wa kuigwa na uadilifu wake ni wa kiwango kisichotiliwa shaka. Amekitumikia chama cha mapinduzi ,serikali na taifa kwa heshima kubwa sana. Kama mkereketwa wa aina ya uongozi nafarijika mtu ninayemuamini kama Mwalimu wangu ana maadili mema ya kufuatwa.

Katika nyakati mbalimbali za giza Mzee Mangula amebaki kuwa nuru na sauti yake kuleta muafaka. Katika nyakati za mingongano wa mawazo na mtazamo juu ya masuala mbalimbali ,sauti ya Mzee Mangula ndio iliyohitajika.

Mwaka huu ndio mwaka wa uchaguzi ndani ya CCM, pengine atapumzika kutokana na kazi nzito za ujenzi wa chama chetu. Akiwa kakitumikia chama kwa heshima kubwa na anastaafu akiacha alama ya juu ya utumishi uliotukuka.

Swali litabaki kuwa: Sauti ya mamlaka ya Mzee Mangula ilihitajika sana kuleta muafaka, je itatoka wapi sauti kama hiyo? Sauti iliyosikika kama mwangwi kwa mafisadi? Yupo wapi Mzee Mangula mwingine? Atakuwa nani mwengine atakayeogopwa mpaka kufukia kunyweshwa sumu?

CCM bado inahitaji sauti yake iendelee kusikika ,sauti ya mamlaka kweli kweli.
 
Kazi za makamu mwenyekiti wa chama cha CCM ni zipi?
 
Natamani Mangula aendelee hata mwaka huu, maana sioni mbele bila yeye
 
Back
Top Bottom