Kila Mwenye Kamera Inabidi Kuwa Na Vitu Hivi 5

Ryan Herman

Member
Jul 26, 2019
42
46
Umepewa au umejipatia mwenyewe kamera yako (mpya) hongera!. Ukiwa na kamera yenye uwezo (mega pixels) mkubwa na ukiwa unapenda piga picha hapo kuna maisha flani hivi unayaishi na kupata uzoefu flani wa kuitwa mpiga picha (photographer).

Lakini kabla hujatoka na kuenda kuanza kupiga picha hizo inabidi kwanza uwe na vitu muhimu kwa ajili ya kamera yako.

Haya mambo yatafanya maisha yako kuwa rahisi na kuisadia kamera yako kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na mwisho wa siku inatakufanya kupiga picha nzuri zaidi.

1. Vifaa Vya Kusafishia
Sawa hii inaweza kuwa sio njia ya kutumia pesa zako ulizozipata kwa shida lakini tuamini sisi kuwa inafaa kununua vifaa hivi vya kusafishia kamera yako. Katika kamera, vumbi na alama za vidole vinaweza kusababisha uchafu mkubwa katika lensi.

Kwa kutumia vitambaa laini na maji maji spesho unaweza safisha kamera yako yote kwa ujumla. Ni rahisi kutoa vumbi na uchafu mwingne katika lensi na pande zingine.

Wapiga picha ambao huwa wanabadilisha lenzi mara kwa mara hii itawasaidia kuziwezesha ziwe safi na kupiga picha nzuri. (Kama unaona huwezi, usilazimishe peleka kwa mtaalamu akakusafishie kamera yako)

2. Kamba Bora Zaidi
Kamera kubwa nyingi huja na mikanda yake ya shingoni ndani ya boksi. Mikanda hii haiwagi mizuri sana na hata hivyo inakua inatangaza kampuni. Mara nyingi inakuwa na jina la kampuni lailiotengeneza kamera hiyo.

Mara nyingine inaamsha wezi na kujua moja kwa moja umebeba kamera gani mfano Nikon au Canon. Lakini kuna makampuni amabayo yanatengezea mikanda hiyo ukiachana na yale ya kamera. Wapiga picha wengi wanapenda kutumia mikanda ya ” BlackRapid straps” .

Mikanda hii ni mizuri na ukishavaa kamera yako shingoni lenzi ya kamera itaangalia chini, pia mikanda hii ina kazi mbali mbali tofauti na ile ya makampuni ya kamera.

3. Betri Za Hakiba
Hakiba haiozi! kamera nyingi za kidigitali zinakuja na betri. Ukiwa na betri la ziada ni vizuri zaidi kwa sababu unaweza hata ukaacha chaji yako nyumbani na kufurahia kupiga picha.

Hii inamaanisha utakua hauna haja ya kuangalia salio la chaji katika kamera yako kila saa. japokuwa mabetri ya makampuni mengine ni mengi inashauriwa kusoma mapitiao (review) kwa wanunuzi wengine ili kununua kitu bora. Betri la ziada ni lazima kununua kwa baadhi ya kamera


4. Tripod Ambayo Ni Imara
Tripod nzuri ni muhimu kwa kila mpiga picha na itadumu milele. Kwa kuwa ‘tripod’ zinatumika kwa kila aina ya kamera basi ni vizuuri kuwa nayo kwani ni uwekezaji mzuri. kuna picha zingine utataka piga kwa utulivu, bila kutikisika,, tripod imara itafanya ypte hayo.

Makampuni kama Manfrotto , Giottos, au hata Three Legged Thing yana tripod nzuri amabzo zinatoa mchango mkubwa katika kamera

5. Maarifa
Maarifa ni kitu muhimu sana na sio kitu cha kununua kama vingine. Sawa unaweza ukawa na vyote hapo juu, lakini ukikosa maarifa tuu hautakua mpiga picha nzuri.

Kama hujui kutumia kamera ya kidigitali au hujui mbinu tofauti tofauti za swala zima la upigaji picha (photography) ni bora ukang’ang’ania simu-janja au kisimu chako cha mchina. Kama unataka kutumia Kamera yako kwa 100% basi haina budi kufanya utafiti kwanza na hili halimaanishi inabidi urudi shule na kupata degree ya ‘photography’

Makampuni kama Lynda.com na KelbyOne yanajitolea katika kumfundisha yeyote anaetaka kujifunza kuhusu ‘photography’ kwa kupitia mtandao. Kama hutaki kutumia pesa zako pia unaweza kujiunga katika makundi mbali mbali mitaani yanayojihuusisha na kupiga picha na kupata maarifa flani hata kwa kuangalia video mtandaoni (youtube)

Photography ni moja kati ya vile vitu nnavyopendelea fanya sana. Ukifuatila hizo njia tano hapo juu zitakusaidia.
 
Mkuu Kwa Mie Beginner Photography nitumie au nianze na camera yenye sifa zipi,ili niweze kuzipata picha kama hizi??

makande_jr7-20190911-0002.jpg
 
Kaingia mitini..ila lilikua ni swali zuri sana ambalo lingefunza wengi
Binafsi sijui kitu
Nje ya Kamera bora na maarifa, utahitaji uwezo wa upapasaji uchakataji “Retouching Skills” na urudufu usanifishaji “Editing Skills”, pia mwanga akisi “Lighting” kuweza kupata picha yenye hadhi ya namna hiyo.
 
Back
Top Bottom