Kila mwanaume anaetangaza kuniowa namuacha

Miaka 23 tu?, tayari na mtoto unaye! inaonekana ulianza hili game zamani,vp..na baba wa huyo mtoto ulishamtupilia mbali? Au humjui? Ushauri wangu ni kwamba, muogope mungu! acha ufuska na utubu haraka sana!!!

Nlivyobikiriwa tu ndo nlipata mimba nkiwa na miaka 20.na wala me syo fuska kama usemavyo namuogopa mungu ndiyo maana nmeomba ushaur kwan nmeona njia nienday siyo salama
 
1. Wewe sio mgeni huku jamvini. Wageni wote wanabisha hodi
2. Wewe sio mchanga kwenye mambo ya mapenzi....kitendo cha kufikia una mtoto umefuzu kwenye mambo ya kikubwa...age aint nothing..
3. Una matatizo kisaikolojia...unahitaji kuonana na wataalamu wa saikolojia watakushauri vizuri endapo utakuwa mkweli na kuweka wazi matatizo yako....huenda unajiona wewe ni mzuri mno, ubinafsi au dharau na kutochukulia relationship serious issue.

Huna upendo wa kweli na wa dhati kwa hao wanaume unaobahatika kuwa nao. Unajenga uhusiano kwa maslahi tofauti au kwa sababu tuu basi mwanamke anatakiwa awe na boyfriend au mwanaume awe boyfriend kama fashion.

Baada ya kusema hayo basi ningependa kuchukua nafasi hii kukushauri kwamba chukulia wanaume wote ni sawa..usijali kipato, elimu au sura. Angalia busara na hekima za mtu na upendo wa dhati. Usichukulie mzaha mzaha inapofikia issue ya mahusiano. Badili mwenendo ondoa hisia hasi juu ya wanaume na utafanikiwa kuwa na uhusiano wa muda mrefu au hata wa maisha na mwanaume utakayempenda kwa dhati.

mankaa;
pole na yanayokukuta. Naomba uufanyie kazi ushauri huu uliopewa na mdau na utakusaidia sana ktk maisha yako. Kaa ukijua kwamba siku zote si jumapili, yaani kila kitu kina wkt wake. Acha tabia ya kuwa na mahusiano na wanaume wengi, jitahidi uwe na msimamo na ujue ni kitu gani unachohitaji kutoka kwa huyo mwanaume na je una malengo gani ya baadaye na hasa mtoto uliye naye.

Mankaa kumbuka ukimwi hauna hodi wala huruma na mimi huyo mtoto uliyenaye ndiyo ananiuma kuliko hayo maamuzi unayofanya ya ndani ya mwaka unakuwa na wanaume wengi na ni likely sasa unataka kubadilisha tena mwanaume.

Naomba nikupe siri moja kubwa ktk maisha na ukiweza kaongee pia na wana saikolojia nao watakuambia: Huwezi kufanya ngono hadi ukafikia hali ya kusema sasa nimetosheka na ngono, bali ni maamuzi tu kutoka ndani yako kutegemeana na malengo yako ya kimaisha. Acha uzinzi na kuwa na malengo na msimamo ktk maisha yako na ujue ni kitu gani unahitaji ktk maisha.

Ngoja nikuulize swali moja; vipi umewahi kwenda posta (dsm) na unapofika maeneo ya fire pale unakutana na watoto wengi sana wakiwa wamechakaa na ni ombaomba? Je umewahi kujiuliza kulikoni hawa watoto wako hapo na wako vile? Je walitokea wapi? Jaribu kujiuliza hilo swali, then utafanya maamuzi na kuwa na msimamo ktk maisha na kuachana na tamaa.

Mungu akusaidie ili uweze kuwa salama na hata mtoto wako afurahi kuwa na mama mwenye msimamo na si mama ambaye kila robo ya mwaka anamletea baba mwingine, kwani hata mtoto wako naye ataharibikiwa kwasababu watoto hujifunza zaidi kwa kuona na si kwa kuambiwa.
 
Mungu akubariki kwa ushauri ntaufanyia kazi..pia unikumbuke katika maombi
 
Wadau nisaidieni je naweza kuwa na tatizo su ni hali ya kawaida nachanganyikiwa kwani kunuacha.mtu mliekuwa mnapendana anaweza hata kuniloga au kubifanyia kitu kibaya pia nahisi namkosea hata mungu kwa kufanya hivi.

hujatoa taarifa za kutosha....................kwa nini huwataki lazima una sababu kwa nini umewachoka...................labda una siri fulani ambayo unaona ukiolewa na mmoja wao itafichuka......................naona una khofu ya jambo fulani....liafakari na dawa ya khofu nikufanya kitu unachohofia............
 
Sina ninachokihofia kwao kwan huwa nakuwa waz cna
 
Mungu anakupenda kukufarakanisha na wanaumme ili umrudie but huelewi.
unashangaza sana dada wewe uko chuo na katika age 23 una mtoto wa mtu ambaye hajakuoa,hujakoma huyo aliyekupa mimba?,au unataka mimba nyingine?

ushauri.
1.kapime Ukimwi kama huna achana kabisa na wanaume.
2.Fuata masomo achana na mambo ya wanaume,wanaume wapo tu hata ukimaliza chuo.kuwa na wanaume wengi wanakufuata siyo ndo uzuri.
 
Wasema una bahati ya kupendwa na wakaka wenye nia ya kukuoa co? Je yuko wapi baba wa mtoto au yy hukuwa na bahati naye...
Minadhani una matatzo coz huwez tu kuamua kumwacha mtu bila sababu yyte. Na pengne unawatumia tu.
 
Baba wa mtoto ananicare lkn pia simuhitaj
 
Khaa...shauri yako..crazy GK aliwahi kuimba akasema dunia hadaa lkn ulimwengu chuo kikuu
Hujisikii vby kila robo mwaka unalala na mwanaume mwngne. No wonder makuzi yko hayakuwa mazuri

Baba wa mtoto ananicare lkn pia simuhitaj
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom