Kila mwananchi lazima apake nyumba yake rangi - DC Kinondoni

Wanaacha mambo ya msingi kama usafi wanahangaika na mambo ya kipuuzi.

Vituo vya dart vichafu, madaraja watu wanakojoa na kutupa taka ovyo, zahanati hazina vyoo, mitaru unanuka uchafu kisha mtu anakuja eti pakeni rangi? Akiki za kuazima ni shida?
mwingine mkubwa wao amepiga marufuku shisha kumuunga mkono yule mdogo....

nchi hii jaiishi vituko
 
Jamani hivi mtu ambaye anaishi chini ya dola moja kwa siku anawezaje kupaka nyumba rangi ambayo amepewa ya urithi mathalani.
Wawe wanaomba ushauri kwanza kabla hawajatoa matamko yao.Huyo bwana aombe kampuni mbalimbali kama za simu wawasaidie hao wasiokua na uwezo maana mtu hawezi kuacha kununua kilo ya unga akanunua kopo la rangi
 
Waingie mkataba na airtel, safari lager au halotel wapake rangi na kupiga chata ya brand yao kwenye nyumba za raia wastahimivu wa kinondoni.
 
Vizuri sababu kuna nyumba ni chafu kuta zake hadi unasikia kinyaaa....
 
Nakumbuka nikiwa mdogo miaka ya 90 kijijini kwa bibi kule Mpui, kipindi hicho bado kuna elements kidogo za mfumo wa chama kimoja (japo tayari tulikuwa kwenye vyama vingi). Ilikuwa ukipita mwenge wa uhuru ni lazima msilibe upya vijumba vyenu na kuvipaka rangi na milangoni muandike maneno ya kukisifu chama na mwenge. Ole wako upuuze sasa.
 
Dah ujue izi ni siasa za mwendo kasi ila wajue mkuu ana wacheki tu mkizingu anatumbua ivi DAR ES SALAAM kuna changamoto ngapi za msingi adi mtuambie mambo ya kupaka rangi kwani nyumba tumejenga kwa gharama zetu nani aje kutupangia
 
Nilikua najiuliza sana kwanini humu jamvini kuna watu wanapinga kila kitu?? hata kiwe kizuri vp wao ni wapinzani tu yaani wanajua kila kitu aisee!! sasa nimeanza kujua sababu.
 
Watenge fungu kwa wananchi sasa. Maana kama hawakuwa na bajeti ya kupaka rangi,huwezi kuwalazimisha.
 
Wanaacha mambo ya msingi kama usafi wanahangaika na mambo ya kipuuzi.

Vituo vya dart vichafu, madaraja watu wanakojoa na kutupa taka ovyo, zahanati hazina vyoo, mitaru unanuka uchafu kisha mtu anakuja eti pakeni rangi? Akiki za kuazima ni shida?

Duh, ndugu kati ya watu waliochangia pumba wewe nimekuchagua namba moja,hivi suala la kutupa taka ovyo, kukojoa katika madaraa mitaro inanuka nayo yanahitaji mkono wa moja kwa moja wa serikali?

NINAVYOJUA Mimi masuala kama hayo kila mmoja anapaswa kuwajibika ipasavyo na sio kungoja serikali,inamaana wewe ukimwona mtu anakojoa nnje ya nyumba yako utakimbilia kwa mwenyekiti wa mtaa kwanza au utamkalipia na kumfukuza?

Je ukiona mtu anavunja kingo za barabara utakimbilia polisi kwanza au utamfukuza? Ndugu kuna baadhi ya vitu ni vema sisi kama jamii tukashiriki moja kwa moja na sio kuiachia serikali kwani serikali ni kikundi cha watu wachache walioaminiwa kwa ajili ya kuongoaza njia tu.
 
Mbona issue ya aina ya rangi za kupakwa, Nyumba inapopaswa kuelekezwa na mengine mengi mbona ni mambo muhimu kwenye mipango miji. Sasa mnaomlaumu Mkuu wa wilaya ni kwamba hamuelewi au ni kwa kuwa mmezoea kupinga kila kitu? Kama unaishi katikati ya mji na huna uwezo wa kuweka Nyumba yako vizuri basi uza uhamie makabe ukajenge Nyumba nzuri zaidi. Mnaharibu muonekano wa jiji
Kila Mtanzania ana haki ya kuishi popote (eneo halali kwa makazi) bila kujali jinsia yake kipato chake au rangi yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom