Kila mwananchi lazima apake nyumba yake rangi - DC Kinondoni

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,540
7,452
Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe. Ally Hapi, amesema kila mwananchi wa Kinondoni lazima apake rangi nyumba yake, na watakapoanza zoezi hilo hakuna mchezo mchezo.

Chanzo: EA Radio

NB: Mjiandae huko Kinondoni. Tena nilikuwa na mpango wa kufungua duka la kuuza rangi kwa Manyanya ngoja nifanye haraka.
 
Hio cwez kupinga kiukwel kwa sababu hio sheria pia ilipitishwa tanga.. Yan nyumba zote zilizokua zipo pemben ya barabara zilitakiwa zipakwe rangi. Na pia ilitakiwa kusiwe na kiwanja cha mtu kilicho pemben ya barabara alaf hakijajengwa.. So co suala baya sana.. Kwa mara ya kwanza labda naweza nikawaunga mkono wazee wa kukurupuka
 
Hio cwez kupinga kiukwel kwa sababu hio sheria pia ilipitishwa tanga.. Yan nyumba zote zilizokua zipo pemben ya barabara zilitakiwa zipakwe rangi. Na pia ilitakiwa kusiwe na kiwanja cha mtu kilicho pemben ya barabara alaf hakijajengwa.. So co suala baya sana.. Kwa mara ya kwanza labda naweza nikawaunga mkono wazee wa kukurupuka

na zile za makuti mitaa ya mkwakwani je?
 
Tatizo sio kupaka rangi kila mmoja angefurahi kuwa na nyumba nzuri yenye kuvutia lakini tatizo Ahadi ya Magu ya kushusha bei ya vifaa vya ujenzi haijatimia hivi fikiria MTU ana nyumba along the road hata Ripu haijapigwa miaka na miaka alafu Leo uje umwambie utamkamata na kumshtaki kisa hajapaka rangi kweli?? Tunakwenda wapi sasa!? Tuacheni vitisho tuangalie maisha ya watu kwa jicho la Tatu Dar hii kuna watu hata Milo mitatu hawapati na wanapojishikiza maisha yao ni kwenye banda la urithi la wazee wao Leo badara ya kumpunguzia mnamuongezea msiba
 
Mbona issue ya aina ya rangi za kupakwa, Nyumba inapopaswa kuelekezwa na mengine mengi mbona ni mambo muhimu kwenye mipango miji. Sasa mnaomlaumu Mkuu wa wilaya ni kwamba hamuelewi au ni kwa kuwa mmezoea kupinga kila kitu? Kama unaishi katikati ya mji na huna uwezo wa kuweka Nyumba yako vizuri basi uza uhamie makabe ukajenge Nyumba nzuri zaidi. Mnaharibu muonekano wa jiji
 
Wanaacha mambo ya msingi kama usafi wanahangaika na mambo ya kipuuzi.

Vituo vya dart vichafu, madaraja watu wanakojoa na kutupa taka ovyo, zahanati hazina vyoo, mitaru unanuka uchafu kisha mtu anakuja eti pakeni rangi? Akili za kuazima ni shida?
 
Ufipa boys wanahaha kupinga hili agizo kwa sababu wanajua ofisi yao ni chafu chafu
 
Hiki sio kituko huu ni utamaduni labda kwenu ni mgeni, huwezi kumiliki nyumba mjini halafu ikawa kama jalala, ni aibu na badala yake mnakuja hapa mnaandika nchi hii imekosa uongozi imara wa kusimamia majukumu.

Hili sio lifanywe kinondoni tuu, mji mzima na wale waliacha magofu katikati ya mji wapewe muda au warejeshe serikalini, kwa wenzetu walipitia vipindi vigumu sana lakini sahivi tukiwa nje tunapiga picha kila sehemu. yale yamekuja kkwa gharama na sio kuchukuliana poa tu.
 
Hivi issue ni rangi kweli??? Niliwahi kupanda ndege na mjerumani tukienda zenj alipoangalia chini akaniuliza "what are those?" Nikamjibu houses. Nilijua alishangaa mabati mekundu yaliyowekwa mawe, matairi, magogo na makochi mabovu.
 
Tanzania ya Magu, Dar ya makonda, kinondoni ya hapi: ukiangukia mikono hiyo yote unalo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom