Kila mwaka Madarasa yatakuwa yanajengwa mapya ku-accomadate Kidato cha kwanza?

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,472
8,692
Wakuu mliotembea huko Duniani wenzetu wanafanyaje? Maana yake huku kila mwaka mazingira ya Shule Madarasa huongezwa na huenda ikafika wakati eneo lote la shule likajaa Madarasa.

Hizi zima moto zina tija kweli?
 
Duniani vyama chakavu vilishaondolewa na kufutwa siku nyingi, hivyo wanaongozwa na watu wenye vision mpya.

Lowasa licha ya ufisadi wake ndio mastermind wa UDOM.

Sisi tuliisoma zamani kabla ya shule holela, shule zetu zilikuwa majengo ya ghorofa.

Nashangaa mpaka leo watu wanajenga maboma ya chini badala ya kujenga magorofa na kuacha matoleo juu.
 
Nchi zingine wamedhibiti uzazi sisi tunazaliana sana kila mwaka watoto wanaongezeka Ulaya na Marekani ni kinyume ndio maana wanatoa hadi Green Card kwa raia wa nchi zingine kwenda nchini kwao. Sisi kila hatua mbili lazima ukutane na watoto au mama mjamzito au mwenye mtoto mgongoni.

Usilaumu serikali
 
Nashangaa mpaka leo watu wanajenga maboma ya chini badala ya kujenga magorofa na kuacha matoleo juu.
Na wewe unashangaza, Ghorofa zinajengwa sehemu zenye uhaba wa ardhi sisi tuna ardhi tele ghorofa la nini kama sio ushamba tu.Mtu unakuta ana eneo la heka kumi halafu anajenga ghorofa ni ushamba uliopitiliza na ulimbukeni.

Teknolojia ya ujenzi wa magorofa ulianzishwa baada ya kuweko tatizo la ardhi mtu nafasi ndogo anataka kujenga nyumba nyingi.

Mtu unakuta kijijini ana heka hamsini kashusha ghorofa ushamba mzigo mzito.
 
Inaonekana wanafunzi wakiwaliza kidato cha kwanza, madarasa huwa wanaenda nayo majumbani mwao, ili watakaoanza yajengwe mapya.
 
Hadi leo tokea uhuru madarasa hayajakamilika kujengwa, hadi inafanyika kampeni ya kujenga madarasa? ni balaa..
 
Idadi ya wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne ni ndogo ukilinganisha na wanaotakiwa kuingia kidato cha kwanza. Ufaulu "unaongezeka"
 
Nchi zingine wamedhibiti uzazi sisi tunazaliana sana kila mwaka watoto wanaongezeka Ulaya na Marekani ni kinyume ndio maana wanatoa hadi Green Card kwa raia wa nchi zingine kwenda nchini kwao....
Hujajibu swali la mleta mada,...hii ndio shida yenu MATAGA.

Au unapingana na kauli ya mwenyekiti wenu anaepinga uzazi wa mpango?

Mleta mada anauliza, tutaendelea kuongeza madarasa kila disemba hadi lini?
 
Mimi naona serikali imefail kidogo katika hili Kwanini; ni wazi kabisa idadi ya wanafunzi wa s/m waliopo shuleni wanafahamika (kuna data kamili) hivyo tamisemi wanafaham wazi kabsa mwaka huu idadi itakuwaje na je madarasa tuliyonayo Nchi nzima yanaweza kuhimili watoto wote au la.

Hivyo no rahisi kwao kufanya maandalizi mapema na maboresho (kujenga madarasa kama kuna uhitaji). Hivyo suala la kusubiri hadi wanafunzi wajae ndo waanze kujenga huo ni ushamba na uzembe.
#jr
 
Miaka ya zamani darasa la saba wakimaliza kiwango cha wanaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza walikuwa wachache sana.

Pamoja na wanafunzi wengi kufaulu nafasi zilikuwa chache kwa kuwa tuliliwa na shule chache za secondary.

Baada ya kuongeza ufanisi wa kufundisha, kiwango cha ufaulu kimeongezeka na wanaofaulu wanachaguliwa kwenda shule bila kuwa na coordination ya utoshelevu wa madawati na vyumba vya madarasa.

Ipo siku tuta-stabilize; japo nchi hii tuna shida ya uratibu kwa wanaofaulu vs kule wanakopokelewa.

Ni kama sasa, wanafunzi wanakopeshwa fedha kusoma vyuo vikuu.

Je kuna taasisi inaratibu mara baada ya kuhitimu shahada wanaenda wapi ili kutumia akili na nguvu zao kuzalisha na wakati huo wanalipa marejesho ya mkopo wa Elimu.

Ni miaka 35 iliyopita mtu anaehitimu kidato cha nne bila kujali atafaulu vip, alipata kazi kama afisa wa serikali bila hata usaili.

Leo hata masters sio rahisi kupata kazi serikalini.
Private sector ukifika wanataka uzoefu. It a chaos now.

Unless tujenge mfumo jumuishi wa kuratibu mambo kati ya serikali na sekta binafisi; hapo ndio tutatoboa.

Ila tukifanya kazi kwa competition kila mmoja aonekane anafanya kazi bila kujali kule mbele itakuwaje; inakuwa mapema sana hata kabla hatujasheherekea miaka 60 ya uhuru; Rais (mst) JK hana suluhusho la kuwambia vijana wanaohitimu shahada za kwanza UDSM, nini wafanye.

Tutafika lakini kama tutasikilizana na kama kila mmoja hasa walio kwenye mamlaka watakuwa tayari kushirikiana na wengine hata wale walio nje ya "mifumo".
Sio kila suluhisho la Tanzania litatokea huko kwenye "mifumo" ila mifumo ina wajibu kuwa accommodate na wengine wewe sehemu ya suluhu.

Niliwahi kushauri kwa public forum, bado nina imani ushauri wangu uko relevant kwa yeyote alie kwenye mamlaka ya kuendesha "mifumo"
 
Wakuu mliotembea huko Duniani wenzetu wanafanyaje? Maana yake huku kila mwaka mazingira ya Shule madarasa huongezwa na huenda ikafika wakati eneo lote la shule likajaa Madarasa.

Hizi zima moto zina tija kweli?
Inatokana na agizo la kufyatua viumbe
 
Miaka ya zamani darasa la saba wakimaliza kiwango cha wanaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza walikuwa wachache sana.

Pamoja na wanafunzi wengi kufaulu nafasi zilikuwa chache kwa kuwa tuliliwa na shule chache za secondary.

Baada ya kuongeza ufanisi wa kufundisha, kiwango cha ufaulu kimeongezeka na wanaofaulu wanachaguliwa kwenda shule bila kuwa na coordination ya utoshelevu wa madawati na vyumba vya madarasa.

Ipo siku tuta-stabilize; japo nchi hii tuna shida ya uratibu kwa wanaofaulu vs kule wanakopokelewa.

Ni kama sasa, wanafunzi wanakopeshwa fedha kusoma vyuo vikuu.

Je kuna taasisi inaratibu mara baada ya kuhitimu shahada wanaenda wapi ili kutumia akili na nguvu zao kuzalisha na wakati huo wanalipa marejesho ya mkopo wa Elimu.

Ni miaka 35 iliyopita mtu anaehitimu kidato cha nne bila kujali atafaulu vip, alipata kazi kama afisa wa serikali bila hata usaili.

Leo hata masters sio rahisi kupata kazi serikalini.
Private sector ukifika wanataka uzoefu. It a chaos now.

Unless tujenge mfumo jumuishi wa kuratibu mambo kati ya serikali na sekta binafisi; hapo ndio tutatoboa.

Ila tukifanya kazi kwa competition kila mmoja aonekane anafanya kazi bila kujali kule mbele itakuwaje; inakuwa mapema sana hata kabla hatujasheherekea miaka 60 ya uhuru; Rais (mst) JK hana suluhusho la kuwambia vijana wanaohitimu shahada za kwanza UDSM, nini wafanye.

Tutafika lakini kama tutasikilizana na kama kila mmoja hasa walio kwenye mamlaka watakuwa tayari kushirikiana na wengine hata wale walio nje ya "mifumo".
Sio kila suluhisho la Tanzania litatokea huko kwenye "mifumo" ila mifumo ina wajibu kuwa accommodate na wengine wewe sehemu ya suluhu.

Niliwahi kushauri kwa public forum, bado nina imani ushauri wangu uko relevant kwa yeyote alie kwenye mamlaka ya kuendesha "mifumo"
Aliekwambia ufanisi was kufundisha umeongezeka nani? Acha kusikiliza propaganda za wanasiasa.Kundi la vilaza ni kubwa sana lilinalosukumwa kwenda form one na matokeo ta form two na four huwaumbua.
 
Nchi zingine wamedhibiti uzazi sisi tunazaliana sana kila mwaka watoto wanaongezeka Ulaya na Marekani ni kinyume ndio maana wanatoa hadi Green Card kwa raia wa nchi zingine kwenda nchini kwao. Sisi kila hatua mbili lazima ukutane na watoto au mama mjamzito au mwenye mtoto mgongoni.

Usilaumu serikali
Hizo nchi unazotolea mfano zinaidad ya wat wengi kuliko tz
Marekani kuna zaidi ya watu milion 200
China zaid ya bilion 1.4

Ss kwa wat milion 50+ kuna haja ya kuwa na uzaz wa mpango

Nchi kama Denmark,Ukrain leo hii wanalia kuwa na idad ndog ya watu
Nchi imejaa wazee t vijana hakuna na hayo ndo matokeo kuwa na sera za uzaz wa mpango usiokuwa na tija kwa nchi hapo baadae
 
Back
Top Bottom