Kila Mtu sasa kusafiri kwa ndege yake mwenyewe..

GAMBLER

JF-Expert Member
Nov 22, 2009
303
11
Kila Mtu Kusafiri Kwa Ndege Yake Mwenyewe...
3974574.jpg

Ndege ya mtu mmoja "Puffin" inavyokuwa ikiwa anganiMonday, January 25, 2010 8:37 PM
Muda si mrefu kila mtu atakuwa na uwezo wa kumiliki ndege na kufanya safari zake mwenyewe kwani shirika la utafiti wa anga la Marekani NASA limevumbua ndege ya mtu mmoja yenye kutumia umeme yenye uwezo wa kutua kwenye makazi ya watu.Ndege hiyo iliyopewa jina la Puffin ina uwezo wa kupaa mita 9,150 toka ardhini na ina uwezo wa kusafiri kwa spidi ya kilomita 225 kwa saa ingawa spidi hiyo inaweza kuongezeka hadi kufikia kilomita 450 kwa saa.

Ndege hiyo ya mtu mmoja yenye kutumia umeme hupaa na kutua kama helikopta.

Ndege hiyo huanza kupaa mtu akiwa amesimama na inapofika angani huanza kuchanja mbuga mtu akiwa amelala.

Iwapo betri la ndege hiyo litakuwa limechajiwa full, basi ndege hiyo ina uwezo wa kusafiri kilomita 80. Utafiti zaidi wa betri unaendelea ili kuiwezesha ndege hiyo kuwa na uwezo wa kusafiri kilomita 300 bila kupumzika.

Pia kutokana na kwamba ndege hiyo ni ndogo sana, haitahitaji kutua kwenye uwanja wa ndege na pia kwa kuwa haitoi kelele sana kama helikopta itakuwa na uwezo wa kutua kwenye makazi ya watu bila kusababisha kero kwa watu.

Ndege ya kwanza inatarajiwa kuwa tayari mwezi machi mwaka huu.

Chini ni VIDEO ya ndege hiyo.[ame]http://www.youtube.com/watch?v=lj4UOAWGNyQ[/ame]
 
Hii imekaa vizuri, hasa kwa sisi tunaoishi IGogo kusiko na barabara!...lol...sijui itakuwa bei gani.
 
matrafiki watakuwa wanapiga doria hadi huko

Mi nadhani the whole thing is misuse of science. Sidhani kama huu uvumbuzi utaisaidia mankind.

Kwa upande wa Tz hii ni ndoto kutokea. Kama barabara na matreni tu vinatushinda kuvimanage na kuvipataia thamani na ufanisi unaotakikana, sasa huko angani si itakuwa kuokota maiti tu kila siku??
 
Du!! wazungu balaaaaaaaaa!!! Yaaani uchawi wao wanataka nasisi waturithishe kwani wameona waafrica wanawanga pasipo sababu
 
Back
Top Bottom