Kila mtu kwa nafasi yake tutendeane haki kuhusiana na janga hili la COVID-19

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,824
35,822
Haieleweki hawa watu ambao wamependa kusema serikali iko makini au wapo makini kuudhibiti ugonjwa huu wana maana au nia gani na taifa hili. Watu hawa, hawakuweza kuuzuia ugonjwa kuingia nchini wala hawana mpango wowote thabiti uliowazi wa kuudhibiti ugonjwa huu usisambae.

Matokeo yake ugonjwa unazidi kusambaa na watu wanazidi kuambukizwa. Ikumbukwe kuwa 5% - 10% ya walioambukizwa hupoteza maisha. Hivyo idadi ya vifo itaendelea kupanda kulingana na maambukizi yanavyokua.

Nchi zote duniani zinachukua hatua. Sisi tokea kwenye maombi sasa tumefikia kwenye mitishamba. Hadi sasa tunaongelea kwenye dawa za kufukiza. Hatujadhamiria (We are not serious).

Maendeleo na ustawi wa nchi hii hauwezi kuachwa mikononi mwa watu fulani wawe wengi au wachache, werevu au wajinga nk. Si kweli kuwa wana CCM wote wanamwunga mkono Magufuli kwenye hili ninaamini hata yeye anajua hilo.

Si kweli kuwa anaungwa mkono na watanzania walio wengi katika hili. Hili pia atakuwa analijua. Wala si kweli kuwa hata serikali yake yote iliyo sheheni madokta na maprofesa kuwa eti inamwuunga mkono kwenye hili la miti shamba. Ninaamini hilo nalo analijua pia.

Si mbaya mheshimiwa akajua kuwa kwa hakika katika tupo watanzania wengi tu ambao hatumwungi mkono kabisa kwenye haya. si mbaya pia akajua wanaomwuunga mkono kwenye haya ya miti shamba na Corona, sana sana ni wale wajinga kabisa katika jamii na zaidi kabisa hasa wale ambao hawakusoma tokea katika kabila lake (ambalo zaidi ya 80% yao ni wapagani).

TWAWEZA wanaweza mpa ufafanuzi zaidi kwenye hili maana wangali nayo sifa Tao ile adimu ya kutokupendelea upande wowote pamoja na shinikizo tokea katika serikali hii.

Takwimu tunazopewa tokea serikalini za maambukizi, za wanaopona na hata za vifo ni wazi kuwa zimekuwa utata mtupu. Magufuli mwenyewe amekubali hilo. Tunasikia kuna wagonjwa wa Corona wanatoroka mahospitalini.

Mikusanyiko ikiwamo ya ibada na masokoni inaendelea. Usafiri wa umma mijini na mikoani, zikiwamo ndege na mabasi ya abiria unaendelea. Hii ikiwa kinyume kabisa na maonyo yote tunayopata tokea katika jamii zote za kimataifa.

Hii yote ikiwa ni kiongozi wetu mmoja tu ambaye amechagua kujifanya kichwa ngumu kwa niaba yetu sote. Hii siyo sahihi na ni muhimu tukawajibika kumfahamisha hilo.

Katika hali ya sasa ni biashara ipi ambayo inaendelea? Labda kama ni serikali pekee ambaye ndiyo mnufaika.

Kodi za serikali ziko palepale, marejesho ya mikopo benki yako palepale, sekta binafsi mishahara iko palepale, nk huku ugonjwa ukiendelea kusambaa.

Haihitaji elimu kubwa kuliona shimo kubwa lililoko mbele yetu.

Hili ni letu sote. Kuacha watu wa kufa wafe tu (eti kuwa yalikuwa mapenzi ya Mungu), hadi dawa au kinga itakapopatikana haiwezi kuwa uchaguzi sahihi.

Pana hatua za kuchukua ambazo wenzetu wengi walio kama sisi wamechukua na hali za maisha yao leo haziko hatarini tena. Hauwezi kuwepo wakati zaidi ya huu sasa.

Tusiokubaliana na status quo tunapaswa kupazwa sauti zetu waziwazi kutafuta mstakabala tofauti.

Kutokubaliana ni jambo la afya tu na ndiyo maana huwa kunakuwa chaguzi. Aliimba pia "hata watoto mapacha hukosa kuelewana, sembuse mimi nawe..." Mwisho wa kumnukuu.

Ni muda sasa badala ya kuendelea kukaa kimya kusubiria kuangamia 'naturally' kwa Corona, tukaamka kila mtu katika nafasi yake kudai kwa nguvu kabisa njia muafaka zaidi za kuudhibiti ugonjwa huu. Ni kweli kuwa haihitaji amri ya serikali kufunga misikiti na makanisa.

Maaskofu, ma Sheikh, wachungaji nk mnaoona umuhimu wa kuwa na approach tofauti ni vyema mkasimamisha mikusanyiko ya ibada makanisani na misikitini mwenu kwanza. Ili tupambane sote kwa umoja wetu kupiga vita mikusanyiko yote inayotuweka katika hatari ya maambukizi zaidi.

Sote bila kujali tulipo tunaweza kudai uwajibikaji tofauti sasa kabla hatujawa wahanga wa ugonjwa huu. Ni sasa wakati tukiwa na afya zetu au never. Bila hivyo tunaweza jikuta katika hali mbaya zaidi muda si mwingi kutoka leo.

Pamoja tunaweza kudai tukapata tunachotaka tokea kwa rais huyu. Rais ni mtumishi wetu. Kwa vile yeye siyo mtawala wetu tunayo haki ya kudai atusikilize na akatusikiliza.

Shukurani na pongezi ziwafikie wote walioonyesha ujasiri wa wazi na hata wa kuyatamka mengi ya nini kifanyike pasipo kuwa na woga.

Ugonjwa huu hautaondoka wenyewe. Utaondoka kwa jitihada ambazo kwa hakika hazitakosa maumivu.

Nawasilisha.
 
LIKE,
Baba wa taifa (rip) hayupo asingekubaliana na upuuzi huu.

Huyu tunapaswa kumkabili sote kila mtu kwa nafasi yake. Ikibidi iundwe tume ya viongozi wa dini, wabunge na wenye mawazo mbadala kuonana na huyu mheshimiwa.

Hayuko sahihi kwenye hili. Hapana sababu ya kupepesa macho au kumung'unya maneno tena.

Ikibidi atwambie maambukizi au vifo vingapi vikifika atakuwa ameshindwa kuudhibiti ugonjwa huu.
 
Back
Top Bottom