Kila mtu atakula kwa jasho lake-mkulo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kila mtu atakula kwa jasho lake-mkulo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bajabiri, Mar 19, 2011.

 1. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Waziri wa fedha mustafa mkulo amesema kuwa kila mtu atakula kwa jasho lake,na kuwataka wananch wasitegemee hali ngumu ya uchum waliyonayo kama itaisha,pia amesema serikali haitafuta kodi za mafuta ng'o
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Ningeruhusiwa kumtukan... ningeridhika kidogo
   
 3. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Nani kasema huruhusiwi? Mtukane kimoyomoyo, u will feel better!
   
 4. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  jina lake ni matusi tosha....watu wa kusini ya tz wananipata???
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Yaani nchi hii bana, mtu akiwa waziri wa fedha huwa anajisahau sana, nakumbuka Mramba aliwahi kusema "tupo tayari watanzania wale nyasi lakini ndege ya rais(ya kifisadi) ni lazma inunuliwe"
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  nami nimewaza nikawazua kama wewe
   
 7. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkullo anapashwa kuwataka radhi watanzania; haiwezekani akatamka maneno kama hayo wakati yeye ndiye aliyepewa dhamana ya kusimamia rasilimali yetu wote, badala ya kuhakikisha rasilimali hiyo inatumika kwa maendeleo ya wote, ametumia sehemu kubwa ya mali hiyo kuwagawia watu wachache, sehemu ya rasilimali iliyosalia ameitumia katika mambo ya anasa, na ako kakiduchu kalikosalia ndiko anataka watu tulio wengi tugawane. Hama budi abanwe kweli kweli atuonyeshe alikoiweka mali yetu.
   
 8. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kila mtu kula jasho lake sio tatizo, Bwana Mustafa, tatizo linakuja pale wengine wanapokula kwa jasho la wengine. Hela za serikali zinachotwa (epa,meremeta, richmond, dowans, rada etc ), wewe kama waziri hukumei, mapato ya serikali yanapotea ( utalii, uwindaji na madini) husemi kitu, rais anasafiri bila sababu nje ya nchi na waziri wake anasinzia pembeni, unaona sawa tu, wewe unakodiwa ndege kwenda dodoma na gari inafuta ikiwa na dereva unasema watu wanatoa siri za ofisi nje.

  Mashangingi yananunuliwa na serikali kwa kila idara na mengi kati ya hayo huwa hayatumiki , yanapaki miaka yote yanangoja yawe "written off in the books", myanunue wewe na idara yako ya ukaguzi mnakoroma tu. Ukiambiwa punguza kodi ndo unang'aka kila mtu atakula jasho lake.

  Kwa nini usiwakemee wanaokula jasho la wengine, Mustafa, kama waziri kazi yako ni kudhibiti mapato ya nchi tena hiyo ndio muhimu zaidi, uking'ang'ania msemo wako utagundua kuwa wengi wa watanzania kwa hivi sasa hata jasho hawana, limeliwa lote na wengine, sijui kesho utasema tule nini.

  Anyway ndo maisha bora hayo uzalendo huyo ambao clouds wanataka tuufurahie kwa kucheza kiduku pale biafra.

  Mungu wa Israel uko wapi utuokoe wanao????
   
 9. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mkulo anatamka hayo maana yeye ameshakula akavimbiwa na sasa anaona watz ni takataka. Haya yana mwisho na ajiulize Mramba alipo.
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  You couldnt have said better, it seems, as a minister Mustafa does not know the scope of his duties. He should be sacked with immediate effect.
   
 11. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,322
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280
  Msisahau jamani kauli kama hizi zitaendelea kusemwa na na viongozi vipofu watokanao na ccm waliokula rasilimali za nchi hii. Sisi tutakula kwa jasho lakini mkulo anakula vya wavuja jasho, zitakuja kukutoka puani. analipwa kwa kodi zetu huyo acha kauli za madharau uliza mwenzako mramba yuko wapi na kauli za kula nyasi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 12. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu Mkulo ninakujua fika kweli haya maneno unayazungumza leo kweli...!!!!!....???
  Unakumbuka ulikotoka? NA kama si washikaji wa JK kukupigia debe ukatoka kunywa gongo pale
  kilosa ukapewa hicho cheo leo hii kweli unatukana!
  Naona unamtukana Jk na sio watz,juzi tuu kakuomba uangalie uwezekano wa kupunguza kodi esp. mafuta
  walao wadanganyika wapate ahueni ya maisha ww unamtukana.
  DUA ZA WATZ ZINAWEZAKUKUFANYA KITU KIBAYA.omba radhi.
   
 13. m

  msosholisti Member

  #13
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkula nakwambia punguza kodi kwenye mafuta. laa sivyo nitakuona 2015 siyo mbali, tutapambana jimboni kwako.
  Halafu watz kuna baadhi vitu havina jinsi kupanda bei, mfano unga,mchele,maharage. Wtz wengi mnang'ang'ania town. Jamani hata kama upo mjini anzisha kimradi angalau cha ekari hata mbili ulime chakula. Tafuta kijana pale kijijini muwezeshe japo ekari 5 theni zako 3 zake mbili. Nadhani kila alie mjini akilima angalau ekari moja tu ya chakul, kisingepanda bei. Lakini wana JF mpo mjini tu the nanai akuzalishie chakula wewe ule tu. Sisi wakulima tukipandisha bei nyie mnalalamikia serikali. wewe unataka wafanyeje kwenye bei ya mchele, au unga, au maharage. tutumie akili zetu wtz kuna baadhi ya bidhaa hasa ya vyakula vyetu ambavyo vingi tunalima wenyewe. Mashamba mengi yapo poli tu hata ukienda hapo karibu na mjini-bonde la mto ruvu -ni pori tu linalalalia. Na ukija huku kwetu moro-ndo kabisa mabinde kibao yanalalia mapori. Tena yanagawiwa na vijiji vyetu.
   
 14. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mbona hata mvuazinasumbua Jamani?
   
 15. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,580
  Likes Received: 1,942
  Trophy Points: 280
  Mkulo amesahau kuwa na wao wanakula kwa jasho la wananchi?Kama wananchi wangekuwa wanaruhusiwa kula kwa jasho lao nani angwapigia kelele?Tatizo ni wao wanakula jasho la wananchi.
   
 16. Msolopagazi

  Msolopagazi JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 659
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Hii ndo ari zaidi,nguvu zaidi na kasi zaidi sasa mnalalamika nini:angry::angry::angry:
   
 17. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,056
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Kujisahau kubaya jamani.. Looh!! Huyu bwana Mkulo kajisahau huyu.
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kama unaenda kilosa kati nitakuwa kampen meneja wako,kuanzia maeneo ya kimamba,rudewa,madoto,dumila,
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  alikua kwenye mikonge rudewa+kimamba.leo yupo dar kajisahau,anasahau kuwa waliompa kura ni watu wa dumila,kilosa,
   
 20. M

  MZAWATA JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  wameshashiba jaman, watatukumbuka sisi wallala hoi, huo ndo msimamo wa CCM, tutaendele kuumia jaman kama tutashindwa kuwa na nia ya mabadiliko WATANZANIA
   
Loading...