Kila mtu analalamika Magufuli kabana,je amebana vipi?wachumi nisaidieni

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,463
Habari wanabodi?
Mimi siongelei na wala sijishughulishi na habari za bwana Bashite maana hazinisaidii katika maisha yangu.Kuna msemo unasema "bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi".

Mimi kuna jambo linanitatiza sana,huku mtaani karibia kila mtu analalama eti Magu kabana.Sasa najiuliza amebana vipi?

Kama mjuavyo mimi sijaajiliwa na sijawahi kuajiliwa na sifikirii kuajiriwa either na serikali au private sector. Nimejaribu kuuliza baadhi ya watu wangu wa karibu walioajiriwa na serikali kama labda mshara hawalipwi kabisa au hawalipwi kwa wakati,nimeambiwa wanalipwa mapema kabisa na wala hawajawi kucheleweshewa.

Sasa nashangaa watu hao pia wanalalamika eti Magu kabana,najiuliza wamebanwa nini wakati mishahara wanapewa? Kuna hawa ambao hawajaajiliwa nao wanalalamika,sasa mtu hujaajiliwa na Magufuli bali umejiajili bado ulalame Magu kabana,kakubana nini?

Mfano mimi binafsi biashara zangu zinaenda vizuri tu na Magufuli hahusiani na chochote,sasa ananibana nini?

Wachumi nisaidieni ni vipi watu wanasema Magufuli amebana? Yaani amebana vipi?

Mfano dereva bodaboda,kondakta,mfanyakazi wa ndani,mwalimu,daktari yaani magufuli amewabana vipi?
 
Kuna kulalamika kwa kufuata mikumbo na pia kuna kulalamika kwa kuona hali halisi wengi tunao lalamika tupo katika kundi la mkumbo lakini pia huku kubana kana tokana na miradi mingi kuto kuanaza au kuendelezwa maana mradi ukianzishwa katika eneo lako vijana watapata ajira na mamantilie ataweza kujiajiri kwa kupika chakula katika huo miradi na kumbuka huyu mamantilie ataenda kununua mahitaji yake sokoni na hawa wengne walio ajiriwa katika huo mradi watakuwa wanafanya manunuzi ya vitu mbalimbali ndo mzunguko wa hela utaonekana sasa inapo kosekana miradi kuanzishwa ndo kubana kwenyewe
 
Kiuchumi iko hivi; mtumishi akiwa na hela jamii yote inanufaika kupitia expenses mbalimbali. Lakini ukiangalia sana rais tulie nae Mh Magufuli amekusanya saaaana ila bado hajaachia hela wala kuongeza huduma za jamiii.

Ikumbukwe kuwa kiuchumi ukikusanya sana bila kuachia ni tatizo maana serikali inakuwa na hela hazina ila watu wake hawana kitu meanz mzunguko wa hela Mdogo sana.
Pili unaweza kukusanya sana hela alafu zikatumika kwenye huduma za jamii.
Kwa mliosoma uchumi nadhani mtakubaliana nami na mbinu hii alitumia sana Mh Mkapa.
 
Inawezekana kwako unaona kila kitu kipo sawa kumbe hakipo sawa!!!

Ukiwauliza Agricultural Extension Officers watakuambia shida wanazokutana nazo wanapokutana na wakulima wasio na uelewa!

Ukimwambia, kati ya shimo na shimo acha inchi kadhaa na pia uwe unapanda kwa mistari... atakujibu mbona tangu zamani napiga mashimo hapa na pale (randomly) na bado mavuno napata!!!

Asichofahamu ni kwamba anachopata sio optimum produces... huenda alitakiwa kupata gunia 30 lakini anaishia kupata 15 na anaona anapata!!!

Jana nilikuwa napitia financial reports za benki mbalimbali!!

Ukiangalia financial reports za CRDB, unakuta as at December 31, 2015 beniki ilikuwa na 8% ya mikopo isiyolipika ambayo thamani yake ni takribani 271 Billion. Mwaka mmoja baadae, mikopo isiyolipika imefikia 436 Billion ambayo ni 11% ya mikopo yote iliyotelewa!! Hilo ni ongezeko la TZS 165 Billion!!

Tafsiri ya haraka haraka hapo ni kwamba kuna ongezeko la watu wanaoshindwa kulipa mikopo na wala usidhani kwamba hawataki kulipa bali biashara zinawaendea hovyo!!

Na kama zinawaendea hovyo, unaweza kupata picha ni wangapi wameathirika wanaotokana kushindwa kufanya vizuri hizo biashara ambazo mikopo yake ni takribani 165 Billion! Ukichanganya na mitaji yao ya awali; hizo ni biashara za above 500 Billion!!!!

Hiyo ni benki moja tu.... CRDB!!!

Hapo kuna ambao waliajiriwa na huenda wameachishwa kazi; hao nao kulikuwa na watu wanaofanya nao biashara (suppliers) ambapo biashara kati yao nao zimeathirika! Na katika hapo usikute kulikuwa na kampuni zenye wafanyakazi +25 ambapo kutokana na kuyumba; wakalazimika kufunga biashara na kuathiri hizo ajira +25 lakini pia kuathiri ajira za wauza chai!!!

Hao nao purchasing power yao imepungua na kukuathiri hata wewe ingawaje unadhani kila kitu kwako kipo shwari!!!
 
Kuna kitu ktk uchumi kinaitwa multiplier effect,yaani ni namna ambavyo kutokea kwa jambo moja kunavyoweza kuathiri jambo jingine, sasa tuone Sera za Magu zilivyoathili maisha yetu,
1- alivyozuia serikali isitumie hoteli binafsi kufanya mikutano na vikao, moja kwa moja ikaathiri revenue ya hoteli nyingi zilizokuwa zinategemea serikali kama mteja mkuu ,hivyo kulazimika kupunguza wafanyakazi baada ya kushindwa kuwalipa ,hoteli nyingine zilifungwa na kugeuzwa hostel MF. (Ubungo plaza)
2-alipohamisha accounts zote za mashirika ya umma kutoka benki binafsi mpaka BOT,ikafanya benki nyingi kuyumba kwa kupungukiwa na kiwango kikubwa cha Pesa kilichokuwa kuwa kinatumika kukopesha wananchi kwahiyo faida ikapungua ktk mabenki,na wananchi waliokuwa wanakopa Ili kuboresha biashara zao nao wakaathirika kwa kupungukiwa na hela za kuwekeza Mtaani,matokeo yake hata Ajira nazo walizotegemea kuzalisha kwa raia zikapungua na kuleta ugumu wa maisha,
3-kuipa taasisi ya serikali Kazi muhimu za ujenzi,kukapelekea kuyumbisha makampuni binafis ya ujenzi yaliyokuwa yanategemea yapate miradi Ili yapate kipato cha kulipa watu na kuwekeza kwa RAIA,
4- ameshindwa kuajiri kwa zaidi ya mwaka sasa,tulitegemea kwa kiwango cha chini serikali kama muajiri mkuu ingeweza kutoa Ajira kwa takribani watu laki moja ndani ya mwaka mzima unaoisha,kwa wastani kwa takwimu zisizo rasmi MTU mmoja muajiriwa anategemewa na watu wa 4,sasa angetoa Ajira kwa watu 100,000 angekuwa amesaidia kuboresha maisha ya watu laki 4,kushindwa kufanya hivyo ni kuwafanya watu kuwa tegemezi etc.
Mifano ni mingi sana,ila hiyo ni kwa ufupi tu,elewa Pesa inatoka ssrikalini kuja kwa RAIA kupitia uwekezaji ,serikali haimwagi hela kwa watu barabarani,sasa kama serikali imeshindwa kufanya uwekezaji wa maana kwackipindi hiki tegemea hali maisha ya watu kuwa magumu,
Kuongezeka kwa kiwango cha kodi kumefanya wafanya biashara wengi kuongeza bei za bidhaa,Sera mbovu za uhifadhi kumefanya bidhaa muhimu za maisha kama Michele,unga na sukari kupanda bei kwa zaid ya asilimia 100,unga sasa kilo ni 2200/- kwa hapa nilipo ,kumefanya maisha ya watu kuzidi kuwa mabaya,imagine hela hakuna na gharama za maisha zimepanda,halafu mwenyewe anajisifa anainyoosha nchi!
 
-KAFUTA AJIRA
-NO INCREMENT
-HAKUNA KUPANDISHWA MADARAJA
-HAKUNA UHAMISHO WA WAFANYAKAZI
-WATOTO WA MASIKINI WAMENYIMWA MIKOPO
-BEI YA VYAKULA IPO JUU SUKARI 3000, DEBE LA MAHINDI 23,000
- HELSB 15%
Item 1=1v zinasaidia kukua kwa uchumi wa nchi au ni miradi ya maendeleo? Ambayo labda itazalisha hatimae kuwa chanzo cha uchumi?.
Nafikiri hayo yote yapo ktk kundi alilosema JPM hewa hewa hewa hewa tumuache asafishe ili hata akihamisha ahamishe mtu kweli na sio hewa.
Ndio mtazamo wangu na naamini pia JPM na serkali yake.
 
Kiuchumi iko hivi; mtumishi akiwa na hela jamii yote inanufaika kupitia expenses mbalimbali. Lakini ukiangalia sana rais tulie nae Mh Magufuli amekusanya saaaana ila bado hajaachia hela wala kuongeza huduma za jamiii.

Ikumbukwe kuwa kiuchumi ukikusanya sana bila kuachia ni tatizo maana serikali inakuwa na hela hazina ila watu wake hawana kitu meanz mzunguko wa hela Mdogo sana.
Pili unaweza kukusanya sana hela alafu zikatumika kwenye huduma za jamii.
Kwa mliosoma uchumi nadhani mtakubaliana nami na mbinu hii alitumia sana Mh Mkapa.
Amesema haachi na hatishwi na mtu hewa hewa hewa akijiridhisha zimeisha ataachia pesa lkn bado watakaonufaika naona watakuwa wachache wa halali. Tukumbuke atakuwa ameziba na kudhibiti gap kubwa ya hewa.
Ni vema tu tukaanza kujishughulisha kihalali tuwe na uhakika wa kuwepo ktk mzunguko.
Ben hakuwahi kusaka hewa ivo watu walitumia mwanya huo kujiingizia pesa nyingi chafu mtaaani.
 
1.Mwajiriwa wa serikali (private sijui) aliyesoma chuo kikuu, sasa hivi anakatwa 15% badala ya 8% ya Mshahara wake, mbano wa kwanza.
2. Mbano wa pili, ile increment ya kila mwaka na ongezeko la kila mwaka kwenye mshahara (kutokana na presidential grace/kupanda gharama za maisha kila mwaka) halipo tena.
3. Kutokana na mbano huo, huyu mwalimu, huyu nesi, huyu mtumishi amepunguza msaada kwa wazazi/ndugu zake kwakuwa kipato chake pia kimepungua.

Hii haiitaji kusoma uchumi, kila kitu kipo uchi ndugu. Mbano upo tuu, kama wewe huuoni shukuru Mungu.
 
Habari wanabodi?
Mimi siongelei na wala sijishughulishi na habari za bwana Bashite maana hazinisaidii katika maisha yangu.Kuna msemo unasema "bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi".

Mimi kuna jambo linanitatiza sana,huku mtaani karibia kila mtu analalama eti Magu kabana.Sasa najiuliza amebana vipi?

Kama mjuavyo mimi sijaajiliwa na sijawahi kuajiliwa na sifikirii kuajiriwa either na serikali au private sector. Nimejaribu kuuliza baadhi ya watu wangu wa karibu walioajiriwa na serikali kama labda mshara hawalipwi kabisa au hawalipwi kwa wakati,nimeambiwa wanalipwa mapema kabisa na wala hawajawi kucheleweshewa.

Sasa nashangaa watu hao pia wanalalamika eti Magu kabana,najiuliza wamebanwa nini wakati mishahara wanapewa? Kuna hawa ambao hawajaajiliwa nao wanalalamika,sasa mtu hujaajiliwa na Magufuli bali umejiajili bado ulalame Magu kabana,kakubana nini?

Mfano mimi binafsi biashara zangu zinaenda vizuri tu na Magufuli hahusiani na chochote,sasa ananibana nini?

Wachumi nisaidieni ni vipi watu wanasema Magufuli amebana? Yaani amebana vipi?

Mfano dereva bodaboda,kondakta,mfanyakazi wa ndani,mwalimu,daktari yaani magufuli amewabana vipi?

kama ni elimu katika uchumi uko chekechea na haiwezekani mtu akakueleza hapa ukaelewa. labda kwa kukusaidia kafanye homework utafute wewe kama kama mtu uliyejiari serikali inaweza kukusaidiaje. lipo tatizo hapa ukisema hivyo wengi wanafikiri mikopo lakini kwa ufupi serikali ndiyo inayomonitor biashara yoyote katka nchi.

kila mwananchi ni mfanya biashara, akiuza huduma au bidhaa. wapo wanaouzia huduma katika ofisi za serikali au binafsi hawa tumezoea kuwaita wafanyakazi na wapo wanaouza bidhaa na huduma kwa mtu mmoja mmoja au ofisi na hawa tumezoea kuwaita wafanya biashara.

lakini serikali ni katika biashara hii ni kama refa akisimamia kanuni tulizojiwekea katika biashara lakini ni zaidi ya refa maana kanuni hizi anatunga mwenyewe. hivyo serikali inatunga na kusimamia na kuwezesha biashara kufanyika.

anaweza kumlipa kwa wakati mtumishi lakini wakati hajaongeza kipato akaongeza gharama kwenye matumizi. mfano kwa sasa kodi nyingi sana zimeongezeka hivyo mtu kipato alichokuwa akipata kinakuwa hakitoshi mahitaji yaleyale aliyokuwa anamudu. wachumi huwa wanapandisha kodi taratibu huku wakitumia kodi hizo kuchochea vyanzo vya mapato vya wananchi ili vipato vikue na kipato kikikua anaongeza tena.

kwa mfanya biashara anategemea wafanya kazi hawa wanunue hivyo kama wakilipa kodi nyingi fedha inayobaki kufanyia manunuzi inapngua, wanachokifanya ni kubana matumizi kwa kupunguza baadhi ya vitu walivyokuwa wakinunua au vingine kuacha kabisa. maana yake kutokana na kanuni anazozibadilisha serikali na kuzisimamia unakuta wateja wanapungua hivyo tayari serikali inakuwa imefanya maamuzi yanayoathiri biashara.
 
Item 1=1v zinasaidia kukua kwa uchumi wa nchi au ni miradi ya maendeleo? Ambayo labda itazalisha hatimae kuwa chanzo cha uchumi?.
Nafikiri hayo yote yapo ktk kundi alilosema JPM hewa hewa hewa hewa tumuache asafishe ili hata akihamisha ahamishe mtu kweli na sio hewa.
Ndio mtazamo wangu na naamini pia JPM na serkali yake.
Mtu kutoka sehemu mmoja kwenda nyingine husaidia kuongez kipato cha watu.
Mfano.
Huyu mwalimu anafundisha wilaya ya misungwi kata ya Kolomije. Kwahiyo anapohama kwenda mkoa mwingine km Shinyanga wilaya ya kahama kata ya mzizima huhitaji nyumba ya kupanga, mashamba, mbali na hivyo kuna mahitaji ya kila siku hasa ya chakula. Km mtu anakibanda chake cha nyanya, mchicha, mkaa na mahitaji mengine ni fursa ya kujiingizia kipato kupitia huyu mfanyakazi.
Hukwenda shule nn?
 
Kuna kitu ktk uchumi kinaitwa multiplier effect,yaani ni namna ambavyo kutokea kwa jambo moja kunavyoweza kuathiri jambo jingine, sasa tuone Sera za Magu zilivyoathili maisha yetu,
1- alivyozuia serikali isitumie hoteli binafsi kufanya mikutano na vikao, moja kwa moja ikaathiri revenue ya hoteli nyingi zilizokuwa zinategemea serikali kama mteja mkuu ,hivyo kulazimika kupunguza wafanyakazi baada ya kushindwa kuwalipa ,hoteli nyingine zilifungwa na kugeuzwa hostel MF. (Ubungo plaza)
2-alipohamisha accounts zote za mashirika ya umma kutoka benki binafsi mpaka BOT,ikafanya benki nyingi kuyumba kwa kupungukiwa na kiwango kikubwa cha Pesa kilichokuwa kuwa kinatumika kukopesha wananchi kwahiyo faida ikapungua ktk mabenki,na wananchi waliokuwa wanakopa Ili kuboresha biashara zao nao wakaathirika kwa kupungukiwa na hela za kuwekeza Mtaani,matokeo yake hata Ajira nazo walizotegemea kuzalisha kwa raia zikapungua na kuleta ugumu wa maisha,
3-kuipa taasisi ya serikali Kazi muhimu za ujenzi,kukapelekea kuyumbisha makampuni binafis ya ujenzi yaliyokuwa yanategemea yapate miradi Ili yapate kipato cha kulipa watu na kuwekeza kwa RAIA,
4- ameshindwa kuajiri kwa zaidi ya mwaka sasa,tulitegemea kwa kiwango cha chini serikali kama muajiri mkuu ingeweza kutoa Ajira kwa takribani watu laki moja ndani ya mwaka mzima unaoisha,kwa wastani kwa takwimu zisizo rasmi MTU mmoja muajiriwa anategemewa na watu wa 4,sasa angetoa Ajira kwa watu 100,000 angekuwa amesaidia kuboresha maisha ya watu laki 4,kushindwa kufanya hivyo ni kuwafanya watu kuwa tegemezi etc.
Mifano ni mingi sana,ila hiyo ni kwa ufupi tu,elewa Pesa inatoka ssrikalini kuja kwa RAIA kupitia uwekezaji ,serikali haimwagi hela kwa watu barabarani,sasa kama serikali imeshindwa kufanya uwekezaji wa maana kwackipindi hiki tegemea hali maisha ya watu kuwa magumu,
Kuongezeka kwa kiwango cha kodi kumefanya wafanya biashara wengi kuongeza bei za bidhaa,Sera mbovu za uhifadhi kumefanya bidhaa muhimu za maisha kama Michele,unga na sukari kupanda bei kwa zaid ya asilimia 100,unga sasa kilo ni 2200/- kwa hapa nilipo ,kumefanya maisha ya watu kuzidi kuwa mabaya,imagine hela hakuna na gharama za maisha zimepanda,halafu mwenyewe anajisifa anainyoosha nchi!
Nimeipenda analysis yako kiongozi, nimeishia kuumia tu hasa ninapofikiria hali ya nyumbani na mimi ni mwajiriwa ambaye nyumbani kiasi flani wananitegemea halafu hela hakuna, unga kilo si chini ya 2000 jumlisha na huu ukame kwa kweli inaniuma sana mbaya zaidi nina nyumbani nina mgonjwa. Acha tu mkuu analysis yako imeniumiza sana.
 
Asilimia kubwa ya watanzania wako katika sekta isiyo rasmi / binafsi ambazo kwa asilimia kubwa zinategemea mikopo ya benki.ni vigumu sana kwa benki kusema tumepata hasara ili kutokuwaweka wateja kwenye hofu na kuweza kuhama benki. Ni kama wanajeshi wanavyokuwa vitani siyo rahisi nchi kuambiwa idadi kamili ya waliyokufa na hiyo ni kuwapa moyo wananchi na wanajeshi wenyewe. Mizunguko mikubwa ya benki ilikuwa katika fedha za serikali. Ambapo taasisi zilipokuwa zikiweka benki zilikuwa na uwezo wa kuwakopesha wateja wake. Leo hii baada ya serikali kuhamishia bot benki zimeshindwa kuendelea kutoa mikopo kama ilivyokuwa awali. Kuna baadhi ya makampuni yalikuwa yanachukua mkopo kwa short term ma hivyo kukimbizana na soko la kipindi hicho ambacho walikuwa na uhakika wakurudisha fedha benki ili pindi taasisi zitakapohitaji ziwezekupata fedha zao. Sasa kutokana na matajiri kutokuwa na fedha ambayo itakidhi soko kinachotokea ni kupunguza mzunguko wao wa fedha ambao anao yeye kama yey na hivyo kupunguza mzunguko hadi kwa wafanyakazi wake. Pindi inapokuwa hivyo ni dhahiri hadi nje ya wafanyakazi mzunguko lazima upungue. Hutakaa usikie tajiri akisema maisha magumu,mfano mengi akiona bidhaa hazinunuliki sana anachokifanya anapunguza uzalishaji na hivyo kama kwa siku magari 10 yalikuwa yatoka atafanya zitoke 7. Hapo utaona gari 3 hazitoki,maana yake dereva,wapakiaji/washushaji na wafanyakazi wa kuzalisha watakuwa wamekosa kazi. Katika hizo gari 3 utakuta mafuta ambayo kila yanapoingia tra wanatoza kodi haitozwi tena. Kodi ya wafanyakazi zaidi y 10 ya hao wafanyakazi haziendi tena tra. Hao watu wanaporudi mtaani hawana chochote kitakachoweza kuiwezesha serikali kupata kodi.mengi katika kulip mapato hatalipa kama kabla hao wafanyakazi hawajaachishwa kazi. Mfano wa pili ni kwamba asilimia kubwa ya mapato yetu yapo ndani zaidi.sisi hatuuzi nje bali tunanunua maana yake sisi tunatoa hela nje zaidi ya kuingiza ambapo ni hasara kwetu. Leo hii asilimia kubwa ya wanaoendesha serikali ni wafanyakazi wa serikali na siyo sekta binafsi. Serikali inauhakika wa kukata kodi kwa wafanyakazi wake kuliko wengine maana leo wapo 100 kesho wako 80. Katika bunge la bajeti lijalo usishangae kusikia zaidi ya 80% ya bajeti haikufanikiwa kutokana na bajeti kutokutosha. Bajeti haitofutiani na biashar ya utalii ambayo unapigia mahesabu iliyoko katika mfuko wa mtu na hujui kama ataitoa au la.
 
Kiuchumi iko hivi; mtumishi akiwa na hela jamii yote inanufaika kupitia expenses mbalimbali. Lakini ukiangalia sana rais tulie nae Mh Magufuli amekusanya saaaana ila bado hajaachia hela wala kuongeza huduma za jamiii.

Ikumbukwe kuwa kiuchumi ukikusanya sana bila kuachia ni tatizo maana serikali inakuwa na hela hazina ila watu wake hawana kitu meanz mzunguko wa hela Mdogo sana.
Pili unaweza kukusanya sana hela alafu zikatumika kwenye huduma za jamii.
Kwa mliosoma uchumi nadhani mtakubaliana nami na mbinu hii alitumia sana Mh Mkapa.
Kweli kakaa
 
Back
Top Bottom