Kila mtu ana zake na kila mtu ana chake. Tusilazimishe kufanana

Mwanamwaiche

JF-Expert Member
Apr 13, 2022
667
966
Hello Hello

Hivi hii kasumba ya watu kutaka wengine wafanane au wawaze kama wao, fikra na mitizamo au maoni viwe kama wao ni uzuzu wa kielimu au ni dhana ya unyani?
Upekee wa kiumbaji ni pamoja itikadi, ufahamu, imani, ufuasi, kutumwa, kutumika, unafiki, uoga, etc.

Imeonekana kizazi cha Sasa hakijui uhuru, haki, demokrasia ya mtu binafsi au kikundi Cha watu.

Kukubali kutokukubaliana si sehemu ya elimu ama Utamaduni kwa watanzania. Tofauti ya mtizamo, maoni, huleta matusi na kebehi.

Imekuwa nadra sana maoni au mawazo tofauti ya wengine kwa baadhi ya watu manyani huonekana sivyo hata wakiwa na utofauti Kwa mrengo wa itikadi, falsafa, ufuasi na etc

Free thinking and independence of opinion and ideas hata watu wasipozijua hizo ideas hawataki kukubali kutokukubaliana ama kutofatiana.

Kuna misingi na fact za uwelewa na ufahamu wa pamoja ifahamike ipo na inapaswa jamii iwe na kiwango hicho Cha ufahamu na maarifa ya upamoja.

Na inapotokea kwa weledi, maarifa, Utamaduni, ufuasi, imani, malezi, na uzuzu kama uzuzu wa mtu ama watu iwe ni sehemu ya kufunga mjadala.

Nashangazwa ukosefu wa amani na heshima, kulinda haki na uhuru wa kimawazo katika jamii zetu.

Jazba, matusi, kejeli, nini hasa hasa tatizo kwenye jamii zetu what's wrong?


Why why why hatuwezi kutofatiana mitizamo, maoni kwa amani kabisa na maisha ya amani yakaendelea vizuri.

Ndio utani, au purposeful ukorofi upo lakini ulenge kudadisi au kumchimba mtu lakini isiwe ugonjwa wa kweli kwa jamii.

Naomba kuwasilisha karibu kwa ushuhuda na kutanua wigo wa fikra.


Kuna umuhimu pia wa kujifunza subra, staha, stahimilivu, maisha hayataki hasira. Swallow all negatives and forget.
.
 
Ewaaa hapa umenigusa kuna ndugu yangu nilienda kumsalimu kwakuwa ni mda mrefu hatujaonana, aisee nilipofika kwake nilijuta siwezi ongea jambo kwake kila kitu anajua yeye na hapendi kukubali kwamba kuna vitu nimemzidi na anachotaka yeye wote anataka mfate ila si wewe jambo uwe unaona sio uweke hata mchango kwake kosa, nikaona ngoja niishi atakavyo ikawa bora niwe kila jambo namuuliza ili twende sawa kuepuka lawama mbeleni nayo pia kosa hata uulize atakutoa kasoro kwamba kwani huwezi kujiongeza ukisema ujiongeze pia kosa atakwambia kama hauwez si uulize.

Mkewe wanagombana kila uchwao kwa tabia yake mana mpaka kwenye vyakula hapendi na yeye anapenda basi atalemletea visa kwanini kunapikwa mara mbilimbili, sasa hasichopenda yeye marufuku kupikwa kabisa yani ni mtu wa anything which is good started from him.
 
Back
Top Bottom