Kila mtu alitishwa na mwendazake, Mbowe usijifanye hujui hili

Kimbakuli

JF-Expert Member
Jul 11, 2013
405
427
Mwendazake alinyenyekea-nyenyekea kipindi cha uteuzi pale na kampeni baada ya kukalia kiti hamkuheshimu mtu, hadi wanaCCM nao wakapigwa na butwaa wakajiuliza eh huyu ndio yule yule, Viongozi wakuu waastaafu wa nchi hawakuheshimiwa, Viongozi wenzake wa serikali, bunge na mahakama nao walibaki kusema ndio mzee, alishauri washauri wake ikitokea umetoa maoni tofauti basi cha moto utakiona, kila mtu aliweka mikono nyuma na kuinamisha kichwa chini, sasa utawalaumu CCM hapo, utawalaumu Viongozi wastaafu hapo, utawalaum washauri wake hapo, utawalaumu viongozi waandamizi hapo.

Hakuna wa kumlaumu maana kwa yule mzee ungejaribu kumpinga usingebaki salama, waulize wa kina Kinana na Makamba kilichowakuta ilibidi na waufyate na wao waje kuimba mapambio ya kumsifu tu.

Kwa hiyo Mr Mbowe utalaumu watu bure wakati wewe mwenyewe unajua aliyekuwa ameshika rungu alikuwa yukoje.

MY TAKE: BINADAMU ACHA KUPENDA SIFA, SIFA ZOTE PELEKA KWA MUNGU, NA HATA UKIPATA CHEO CHA KUONGOZA DUNIA HESHIMU MAWAZO YA WENZIO, UTAISHI VIZURI SANA MAISHA YAKO YOTE ILA USIJIFANYE WEWE MWAMBA, MWAMBA NI MUNGU TU.
 
Ha ha ha ngoja waje wakeze.

Moja kwa mia Mbowe huwa natulia kwa kumsikiliza sio yule mbeligiji roporopo.
 
Mbowe hakutishwa isipokuwa aliumizwa kuliko mtu yoyote na utawala dhalimu wa kishetani kabisa, sisi ndiyo wapumbavu haswa, kwanini tutishwe na mwanaume mmoja?
Hivi we mke wa Mbowe una hakika Mbowe aliumizwa kuliko mtu yeyote kwa ushahidi upi?

Au Mbowe ana kipi Cha kuumizwa kuliko mtu yeyote?

Au hiyo kukkosa wabunge?.

MSIMCHAFUE MH.MBOWE
 
Ni kweli mkuu, na ukitaka kulijua kubwa jinga la kujipendekeza basi angalia maneno ya ndugai wakati ule na leo, yaani utaona akili ya kujikomba iko wazi kabisa ktk macho na ubongo wa yule mzee.

Ndugai ameboa sana.
 
Tatizo ni ugonjwa wake uliompelekea kwenda kuteketeza mabilioni yetu kule kwa kina Mithun Chakrabot
 
Hivi we mke wa Mbowe una hakika Mbowe aliumizwa kuliko mtu yeyote kwa ushahidi upi?

Au Mbowe ana kipi Cha kuumizwa kuliko mtu yeyote?

Au hiyo kukkosa wabunge?.

MSIMCHAFUE MH.MBOWE
Naona unaongea kwa machungu baada ya kuachwa MJANE.
 
Ha ha ha ngoja waje wakeze.

Moja kwa mia Mbowe huwa natulia kwa kumsikiliza sio yule mbeligiji roporopo.
Wewe mume wako kashatangulia mbele ya haki.
Punguza ukali kwa binadamu wenzako
 
Mwendazake alinyenyekea-nyenyekea kipindi cha uteuzi pale na kampeni baada ya kukalia kiti hamkuheshimu mtu, hadi wanaCCM nao wakapigwa na butwaa wakajiuliza eh huyu ndio yule yule, Viongozi wakuu waastaafu wa nchi hawakuheshimiwa, Viongozi wenzake wa serikali, bunge na mahakama nao walibaki kusema ndio mzee, alishauri washauri wake ikitokea umetoa maoni tofauti basi cha moto utakiona, kila mtu aliweka mikono nyuma na kuinamisha kichwa chini, sasa utawalaumu CCM hapo, utawalaumu Viongozi wastaafu hapo, utawalaum washauri wake hapo, utawalaumu viongozi waandamizi hapo.

Hakuna wa kumlaumu maana kwa yule mzee ungejaribu kumpinga usingebaki salama, waulize wa kina Kinana na Makamba kilichowakuta ilibidi na waufyate na wao waje kuimba mapambio ya kumsifu tu.

Kwa hiyo Mr Mbowe utalaumu watu bure wakati wewe mwenyewe unajua aliyekuwa ameshika rungu alikuwa yukoje.

MY TAKE: BINADAMU ACHA KUPENDA SIFA, SIFA ZOTE PELEKA KWA MUNGU, NA HATA UKIPATA CHEO CHA KUONGOZA DUNIA HESHIMU MAWAZO YA WENZIO, UTAISHI VIZURI SANA MAISHA YAKO YOTE ILA USIJIFANYE WEWE MWAMBA, MWAMBA NI MUNGU TU.
Magu hakuwa na kawaida ya kumuogopa mtu ata kipindi cha kampeni hakuwa mtu wa kuogopa, nakumbuka 2015 akiwa kwenye kampeni aliwah sema kuwa "kuna tajiri kajenga sehemu ambayo inatakiwa lipite bomba la maji huko kimara, alafu wenzie wote wameondoka ila yeye kaenda Mahakamani, Mahakama haitaki kuamua inapiga karenda! Sasa subiri niwe Rais!" Huyu ndo alikuwa Magu
 
Back
Top Bottom